Osama bin Laden killed!

Osama bin Laden killed!

Status
Not open for further replies.
Hizi helicopter zimetengenezwa specifically kwa ajili ya hii mission? Maana nimesoma sehemu wanasema zinaonekana zina stealth capabilities.

Babu inaelekea unaamini kwa ujumla mno habari za Wamarekani. Hawa watu wakitoa habari lazima wataipa spin inayoegemea upande wao. Wanatuambia hizo helikopta zilikuwa na stealth capability lakini hatuulizi maswali kama zinawezaje kuwa 500 yards kutoka chuo cha kijeshi cha Pakistan bila hata kujulikana au kuonekana. Kwani hazipigi makelele? Au hata kwa macho hazionekani? Maana helikopta huwaga hazipai juu kihivyo. Yaani Pakistan walioweza kutengeneza mabomu ya nyuklia washindwe kujua kuna mahelikopta ya Wamarekani ujirani na chuo cha kijeshi? Hahahaaaaa kama ni kweli basi India itakuwa inachekelea tu sasa hivi.
 
Hizi helicopter zimetengenezwa specifically kwa ajili ya hii mission? Maana nimesoma sehemu wanasema zinaonekana zina stealth capabilities.

"Stealth Capabilities" or not, that helicopter most likely went down because it got hit by some roof-fired Al Qaeda RPG. That being said, these Navy SEAL commandos weren't that perfectly trained, invincible, All-American heroes as the US now purports them to be. Surely the handful-or-so Al Qaeda dudes in that doomed OBL hideout were way overpowered given the 79 or so well-prepared and heavily-armed US commandos. However, man-to-man (or pound-for-pound if you will): Al Qaeda probably won 7.9 against the US's 1.
 
Babu inaelekea unaamini kwa ujumla mno habari za Wamarekani. Hawa watu wakitoa habari lazima wataipa spin inayoegemea upande wao. Wanatuambia hizo helikopta zilikuwa na stealth capability lakini hatuulizi maswali kama zinawezaje kuwa 500 yards kutoka chuo cha kijeshi cha Pakistan bila hata kujulikana au kuonekana. Kwani hazipigi makelele? Au hata kwa macho hazionekani? Maana helikopta huwaga hazipai juu kihivyo. Yaani Pakistan walioweza kutengeneza mabomu ya nyuklia washindwe kujua kuna mahelikopta ya Wamarekani ujirani na chuo cha kijeshi? Hahahaaaaa kama ni kweli basi India itakuwa inachekelea tu sasa hivi.
Sijasema naamini, nimeuliza swali. After all Pakistan wanaweza kuwa na Nuclear lakini kwenye defence capabilities ni weupe ukilinganisha na India, heck kila siku wanalalamika Drone za USAF zinaingia kwenye anga yao na kulipua terrorists. Kuna scenario nyingine ambayo sintoshangaa Pakistan wakiitumia "walijua wanajeshi wako kwenye mazoezi ya kijeshi".
 
Mimi bado sijashawishika kuwa Wapakistan hawaku detect mahelikopta ya Marekani kuingia kwenye anga yake hususan ukizingatia kuwa hiyo nyumba waliyoenda kuivamia iko takribani yards 500 kutoka kwenye chuo chao cha kijeshi.

Na sijashawishika kabisa kuwa intelijentsia ya Pakistan haikujua kuwa Osama anaishi hapo karibu na hicho chuo chao cha kijeshi.

Kuna mengi sana hayaingii akilini kuhusiana na hili tukio.
Wakati Osama akipambana na Warusi,wamarekani ndiyo walikuwa wakiwapa kina Osama Silaha lakini kwa kupitia Pakistani Intelligence.Anzia hapo...
 
Wakati Osama akipambana na Warusi,wamarekani ndiyo walikuwa wakiwapa kina Osama Silaha lakini kwa kupitia Pakistani Intelligence.Anzia hapo...

The whole thing is full of convolution and confusion. I'm starting to get tired of it.
 
Obama hasipokuwa makini hii issue itakuja kum-cost kwenye uchaguzi.

Prof. wewe uko wapi kwani? Watu tunaumia sana kwenye gas pumps na kama hizo bei zisiposhuka chini ya dola 3 basi hicho ndo kitakachomgharimu.

Sasa hivi atapata bump kwenye polls kama ilivyo kawaida halafu hali itatulia na kurudia kawaida. Mwisho wa siku Wamarekani wataangalia mifukoni mwao na kufanya uamuzi.
 
Prof. wewe uko wapi kwani? Watu tunaumia sana kwenye gas pumps na kama hizo bei zisiposhuka chini ya dola 3 basi hicho ndo kitakachomgharimu.

Sasa hivi atapata bump kwenye polls kama ilivyo kawaida halafu hali itatulia na kurudia kawaida. Mwisho wa siku Wamarekani wataangalia mifukoni mwao na kufana uamuzi.
Kilichopandisha bei ya mafuta si kwenda kumvamia Ghadafi?

Kila siku mnakumbushwa nyie mnalalamika dollar 4 wakati uk wenzenu wanalipa dollar 8 lol.

Kifo cha Osama kimepandisha polls zake lakini hili swala linavyokwenda sasa zinaweza kushuka na ndio atakapo amua kuzionesha hizo picha za Osama sasa lol.
 
The whole thing is full of convolution and confusion. I'm starting to get tired of it.
I know, but it will eventually be beneficial to Obama. After getting tired with the news that lingers around, clouded with conspiracies and innuendos, most republicans will get irritated and they will lose,provided that they attack him on the issue that made him somewhat a hero and one of historical US presidents. It's more likely that most people will believe the president whether he releases a photo or not.All in all i do like their moves.Well calculated and smart ones
 
AND LEST YOU FORGET ONE MORE IMPORTANT FACT: It's very rare that a whole freakin' helicopter would just crash down to earth with virtually zero casualties. But, again, since its mostly only the CIA and White House who have a hold on whatever heavily biased "truth" that gets served to the media: there's really no way of telling whether there were any American casualties in that mission. In other words: ITS ALL ONE SIDED FELLAS!! 79 or more Navy SEAL commandos against 10 or 12 Qaeda dudes...that about sums it all!!
 

By MICHELLE TRAVIERSO – Wed May 4, 5:40 pm ET
A picture of the tail rotor of the chopper that the Navy Seals' Team Six detonated revealed unfamiliar features. Reports say it could be a new, secret helicopter.
When the Team Six members reached Osama bin Laden's compound in Abbottabad one of the choppers made a "controlled but hard landing," according to reports, probably due to higher than expected temperatures.
Temperatures affects the density of the air, and low density makes it harder for the rotor to sustain the weight of the chopper, especially if it was near its maximum weight (being packed with soldiers and fuel to fly in from Afghanistan). Abbottabad is about 1200 meters above the sea level, and altitude also affects air density. (Inside the Osama bin Laden Strike: How America Got Its Man.)
So what machine exactly experienced the hard landing described above? Short answer: we don't know for sure. Long answer: It seems that the tail rotor visible in the picture belongs to a highly modified version of the H-60, the chopper of choice of the special forces for more than 30 years. Aviation Week doesn't beat around the bush, claiming: "A previously undisclosed, classified stealth helicopter apparently was part of the U.S. task force that killed Osama bin Laden in Pakistan on May 1."
Stealth technology on helicopters is not itself new, but the fact that a previously unknown machine was used in this raid is yet another proof of the degree of importance that this mission had for U.S. commanders. (Watch President Obama's announcement of Osama bin Laden's death.)
Aviation Week then goes techie and explains what we can see from that picture: "Photos disseminated via the European PressPhoto agency and attributed to an anonymous stringer show that the helicopter’s tail features stealth-configured shapes on the boom and the tail rotor hub fairings, swept stabilizers and a 'dishpan' cover over a five-or-six-blade tail rotor. It has a silver-loaded infrared suppression finish similar to that seen on V-22s."
Low radar visibility was essential, for the Pakistani air force would have either scrambled its jets if an unknown threat to its airspace (and near the country's best military academy!) was detected, or fired its surface to air missiles. It's possibly more proof of the fact that Pakistan really knew nothing about the mission - or at least its first wave of attack - until it ended. (See pictures of Osama bin Laden.)
This would explain why the Seals wasted critically precious time to blew up the mysterious helicopter and why many experts had problems identifying its remains. It's unclear what Pakistan could have made of the downed chopper, but growing ties between Pakistani and Chinese armed forces could have made the destruction of such new machine a must. China and Pakistan, over the past two decades, have developed a multi role combat aircraft called JF-17 and an advanced trainer, the JL-8.
The Navy Seals usually fly in the famed Sikorsky UH-60, popularized by the movie Black Hawk Down, in which two UH-60 were shot down in Somalia, resulting in the death of 18 men.
Black Hawk Down was a scenario, insiders say, that together with first attempt to rescue the hostages held at the U.S. embassy in 1980 in Iran, that's been evoked constantly in the planning phases leading to the May 1 raid, as examples of potentially disastrous outcomes. (Via Aviation Week)
See continuing coverage of Osama's death.
See TIME's al-Qaeda covers.
View this article on Time.com
Most Popular on Time.com:

