Osama bin Laden killed!

Osama bin Laden killed!

Status
Not open for further replies.
Wapuunzi wenzake ni mashujaa.gaidi ni mtu anegombani haki.g. Washington rais wa kwanza wa marekani alijulikana kama gaiidi kwa taifa la uingereza alipokuwa anapigania haki.kumbe kugombania haki unakuwa gaiidi.sasa osma alikuwa hagombani haki.kama osama ameuwa je bomu la hiroshima japan limeuwa watu laki mbili ulisikia marekani wakiitwa nmagaidi.iraq walisema kuna mabomu makubwa mbaka leo hayajaoneshwa.911 ilipangwa ili watu wajue marekani anajilinda bali anawinda!
 
Jamaa alikuwa anavuta bangi?
94542-marijuana-plants-growing-outside-osama-bin-ladens-compound.jpg

It is good to ask allah his deity.
 
Me naona humu jf kuna malimbukeni wa habari mimi ktk maisha yangu osama atabakia kuwa hero mbele ya kupinga udhalimu wa nchi za west ni ukweli namba ya vidume duniani inapungua lkn mugabe,fidel castro, hugo chavez, ahmed najad , hun jin tao, na kidume cha korea kaskazini hawa ni mashujaa 7bu hawataki kupelekeshwa co cc wa***** kisa 2napewa msaada wa neti hebu angalieni mifano michache USA mpaka leo hawajaondoa hukumu ya kunyongwa lkn hakuna m2 anayepinga kwa ukali bt ingekuwa nchi nyengine ungeckia UN na vikwazo vyao pili kwa mujibu wa sheria na pia wanasheria waliomo humu watakubaliana na mimi kuwa USA wanakesi za mauaji mengi moja wapo ya osama kwa mujibu wa sheria hata mtu umkamate anafanya mauaji atabakia kuwa m2humiwa mpaka mahakama itakapothibitisha sasa wao wamethibitisha vp km osama ana hatia wakati mahkama haijathibitisha au na mimi nikiwa na mtuhumu m2 kunikosea naruhusiwa kuchukua hatua mkononi HILI SWALI KWA VINAZI VYA MAGHARIBI

1. Kama sheikh Osama ni hero kwako that's ok. Kila mtu ana personal hero wake

2. Mugabe, Kim Ill jong na wenzao kama wao ni mashujaa kwako ni sawa. Lakini jiulize mbona hawachukui hatua zozote kimatendo kuipinga US kama kule Libya, Afghanistan, Abotabad etc. kama kweli ni mashujaa basi wasiishie kupiga kelele na kuufyata mkia, waonyeshe vitendo. Nao watume majeshi ama silaha Libya, Afghanistan, abbotabad na kwengineko.

3. Kuna baadhi ya states zina death penalty na nyingine hazina. Hata Iran, Iraq, Saudia, Tanzania, China, N. Korea etc. nako wananyonga na bado ni UN members

4. Kama US wana kesi basi waambie UN, China, Russia, N Korea waishtaki ama waiwekee vikwazo.

Shukran
 
Kuna utata mwingi kwenye suala zima. Hivi mtu fugitive anayetafutwa masaa 24 anaweza kupanga nyumba na kuishi na wake zake na watoto?. Pia aliyesema mipira ya watoto ikianguka ndani kulikuwa na mtu alikuwa anatoka na kuwalipa tu pesa watoto-huu nao ni utata mkubwa!. Huyo anayelipa pesa si angeokota tu hiyo mipira na kuwarushia hao watoto!?. Kulikutwa na mipira mingapi humo ndani?. Habari nyingi zinakosa uzito but i think it is just a matter of time mwanga utapatikana.
 
BINTI wa Osama Bin Laden ameeleza kwamba baba yake alikamatwa akiwa hai katika makazi yake huko Pakistani, kisha kuuawa kwa kupigwa risasi na makomandoo wa Marekani.Mtandao wa habari wa Uarabuni, Al-Arabiya ulimnukuu mmoja wa maofisa wa usalama wa Pakistani akieleza kwamba binti huyo mwenye umri wa miaka 12, alishuhudia tukio hilo na huku akieleza kwamba baada ya mauaji, mwili wake ulichukuliwa na kupakizwa katika helikopta.

