Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
message distortion.tunaenda kwenye vita
message distortion.tunaenda kwenye vita
Pengine damu ya waliuwawa hajapendezewa nayo pia hana la kufanya sababu ya system tu inamtaka afuate aendelee kuwemo au akatae atoke nimemsikia mwishoni na ameonesha kuna kitu kinamuumiza kwenye nafsi yake...Nape leo anaonekana mpole kweli
kwa akili za ushabiki wa kichama ni lazima useme hivyo. R.I.P CCM
peace is not the absence of conflicts, but it is the ability to solve conflicts in peaceful way.
message distortion.
Raia ama mwananchi yeyote katika nchi huru yenye kufuata utawala wa sheria anao wajibu wa kutimiza katika kulilinda na kuliendeleza Taifa hili.,haitoshi kwa mtu kunadi kuwa sikumuua kwa kuwa sikushika bunduki kumuua lakini ni lazima kupima na kufikiri zaidi juu ya kauli tunazotoa zinazopelekea watu wetu kufa.
Kimsingi ni kuwa Chadema wanatamani madaraka na wanatumia njia zozote wanazofikiria zitawawezesha kufika ikulu, hata ikiwa njia hizo ni za kuharibu na kutoa uhai wa watu wetu. Amani ya nchi hii ni kitu kikubwa kuliko U-CCM na U-CHADEMA
Huyo JUJU Ni mtu toka DRC? mbona kiswahili yake mbovumbovu?
Swali kwa Nape:
Kama waziri mkuu ameweza kutoa amri kwamba ma- rc na ma- dc lazima wafanye kazi za CCM maeneo wanayoyaongoza. Je, ni sababu zipi zinakufanya utuaminishe kwamba hatoi maagizo ya polisi kuhujumu shughuli za vyama vya upinzani ikiwepo mikutano ya siasa?
Nakubaliana na Mnyika Tatizo ni Raisi Dhaifu... huyu ndie asababishae yote... Nape hivi haya yote yanatokea sababu ya kuacha kwa makusudi mali za nchizinachezewa na kuchukuliwa wapeni wananchi maisha bora hakuna atakaye fungua mdomo na kulalamika haki itolewe kwa wakatiAhsante Star TV kututambua wana JF na JF yenyewe kwa ujumla.
Amani inavunjwa na hii katiba mbovu tuliyonayo, inampa madaraka makubwa rais wa nchi ambaye kila idara yeye ndo anateua wakuu wake.
Kutoka waziri wa mambo ya ndani, msajili wa vyama, IGP, RPC awote ni wateule wa rais, hata iweje watamtumikia kwa chochote atakachosema juu ya maslahi ya chama chao.
Polisi haiwezi kuwa huru katika mfumo huu wa katiba hii mbovu, tubadirishe huu mfumo wa wateule wa rais kila idara, hapo jeshi litakuwa huru na kuepuka kutekeleza amri za chama tawala
Kauli hii ya tunaenda kwenye vita ya tundu lissu ina maana gani..?
Ni kuwa wamejiandaa kwa hili..? Wamejiandaa na kupima madhara yatakayotokana na hilo...!
Watu hawa ni lazima kuwa nao makini sana...!
aisee hongera kwa kuwa kada mwaminifu wa CCM, lazima uwaze hivyo kwa akili za uccm na ushabiki. Pole sana ila chamsingi Lissu kakujibu.
Nape amefafanua sawa juu ya mgawanyo baina ya serikali na Chama, utendaji na mgawanyo wa majukumu, hakuna katika utaratibu ambao wengine wanaufikiria kuwepo kuwa unatoa fursa na upenyo kwa chama tawala kuwabana wapinzani kwa kutoa direct order kwa wakuu wa polisi, utaratibu huu unafuatwa...!
Hiyo kauli ni Onyo kwani mwanzo wa vita huanzia kwa mambo yanayotokana na hali tunayoelekea unamchezea Lissu wewe jamaa kichwa kaona mbali...Civil war ni noma kuna nchi zilianza hivi polisi waliuwawa hadi majumbani mwao vita ya ndani ni noma... inafikia hadi wakuu wa dini ukimsogelea anakutolea silaha na ukizidi anakuua... tuombe amnani vita ni sooo polisi waache ujinga wao then wanaficha siri ya muuaji kwa kiini macho hakuna aliyeshtakiwa paleKauli hii ya tunaenda kwenye vita ya tundu lissu ina maana gani..?
Ni kuwa wamejiandaa kwa hili..? Wamejiandaa na kupima madhara yatakayotokana na hilo...!
Watu hawa ni lazima kuwa nao makini sana...!
Nakubaliana na Mnyika Tatizo ni Raisi Dhaifu... huyu ndie asababishae yote... Nape hivi haya yote yanatokea sababu ya kuacha kwa makusudi mali za nchizinachezewa na kuchukuliwa wapeni wananchi maisha bora hakuna atakaye fungua mdomo na kulalamika haki itolewe kwa wakati
Swali kwa Nape
Kwanini iwe dhambi kwa CDM Nyololo na iwe Haki kwa CCM BUBUBU?
CHADEMA wanakosoa kiwango cha elimu cha askari na wanaponda uelewa wao juu ya sheria na mitazamo ya kiutawala,katika hili wanajijengea uadui katika kufanya hili na wajue kuwa hata wakiingia madarakani watalindwa na jeshi gani ikiwa wao hawana mnasaba mzuri na jeshi.
Polisi tangu awali walialikwa lkn hawakutokea; bilashaka walistuka, wangeumbuliwa..