Kama US kiteknolojia yupo mbali basi abuni defence system ambayo itakuwa within us soil na iwe na uwezo wa kuzuia makombora yasiingie kwenye anga yake kama mrusi anavyofanya mbona anaangaika kuweka mitambo dunia nzima kujilinda?
Swali zuri sana - hajiamini kijeshi, makeke tu na majivuno ya kitoto, mitambo yake ya kisasa ya kuongozea missiles anayojivunia kwenye media mbona ilizimwa na ndege za jeshi la anga la Urusi kama tunavyo zima TV zetu sebuleni kwa kutumia remote control!!
Si Urusi tu hata Korea kasikazini juzi juzi hapa ilifanikiwa kuparaganya mawimbi ya GPS yanayo tumiwa na jeshi la Marekani na washirika wake kuongozea ndege na smart bombs, meli za kivita na makobola yake vyote hivyo vilikuwa karibu na pwani ya Korea na anga la Korea Kasikazini/mpakani.
Kitu cha kujiuliza hapa hivi nchi kama Korea inavuruga masuala yote muhimu ya kieletroniki ya jeshi la Marekani mpaka wanashindwa kujikwamua leo hii ndio watake kuwatunia misuli Warusi!! - wanamdanganya nani? Wataishia kuwalazimisha wanajeshi wa Ulaya kufanya mazoezi ya mara kwa mara mipakani mwa Urusi lakini hawatathubutu kujaribu ku confront jeshi la Urusi na mifano tunayo to prove a point: Walifanya nini Urusi ilipo rudisha Crimea kwenye himaya yake, je, jeshi la anga la Urusi lilipoingia Syria kwa kushtukiza na kuanza kufanya vitu vyake vya uhakika Marekani walifanya nini si wamekaa kimya mpaka sasa - si wanajiona wao zaidi kijeshi Duniani kwa nini hawaja liondoa kwa kinguvu jeshi la anga la Urusi ambalo bado lipo nchini Syria linaondoka in phases baada ya kutekeleza plan zao walio jiwekea ku degrade kwa kiwango kikubwa uwezo wa kundi hatarishi la ISIS, Dunia gotta lot 2 thank Putin 4 taking a bold step kumaliza nguvu za kikundi hiki hatarishi.
Haya ni baadhi ya masuala muhimu ambayo some members hawataki kujiuliza kwa nini Urusi ikihamua kuchukua hatua kali wakati usalama Taifa lake unapotishiwa anachuka hatua bila ya kuomba kibari kutoka
Taifa lolote, katika kukua kwangu sijawahi kusikia/soma popote kwamba Marekani iliwahi kuvurumusha Urusi kijeshi/kibabe hawana ubavu wa kufanya kosa hilo wanaishia kulalama tu na kukazania vikwazo vya kiuchumi.
Chunga sana Taifa ambalo halizungumzi sana kumbuka matendo uzumgumza zaidi kuliko majigambo, tumeyaona Syria.