Birth certificate ya Obama unaweza ukachelewesha kutoa na isiwe tabu lakini death certificate ya Osama ikichelewa kutoka haitofaa tena.
Obama anasema hatotoa picha za maiti ya sheikh Osama.Si kwamba ana huruma na heshima bali hana!.Vyenginevyo mafundi wa kutenngenezo hizo picha hawajaimudu kazi.Wengine wametoa ikionesha maiti imevimba kama vile alikufa juzi,hii haikubaliki.Mwengine katoa eti Osama kavaa kilemba na ile sare ya jeshi,hilo haliwezekani kwani ilikuwa ni wakati wa kulala walipovamia.
Mungu(Allah) yuko karibu sana nao ili kuwafedhehesha na uwe mwisho wao.Kila wanachokifanya tangu watangaze hicho kifo kimejaa utata mtupu.
1.Osama hawezi kuishi kwenye kambi ya jeshi,angehiyari kule kule mapangoni.
2.Kama kweli ile nyumba alijenga yeye basi asingechagua kuijenga sehemu ya wazi namna ile.Nyumba yake ingekuwa imejigandamiza na mlima na kuwa na handaki ambalo pindi akisikia vishindo angepotelea huko.
3.Iwapo alilazimishwa kukaa pale na ISI kwa amri za US bila Osama kujua,basi asingechagua kuishi na mke wake ghorofa ya pili kama vile mtalii.
4.Panetta katika kuchanganyikiwa na hisia za walimwengu kuhusu ukweli wa tukio la kifo cha Osama anasema habari ya namna gani wangefanya na picha za maiti ya Osama walishajadiliana tangu mwaka jana.Hebu fikiria itakuwaje wajadili jinsi ya kufanya na picha za maiti badala kujadili uwezekano wa kuipata hiyo maiti kwanza.
Hii ni kuonesha walianza kuhangaika zamani kutengeneza mchezo.
5.Majirani wa lile jumba wanasema wala hawawajuwi vyema watu waliokuwa wakiishi.Inaonekana aliyekuwa akielewa ni mzee Muhammad Qassim,huyu ndiye wa mwanzo aliyekamatwa na jeshi la Pakistan na mpaka sasa hajulikani alipo.
6.Iwapo lile jumba ni la Osama wala asingechagua kujenga kuta nene za uwa,badala yake angechimba handaki au angeimarisha mapaa ya nyumba.Anajuwa maadui zake si vibaka wa Abbotabad bali ni wamarekani wenye teknolojia na vifaa vya angani.
Maswali na shaka zipo nyingi ila ukweli ninaouamini ni kuwa Osama hakuwepo kwenye shambulizi la juzi,hayupo duniani na wala hatojitokeza tena na wamarekani hawatopata picha yake yoyote nyengine.