Kwa mujibu wa maelezo ya binti huyo, makomandoo hao wa Kikosi Maalumu cha SEAL hawakupata msukosuko wowote baada ya kuingia na kumasa Osama.

Kwa mujibu wa Shirika la Fox News, taarifa hizo mpya zilizopatikana kwa binti huyo zinaeleza kwamba Bin Laden alikuwa na fedha na namba za simu kwenye nguo zake, wakati alipofikwa na mauti.

Iwapo taarifa hizo zitakuwa za kweli, hiyo ni dalili kwamba kiongozi huyo wa al-Qaeda alikuwa mbioni kuondoka katika makazi hayo iwapo kungetokea uvamizi.Ofisa mmoja wa Pakistani alikanusha taarifa zilizotolewa awali na Marekani kwamba kulikuwa na mapambano makali walipotaka kumkamata Osama, akisema kwamba hakuna hata risasi moja iliyofyatuliwa kwa askari wa Marekani wala kwa helikopta zao.

"Helikopta yao ilipata matatizo ya kiufundi na kuanguka, kisha mabaki yake kuachwa katika eneo la tukio," alisema.Taarifa zilieleza pia kwamba ndugu wa Bin Laden walionusurika wakiwamo watoto wake sita na mmoja wa wake zake, walipelekwa kwenye hospitali ya mjini Rawalpindi.


Bush amtosa Obama sherehe za mauaji ya Osama Bin Laden

Katika hatua nyingine, Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush amesusia mwaliko wa Rais Barak Obama kwenda katika Viwanja vya Ground Zero, jijini New York kusherehekea mauaji ya Osama bin Laden, msemaji wa rais huyo wa zamani wa Marekani, David Sherzer alisema.

“Rais Bush hatahudhuria mwaliko wa Alhamisi (leo), ameheshimu wito, lakini amechagua kutokuhudhuria shughuli hiyo ili aendelee kufaidi matunda ya ustaafu wake. Ataendelea kusherehekea na Wamarekani wenzake ushindi huo muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi,” Sherzer.

Ikulu ya Marekani bado haijathibitisha kama ilitoa mwaliko kwa Bush au hata kuzungumzia uamuzi alioufanya Rais huyo mstaafu.Wiki hii Rais Obama alizungumzia matumaini yake kuwa mapambano dhidi ya ugaidi yaliyofanyika katika viwanja alivyokuwa akiishi Bin Laden yanaweza kuwa sababu kubwa ya kuliunganisha taifa hilo lililokuwa linakabiliwa na matatizo kadhaa yakiwamo migogoro ya kifedha.

Wafuasi wengi wa chama cha Republican wamefurahia operesheni hiyo iliyofanywa chini ya utawala wa Obama wa Democrat.

Tangu kuondoka kwake kwenye Ikulu ya Marekani, Bush amekuwa haonekani katika hadhara za watu na pia amekuwa akiepuka kutoa maoni dhidi ya Obama ingawa mwaka jana alijitokeza hadharani akiwa na Rais mwingine mstaafu wa nchi hiyo, Bill Clinton na kusafiri pamoja hadi Haiti baada ya kutokea tetemeko la ardhi wakiwa wajumbe mahsusi wa Obama.

Wakati akiwa madarakani Bush aliutumia muda wake mwingi kumwinda Bin Laden. Siku chache baada ya Septemba 11, alijitokeza hadharani akiwa amesimama juu ya masalia ya majengo yaliyoharibiwa na Bin Laden na kuzungumza na wafanyakazi wa kikosi cha uokoaji.

Jumatatu iliyopita, Ofisa mmoja wa Ikulu ya Marekani alisema kuwa Rais Obama angetembelea eneo maarufu la Lower Manhattan leo ili ambako ndiko kilipokuwa Kituo cha Biashara cha Kimataifa (WTO) kilichoteketezwa na kubakia shimo kubwa maarufu kama Ground Zero ili kukutana na familia zilizopoteza ndugu zao katika tukio la mashambulizi ya Septemba 11, 2001 lililoandaliwa na Bin Laden.

