Ufalme upi huo akipoteza?
Mfalme wa dunia kwa sasa ni marekani,
Dunia nzima tunatumia pesa ya marekani kuuza na kununua
Marekani inaweza kuziamuru chochote nchi nyingi duniani na zikafuata, zikiwemo nchi kubwa za dunia ya pili, Brazil, India, Pakistan, Nchi za ulaya mashariki, hizi za Africa ndio usiongee
Marekani ndio nchi pekee inaweza kumuwekea vikwazo mtu au taifa lolote, hata tunavyozungumza hapa Russia iko Chini ya vikwazo vya marekani na anabembeleza viondolewe
Kwa taarifa zilizopo, kulingana na maelezo ya wachunguzi na wafuatiliaji wa mambo ya kijeshi bado Kuna gap la kitechnologia kati ya marekani na Russia Ingawa gap hilo linapungua siku hadi siku, kwa maneno mengine America bado iko mbali ya Russia kijeshi, warusi hawajakataa ila wanafanya jitihada kuifikia marekani, unless kama unasoma taarifa za upande mmoja zinazokupotosha
Mgogoro mmoja tu wa Syria hauwezi kulifanya taifa likaitwa supper power, na bado mgogoro wenyewe ni mbichi na haujapata mshindi kwa maana ya ufumbuzi wa kisiasa, na bado marekani ina plan nyingi
Marekani ataendelea kuwa Mfalme wa dunia kwa Muda mrefu akitawala sekta ya fedha na mifumo yote ya kifedha duniani, ndio maana Iran hata sasa analalamika kuwa wamarekani hawajamuingiza kwenye financial system ya dunia hivyo anapata taabu kuuza na kununua
Russia na China ni global powers lakini sio supper powers, hawajakidhi vigezo vya kuitwa hivyo, in fact Hali ya uchumi wa Russia ni mbaya, hili ni jambo ambalo wengi hatulijui, ndio maana anaingizwa mwishoni kama G8, wenzie wote wale saba G7 wanamzidi utajiri
Silaha
Silaha anayotengeneza mrusi ni kawaida kabisa kwa mataifa makubwa, haina maana wenzio hawatengenezi, Defense magazine kila siku inaeleza air defenses mbali mbali ikiwemo hizo portable za ku ku drop sehemu flan, hakuna ambacho mrusi anatengeneza marekani hatengenezi
Hata media yenye propaganda kuliko zote Russia inakubali kupitia makala zake mbali mbali kuwa America iko mbele ya Russia isipokua Russia inafanya kazi kubwa kuliziba hilo gap
Bahati mbaya Sana wengi mnauchukulia mgogoro wa Syria pekee kama kigezo, mgogoro ambao unabadilika sura kila kukicha and is far from over, mnasahau marekani ambae katika hii miaka kumi iliyopita amewaondoa madarakani kwa nguvu wababe wa dunia waliiogopwa kote saddam hussein, muamar Gaddafi, utawala wa taliban, na kununua Osama bin laden, na anaweza kumuondoa yoyote anaeleta ujeuri
Russia hajafika huko,
Kwa mujibu wa takwimu za kijeshi America ana ndege za kivita 13,400 Russia ana 3,000 na China 2,000
Hapo hatujaenda kwenye ubora
Itachukua miaka mingi au mwisho wa dunia kwa urusi kuwa Mfalme wa dunia hii