Tutaweka ilani yetu kwenye tovuti ndani ya siku chache
Shukrani,nitasupport chama chenye ilani ya kumuondolea mzigo mwananchi na kukipigia kampeni sehemu yeyote endapo kitaondoa kodi kero zisizokuwa na kichwa wala miguu kama kitashika madaraka.
Kodi Kero hizo ni:-
1.Service Charges za Umeme za kila mwezi,Kulipa EWURA na REA.
2.Kulipia Road License(TLB) kila mwaka na hapo hapo unakatwa fedha ya kuchangia barabara ukinunua mafuta,hapo hapo serikali imeshapata kodi kwenye hayo mafuta.
3.Kulipia Fire Extinguisher kuanzia Sh 10,00/= na kuendelea inategemea na cc ya gari bila kupewa mtungi huo uliolipia.
4.Bima ya Gari ipunguzwe hii Third Party ni Kubwa Mno.
5.Kuwe na Limit ya Kuchangia Kodi kwa mtu kama ilivyo USA,Ukilipa kodi ikazidi kiwango unarudishiwa ile iliyozidi,Huku kwetu Unakatwa PAYE,Unakatwa VAT(indirect) hapo hapo ukiagiza kitu nje hakuna unafuhu hata kidogo yaani mmachinga asiyelipa kodi na mfanyakazi anayekatwa PAYE kila mwezi wakiagiza magari wote wanakatwa kodi sawa wakati mfanyakazi ameshachangiaa PAYE nyingi na hana msamaha wowote.
N.B Serikali ina vyanzo vingi vya mapato kutoka kwenye mali asili(Misitu,Bahari,Madini,Gesi),Sisemi kwamba serikali isikusanye kodi kwa mwananchi la hasha bali iondoe kodi kero.