Source: Could the bin Laden Raid Have Revealed a Secret New Helicopter? - Yahoo! News
 
AND LEST YOU FORGET ONE MORE IMPORTANT FACT: It's very rare that a whole freakin' helicopter would just crash down to earth with virtually zero casualties. But, again, since its mostly only the CIA and White House who have a hold on whatever heavily biased "truth" that gets served to the media: there's really no way of telling whether there were any American casualties in that mission. In other words: ITS
ALL ONE SIDED FELLAS!! 79 or more Navy SEAL commandos against 10 or 12 Qaeda dudes...that about sums it all!!
The truth will come out soon.
 
AND LEST YOU FORGET ONE MORE IMPORTANT FACT: It's very rare that a whole freakin' helicopter would just crash down to earth with virtually zero casualties. But, again, since its mostly only the CIA and White House who have a hold on whatever heavily biased "truth" that gets served to the media: there's really no way of telling whether there were
any American casualties in that mission. In other words: ITS
ALL ONE SIDED FELLAS!! 79 or more Navy SEAL
commandos against 10 or 12 Qaeda dudes...that about
sums it all!!
Mkuu helicopter gani hiyo inachukua 79 people? Chinook inachukua 35 na from the look of the wreckage hiyo sio chinook, imekaa kama Sikorsky (14-16 people). Kuhusu casualities tutajua tuu unless hao seals wote wasiwe na immediate family members au marafiki.
 
NN hii kitu hivi sasa inaanza kutia mashaka sana. Maana tangu habari hii itangazwe rasmi kumekuwa na kubadilika badilika kwa habari hii kila siku iendayo kwa Mungu. Mara baadhi ya masenators wamesema wameziona picha leo wanaulizwa authenticity ya hizo picha wanaingia mitini wengine wanadai picha walizoziona zilikuwa fake, mara aliuawa ghorofa ya pili mara ya tatu, mara jamaa alikuwa na bunduki mara alikuwa hana bunduki ali mradi utata umekuwa mwingi mno kuweza kuamini ukweli wa habari hii. Nikikumbuka ile hotuba ya kutoa ushahidi pale umoja wa mataifa kwamba kulikuwa na silaha za maangamizi na wanajua pale zilipo na hatimaye kuivamia nchi ile na kufanya uharibifu mkubwa sana halafu ikaja kuthibitishwa kumbe ulikuwa ni uwongo mtupu, hii habari nayo inaanza kukosa mshiko kama ina ukweli wowote.
 
The truth will come out soon.

The fact that OBL may be dead is one thing, but there seems to be a deliberate effort from the CIA and White House to offer conflicting, and constantly changing versions of what really happened, that unfortunately, leaves a lot to be desired. The "truth" may already be out there: namely that OBL is probably dead. But why all the biased, hyped, and contradicting information that we keep getting served from CIA and White House controlled media on a daily basis (and if only just a couple of days so far since the event supposedly took place?) I think there's a whole lot more that we'll never find out about as far as what really went down that night other than "OBL got his ass killed."
 
Kinachotokea sasa hivi ni kuwa wale wanajeshi wanafanyiwa debriefing mpaka mwisho wa wiki tutakuwa tumesikia story tofauti tofauti sana. Nadhani wangesubiri mpaka debriefing iishe ndio watoe story kamili.

Alafu hizi picha zimekuwa cropped out hazionyeshi mikono au mwili mzima.

Hawa watu walituwekea picha wakati ambao walikuwa wanaitazama operation in "real time".
debriefing?...tusubiri....huenda wanatengeneza evidence!
 
Hawa watu walituwekea picha wakati ambao walikuwa wanaitazama operation in "real time".
debriefing?...tusubiri....huenda wanatengeneza evidence!
Yes, debriefing sijui kwa kiswahili maana yake ni nini, Kuhoji nadhani.

Debrief
1. to interrogate (a soldier, astronaut, diplomat, etc.) on return from a mission in order to assess the conduct and results of the mission.
2. to question formally and systematically in order to obtain useful intelligence or information: Political and economic experts routinely debrief important defectors about conditions in their home country.
3. to subject to prohibitions against revealing or discussing classified information, as upon separation from a position of military or political sensitivity
Debriefing | Define Debriefing at Dictionary.com

221886_10150164271151747_53081341746_7016009_7930350_n.jpg
 
BINTI wa Osama Bin Laden ameeleza kwamba baba yake alikamatwa akiwa hai katika makazi yake huko Pakistani, kisha kuuawa kwa kupigwa risasi na makomandoo wa Marekani.Mtandao wa habari wa Uarabuni, Al-Arabiya ulimnukuu mmoja wa maofisa wa usalama wa Pakistani akieleza kwamba binti huyo mwenye umri wa miaka 12, alishuhudia tukio hilo na huku akieleza kwamba baada ya mauaji, mwili wake ulichukuliwa na kupakizwa katika helikopta.

Kwa mujibu wa maelezo ya binti huyo, makomandoo hao wa Kikosi Maalumu cha SEAL hawakupata msukosuko wowote baada ya kuingia na kumasa Osama.

Kwa mujibu wa Shirika la Fox News, taarifa hizo mpya zilizopatikana kwa binti huyo zinaeleza kwamba Bin Laden alikuwa na fedha na namba za simu kwenye nguo zake, wakati alipofikwa na mauti.

Iwapo taarifa hizo zitakuwa za kweli, hiyo ni dalili kwamba kiongozi huyo wa al-Qaeda alikuwa mbioni kuondoka katika makazi hayo iwapo kungetokea uvamizi.Ofisa mmoja wa Pakistani alikanusha taarifa zilizotolewa awali na Marekani kwamba kulikuwa na mapambano makali walipotaka kumkamata Osama, akisema kwamba hakuna hata risasi moja iliyofyatuliwa kwa askari wa Marekani wala kwa helikopta zao.

"Helikopta yao ilipata matatizo ya kiufundi na kuanguka, kisha mabaki yake kuachwa katika eneo la tukio," alisema.Taarifa zilieleza pia kwamba ndugu wa Bin Laden walionusurika wakiwamo watoto wake sita na mmoja wa wake zake, walipelekwa kwenye hospitali ya mjini Rawalpindi.


Bush amtosa Obama sherehe za mauaji ya Osama Bin Laden

Katika hatua nyingine, Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush amesusia mwaliko wa Rais Barak Obama kwenda katika Viwanja vya Ground Zero, jijini New York kusherehekea mauaji ya Osama bin Laden, msemaji wa rais huyo wa zamani wa Marekani, David Sherzer alisema.

“Rais Bush hatahudhuria mwaliko wa Alhamisi (leo), ameheshimu wito, lakini amechagua kutokuhudhuria shughuli hiyo ili aendelee kufaidi matunda ya ustaafu wake. Ataendelea kusherehekea na Wamarekani wenzake ushindi huo muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi,” Sherzer.

Ikulu ya Marekani bado haijathibitisha kama ilitoa mwaliko kwa Bush au hata kuzungumzia uamuzi alioufanya Rais huyo mstaafu.Wiki hii Rais Obama alizungumzia matumaini yake kuwa mapambano dhidi ya ugaidi yaliyofanyika katika viwanja alivyokuwa akiishi Bin Laden yanaweza kuwa sababu kubwa ya kuliunganisha taifa hilo lililokuwa linakabiliwa na matatizo kadhaa yakiwamo migogoro ya kifedha.

Wafuasi wengi wa chama cha Republican wamefurahia operesheni hiyo iliyofanywa chini ya utawala wa Obama wa Democrat.

Tangu kuondoka kwake kwenye Ikulu ya Marekani, Bush amekuwa haonekani katika hadhara za watu na pia amekuwa akiepuka kutoa maoni dhidi ya Obama ingawa mwaka jana alijitokeza hadharani akiwa na Rais mwingine mstaafu wa nchi hiyo, Bill Clinton na kusafiri pamoja hadi Haiti baada ya kutokea tetemeko la ardhi wakiwa wajumbe mahsusi wa Obama.

Wakati akiwa madarakani Bush aliutumia muda wake mwingi kumwinda Bin Laden. Siku chache baada ya Septemba 11, alijitokeza hadharani akiwa amesimama juu ya masalia ya majengo yaliyoharibiwa na Bin Laden na kuzungumza na wafanyakazi wa kikosi cha uokoaji.

Jumatatu iliyopita, Ofisa mmoja wa Ikulu ya Marekani alisema kuwa Rais Obama angetembelea eneo maarufu la Lower Manhattan leo ili ambako ndiko kilipokuwa Kituo cha Biashara cha Kimataifa (WTO) kilichoteketezwa na kubakia shimo kubwa maarufu kama Ground Zero ili kukutana na familia zilizopoteza ndugu zao katika tukio la mashambulizi ya Septemba 11, 2001 lililoandaliwa na Bin Laden.

Makazi ya Osama
Majirani katika eneo ambalo Bin Laden alikuwa akiishi, hawakuwahi kubaini kuwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba ndiye aliyekuwa akiendesha maisha yake katika makazi hayo.

"Nimekuwa nikienda kwenye nyumba yao. Alikuwa na wake wawili, mmoja alikuwa akiongea Kiarabu na mwingine alikuwa akiongea Kiurdu. Walikuwa na watoto watatu, msichana mmoja na wavulana wawili. Walinipa sungura wawili. Waliweka kamera kwenye geti la mbele ili waweze kumuona yeyote kabla hajaingia ndani ya nyumba yao," alisema Zarar Ahmed.

Ilibainika jana kwamba watoto wengine wa eneo hilo walianza kunufaika na mara nyingi walifaidika na uwepo wa kiongozi huyo wa kundi la kigaidi kwenye eneo hilo bila ya kujua... "Iwapo mpira ukianguka ndani ya ukuta wa makazi ya Bin Laden watoto waliokuwa wakiuchezea hawakuruhusiwa kuuchukua tena," muuzaji wa ‘ice cream’ wa eneo hilo, Tanvir Ahmed alisema: "Walikuwa wakipewa fedha badala yake; kati ya rupia100-150 (dola mbilui mpaka tatu) kwa kila mpira."

Kijana mwingine, Daniel Alvi alisema mara nyingi alikuwa akimwona mtu akiingia na gari nyekundu aina ya Suzuki akiwa na mbuzi, huku mtu mwingine aliyekuwa akipeleka maziwa akiishia getini na kupokewa wakati huohuo kabla hata hajapiga kengele.

Kwa mujibu wa wenyeji, magari hayo yalikuwa yakiendelea kusafiri kuelekea katika maeneo ya makabila ambayo wakufunzi wa al-Qaeda walikuwa wakifanya kazi zao.

"Kulikuwa na tetesi kwa majirani kwamba mtu aliyekuwa akiishi pale ni ndugu wa Baitullah Mehsud, alisema Daniel akimaanisha aliyekuwa Mkuu wa Kundi la Taliban, Pakistani ambaye kwa sasa ni marehemu.

"Niliwahi kwenda pale mara mbili nilipopiga mpira ukadondoka ndani ya ukuta lakini sikukuta mtu. Ninakumbuka kulikuwa na zawadi ya dola20 milioni kwa yeyote atakayemwona na kutoa taarifa, lakini sikuwahi kudhani kuwa ni yeye."

Vijana wawili kutoka katika makazi hayo walikuwa wakienda dukani mara mbili kwa wiki kwa ajili ya kununua mahitaji mbalimbali. Ununuzi wao mara nyingi ulihusisha mbogamboga, matunda, mchele, biskuti, jam, asali na ice cream kwa ajili ya watoto.

Muuza duka, Raja Shuja alisema vijana hao walikuwa werevu na muda wote walikuwa wakiuliza maswali kuhusu nini kinachoendelea katika maeneo hayo, pia iwapo kuna mtu mgeni aliyefika kwenye maeneo hayo.

Mmoja wa wauza magazeti alieleza namna alivyofikisha magazeti kwenye makazi hayo kila siku na kila mwisho wa mwezi alilipwa fedha zake kwa usahihi, mara zote akizipokea kwa mtu mmoja.

Makazi hayo ambayo yamepewa namba 25 kwenye mtaa huo hayakuwa na vifaa kama dishi la satelaiti, simu wala viyoyozi.Kwa mujibu wa mwandishi wa CNN, mimea ya bangi imekutwa katika maeneo yanayozunguka makazi yake, suala linaloibua maswali mengi.

Mwandishi huyo, Nic Robertson alisema mimea hiyo imezunguka kama maua ndani ya ukuta mkubwa unaozunguka makazi hayo, pia katika bustani za mbogamboga.Mwandishi huyo alieleza kuhuhudia kwa macho yake mmea huo ukiwa umetapakaa katika maeneo mengi yanayozunguka makazi hayo.

Japokuwa anaeleza kwamba huenda kuna baadhi ya watu walioupanda katika eneo lake, hata askari wa jeshi la Pakistani wamekuwa wakipita katika eneo hilo bila kujali.Katika miaka ya hivi karibuni, Bin Laden aliripotiwa kuwa na matatizo ya figo ambayo ilielezwa kwamba muda mwingine mmea huo hutumika kama kitulizo cha maumivu.
 
SERIKALI ya Marekani imesema inasita kuonyesha hadharani, picha ya mwili wa Kiongozi wa Mtandao wa Ugaidi wa Al Qaeda, Osama bin Laden, kwa kuwa uliharibika vibaya katika mashambulizi yaliyofanywa na makomandoo waliomuua.

Kwa mujibu wa Mtandao wa The Dailymail wa Uingereza, taarifa hiyo ya Serikali ya Marekani, imekuja wakati makundi mbalimbali ya kigaidi, likiwamo la Taliban, yakidai uthibitisho kuhusu kuuawa kwa Osama, ambaye amekuwa akisakwa kwa cha zaidi ya miaka kumi.

Rais Barrack Obama wa Marekani, alisema serikali yake, inasita kuonyesha hadharani picha ya mwili wa Osama kwa sababu ulikuwa umeharibika vibaya kwa majeraha na kwamba hatua hiyo, imemkosesha Osama heshima na ni kinyume cha maadili ya Kiislamu na kwamba hiyo inaweza kuamsha hasira miongoni mwa waumini wa madhehebu ya dini hiyo.

Habari zilisema kukosekana kwa uthibitisho wa picha kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kuhusu kifo cha Osama, kunawafanya wengine waendelee kutoamini kama kweli ameuawa kama inavyodaiwa na Marekani.

Habari zaidi zilisema juzi asubuhi, Rais Obama aliitisha kikao cha Baraza lake la mawaziri na baadaye ilidokwezwa kuwa huenda ataruhusu picha zinazoonyesha operesheni hadi kifo cha Osama, zionyeshwe hadharani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), Leon Panetta, alisema serikali ya nchi hiyo, ilikuwa ikitafuta namna bora ya kuonyesha hadharani picha za Osama.

"Serikali ilikuwa ikitafuta namna bora ya kuonyesha picha hizo, lakini nadhani hakuna swali kwani picha zitaonyeshwa mbele ya jamii," alisema Panetta.

Alisema "nimeona picha hizo hapana shaka. Tumezichunguza na hakuna shaka kuwa aliyeuawa ndiye Osama Bin Laden . Nafikiri hakuna swali wala mjadala kuhusu matokeo ya kuonyeshwa kwa picha hizo, ukweli unabaki kwamba tumempata Osama na tumeionyesha dunia kuwa tumeweza kumpata na kumuua."

Mapema, Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jay Carney, alithibitisha kuwapo kwa picha za Osama na jinsi alivyouawa, lakini alisema zinaweza kuzusha hasira miongoni mwa baaadhi ya watu.

Baadhi ya vikundi vya kiislamu vimeendelea kutishia kuwashambulia raia wa Marekani kama njia ya kulipiza kisasi baada ya serikali ya nchi hiyo, 'kuutupa' baharini, mwili wa Osama, jambo linalopingana na matakwa ya dini Kiislamu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom