One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

Unaposema usaliti na uchonganishi weka ushahidi haiwezekan mtu yule yule kupewa kashafa zile zile watanzania wanaitaji kuaemewa sio kusikiliza hekaya kilasiku

Bavicha wengi hukariri na kusema yale yale kila leo ...ndani ya Bavicha ni Ben saanane pekee ambaye ana uwezo wa kifikiri na kujenga hoja ndio maana wakamnyima uenyekiti.
 
Hivi kwenye ESCROW ni kitu gani kipya ulichofanya, kusoma ripoti bungeni?

Report inayotaja waliopta hela Mkombozi na kufungia macho wale waliopokea Stanbic.

Makes you wonder atatumika mpaka lini.
 
Tumeshaonya wanachama wetu wote kutoshambulia chama chochote cha upinzani. Walikuwa wanachokozwa na wao kujibu mapigo. Hata hivyo haina tija na tumeamua kuwa hata tukichokozwa tunasema " tumeshapiga mstari. Forward ever backward never". Hatutachokozeka tena. Kazi yetu kueneza Sera za ACT Wazalendo
kati ya watu wanafiki na wachawi wewe unaongoza. naomba ujibu haya
1. nani aliwashawishi kaijage na masud kwenda ACT ata kabla haijasajiliwa?
2. je habari za kaijage kumtukana dr slaa, mbowe na lisu mbona hatujaona unakemea?
3. huko tayari na azimio la arusha. je vitaru vya maragaladi, mtwara, na ardhi ya mwandika huko tayari kurudisha kwa wananchi?mwl nyeerere alipewa elykopta akaigawa kwenye chams. wewe utajiri wako unaigawa lini?
 
Unaposema usaliti na uchonganishi weka ushahidi haiwezekan mtu yule yule kupewa kashafa zile zile watanzania wanaitaji kuaemewa sio kusikiliza hekaya kilasiku

Hivi wewe Hansel Nasri bado hujui dhana ya Usaliti?

Kwa mujibi wa kamusi ya Tuki,Usaliti ni tendo la kwenda kinyume na makubaliano ambayo yamefanyika awali.

Majambazi huweka makubaliano kuwa hata atakapokamatwa mmoja wao,basi asithubutu kutoa siri zao hata kama atateswa kwa kiwango gani.

Zitto ni mtu anaeamini katika usawa ,uwazi na uwajibikaji.

Zitto ni Kijana anaeamini katika kutenda yale unayoyahubiri.

Sasa Chadema walikubaliana kutochukua posho Zitto akatii agizo hilo la chama kwa kukataa posho tangu 2011 hadi anag'atuka.

Kumbe wenzake walifanya makubaliano mapya ya kuchukua posho hivyo Zitto aliwasaliti kukataa posho wakati hata kiongozi wao mkubwa anakuwa wa kwanza kuchukua.

Zitto anaamini katika misingi ya Kijamaa lkn wenzake wanaamini katika ubepari huo nao ni usaliti mwingine.

Zitto ndie aliemuagiza CAG akague vyama vya siasa bila kufanya cinsultance na chama chake,Zitto alilenga kukidhalikisha chama badala ya kufunika uchafu ili watanzania wasiyajue madhaifu yao.

Kitendo cha Zitto kumuagiza CAG kukagus vyama ikiwemo chadema hakika ni kiwango cha juu cha usaliti.
 
Watoto wa cdm wanajitaidi sana kupiga vita act naamini hamtaweza hamuoni mshangao tu namna act ilivyoanza na sasa ilivyo mabadiliko makubwa sana imekusanya vijana wengi tu wenye kushambulia kama nyinyi tofauti na awali tulivyokua tunapata shida na page zote zinakua za cdm
Nyambafu mfikshieni mfalme mbowe

Mmeambiwa na "Taswira ya Chama" ACT mmeamua kuangalia mbele, pia mmepewa karipio kuifatafata CHADEMA NA CUF!

Kawaambia enezeni sera za chama chenu (Sijui hata kama mnazifaham zaidi ya kusikia ni ujamaa na demokrasia!)

Achanene na mijitusi na kuvishambulia vyama pinzani. "Kiongozi wa chama" pia amewataka kujadili issues na sio watu. Hivi hamumuelewi muota maono wa chama jamani?

Kama hamtii mtu muhimu hivi ndani ya chama chenu, tegemeeni ACU-WAZANDIKI chama kipya kabisa toka Chama chenu!
 
kwanini hukwenda chama kingine tofauti na cdm kwani kuna vyama vingi tu vinavyofikia 22 na ukaamua kujaza utitiri WA chama kin fine?
 
Hivi wewe Hansel Nasri bado hujui dhana ya Usaliti?

Kwa mujibi wa kamusi ya Tuki,Usaliti ni tendo la kwenda kinyume na makubaliano ambayo yamefanyika awali.

Majambazi huweka makubaliano kuwa hata atakapokamatwa mmoja wao,basi asithubutu kutoa siri zao hata kama atateswa kwa kiwango gani.

Zitto ni mtu anaeamini katika usawa ,uwazi na uwajibikaji.

Zitto ni Kijana anaeamini katika kutenda yale unayoyahubiri.

Sasa Chadema walikubaliana kutochukua posho Zitto akatii agizo hilo la chama kwa kukataa posho tangu 2011 hadi anag'atuka.

Kumbe wenzake walifanya makubaliano mapya ya kuchukua posho hivyo Zitto aliwasaliti kukataa posho wakati hata kiongozi wao mkubwa anakuwa wa kwanza kuchukua.

Zitto anaamini katika misingi ya Kijamaa lkn wenzake wanaamini katika ubepari huo nao ni usaliti mwingine.

Zitto ndie aliemuagiza CAG akague vyama vya siasa bila kufanya cinsultance na chama chake,Zitto alilenga kukidhalikisha chama badala ya kufunika uchafu ili watanzania wasiyajue madhaifu yao.

Kitendo cha Zitto kumuagiza CAG kukagus vyama ikiwemo chadema hakika ni kiwango cha juu cha usaliti.

Hizo hoja uwa zinakwepa sana na watu ambao tunaamini wanatakiwa watupe majibu, sasa na Shangaa sana baadhi ya watu kunyooshea wengine vidole ndo maana mm uwa sibabaiki na watu fulani ila uwa naweza kukupongeza pale panapostaili ingawa wenyewe ukitaka kuwakosoa wanakuja na matusi balaa. Ndio maana hata sasa kama mtu fulani hv atagombea urais nitampa pamoja na sifa mbaya wanayompa sababu najua ubora wake ni mkubwa kuliko udhaifu wake
 
Karibu tena Ndugu Zitto Kabwe katika mjadala juu ya hatma ya nchi yetu.

Tofauti na vijana wengi walioamua kufia vyama vyao kuliko maslahi ya taifa.

Mimi ninamaswali kadhaa naomba uyajibu kwa manufaa ya Jukwaa na Watanzania kwa ujumla.

1.Watanzania ni wazito kupokea mabadilko,tejea matumizi ya Mita za LUKU na sasa Kugomea matumizi ya EFDs Ktk kulipa kodi.
Je Wafanya biashara kuendelea kugomea mashine inatija kwa taifa linalitaka kujitegemea?

2.Hoja ya upatikanaji wa hifadhi ya jamii kwa watanzania wote bila ubaguzi linawezaje kufanikiwa bila kuathiri hiyo mifuko na serikali kwa ujumla? pia tunaomba mifano ya Mataifa inayotoa hifadhi ya jamii kwa wananchi wote.

3.Ukiwa kiongozi wa ACT -Wazalendo na unaekubalika sana Tanzania ,Je utakuwa tayari kuungana na UKAWA ili uwe mstari wa Mbele kumfanyia kampeni mhombea wa ukawa dhidi ya serikali dhalimu ya ccm?
 
Report inayotaja waliopta hela Mkombozi na kufungia macho wale waliopokea Stanbic.

Makes you wonder atatumika mpaka lini.

Jambo lolote chafu linalohusu Ikulu akiletewa "Ayatollah ili alipue lazima avujishe details Ikulu,matokeo yake Upinzani ulipoteza asset zote zimebaki za Lowassa tuu

List ya stanbic anaijua lakini hakuiweka kwenye report ya PAC.kuna cash 9B mmh!
 
Nimefarijika kiasi kwa alichoandika mdogo wangu Zitto. mchana nadhani hata jana nilicomment katika mojawapo ya threads zinazomhusu Zitto na ACT nikatahadharisha kuwa CCM haina urafiki katika kugawana madaraka nikimaanisha viti vya udiwani na ubunge pamoja na urais. Wataisifu ACT Kwa kuipaka mafuta kwa chupa ila wataifanyizia undava wa hali ya juu inapotokea kugombea viti.Naona somo hili limeeleweka vema.

Jambo jingine muhimu nililosoma kwa ndugu yangu ni kuwa kuna maeneo mengi ya Pwani yanahang ni vizuri wakakaza buti huko maana CUF haionekani kuweza kuyamudu yote na huko ndiko CCM ilikoatamia. Kama ACT itakwenda huko kwenye virgin lands hakuna tatizo ninaunga mkono kwa dhati na ninaamini Zitto anazo strategy za kuingia huko asaidiwe na vyama vyote .Mfano Bagamoyo ,Kisarawe,Mafia,Kilindi, mkoa wa Tanga bado kuna maeneo yanatakiwa gia mpya kuendana na tamaduni za wenyeji

Kama hoja ya pili iko hivyo ni muhimu basi ndugu zzito ukalifafanua hilo kwa kina hasa kwa Mwigamba maana ana nyongo itakayokidhoofisha chama , kwa kifupi idea ya Samson ni kupambana na UKAWA akidhani CCM ni rafiki. Kaa na Samson hata hotelini umfunze na aandike notes ili akisahau asome.

Mbowe alipokuwa Kigoma aliahidi kushirikiana na chama chochote lengo kuitoa CCM madarakani na alitaja ACT kama chama mojawapo, naamini alimaanisha hivyo. Nikiwa mpenzi wa mageuzi nakushauri shirikiana na UKAWA muingie makubaliano waiachie ACT maeneo kadhaa huu mwaka CCM isizidi 50% ya wabunge kazi hii ni ngumu ila ni rahisi mkishirikiana. Ikitokea UKAWA wameweka mgombea na ACT basi jimbo litakwenda CCM na si UKAWA wala ACT jifunzeni serekali za mitaa huko Kigoma.

unapaswa kujua kuwa jimbo utakalogombea litakuwa na vita kubwa maana CCM hawakutaki bungeni.Maescrow watatoa hela zao zote ili ushindwe uchaguzi. Na kama una bifu na wapinzani wenzio nao wataingiza nguvu kubwa alimradi ashinde hata fisadi wa CCM . ni vizuri ukawa makini katika kuzungumzia nia ya kugombea kwenye majimbo maana utakapoweka hadharani mapema strategy dhidi yako zitaanza mapema pia

Mwisho hichi ulichoandika hapa kama ni kweli Zitto Kabwe kiko poa kiwe moyoni si mdomoni maana watu watagundua tu. Kiweke vizuri kisha kitupe kwenye gazeti. Kwa ujumbe huu CCM wataanza vita rasmi maana wamejua hudanganyiki jiandae kwa vita ya CCM kuanzia sasa
 
SEHEMU YA TANO

AZIMIO LA ARUSHA

Kwa hiyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika Community Centre ya Arusha , inaazimia ifuatavyo:-

A. VIONGOZI

1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au kikabaila.

2. Asiwe na hisa katika makampuni yoyote.

3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.

4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi

5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.

6. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama
vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya34 Kiserikali. Viongozi kutokana na kifungu cho chote cha Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki
kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe).

zitto naona analeta dhihaka kuhusu azimio la Arusha
 
6. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya34 Kiserikali. Viongozi kutokana na kifungu cho chote cha Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe).

zitto naona analeta dhihaka kuhusu azimio la Arusha
Kweli mkuu analeta dhihaka ya dhahiri
 
Zitto kete pekee muliyobaki nayo ni hicho chama chenu kujiunga na UKAWA nje ya hapo hakika hatutawatofautisha na ccm, haiwezekani leo wapinzani tumeungana halafu kaibuke kachama kakugawa kura zetu halafu tukachekee, vita yetu itakua ni UKAWA v/s CCM+ACT, hamuwez kututoa nje ya mstari sahh
Tutafia ukawa, wahuni hawa hatuwataki hata UKAWA wakafie mbali
 
Tuambie ni kwanini uliizinisha mwanasheria wenu wa awali afukuzwe na kupewa Msando?pili ni kwanini unahitaji kugombea ubunge tena kwa wamu ya 3,ni kipi ambacho hujakifanya unataka ukifanye awamu hii,ama bungeni umesahau nini?4,kwanini usijenge chama chenu kama mwenyekiti ukaachana na ubunge?5 na mwisho,unafikiri mimi mwanaKigoma wa Kibondo nitajivuniaje umaarufu wako?umezisaidiaje wilaya za Kakonko,Kibondo na Buhigwe?
 
Kwanini hujawahi ishambulia CCM bali serikali yake?na je unalizishwa na utendaji.kazi wa Jk?mbona hujawahi mshambulia yeye kama rais?
 
Zitto, niko tayari kumwamini Shetani kuliko kukuamini wewe. Ni kijana msomi lakini ni hatari katika jamii inayotafuta ukombozi wa kweli. Watanzania tumenyonywa na kufanyiwa mambo machafu sana na CCM, tunapigana usiku na mchana ili kuindoa CCM madarakani lakini wewe umekubali kutumika na CCM ili kupunguza nguvu za watanzania katika kutafuta uhuru wao wa kweli. Shetani anaweza kusamehewa dhambi na akaingia peponi lakini si wewe.

Hivi kweli unajisikiaje ulipowasaliti watanzania hasa wana Chadema katika uchaguzi mkuu uliopita wa 2010 kwa kuisadia CCM kupata ushindi wa wizi?. Bila haya wala aibu ukaanzisha chama ndani ya chama kwa lengo la kupunguza nguvu ya upinzani, hivi kweli wewe bwana mdogo unajisikiaje?.

Muda mwingi nimekuwa nikimuuliza Mungu kwanini ulizaliwa?. Mimi ni muislamu, lakini naona naweza kuishi nyumba moja na nguruwe kuliko wewe.
 
Mkuu Zitto hiki chama kimesajiliwa kama ACT Tanzania hii ACT Wazalendo imetoka wapi, au ni chama tofauti?

Lakini pia ninaomba utupe tofauti ya kiongozi mkuu wa chama na mwenyekiti wa chama, majukumu yako ni yapi ukitofautisha na yale ya mwenyekiti.

Pia ulisikika ukiri kwamba wewe ni mwanzilishi wa chama ukiwa bado chadema, huoni huu ni usaliti na uhaini?

Namimi Pia nikitaka kujua hili .......all of the sudden ....ni ACT TANZANIA au ACT WAZALENDO ???

Hili la kutuhumiwa usaliti Nadhani Mrema Ndio alikuwa akituhumiwa na Kina Mtikila na wengine ...., sijawahi kusikia propaganda Za Chadema kuwa chama cha mashushushu wa BOT...Kwani nilikuwa sijui Kama BoT ni MAJASUSI ...Zaidi najuwa kuna ma Analyst wa Uchumi tu...
Ila ni ukweli kuwa Chadema ni chama kilichoasisiwa na watu waliiotofautiana sera na Mwalimu ...Edwin Mtei .,Bob Makani Nyanga ,Brown Ngwilulupi ,Weid Mwasakafyuka...etc

Labda Kama lengo ilikua kuonesha kuwa Chadema nao washawahi kutuhumiwa usaliti ...
 
Zitto, niko tayari kumwamini Shetani kuliko kukuamini wewe. Ni kijana msomi lakini ni hatari katika jamii inayotafuta ukombozi wa kweli. Watanzania tumenyonywa na kufanyiwa mambo machafu sana na CCM, tunapigana usiku na mchana ili kuindoa CCM madarakani lakini wewe umekubali kutumika na CCM ili kupunguza nguvu za watanzania katika kutafuta uhuru wao wa kweli. Shetani anaweza kusamehewa dhambi na akaingia peponi lakini si wewe.

Hivi kweli unajisikiaje ulipowasaliti watanzania hasa wana Chadema katika uchaguzi mkuu uliopita wa 2010 kwa kuisadia CCM kupata ushindi wa wizi?. Bila haya wala aibu ukaanzisha chama ndani ya chama kwa lengo la kupunguza nguvu ya upinzani, hivi kweli wewe bwana mdogo unajisikiaje?.

Muda mwingi nimekuwa nikimuuliza Mungu kwanini ulizaliwa?. Mimi ni muislamu, lakini naona naweza kuishi nyumba moja na nguruwe kuliko wewe.

Ufipani hakukaliki,mpaka sasa hamjalala ,kweli Zito ni mwiba mkali
 
SEHEMU YA TANO

AZIMIO LA ARUSHA

Kwa hiyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika Community Centre ya Arusha , inaazimia ifuatavyo:-

A. VIONGOZI

1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au kikabaila.

2. Asiwe na hisa katika makampuni yoyote.

3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.

4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi

5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.

6. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama
vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya34 Kiserikali. Viongozi kutokana na kifungu cho chote cha Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki
kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe).

zitto naona analeta dhihaka kuhusu azimio la Arusha

Nimemsoma hapa Azimio la Arusha linatumika vibaya kwa watu wanaotaka kuwatia maskini MATUMAINI ....mnaleta utani na Azimio ..watu mna share kwenye makampuni ..hata mkisema non profit ...,mna nyumba Zaidi ya Moja .., mnahodhi Zaidi ya Moja Za NSSF ..sijui mmeuziwa hamsemi ...mna hadi Vitalu Vya Madini sijui gas ...tunajua dhamani ya kitalu hutokana na Geological survey ..it can be Billions ..in a 25 acres area ya kitalu ..huwezi kuniambia eti kitalu bei yake 25 million
Watu mna Magari ya kifahari .......na mnaishi kwa majivuno..., nashangaa bwana mdogo Kama Albattle anaweza VIPi kuwa Mjamaaa .....na ile Magari ya kifahari ....ma estate mengine...sitaki kusema Kama kapataje ...ila hapa tunaongelea kuishi kijamaa ...

Nakumbuka Mjamaa wa Kweli hata kama ni tajiri hakai na ziada ....faida yake hutumia kwenye Jamii ...,Ndio maana misingi ya tajiri kwenye Ujamaa ni kugawana na maskini kwa Kulipa Kodi kubwa ...Kama mfumo wa Kodi si mzuri basi utaona CSR zake ...ni kubwa kabisa ..na Maisha yake Huwa humble
 
Duh, watu mna maswali magumu.

In fact Ujamaa wa Nyerere hautekelezeki kwa uhalisia wa sasa wa dunia. It's too radical a step, labda wameamua kwenda kwa hatua.

Ingawa nisingependa wafike kwenye Ujamaa wa Nyerere, kwani kuna mambo mle yalikuwa ni makosa flani, na yeye mwenyewe Nyerere alikiri kuwa alifanya makosa, hakuna haja ya kurudia makosa wakati tumekuwa na miaka 50 ya kuyasoma mafundisho na practice ya ujamaa wa nyerere.Hata uchina alikojifunzia Nyerere na Cuba wamefanya updates za ujamaa wao.

Kabisa Mwalimu kabla ya kufariki Alisema kuwa Angepata muda wa kurudisha wasaa nyuma kuna mambo ambayo hangeyafanya ...ESP utaifishaji wa baadhi ya sekta..akitokea mfano mashamba mengi makubwa yalikufa ESP Kuanguka kwa Uchumi wa Tanga ..na maeneo yaliyotegemea ukulima mkubwa ..hakupendezwa na utekelezaji wa vitu Kama operesheni Maduka na vijiji etc

Mimi ni MFUASI wa Ujamaa wa Mwalimu lakini nitamuamini mtu Leo akasema anatunga sera Zenye kufuata baadhi ya misingi ya Azimio la Arusha ...mtu akiniambia anafuata Azimio la Arusha persie ....namuona ni Muongo ...na anadharau watu na pengine anataka kudanganya wasiojua ambao Ndio wengi...mass support .

Hata wafuasi wa Mwalimu Kama Warioba wanapoongelea Azimio la Arusha ..huongelea baadhi tu ya misingi Kama MAADILI YA VIONGOZI Na sio 100 %
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom