Mkuu kwa ufupi tu ni kuwa najua nachokisema, ukweli ndio huo
Hivi kweli ndugu masunga Kuna mtu mwenye akili timamu anae weza kukataa kuwa marekani sio baba wa dunia kwa maana ya super power, ukiona mtu anabisha hilo kimbia kabisa usihangaike hata kubishana nae
Naikubali sana Russia, kama global power anae rise kwa kasi, lakini bado ana safari ndefu hasa kwenye uchumi, in fact China anamfukuzia America kwa karibu sana, uchumi na biashara, biashara kati ya China na mabara mengine ikiwemo America ni ya kiwango cha kuogopesha, currency ya China inaitisha dollar kwa sasa Ingawa bado lakini ni tishio
China inafahamu kuwa na military might pekee hakuwezi kufanya ukawa super power, unahitaji kwanza kuvunja American financial superiority in the world, hii ni pamoja na kuivunja dominance ya dollar katika international trade, pia kuivunja dominance ya America katika banking system,
Nadhan unafahamu kuwa mfumo wa kibenki wa kimataifa umekua dominated na marekani na washirika wake na wameu integret na system zao, mabenki ya kimagharibi ndio yanatumika sana kwenye international trade
Ndio maana ukiwekewa vikwazo na hawa mabwana wa magharibi mabenki karibu yote duniani yana apply hivyo vikwazo dhidi yako, jina la nchi yako au lako lina ingizwa kwenye system ya bank zote, hakuna unachoweza kufanya iwe kuagiza au kuuza bidhaa
Naomba kama huniamini huende bank hata leo ujifanye unataka kulipia mzigo wako ambao umeununua online uone utajibiwa nini, cashier we are sorry sir haturuhusiwi kufanya transaction kwenda nchi hiyo, na ukienda bank zote utajibiwa hivyo, bank ikikaidi vikwazo vya marekani ikigundulika inakua imejiua,
That is what it takes to be a super power au mfalme wa dunia, unashikilia vitu vyote muhimu duniani, uchumi, military, sports, science, njia za mawasiliano,karibia wote duniani ikiwemo watu wa Russia na China tunatumia yahoo, instagram, tweeter, Facebook, vyote hivyo ni vya kimarekani
Itachukua miaka mingi sana even life time kwa marekani kunyanganywa ufalme wa dunia
Kwa habari ya silaha wote tunajua marekani yako mbele ya kila mmoja duniani, Ingawa gap la capabilities limebaki dogo kati ya marekani na Russia lakini militarily ni gap muhimu sana, na Russia anakimbizana na Muda kuliziba kabisa gap hilo lakini sio rahisi kwa sababu za kifedha, ni ngumu sana Russia ambae defense budget yake + ile ya China kwa pamoja hazijaifikia defense budget ya marekani
Na hiyo budget ya marekani sehemu kubwa inaenda kwenye utengenezaji wa silaha na program za silaha kwa ujumla, hii ni pamoja na ndege mpya za kisasa, maintenance ya old aircraft, kuzi mordenise meli za kivita na kuziwekea mifumo ya kisasa, pamoja na program za uzinzi anti missile-defense system zisiweze kushambuliwa na ballistic missiles, sehemu ya pesa hizi pia huwekwa kwenye program za kusaidia majeshi washirika hasa majirani wa Russia ambao marekani ameweka kambi huko akiizunguka Russia kwenye mipaka yote, Estonia, Lithuania, Latvia, Slovenia, Finland, Poland, maldova, etc
Kwa uwepo wa majeshi ya marekani katika nchi zote hizo zinazoinguka Russia ni sawa na kusema marekani imeizingira Russia pande zote that's why Russia iko desperate na suala hilo
Mwisho
Najua kuwa vijana wengi humu wana mihemko na kukaririshwa au kulishwa sumu either na wenzao humu humu ndani au ni wasomaji wazuri wa sputniknews.com, na hivyo kupata habari za kijeshi za upande mmoja unbalanced na ambazo zimetokana na opinion za waandishi au experts ambao ni pro Russians
Pamoja na kufuatilia Russian media nashauri wafuatilie pia media za upande mwingine kuweza ku balance ufahamu wao