Makazi ya Osama
Majirani katika eneo ambalo Bin Laden alikuwa akiishi, hawakuwahi kubaini kuwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba ndiye aliyekuwa akiendesha maisha yake katika makazi hayo.

"Nimekuwa nikienda kwenye nyumba yao. Alikuwa na wake wawili, mmoja alikuwa akiongea Kiarabu na mwingine alikuwa akiongea Kiurdu. Walikuwa na watoto watatu, msichana mmoja na wavulana wawili. Walinipa sungura wawili. Waliweka kamera kwenye geti la mbele ili waweze kumuona yeyote kabla hajaingia ndani ya nyumba yao," alisema Zarar Ahmed.

Ilibainika jana kwamba watoto wengine wa eneo hilo walianza kunufaika na mara nyingi walifaidika na uwepo wa kiongozi huyo wa kundi la kigaidi kwenye eneo hilo bila ya kujua... "Iwapo mpira ukianguka ndani ya ukuta wa makazi ya Bin Laden watoto waliokuwa wakiuchezea hawakuruhusiwa kuuchukua tena," muuzaji wa ‘ice cream’ wa eneo hilo, Tanvir Ahmed alisema: "Walikuwa wakipewa fedha badala yake; kati ya rupia100-150 (dola mbilui mpaka tatu) kwa kila mpira."

Kijana mwingine, Daniel Alvi alisema mara nyingi alikuwa akimwona mtu akiingia na gari nyekundu aina ya Suzuki akiwa na mbuzi, huku mtu mwingine aliyekuwa akipeleka maziwa akiishia getini na kupokewa wakati huohuo kabla hata hajapiga kengele.

Kwa mujibu wa wenyeji, magari hayo yalikuwa yakiendelea kusafiri kuelekea katika maeneo ya makabila ambayo wakufunzi wa al-Qaeda walikuwa wakifanya kazi zao.

"Kulikuwa na tetesi kwa majirani kwamba mtu aliyekuwa akiishi pale ni ndugu wa Baitullah Mehsud, alisema Daniel akimaanisha aliyekuwa Mkuu wa Kundi la Taliban, Pakistani ambaye kwa sasa ni marehemu.

"Niliwahi kwenda pale mara mbili nilipopiga mpira ukadondoka ndani ya ukuta lakini sikukuta mtu. Ninakumbuka kulikuwa na zawadi ya dola20 milioni kwa yeyote atakayemwona na kutoa taarifa, lakini sikuwahi kudhani kuwa ni yeye."

Vijana wawili kutoka katika makazi hayo walikuwa wakienda dukani mara mbili kwa wiki kwa ajili ya kununua mahitaji mbalimbali. Ununuzi wao mara nyingi ulihusisha mbogamboga, matunda, mchele, biskuti, jam, asali na ice cream kwa ajili ya watoto.

Muuza duka, Raja Shuja alisema vijana hao walikuwa werevu na muda wote walikuwa wakiuliza maswali kuhusu nini kinachoendelea katika maeneo hayo, pia iwapo kuna mtu mgeni aliyefika kwenye maeneo hayo.

Mmoja wa wauza magazeti alieleza namna alivyofikisha magazeti kwenye makazi hayo kila siku na kila mwisho wa mwezi alilipwa fedha zake kwa usahihi, mara zote akizipokea kwa mtu mmoja.

Makazi hayo ambayo yamepewa namba 25 kwenye mtaa huo hayakuwa na vifaa kama dishi la satelaiti, simu wala viyoyozi.Kwa mujibu wa mwandishi wa CNN, mimea ya bangi imekutwa katika maeneo yanayozunguka makazi yake, suala linaloibua maswali mengi.

Mwandishi huyo, Nic Robertson alisema mimea hiyo imezunguka kama maua ndani ya ukuta mkubwa unaozunguka makazi hayo, pia katika bustani za mbogamboga.Mwandishi huyo alieleza kuhuhudia kwa macho yake mmea huo ukiwa umetapakaa katika maeneo mengi yanayozunguka makazi hayo.

