One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

Ujamaa wa Nyerere ni ukomunisti na ujamaa wa ACT ni ujamaa wa kisasa ambao unaamini demokrasia

Demokrasia ya ACT iPo wapi Kama Jina la chama limebadilishwa bila hata kuwepo kwenye ajenda ..

Kama nafasi ya kiongozi Mkuu mgombea ni mmoja na ameibuliwa ghafla ..Baada ya Siku Moja nyuma kusema hatagombea CHOCHOTE ...na hata kwenye ratiba ya mwanzo uchaguzi wa kiongozi Mkuu haukuwapo kwenye ratiba
 
Mkuu Zitto naona umekuja na kauli mbiu nzuri yaani hiyo kauli ya Dr. Nkrumah kwamba foward ever backward never. Hii ni kauli ya kiungwana zaidi.

Haina haja ya kulumbana na mtu ama kuanza kukisema chama chako cha zamani. Nakumbuka siku uliyoitisha mkutano wa waandishi wa habari pale Serena watu hasa wa CHADEMA walihamanika wakidhani utaenda kuichafua. Katika kuhamanika huko, ikabidi Naibu Katibu Mkuu kuitisha mkutano na wandishi wa habari pale makao makuu harakaharaka ili kugawa waandishi na matokeo yake akaishia kuongelea habari za maji jimbo la Ubungo. Kitu ambacho angeweza kukiongelea kwenye mkutano wa hadhara huko Bonyokwa.

Katika siasa za Tanzania ni watu wengi wameitwa wasaliti, hakuna mwanasiasa ambaye hajaitwa msaliti. Marando aliwahi kuitwa msaliti, Mrema aliwahi kuitwa msaliti, Maalim Seff aliwahi kuitwa msaliti, Dr. Slaa aliwahi kuitwa msaliti, nk. Hivyo neno usaliti kwa mwansiasa wa Tanzania ninkama fashion vile; leo utakuwa shujaa mkitofautiana na wenzako tayari unaitwa msaliti.

Kazana na kuimarisha chama chako ila hili la kuacha kugombea ubunge Kigoma Kasikazini na kutaka (kuombwa) kugombea Kawe, Segerea, Kahama, nk naona halijakaa sawa. Litafakari kwa makini.
 
fikirikwanza

Siasa ni mapambano. Siwezi kuacha mapambano. Sijawahi fanya usaliti wowote. kuitana majina hayo hakusaidii lolote zaidi ya kufurahisha ego zetu tu. ACT Wazalendo ina shabaha moja tu nayo ni kupambana na mfumo wa uchumi unaonyonya watanzania. Ku surrender mapambano hayo ndio usaliti. Tutaendelea kupambana

Kweli askari mkuu wa ACT, lakn iwapo mbinu zako za mapambano dhidi ya uchumi mbovu zinasaidia CCM kubaki madarakani hata kama wewe binafsi huamini hivyo ni wazi kuwa unasaliti umma, na usaliti uliojificha kiasi kwamba hata msaliti mwenyewe anasema hajui ni hatari sana maana ipo siku kwa kutojua kwake usaliti wake utaangamiza taifa na yeye akiwemo, what a shame ZZK?
 
Mkuu Zitto naona umekuja na kauli mbiu nzuri yaani hiyo kauli ya Dr. Nkrumah kwamba foward ever backward never. Hii ni kauli ya kiungwana zaidi.

Haina haja ya kulumbana na mtu ama kuanza kukisema chama chako cha zamani. Nakumbuka siku uliyoitisha mkutano wa waandishi wa habari pale Serena watu hasa wa CHADEMA walihamanika wakidhani utaenda kuichafua. Katika kuhamanika huko, ikabidi Naibu Katibu Mkuu kuitisha mkutano na wandishi wa habari pale makao makuu harakaharaka ili kugawa waandishi na matokeo yake akaishia kuongelea habari za maji jimbo la Ubungo. Kitu ambacho angeweza kukiongelea kwenye mkutano wa hadhara huko Bonyokwa.

Katika siasa za Tanzania ni watu wengi wameitwa wasaliti, hakuna mwanasiasa ambaye hajaitwa msaliti. Marando aliwahi kuitwa msaliti, Mrema aliwahi kuitwa msaliti, Maalim Seff aliwahi kuitwa msaliti, Dr. Slaa aliwahi kuitwa msaliti, nk. Hivyo neno usaliti kwa mwansiasa wa Tanzania ninkama fashion vile; leo utakuwa shujaa mkitofautiana na wenzako tayari unaitwa msaliti.

Kazana na kuimarisha chama chako ila hili la kuacha kugombea ubunge Kigoma Kasikazini na kutaka (kuombwa) kugombea Kawe, Segerea, Kahama, nk naona halijakaa sawa. Litafakari kwa makini.

Hao wote uliowataja hawajawahi kuanzisha vyama wakiwa ndani ya vyama vyao,na hiyo ndio maana ya u Eskariot.
Huyu jamaa hata mumpe moyo kiasi gani,ukweli kuwa amekwisha kufariki ki Siasa u dhahiri
 
Zito una vituko sana, yani upangishe kila jimbo office, unafanya ziara za gharama huna ruzuku wewe na chama chako, halafu sisi tukuamini eti wewe sio msaliti kweli!? Unatolea wapi hayo Mapesa!? Wakati chadema tuna miaka 21 hatuna huo uwezo wakua na maofisi.
 
Hao wote uliowataja hawajawahi kuanzisha vyama wakiwa ndani ya vyama vyao,na hiyo ndio maana ya u Eskariot.
Huyu jamaa hata mumpe moyo kiasi gani,ukweli kuwa amekwisha kufariki ki Siasa u dhahiri

kweli kabisa anarusha rusha vimiguu...
 
Ni lini Zitto amewahi kuidiss CCM? hata kwenye kikao tu.. Anayejua anisaidie nielewe ataanzaje kupambana na CCM waliomfikisha hapo

Watanzania sio mazuzu..

Juzi akiwa EATV alikiri mwenyewe kuwa alianzisha chama akiwa ndani ya chama..
 
Nimuulize kaswali kadogo tu..
Kwanini maCCM ndio yanayoumia zaidi wakati anaadhibiwa na chama makini Chadema kwa usaliti?

Alishindwa kuwaambia wasiwe mbelembele sana watashtukiwa!?
 
Halafu.. Nimeona inayoelezwa kuwa nakala ya fomu uliyojaza mali na madeni (yanayoweza kuwa public tu)

Umejitambulisha kama Kiongozi wa Chama... Woga ulikuwa upi kujaza "Kiongozi Mkuu wa Chama" kwasababu kiongozi hata kijijini yupo.. Unaona licheo linakuaibisha hivi?

Nimalizie kwa kusema kwamba Chadema iliathirika zaidi kwa kuwa na watu wa dizaini yako kuanzia msimu wote wa ngwe ya Pili ya Kikwete!

Chadema wamepumua mno kwa kuondokewa na zigo la usaliti..wamebaki vidagaa tu kama wapo

Nikukumbushe, Jaribio lako la Mwisho kuiumiza Chadema lilikuwa kwenye Uchaguzi Mkuu ukimtumia Kansa Mbarouk ili uchafuzi usifanyike..kwa zuio la Mahakama.. Chadema wakawa wajanja hawakukupa fursa..uliyemtuma alitakiwa kuenguliwa kugombea kwa kukiuka taratibu lakini hakuondolewa kama mlivyotegemea..

Tukio la mwisho kuonesha uccm wako ni Bungeni wakati wa hitimisho la mjadala wa ESCROW..uliishia kubutua nje mpira na kila kitu kilishaharibika..unajua fika ulilenga nini..precedence ya mwizi Chenge iprevail na Bunge litoke bila heshima yake huku Serikali hasa raia akiwa huru kama hakuna kibaya.. Ukasahahu hata mapendekezo ya PAC yakoje! Ashukuriwe Mbowe aliyehamasisha na wabunge webgine qakagoma kukaa mpaka Bunge likahirishwa ndio mkaandikiwa mapendekezo mengine..otherwise ulishatuuza sana na ndio mchezo wako
 
Ccm ndio wasemaji wakubwa wa Act sasa hapo kimebakizwa nini? Mwenye macho na aone mwenye masikio na asikie
 
Ndugu wana JF,

Kwa muda mrefu na hasa siku za hivi za karibuni kumekuwa na threads nyingi sana humu ndani kuhusu Zitto na kuhusu Chama cha ACT Wazalendo. Kumekuwa na tuhuma kwamba chama cha ACT Wazalendo kinashambulia vyama vingine vya upinzani hapa nchini. Napenda kusema mambo machache sana

Chama cha ACT Wazalendo ni chama cha siasa chenye mrengo wa kushoto na kinajitanabaisha na siasa ya Ujamaa iliyoasisiwa na Azimio la Arusha. Lengo letu ni kueneza siasa zetu zenye mrengo huo.

1. Chama cha ACT Wazalendo kwa sasa ni chama cha upinzani nchini. Kimekuja kuhuisha zaidi siasa za upinzani ili kuiondoa CCM madarakani. Chama cha ACT Wazalendo hakina lengo hata kidogo kuzorotesha upinzani nchini. Tofauti zetu tulizokuwa nazo katika chama tulichokuwamo wengine tumeshazifuta, tumepiga mstari na kutazama mbele.

Ndio maana hutasikia kiongozi hata mmoja wa ACT Wazalendo akihangaika na vyama vingine vya upinzani. Hata tukichokozwa namna gani tumefanya maamuzi kwamba hatutajibizana na chama kingine chochote cha upinzani hapa nchini. Tutapambana na chama tawala ili kubomoa mfumo wa uchumi unaonyonya wengi na kufaidisha wachache. Tutapigania uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi. Tutapambana na ufisadi kwa nguvu zetu zote. Hizo ndizo kazi tulizo nazo.

2. Tunasisitiza, tunayo vita moja lakini una njia nyingi za kupigana dhidi ya adui. Huko tulipokuwa tulitofautiana mbinu hizo. Sasa tumepata jukwaa la kutumia mbinu hizo. Wenzetu watumie mbinu zao pia. Hatimaye kila mmoja alenge shabaha kwa adui mmoja. Tunasema One Struggle, Many Fronts

3. kuitana mamluki, wasaliti nk ni siasa za framing tu. Sio mara ya kwanza siasa hizi kutumika nchini katika kujaribu ku frame watu. Mwaka 1995 Mrema wa NCCR aliita CHADEMA chama cha mashushu kutoka Benki Kuu na kila mtu alimwamini. Leo Mrema yupo wapi na CHADEMA ipo wapi? Mwaka 2000 mpaka 2005 CUF ndio ilikuwa chama kikuu cha upinzani na kuidharau CHADEMA. Mwaka 2013 CHADEMA iliita CUF chama cha mashoga.

Miaka yote Mbatia amekuwa akiitwa pandikizi nk. Yote haya hayajazuia vyama hivi kufanya kazi pamoja hivi sasa. Ni vizuri sana wanasiasa kuweka akiba ya maneno. Hakuna sababu ya kutukanana na kuitana majina mabaya. Tunachohitaji ni kila mmoja kumlenga adui ili kumshinda. Tulishindwa kufanya kazi ndani ya moja, tunaweza kufanya kazi tukiwa majirani. Adui bado ni yule yule.

4. Sisi ACT Wazalendo tutachochea kuni kuwasha moto wa mapinduzi nchini kwa kuendesha siasa za masuala (issues). Tumeanza ziara yetu mkoa wa Ruvuma kwa sababu ni mkoa ambao wabunge wake wote ni CCM. Tutaweka nguvu sana maeneo hayo badala ya maeneo ambayo tayari vyama vingine vya upinzani vina nguvu. Sisi katika ACT wazalendo tunataka kuona uchumi unarudi kwa wananchi wenyewe badala ya uchumi kushikiliwa na watu wachache.

Tunataka kuona Miiko ya Uongozi inarudi ili kurejesha imani ya wananchi kwa viongozi wao. Tunataka kuona mfumo madhubuti wa uwajibikaji nchini. Hayo ndio mapambano yetu. Hayo ndio maelekezo yetu kwa wanachama wetu; Kupambana na adui mmoja tu - CCM.

Mimi nataka kukuuliza swali kuwa ati umefanya mengi sawa lakini si kwa jinsi unavyojisia, kwa kawaida kiongozi wa watu huonekana na watu na siyo kujiona yeye mwenyewe, kwa mara nyingi umekuwa unajisifia umefanya hili mara lile lakini kuna hayo yote eidha uliambiwa useme ukapewa na data na watu fulani unaowajua wewe, lakini yote kwa yote, sijawahi kykuona unafanya vitu kwa vitendo kama anavyofanya Mchungaji wetu na mjasiri wa ukweli kama mtikila umeishia kupewa data na kuzisema bungeni tuu. Na kuna mengine umeyasema lakini mpaka leo umefyata mdomo nalo ni kuhusu watanzania walioficha fedha nje ya nchi, ulisema unawajua tutakuona wewe ni mzalendo wa kweli kama utawataja ili tuone hiyo forward forever yako sio kutuambia wewe ni mzalendo. Hivi unajua maana ya neno mzalendo au unalitamka tu. Uko radhi kufa? Na je humwogopi mtu? Mbona ulimkwepesha rais kwenye issue ya escrow? Rais ndio ana haki ya kuwaibia watanzania kwa sababu ya cheo? Hiyo kwetu ni mirror au kioo kwamba Ukiwa kama mkuu wa ACT TANZANIA uko radhi kukwepesha mambo kisa tu chama kitayumba kisa yamemgusa MKUU wa chama, tukuaminije? Jenga hoja na sio kejeli watu wengine at wanaongea kama kasuku je wewe unaongea kama nani? .............
 
Mkuu Zitto naona umekuja na kauli mbiu nzuri yaani hiyo kauli ya Dr. Nkrumah kwamba foward ever backward never. Hii ni kauli ya kiungwana zaidi.

Haina haja ya kulumbana na mtu ama kuanza kukisema chama chako cha zamani. Nakumbuka siku uliyoitisha mkutano wa waandishi wa habari pale Serena watu hasa wa CHADEMA walihamanika wakidhani utaenda kuichafua. Katika kuhamanika huko, ikabidi Naibu Katibu Mkuu kuitisha mkutano na wandishi wa habari pale makao makuu harakaharaka ili kugawa waandishi na matokeo yake akaishia kuongelea habari za maji jimbo la Ubungo. Kitu ambacho angeweza kukiongelea kwenye mkutano wa hadhara huko Bonyokwa.

Katika siasa za Tanzania ni watu wengi wameitwa wasaliti, hakuna mwanasiasa ambaye hajaitwa msaliti. Marando aliwahi kuitwa msaliti, Mrema aliwahi kuitwa msaliti, Maalim Seff aliwahi kuitwa msaliti, Dr. Slaa aliwahi kuitwa msaliti, nk. Hivyo neno usaliti kwa mwansiasa wa Tanzania ninkama fashion vile; leo utakuwa shujaa mkitofautiana na wenzako tayari unaitwa msaliti.

Kazana na kuimarisha chama chako ila hili la kuacha kugombea ubunge Kigoma Kasikazini na kutaka (kuombwa) kugombea Kawe, Segerea, Kahama, nk naona halijakaa sawa. Litafakari kwa makini.

MwanaCCM yeyote ni lazima amtetee Zitto kwa hiyo sishangai comment yako hii.

Kazaneni ili CCM ipone kupitia huyu..
 
Last edited by a moderator:
Zittooooo! mbona unatukatili mkuu, maswali huku yanaielemea thread.
 
Mkuu umejibu vizuri, lakini kusema kuwa hampimi umakini wa Upinzani kwa kuwekwa ndani utakuwa umefumbia macho siasa za Africa ama hutaki kuamini kinachoendelea, na hapo sitaki kusema lolote, DP ni chama cha mtu mmoja na hakijawahi kwenda public, REV. anafanya siasa za ki intellectual ndio maana anawakera wakubwa wenzake lakini uraiani haonekani..is the man of his kind....Respect to him.

Mkuunakuhakikishia kuwa mtakapojipambanua kuwa kweli nyie ni wapinzani na mnataka kubomoa mahekalu ya CCM ndio utakumbuka huu uzi hapa JF....Unless isiwe Africa ninayoijua mimi
Kuhusu majimbo na kwamba ningesubiri ndio nitoe maoni yangu ni kuto utendea haki ubongo wangu, na hivyo kutilia mashaka mkakati wenu kama chama dhidi ya wapinzani wenzenu.

Out of the topic but valid, mmesema mtaweka wagombea nchi nzima, swali, pesa mtatoa wapi, vipo vyama vinapata ruzuku ya hadi milioni 69 lakini haviwezi kufanya hivyo, nyie fedha mtapata wapi ikizingatiwa mmezungukwa na wanaharakati wa wakawaida wengine hata kazi za kueleweka hawana?

Ni hayo tu mkuu Zitto# All the best.
haya ni maswali ya msingi kabisa
 
Zito una vituko sana, yani upangishe kila jimbo office, unafanya ziara za gharama huna ruzuku wewe na chama chako, halafu sisi tukuamini eti wewe sio msaliti kweli!? Unatolea wapi hayo Mapesa!? Wakati chadema tuna miaka 21 hatuna huo uwezo wakua na maofisi.

Nadhani ule waraka wa chacha wangwe ndio jibu sahihi kwa swali lako, chadema siyo kama inakosa hela ya kupangisha ofisi ila asilimia kubwa ya pesa ya ruzuku inalipa madeni ya mtu mmoja anayekopesha bila hata Chama kuwekeana naye makubaliano ya riba then baadaye yeye ndio a najua sh ngap amekopesha na rib kiasi gani anatakiwa alipwe na Chama. Hvyo anza kuanza kuuliza chadema ndio uende kwa zito
 
zitto unavituko wewe HaHaha waliokudanganya unafanana na Malema "Juju" wako wapi???
 
Nadhani ule waraka wa chacha wangwe ndio jibu sahihi kwa swali lako, chadema siyo kama inakosa hela ya kupangisha ofisi ila asilimia kubwa ya pesa ya ruzuku inalipa madeni ya mtu mmoja anayekopesha bila hata Chama kuwekeana naye makubaliano ya riba then baadaye yeye ndio a najua sh ngap amekopesha na rib kiasi gani anatakiwa alipwe na Chama. Hvyo anza kuanza kuuliza chadema ndio uende kwa zito

Kaka,
Chadema kinakamati kuu ambayo kazi kubwa ni pamoja na kupitia mapato na matumizi ya chama chake kutoka ngaxi ya chini kabisa msingi hadi Taifa.Zitto alikuwa mjumbe iliwezekana vipi kiongozi ajikopeshe kisha viongozi wa cc wakae kimya ajue zitto tu?

Ndani ya cc kuna watu makini sana,Pr Baregu,Pr Safari,Mabere Marando,nk wawe kimya kwa hili?

Mwisho nikuulize no research no right to say hebu tupe vielelexo vya lini,wapi Viongozi hawa wa juu kama walijikopesha.

Pia hatuhitaji Shonza,hatuhitaj Mwapamba na hatuhitaji Mwigullu ambao kwa ego tu waliibuka bungeni na wengine kwenye majukwaa ya cc kuomba kuhamia huko na kutoa kashifa kibao lete ushahidi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom