Naomba unijibu hili
Zitto ACT kabla hujahamia wewe ilikwisha kuanzisha maofisi makubwa makubwa mikoa mingi ikiwamo Arusha mjini ofisi ambazo kwa hesabu ya kawaida kwa mfano ya pale Arusha mjini siyo chini ya Milioni moja kwa mwezi. Chama hiki kichanga chenye wanachama wachache kimetoa wapi fedha za kukodisha maofisi makubwa hivyo? Pia kabla hujahamia Chadema kule Kigoma ulitoa magari yako yakaanze kutumika kufanya kazi za ACT unataka kuniambia wewe ulikuwa moja ya wafadhili na waanzilishi wa ACT ukiwa bado ndani ya Chadema?
Fomu ya mali ya Zitto inaonesha ana gari moja tu!
Hivyo lawama zako zote zina hang kwenye ku-prove kuwa anamiliki hayo magari, baada ya hapo ndio uje kwenye hoja yako. Kama unashindwa kuprove beyond reasonable doubt kuwa Zitto anamiliki hayo magari mengi, ambayo kupitia kiapo cha chama chake amesema anamiliki gari moja tu!implying kuwa hamiliki haya magari unayosema, unaonaje chini ya hizi tuhuma ukaambatanisha na kadi za gari za umiliki wa hayo magari?au hata kum-tie Zitto na umiliki?
Kama unashindwa kufanya hivyo, kweli unategemea watu tukuchukulie serious?binafsi napenda kama tuhuma zinawekwa na mtu mwenye uelewa anaziweka na evidence, sio kuleta hadithi za nimesikia sehemu au kuleta picha Zitto amepanda gari flani, wangapi humu mnapanda na kuendesha magari sio ya kwenu?
nawasihi Bavicha muachane na hizi Siasa Uchwara, they are old, tiring and useless,mfike wakati mjitazame wapi mmekosea, mjirekebishe, mrudi kwa wananchi, mjenge nao hoja, huyu Zitto anawaambia amepigia mstari yote ya nyuma anaanza upya nyie bado mnamrudisha kule kule, hamuoni kuwa, ukiondoa tuhuma za usaliti this usaliti that, mmekosa hoja za kupambana nae?
Humu nimemuona
Ben Saanane tu ameuliza swali la msingi na lenye kumchalenge Zitto kwenye hoja ya msingi.Katazame debate ya UK leadership, uone kama kuna mtu alikuwa napoteza muda kuongelea watu kule, watu walikuwa wanachallenge issues tu. Ifike wakati mjikite huko. By the time mnastuka hao ACT watakuwa wameimaria kwa kuwa wanawaambia wananchi kile wanataka kusikia, halafu mtawalaumu bure tu.