Orodha ya marais wa Marekani, kipindi cha utawala, chama na makamu wa rais

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
940

ORODHA YA MARAIS WA MAREKANI, KIPINDI CHA UTAWALA, CHAMA NA MAKAMU WA RAIS.
Katika Katiba ya Marekani, Rais wa Marekani ni Mkuu wa Taifa pamoja na kuwa Mkuu wa Serikali wa nchi hiyo. Kama mkuu wa tawi la utendaji na mkuu wa serikali ya majimbo, rais ndiye mwenye cheo na madaraka makuu zaidi katika nchi ya Marekani. Rais pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Marekani. Kuchaguliwa kwa rais wa Marekani ni kupitia mfumo wa wawakilishi wenye kura (electoral college), ambapo rais huchaguliwa kwa muhula wa miaka minne. Inawezekana pia kwamba rais achaguliwe kupitia katika Nyumba ya Wawakilishi ya Marekani (US House of Representatives), ikiwa kongamano la wajumbe halikuweza kumchagua rais kwa kumpa mgombea mmoa kura nyingi kuliko mwingine yeyote. Kulingana na Katiba ya Marekani, mtu yeyote hawezi kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo zaidi ya mara mbili. Kukitokea kifo, kujiuzulu au kuondelewa mamlakani kwa rais, Makamu wa Rais wa Marekani atachukulia kiti cha rais. Orodha hii inajumulisha tu wale watu ambao waliapishwa kama rais kufuatia kupitishwa ka Katiba ya Marekani hapo 4 Machi 1789.

Kumeapishwa marais 45, na kumekuwa na marais 46, kwa sababu rais Grover Cleveland alihudumu mihula miwili isiyofuatana, na kwa hivi anahesabiwa mara mbili, kama rais nambari 22 na nambari 24. Marais wanne walifariki kawaida wakiwa mamlakani (William Henry Harrison, Zachary Taylor, Warren G. Harding, na Franklin D. Roosevelt), mmoja akajiuzulu (Richard Nixon), na wanne wakauawa (Abraham Lincoln, James A. Garfield, William McKinley, na John F. Kennedy). Rais wa kwanza wa Marekani alikuwa George Washington, aliyeapishwa 1789 bada ya kupigiwa kura na wajumbe wote katika kongamano. William Henry Harrison alihudumu kwa muda wa siku 31 pekee, mwaka 1841, naye Franklin D. Roosevelt akahudumu kwa muda mrefu zaidi kuliko wote, miaka 12. Rais wa sasa ni Joe Biden, aliyeapishwa 20 Januari 2021.

1. George Washington 1789 - 1797 - Independent - Virginia - John Adams
2. John Adams 1797 - 1801 - Federalist - Massachusetts - Thomas Jefferson
3. Thomas Jefferson 1801 - 1809 Republican (Jeffersonian) Virginia Aaron Burr | George Clinton
4. James Madison 1809 - 1817 Republican (Jeffersonian) Virginia Elbridge Gerry
5. James Monroe 1817 - 1825 Republican (Jeffersonian) Virginia Daniel Tompkins
6. John Quincy Adams 1825 - 1829 National Republican Massachusetts John Calhoun
7. Andrew Jackson 1829 - 1837 Democratic South Carolina John Calhoun | Martin Van Buren
8. Martin Van Buren 1837 - 1841 Democratic New York Richard Mentor Johnson
9. William Harrison 1841* Whig Virginia John Tyler
10. John Tyler 1841 - 1845 Whig Virginia
11. James Polk 1845 - 1849 Democrat North Carolina George Dallas
12. Zachary Taylor 1849 - 1850* Whig Virginia Millard Fillmore
13. Millard Fillmore 1850 - 1853 Whig New York
14. Franklin Pierce 1853 - 1857 Democrat New Hampshire William King
15. James Buchanan 1857 - 1861 Democrat Pennsylvania John Breckinridge
16. Abraham Lincoln 1861 - 1865* Republican Kentucky Hannibal Hamlin | Andrew Johnson
17. Andrew Johnson 1865 - 1869 Democrat North Carolina
18. Ulysses Grant 1869 - 1877 Republican Ohio Schuyler Colfax | Henry Wilson
19. Rutherford Hayes 1877 - 1881 Republican Ohio William Wheeler
20. James Garfield 1881 - 1881* Republican Ohio Chester Arthur
21. Chester Arthur 1881 - 1885 Republican Vermont
22. Grover Cleveland 1885 - 1889 Democrat New Jersey Thomas Hendricks
23 Benjamin Harrison 1889 - 1893 Republican Ohio Levi Morton
24 Grover Cleveland 1893 - 1897 Democrat New Jersey Adlai Stevenson
25 William McKinley 1897 - 1901* Republican Ohio Garret Hobart | Theodore Roosevelt
26 Theodore Roosevelt 1901 - 1909 Republican New York Charles Fairbanks
27 William Howard Taft 1909 - 1913 Republican Ohio James Sherman
28 Woodrow Wilson 1913 - 1921 Democrat Virginia Thomas Marshall
29 Warren Harding 1921 - 1923* Republican Ohio Calvin Coolidge
30 Calvin Coolidge 1923 - 1929 Republican Vermont Charles Dawes
31 Herbert Hoover 1929 - 1933 Republican Iowa Charles Curtis
32 Franklin Roosevelt 1933 - 1945* Democrat New York John Garner | Henry Wallace | Harry Truman
33 Harry Truman 1945 - 1953 Democrat Missouri Alben Barkley
34 Dwight Eisenhower 1953 - 1961 Republican Texas Richard Nixon
35 John Kennedy 1961 - 1963* Democrat Massachusetts Lyndon Johnson
36 Lyndon Johnson 1963 - 1969 Democrat Texas Hubert Humphrey
37 Richard Nixon 1969 - 1974** Republican California Spiro Agnew | Gerald Ford
38 Gerald Ford 1974 - 1977 Republican Nebraska Nelson Rockefeller
39 Jimmy Carter 1977 - 1981 Democrat Georgia Walter Mondale
40 Ronald Reagan 1981 - 1989 Republican Illinois George H. W. Bush
41 George H. W. Bush 1989 - 1993 Republican Massachusetts Dan Quayle
42 Bill Clinton 1993 - 2001 Democrat Arkansas Al Gore
43 George W. Bush 2001 - 2009 Republican Connecticut Dick Cheney
44 Barack Obama 2009 - 2017 Democrat Hawaii Joe Biden
45 Donald Trump 2017 - 2021 Republican New York Mike Pence
46 Joe Biden 2021 - Democrat

300px-Seal_of_the_President_of_the_United_States.svg.png


450px-WhiteHouseSouthFacade.JPG
 
Sijui kama wamarekani wanapoteza muda kama wewe kukariri viongozi wa nchi yako. Haya madudu yanakusaidi au kutusaidia nini kama siyo mental slavery kama siyo intelectual colonisation mwanangu?
 
Una msongo wa mawazo na Sonona.
Si kweli. Ona unavyoanza uganga wa kienyeji kulinda ujinga wako. Hoja yangu ni rahisi kuwa haya unayoleta yanaonyesha namna ulivyo na mawazo ya kikoloni na kitumwa. Kwanini marais wa marekani na si wa nchi yako? Tukiwajua inatusaidia nini. Mie nakumbuka zama zile tukifundishwa historia ya majangili kama Livingstone, Mungo Park, Henry Morton Stanley, Carl Peters mkono wa damu, Bismack na majambazi wengine waliotulea ukoloni hadi nilipoingia chuo kikuu Ulaya na kugundua kuwa wenzetu walikuwa wanatuchezea akili.

Nilipokwenda Marekani kusoma masters na PhD ndiyo nilibadilika kabisa na kuwa na mawazo chokonozi, tekenyeshi na ya kuasi kama unavyoyasoma kwenye comments zangu kila mahali. Nadhani tumeelewana.
 
Si kweli. Ona unavyoanza uganga wa kienyeji kulinda ujinga wako. Hoja yangu ni rahisi kuwa haya unayoleta yanaonyesha namna ulivyo na mawazo ya kikoloni na kitumwa. Kwanini marais wa marekani na si wa nchi yako? Tukiwajua inatusaidia nini. Mie nakumbuka zama zile tukifundishwa historia ya majangili kama Livingstone, Mungo Park, Henry Morton Stanley, Carl Peters mkono wa damu, Bismack na majambazi wengine waliotulea ukoloni hadi nilipoingia chuo kikuu Ulaya na kugundua kuwa wenzetu walikuwa wanatuchezea akili. Nilipokwenda Marekani kusoma masters na PhD ndiyo nilibadilika kabisa na kuwa na mawazo chokonozi, tekenyeshi na ya kuasi kama unavyoyasoma kwenye comments zangu kila mahali. Nadhani tumeelewana.
Nafuu kama tungeendelea na utawala wa kikoloni wa wazungu kuliko hawa wakoloni wetu weusi, angalia leo nchi ilivyo parara na watu wanavyominywa "Genitalia" kwa kuwa na mawazo kinzani.

Angalia South Africa ya akina Pieter Botha na hii ya hawa manyang'au. Kosa ya akina Botha ilikuwa ni ku-practise ubaguzi wa rangi tu lakini hawakuwa mafisadi kama hawa waswahili. Dola 1 ilikuwa sawa na Randi 3 leo ni balaa.
 
Nafuu kama tungeendelea na utawala wa kikoloni wa wazungu kuliko hawa wakoloni wetu weusi, angalia leo nchi ilivyo parara na watu wanavyominywa "Genitalia" kwa kuwa na mawazo kinzani.

Angalia South Africa ya akina Pieter Botha na hii ya hawa manyang'au. Kosa ya akina Botha ilikuwa ni ku-practise ubaguzi wa rangi tu lakini hawakuwa mafisadi kama hawa waswahili. Dola 1 ilikuwa sawa na Randi 3 leo ni balaa.
We acha ujinga wako hamia sasa huko

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sijui kama wamarekani wanapoteza muda kama wewe kukariri viongozi wa nchi yako. Haya madudu yanakusaidi au kutusaidia nini kama siyo mental slavery kama siyo intelectual colonisation mwanangu?
Bora ungenyamaza, ungeonekana una hekima na busara kuliko hivi!
 
Busara yangu haiwezi kuonekana kwa kuunga mkono utumbo. Bora niupinge nionekane sina busara ila si vinginevyo. Watumwa wa kiakili utawajua kwa mawazo yao.
 
Busara yangu haiwezi kuonekana kwa kuunga mkono utumbo. Bora niupinge nionekane sina busara ila si vinginevyo. Watumwa wa kiakili utawajua kwa mawazo yao.
Ukipewa nafasi ya kwenda kuishi USA na familia yako utakimbilia huko....
 
Ukipewa nafasi ya kwenda kuishi USA na familia yako utakimbilia huko....
Nani. Hata bure siendi. Kwa wasioijua Marekani kama wewe ndiyo mnaiona dili. Kama kuishi nje, nimeishi zaidi ya miaka 20 tena kwenye nchi zenye maisha mazuri kuliko Marekani yako.
 
Back
Top Bottom