Tundu Lissu: Tanzania haijapata Viongozi wa kiroho watakaotuletea viongozi wa Kidini, ampongeza Askofu Mwamakula kwa kujaribu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,722
218,283
Screenshot_2023-12-04-17-30-20-1.png

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara huko Tabata, mbele ya Umati mkubwa wa Wananchi, Tundu Lissu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema. Amesema kwamba, Nchi ya Tanzania bado inatafuta viongozi majasiri wa Kidini wataojitokeza kupigania haki za wananchi ambao pia ni Waumini wao.

Akizungumza kwa uchungu mkubwa, Lissu amedai kwamba Tanzania bado inatafuta Kiongozi wa dini kama Desmond Tutu wa South Africa aliyepambana na Makaburu bila kupepesa macho, huku akishangiliwa na Wananchi, Lissu anasema Tanzania bado inatafuta viongozi wa dini watakaopinga ukandamizaji na wizi wa mali za umma kama Askofu Denis Okuru wa Kenya au Mosengo Pasinya wa DRC ama Askofu Alexander Muge wa Kenya, aliyepinga Udikteta wa kishamba wa Arap Moi, hadi akafa kwa kupigania haki.

Tundu Lissu amempongeza Waziwazi hadharani Baba Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula kwa kujitahidi mno kumtukuza Mungu kwa kupigania haki bila kuchoka.
 
Awe muwazi basi, kwahiyo viongozi wa dini waliopo wakoje na hao akina mamkula wanatafutiwa belgium au?
 
Yupo pia katibu mkuu wa TEC, hanaga mbambamba, ni mkweli kupita kiasi na anajiamini sana
Utumishi wa kweli ni ule unaokataza maovu, kuonya na kuhubiri Toba.

Nje ya hapo ni wahuni tu wanaokusanya sadaka.
 

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara huko Tabata, mbele ya Umati mkubwa wa Wananchi, Tundu Lissu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema. Amesema kwamba, Nchi ya Tanzania bado inatafuta viongozi majasiri wa Kidini wataojitokeza kupigania haki za wananchi ambao pia ni Waumini wao.

Akizungumza kwa uchungu mkubwa , Lissu amedai kwamba Tanzania bado inatafuta Kiongozi wa dini kama Desmond Tutu wa South Africa aliyepambana na Makaburu bila kupepesa macho, huku akishangiliwa na Wananchi , Lissu anasema Tanzania bado inatafuta viongozi wa dini watakaopinga ukandamizaji na wizi wa mali za umma kama Askofu Denis Okuru wa Kenya au Mosengo Pasinya wa DRC ama Askofu Alexander Muge wa Kenya, aliyepinga Udikteta wa kishamba wa Arap Moi, hadi akafa kwa kupigania haki .

Tundu Lissu amempongeza Waziwazi hadharani Baba Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula kwa kujitahidi mno kumtukuza Mungu kwa kupigania haki bila kuchoka .
Yaani hata Sheikh Ponda hafai!
Au lazima awe Mgalatia tu!?
 
Back
Top Bottom