Japokuwa anaeleza kwamba huenda kuna baadhi ya watu walioupanda katika eneo lake, hata askari wa jeshi la Pakistani wamekuwa wakipita katika eneo hilo bila kujali.Katika miaka ya hivi karibuni, Bin Laden aliripotiwa kuwa na matatizo ya figo ambayo ilielezwa kwamba muda mwingine mmea huo hutumika kama kitulizo cha maumivu.

Check red:
Ninavyowapenda wamarekani ni kwamba vifaa vyao vya kijeshi ni bora sana ila tatizo vikifika uwanja wa vita tu ndio hupata hitilafu na kuanguka, sijui tatizo hili litaisha lini???????????????
 
naungana na wewe lakini dubwana kama Osama sio la kuliamini inaweza likawa lilikuwa limejifunga mabomu muda wote....sasa hofu ndo hapo kwamba ukichelewa dakika moja tu hatari kwake hatari kwenu....

Haaaa haaaa aiseeeee umenivunja mbaaafuuuu! Kweli dubwana Usama sio la kuliamini kabisa!
 
haki ipi sasa?kwasababu bongo waliokufa wengi pale ubalozi walikua waislam!!mie mnaposema haki hata siwaelewi na mashambulio mengi wanayofanya hawa jamaa hayaangalii kwamba huyu mkristo au muislam!


Hata mimi huwa sielewi ni haki gani hiyo inayopiganiwa.
 
wasiwasi wako ni wangu pia,naona kama kuna fumbo flani hivi!najiuliza maswali mengi sana aisee
Mtu chake nahisi kuna zaidi ya hilo, let's wait and see
Msitake kulazimisha kitu ambacho hakipo, ebo mbona Mkapa hatokei popote anapoalikuwa na JK na hatuulizi? Bush kama Republican hataki kumpa ujiko Obama (democrat) especially kwenye kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi, Alishatoa press release na kutoa pongezi hiyo inatosha vile vile tangu ameondoka madarakani amekuwa haonekani sana hadharani.
 
Hata mimi huwa sielewi ni haki gani hiyo inayopiganiwa.
Utawaweza hawa, utasikia haki zake za kibinadamu zilivunjwa, sijui hawakuruhusu sheria ifuate mkondo.. Hivi watu wote waliofariki kwa sababu ya mabomu ya Al Qaeda walipewa vyote hivyo?
 
Check red:
Ninavyowapenda wamarekani ni kwamba vifaa vyao vya kijeshi ni bora sana ila tatizo vikifika uwanja wa vita tu ndio hupata hitilafu na kuanguka, sijui tatizo hili litaisha lini???????????????

Ni heri ya vifaa vya kimarekani kuliko mafeki ya wachina!!!
 
Hivi Bill Clinton alialikwa? Manake ugomvi na Osama ulianza kwenye utawala wake na balozi pamoja na USS Cole zililipuliwa yeye ndo akiwa raisi. Hata lile jaribio la '93 Clinton ndo alikuwa raisi. Sasa kwa nini watu wanamkomalia Bush?
 
Hivi Bill Clinton alialikwa? Manake ugomvi na Osama ulianza kwenye utawala wake na balozi pamoja na USS Cole zililipuliwa yeye ndo akiwa raisi. Hata lile jaribio la '93 Clinton ndo alikuwa raisi. Sasa kwa nini watu wanamkomalia Bush?
Sidhani kama Clinton alialikwa, hii ni non issue basi tu watu wanataka kuingiza siasa. Obama alitaka kupull move ya Reagan alipompa Carter ndege kwenda kuchukua mateka wakimarekani na kurudi nao nyumbani.
 
Osama: Umetuletea balaa na tafran kubwa huku ughaibuni. Kabla ya Sept 11 kila kitu kilikuwa shwaaaaaariiiiiiiii. Umeleta balaa za deportations, E-verify, kero za airport, FBI misikitini, sheria mpya za makaratasi kule INS kila kukicha etc.
Familia zimetenganishwa, marafiki wamekuwa deported etc. Mungu akuchome moto mara trillion moja. Ukawe kuni zetu kwenye moto wa kiama.
ROT AND ROT IN HELL, B-ASTARD USAMA!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom