tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Njombe Mjini kupitia Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Sigrada Mligo jana Oktoba 26, 2025 alitumia Jukwaa la ACT kuzungumza na wakazi wa Njombe mjini pamoja na kumnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Mji Mwema kupitia Chama Cha ACT Wazalendo, Abuu Mtamike.
Sigrada alimnadi Mgombea huyo wa ACT huku akisema kinachotakiwa ni kupambana na Chama tawala kwa namna yoyote, hata kwa kuungana ili waweze kuwasemea wananchi watakaposhinda Ubunge na Udiwani.
Soma pia: Mgombea urais CHAUMMA amnadi mgombea udiwani ACT Wazalendo
"Vyama vya upinzani adui yetu ni Chama cha Mapinduzi kwasababu tunahitaji mabadiriko"amesema Sigrada
Amesema Chama hicho katika kata ya Mji Mwema hakina mgombea ndio maana amelazimika kumuombea kura mgombea wa Udiwani kupitia ACT, ili waweze kwenda kupigania haki za wakazi wa Njombe kama walivyofanya wakiwa pamoja walipokuwa madiwani 2015 - 2020 wote wakiwa CHADEMA.