Hapana cheza kabisa na jamiiforums, humu kila mtu ana first class, ndio maana wakina Makamba wanahangaika usiku na mchana kuifungia, humu ni hoja juu ya hoja hakuna kuangalia mtu usoni ni nondo tu.
Tunachohitaji ni kila mmoja kumlenga adui ili kumshinda. Tulishindwa kufanya kazi ndani ya moja, tunaweza kufanya kazi tukiwa majirani. Adui bado ni yule yule.
Mmejipanga nani agombee Urais mwaka huu?
Au ni kweli kua mnamuwekea nafasi Lowassa kama akitoswa CCM?
Alinda asante kwa kusema hili na pia kina mtu Anaitwa Mwl. Kaijage naye alikuja na thread yenye kusema ACT waibomoa ngome ya CHADEMA na leo hii Zitto anasema wamekuja kuongeza nguvu ya upinzani..... Hatuelewi....Ndugu yangu Zitto , acha kutufanya watanzania wote wajinga na hatuoni mnachokifanya au hatusikii mnayoyaongea,
Ni juzi tu hapa Mwigamba kiongozi wa ACT alisema ACT itahakikisha inaifuta CUF Pwani sasa niambie je lengo la Mwigamba ni nini??
Ni majuzi tu hapa ulisema kuwa Ukawa ni wasaka tonge je lengo lako lilikuwa nini?
Ni lini wapi viongozi wa vyama vya upinzani umeishambulia ACT?
nmpongeze MH ZITTO kwa kuja JF na kujibu hoja na duku duku
Mh. hapa.kidogo umeniacha tenge. Ni kweli kuwa unaamini katika utengano na si katika umoja? Maana kupambana na adui mkiwa wamoja ni sawa na kumuattack kwa kombora ambalo laweza kumsambaratisha kuliko kupambana naye kwa kila mmoja akirusha risasi yake kivyake.... what if risasi utakayoitupa wewe ikaishia kuparuza manyoya ya mkiani na ya jirani ikaishia kumjeruhi kucha.... ushindi utakuwepo kweli?
Saa nyingine ninawiwa kuamini kuwa umefanikiwa kupandikiza na kuimwagilia mbegu ya kilimo cha 'Divide and Rule' katika shamba la mfumo wa vyama vingi Tanzania.
Tatizo kuna vyama vya upinzani wabinafsi sana mfano.chadema na ndio maana UKAWA itavunjikamwezi wa nane maana Chadema wana lazimisha kutoa Rais..na chadema hawataki kuungana na chama cha wazalendo ACT chini ya Dr Zitto kabwe kijana makini.
Maelezo na malengo mazuri. Kauli yako hata hivyo ni tofauti na maandiko ya Mwl Kaijage hapartment JF! Pengine anza kwa kumwelimisha makusudio haya ya chama.fikirikwanza
Siasa ni mapambano. Siwezi kuacha mapambano. Sijawahi fanya usaliti wowote. kuitana majina hayo hakusaidii lolote zaidi ya kufurahisha ego zetu tu. ACT Wazalendo ina shabaha moja tu nayo ni kupambana na mfumo wa uchumi unaonyonya watanzania. Ku surrender mapambano hayo ndio usaliti. Tutaendelea kupambana
Zitto,
Chama chako kimejipambanua na Unyerere (Nyerereism) na kufuata misingi ya Azimio la Arusha ambao unaamini mgawanyo wa haki katika raslimali za taifa na pia unaruhusu umiliki wa mali kama nyumba,biashara n.k.
Je, unawezaje kufuata ujamaa wa kidemokrasia wakati huohuo ukijipambanua na Nyerereism ambayo msingi wake ni Ujamaa wa Kikomunisti usioamini katika umiliki wa mali kama nyumba zaidi ya moja na kumiliki biashara ukiwa Kiongozi wa umma?
Sasa tunanze na kifungu kimoja kimoja, maana naposoma Azimio la Arusha linasema hivi:-Kwa muda mrefu na hasa siku za hivi za karibuni kumekuwa na threads nyingi sana humu ndani kuhusu Zitto na kuhusu Chama cha ACT Wazalendo. Kumekuwa na tuhuma kwamba chama cha ACT Wazalendo kinashambulia vyama vingine vya upinzani hapa nchini. Napenda kusema mambo machache sana
Chama cha ACT Wazalendo ni chama cha siasa chenye mrengo wa kushoto na kinajitanabaisha na siasa ya Ujamaa iliyoasisiwa na Azimio la Arusha. Lengo letu ni kueneza siasa zetu zenye mrengo huo.