Kuna mi-JITU humu imejigeuza na kumjibia Zitto utadhani imeanzisha thread yenyewe.Mi-jitu imejaribu ku-neutralize maswali magumu dhidi ya Zitto na kufanya yaonekane mepesi.Inaboa sana.
Bwn Zitto tunakusubiri ujibu maswali yote uliyoulizwa huko juu bila kuacha hata moja na usisingizie una majukumu mengi hivyo huna muda wa kutosha simply umeanzisha thread kwa mapenzi yako mwenyewe.
Nitafurahi sana kuona unajibu maswali haya ambayo pia yameulizwa huko juu.
1) Tutakuaminije kuwa hukuanzisha ACT ukiwa ndani ya CHADEMA na wakati sasa upo kwenye nafasi ya juu zaidi kuliko hata waliokutangulia ilihali umepewa cheo hicho ukiwa hata hujakamilisha wiki moja ndani ya chama kipya.?
2)Ukiwa kwenye mahojiano na EFM ulisema kuwa hutogombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya ACT,chakushangaza ukagombea ,tena nafasi ya juu zaidi ndani ya ACT kulikoni Bwn Zitto huu ndiyo uzalendo..?
3) Katiba yenu imetamka kuwa mwanachama mpya hatogombea nafasi ya uongozi mpaka atimize miezi 6 .Sasa wewe wakati unagombea hiyo nafasi ulitimiza matakwa ya katiba.?
4) Na kama mlibadiri katiba ili ukidhi vigezo vya kugombea huoni huo ni mwendelezo wako wa uroho na ulafi wa madaraka.?
5) Na je,mabadiriko ya katiba yenu ambayo ni tofauti na iliyokuwepo kwa msajili wa vyama mwanzoni yalimfikia msajili kabla ya kufanya uchaguzi na kuzindua chama chenu.?Je,msajili kutokufikishiwa mabadiriko ya katiba kabla ya uchaguzi ni sawa..?