One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

Zitto jipunguzie madaraka yako haya makubwa ili uendane na kauli mbiu yako ya demokrasia

Madaraka yako huna tofauti na Ayatollah wa Iran
 
Zitto,

Nikupe ushauri wa bure.

Nakushauri uajiri mara moja Public Relations Officer ili akusaidie kukupa ushauri wa kujitangaza. Kukimbia maswali ya wapiga kura hapa jukwaani bila ya kutoa sababu yoyote haikujengei sifa nzuri ya uongozi.

Ulivyofanya ziara yako ya kupata mawazo ya mkongwe wa siasa wa Malaysia, Dr. Mahathir Muhamad, hakukuelimisha kuhusu swala hili?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kuhusu majimbo hayo, ni mambo tu. Maombi yanakubaliwa na kukataliwa. Ungesubiri kuona maamuzi yangu nipo uweze kutoa maoni yako.

Kwamba sijawahi kuionya CCM kuishambulia CHADEMA nadhani ni propaganda tu. Maisha yangu yote napambana na CCM ndani na nje ya Bunge. Wao kunisifia ni divide and rule.

Mara ngapi viongozi wa CHADEMA wanasifiwa na mawaziri wa CCM? Hata humu JF imeandikwa mara kadhaa pale mawaziri wa ccm wanapowasifia baadhi ya wabunge wa CHADEMA. Ni kawaida hiyo kwenye siasa.

Mara nyingi sana nimetoa matamko makali kulaani uvunjifu wa amani nchini na ugandamizaji dhidi ya upinzani nchini. Mara kadhaa nimeadhibiwa na CCM nimesimishwa ubunge, kamati ya POAC ilivunjwa, niliswekwa ndani kwenye uchaguzi Kigoma Mjini nk.

Hatupimi umakini wa viongozi wa upinzani kwa kuwekwa ndani na polisi, kama ni hivyo leo DP ingekuwa chama kikubwa kuliko vyote nchini

Hapo kwenye rangi ya chama chako...maamuzi yako kama "KIONGOZI MKUU!!??"...its shame and pathetic..assume umetangulia mbele za haki; kuna Zitto mwingine ataibeba ACT??? Hivi ndugu huoni kwamba kwa umri wako na kujipambanu kwako kwamba wewe unaamini katika misingi ya kidemokrasia na uwazi; hayo maneno sio dalili za udikteta na "zidumu fikra za mwenyekiti wa chama"!!?? Katika dunia ya leo, bado unaamini katika u-Castro, u-Stalin na u-Mao!!??

I can only conclude post yako kwa kusema kwamba; pamoja na madai ya usaliti kwa wapinzani, zamani ulikua vizuri sana katika kupanga hoja, ila kwa sasa umekua mwepesi mno ndugu, sioni mantiki ya ulichoandika, hakionyeshi kutoka moyoni mwako...tuombe uzima, maybe tunakuonea.
 
Kama malengo yenu ni haya kwa nini msijiunge na UKAWA? Katibu mkuu wenu alisikika akisema chama chenu kitaisambaratisha CUF mikoa ya Pwani, huoni kama ulichoandika juu ni kujikosha tu? kwamba lengo lenu ni kupambana na upinzani

Jaribu kufanya maswali yawe mepesi kidogo..ona sasa muhusika hawezi kuja kukujibu kakimbia
 
Kiongozi wa chama ana majukumu mengi ya kitaifa na kuangalia namna gani anatutoa hapa tulipo
 
Ujamaa wa Nyerere ni ukomunisti na ujamaa wa ACT ni ujamaa wa kisasa ambao unaamini demokrasia
 
Zitto, nakuaminia kuhusu integrity yako. Nina tofauti kuhusiana na siasa zako. Siiamini Sana kwenye azimio la arusha. Niko suspicious na left wing politics. Lakini nafikiri umefanya vingi vya kutosha ku-earn respect kama politician. SIKU ukitaka kuenea marekani, get in touch. Cheggy2013@gmail.com or call me on +1-646-744-5498.
 
Kapotolo uko biased from the word go!!! Hauko openminded unaporaise issues zako!

Shame on you!!!
 
Kuhusu majimbo hayo, ni mambo tu. Maombi yanakubaliwa na kukataliwa. Ungesubiri kuona maamuzi yangu nipo uweze kutoa maoni yako. Kwamba sijawahi kuionya CCM kuishambulia CHADEMA nadhani ni propaganda tu. Maisha yangu yote napambana na CCM ndani na nje ya Bunge. Wao kunisifia ni divide and rule. Mara ngapi viongozi wa CHADEMA wanasifiwa na mawaziri wa CCM? Hata humu JF imeandikwa mara kadhaa pale mawaziri wa ccm wanapowasifia baadhi ya wabunge wa CHADEMA. Ni kawaida hiyo kwenye siasa. Mara nyingi sana nimetoa matamko makali kulaani uvunjifu wa amani nchini na ugandamizaji dhidi ya upinzani nchini. Mara kadhaa nimeadhibiwa na CCM nimesimishwa ubunge, kamati ya POAC ilivunjwa, niliswekwa ndani kwenye uchaguzi Kigoma Mjini nk. Hatupimi umakini wa viongozi wa upinzani kwa kuwekwa ndani na polisi, kama ni hivyo leo DP ingekuwa chama kikubwa kuliko vyote nchini
Hivi ulipotoa lile tamko la kulaani viongozi wa CDM walipopigwa mabomu na risasi pale soweto ulikuwa una shida gani Ulikuwa huna taarifa za kutosha,ulikuwa na hang over au?Je umewahi jutia hata in private?
 
Ujamaa wa Nyerere ni ukomunisti na ujamaa wa ACT ni ujamaa wa kisasa ambao unaamini demokrasia
Haha..ndio nyie mnajibunia misemo waganga waliochepuka ndio wanaitisha viungo vya albino badala ya kukubali ukweli kuwa uganga ni uchawi na uchawi siku zote lazima kuwepo na uchawi ndio maana wapo watu wanakwenda kwa hao hao waganga kuponywa na haohao kuwadhuru wengine.Ukomunist na ujamaa ni km ndama na ng`ombe...sasa km unataka kusema ndama anaweza kuwa mwana simba.Utakuwa una shida sana.Mkajipange bhana.ujamaa hauna usasa.uchina wenyewe bado wanahangaika kuweza beba vyote wakati raia wanataka uhuru wa fikra zaidi.Ujamaa unajificha ktk ufanyiwa hujuma kuliko kufanya mambo yanayaowezekana na uhuru wa fikra
 
Kuna mi-JITU humu imejigeuza na kumjibia Zitto utadhani imeanzisha thread yenyewe.Mi-jitu imejaribu ku-neutralize maswali magumu dhidi ya Zitto na kufanya yaonekane mepesi.Inaboa sana.

Bwn Zitto tunakusubiri ujibu maswali yote uliyoulizwa huko juu bila kuacha hata moja na usisingizie una majukumu mengi hivyo huna muda wa kutosha simply umeanzisha thread kwa mapenzi yako mwenyewe.

Nitafurahi sana kuona unajibu maswali haya ambayo pia yameulizwa huko juu.

1) Tutakuaminije kuwa hukuanzisha ACT ukiwa ndani ya CHADEMA na wakati sasa upo kwenye nafasi ya juu zaidi kuliko hata waliokutangulia ilihali umepewa cheo hicho ukiwa hata hujakamilisha wiki moja ndani ya chama kipya.?

2)Ukiwa kwenye mahojiano na EFM ulisema kuwa hutogombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya ACT,chakushangaza ukagombea ,tena nafasi ya juu zaidi ndani ya ACT kulikoni Bwn Zitto huu ndiyo uzalendo..?

3) Katiba yenu imetamka kuwa mwanachama mpya hatogombea nafasi ya uongozi mpaka atimize miezi 6 .Sasa wewe wakati unagombea hiyo nafasi ulitimiza matakwa ya katiba.?

4) Na kama mlibadiri katiba ili ukidhi vigezo vya kugombea huoni huo ni mwendelezo wako wa uroho na ulafi wa madaraka.?

5) Na je,mabadiriko ya katiba yenu ambayo ni tofauti na iliyokuwepo kwa msajili wa vyama mwanzoni yalimfikia msajili kabla ya kufanya uchaguzi na kuzindua chama chenu.?Je,msajili kutokufikishiwa mabadiriko ya katiba kabla ya uchaguzi ni sawa..?
 
Kila la kheri wana act lakini wa tz tunawajua kazi mliyobakia nayo. Nyie hangaikeni tu, halafu huyo Kiongozi mkuu ana roho ngumu sana, mama kafa katika mazingira ya kuhuzunisha, lakini mmm ... wa kigoma tuwaachie wa kigoma
 
Zitto uliwahi kutuasa tusiwaamini wanasiasa. Kwa kuanzisha chama ndani ya chama, kauli yako hii ndio nimeiamini kwamba nyinyi wanasiasa wa kiafrika ni wanafiki na mnaongozwa na tamaa.

Migogoro mingi ktk nchi za kiafrika inasababishwa hasa na ubinafsi wa viongozi.
 
Qn # 401,
Yale magari uliyodai umepewa na Mkono mbona hayapo kwa statement yako uliyotoa juzi?

Qn # 402,
Ulisikika ukijitamba kua kwa mshahara wako wa Ubunge na mapato yatokanayo na ushauri mbalimbali wa kuhusu masuala ya kiuchumi na kifedha pia pamoja na vyanzo vingine si ajabu kumiliki Land Cruiser mbili tatu, ZIKO WAPI ZILE GARI??
 
Naomba unijibu hili Zitto ACT kabla hujahamia wewe ilikwisha kuanzisha maofisi makubwa makubwa mikoa mingi ikiwamo Arusha mjini ofisi ambazo kwa hesabu ya kawaida kwa mfano ya pale Arusha mjini siyo chini ya Milioni moja kwa mwezi. Chama hiki kichanga chenye wanachama wachache kimetoa wapi fedha za kukodisha maofisi makubwa hivyo? Pia kabla hujahamia Chadema kule Kigoma ulitoa magari yako yakaanze kutumika kufanya kazi za ACT unataka kuniambia wewe ulikuwa moja ya wafadhili na waanzilishi wa ACT ukiwa bado ndani ya Chadema?

Mkuu iba Maana wewe huamini kuwa Zitto alianzisha ACT akiwa ndani ya CHADEMA ama unasubiri aje kusema hapa JF ?
Bado sijakusoma Kaka
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Zitto, hukuwahi kupigwa mabomu ukiwa CHADEMA, je tutegemee kupigwa mabomo ukiwa ACT?
 
Last edited by a moderator:
Ninachokiona hapa ni kuwa,tuna tatizo kubwa sana la kukosekana "flexibilty" miongoni mwa viongozi wa vyama vya upinzani kwa upande mmoja na sisi mashabiki wa vyama vya siasa kwa upande mwingine.Kukosekana huku kwa flexibility miongoni mwa wanasiasa wetu ndio kuliko changia umoja kama huu wa UKAWA tulionao leo hii kuchelewa kupatikana.

Hata hivyo,nawapongeza viongozi wa vyama vya upinzani waliogundua tatizo hili la flexibility na kuli-overcome kwa kukaa pamoja na kuanzisha UKAWA.

Hivyo basi,na sisi mashabiki na wapenzi wa vyama vya siasa tunapaswa ku-exercise flexibiliy,lakini kwa tahadhari kubwa,ili tuifikie ile nchi ya ahadi tunayoililia kila kukicha.

Japo wanasiasa hawaaminiki,flexibility katika kufikia maridhiano/makubaliano ni jambo la muhimu sana kwa mafanikio yoyote ya kisiasa ila tu maridhiano/makubaliano hayo yasiwe ya kukurupuka na yafanywe kwa tahadhari.

Tutoe nafasi kuwapima ACT kwani muda pekee ndio msemakweli then flexibility "inaweza" kuchukua nafasi yake.

Note:Kipimo cha muda pekee bila flexibilty ya pande zote ni bure.

ACT ni Chama kikichoanzishwa katika Misingi Haramu.
Hakuna cha fkexibility wala nini.
Kwa mtu anayejitambua hawezi kupoteza muda kukiwazia hiki Chama.
Sana sana ni wale Follower wa ZZK ndio wako dilema.
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa ACT ilianzishwa na Zitto pale alipokoipeleka CHADEMA Mahakamani as a plan B incase akishindwa kesi ?

Kwenda mahakamani ni sehemu ya unafiki wa kujenga dhana ....alikua anatamani kuondoka kishujaa kwa huruma ya kuonewa ...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom