kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
UMOJA wa Taifa (UN), umeitaka Marekani kueleza sababu za kumuua Kiongozi wa Kundi la Al-Qaeda, Osama bin Laden, badala ya kushughulikia suala lake kwa kufuata taratibu za kisheria.Inaelezwa kuwa wakati anavamiwa na kuuawa na makomandoo wa Marekani, katika kasri lake nchini Pakistan, bin Laden, hakuwa na silaha.
Kiongozi huyo wa mtandao wa kigaidi, aliuawa Jumatatu wiki hii.Taarifa ya Ikulu ya Marekani, jijini Washiton, ilisema mashushushu wa Marekani, walilazimika kumuua bin Laden kufuatia kitendo chake cha kukataa kukamatwa.
Hata hivyo Ofisa Mkuu wa Umoja wa Mataifa (Haki za Binadamu), Navi Pillay, alisema ingawa bin Laden alikuwa ni mtu hatari, lakini operesheni ya kukamatwa kwake, ilistahili kufuata taratibu za kisheria.
Wito huo unakuja wakati tayari Rais Barrack Obama wa Marekani, akiwa amesema "hatuwezi kumpa fursa bin Laden au mshirika wake, kulinyoshea silaha jeshi letu."
Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, hakukuwa na komandoo yeyote wa Marekani aliyejeruhiwa katika operesheni hiyo ingawa, kulikuwa na mashaka makubwa wakati helikopta moja ilipopata hitilafu ya kiufundi na kuharibiwa na makondoo wa Osama.
Leon Panetta, Mkurugenzi wa CIA, aliliambia Shirika la Habari la NBC kuwa kikosi hicho kilipewa amri ya kumuua Osama."Lakini hii pia ilitegemea mazingira ya operesheni yenyewe. Kama angenyoosha mikono juu (Osama) na kujisalimisha kwa kikosi hicho, kwa vyovyote vile asingeuawa," alisema.
Bin Laden, (54) alikuwa mwanzilishi na Kundi la al-Qaeda na inaaminika kuwa aliamuru mashambulizi yaliyotokea katika majiji ya New York na Washington 11 Septemba 2001.Hali kadhalika mashambulizi mengine yaliyouawa watu katika nchi mbalimbali duniani.