On STAR TV: Ipi misingi ya Amani? Sehemu ya Pili

Nape boresheni makaz ya polisi wenu bana, pengine itasaidia kuwapunguzia msongo wa mawazo na kwa hiyo wataacha kutulipua na mabomu.
 
Neno amani lisitumike kupumbaza na na kutotolewa mahataji na haki za msingi za raia wa nchi hii, maana siku hizi imeonekana raia (makundi ya kijamii) yakidai haki zao wanahatarisha amani. Kama haki za msingi za kiraia zinapatikana bila ubabaishaji wowote ndio amani yenyewe sio nadharia tu.

Kiufupi kwa tulipofikia amani siwezi kusema ipo kw raia hawapati haki zao za msingi licha ya kulipa kodi zao ili wazipate haki hizo.
 
Raia ama mwananchi yeyote katika nchi huru yenye kufuata utawala wa sheria anao wajibu wa kutimiza katika kulilinda na kuliendeleza Taifa hili.,haitoshi kwa mtu kunadi kuwa sikumuua kwa kuwa sikushika bunduki kumuua lakini ni lazima kupima na kufikiri zaidi juu ya kauli tunazotoa zinazopelekea watu wetu kufa.

Kimsingi ni kuwa Chadema wanatamani madaraka na wanatumia njia zozote wanazofikiria zitawawezesha kufika ikulu, hata ikiwa njia hizo ni za kuharibu na kutoa uhai wa watu wetu. Amani ya nchi hii ni kitu kikubwa kuliko U-CCM na U-CHADEMA
Aisee, siamini kama wewe unaitakia mema nchi yetu, kauli yako imejaa uzandiki kama si uzabizabina.
 
amani kwa CCM si chochote kwani wao kikubwa ni kukilinda chama chao kiendelee kutawala kwa gharama yoyote ile huku wakiwataka wengine kuzitii sheria zao za kimabavu............... hatutaki tena.
 
Watu wengi ni hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu na wanadhani wanaweza kufanya lolote wakati wowote bila kuzingatia sheria, utawala wala mamlaka iliyo juu yao, wakadhani kuwa wanayoyafikria wao ni sahihi na bora kuliko mawazo na fikra za wengine wote wasio wao.

CHADEMA leo wao wanageuka kuwa ni viongozi-malaika wanachofanya chochote kwao ni sahihi na kila anayewaambia wanakosea ni mkosaji. Wanapambana na kila yule ambaye anawaza tofauti na wao.

HII NI HATARI.
 
Chama Cha Mapinduzi kinaendesha serikali yake kwa mifumo mibovu katika sekta mbalimbali na ni wazi sasa kuwa uwajibikaji sio jambo la muhimu kwao..Watendao makosa wanalindwa kwa maslahi ya nani?
 
Star TV mlitumia vigezo gani kumualika mtu dhaifu kama Juju Danda katika mjadala mhimu kama huu?
 
Kudadeki hichi kipindi nimekikuta mwishoni yani ndio naamka Mbona sijawaona Polisi kama waalikwa maana wao ndio wadau haswa wa Amani
 
no way, police can't prove their innocence following the reality of the global media which displays clearly their actions,; and
they cant be away from CCM who have been overwhelming their power
 
Ahsante Star TV kututambua wana JF na JF yenyewe kwa ujumla.

Amani inavunjwa na hii katiba mbovu tuliyonayo, inampa madaraka makubwa rais wa nchi ambaye kila idara yeye ndo anateua wakuu wake.

Kutoka waziri wa mambo ya ndani, msajili wa vyama, IGP, RPC awote ni wateule wa rais, hata iweje watamtumikia kwa chochote atakachosema juu ya maslahi ya chama chao.

Polisi haiwezi kuwa huru katika mfumo huu wa katiba hii mbovu, tubadirishe huu mfumo wa wateule wa rais kila idara, hapo jeshi litakuwa huru na kuepuka kutekeleza amri za chama tawala
 
watu wengi hatar sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu na wanadhani wanaweza kufanya lolote wakati wowote bila kuzingatia sheria, utawala wala mamlaka iliyo juu yao. wakadhan kuwa wanayoyafikria wao ni sahihi na bora kuliko mawazo na fikra za wengine wote wasio wao. CHADEMA leo wao wanageuka kuwa ni viongozi-malaika wanachofanya chochote kwao ni sahihi na kila anayewaambia wanakosea ni mkosaji. Wanapambana na kila yule.
huna jipya
 
misingi ya amani ni kuzilinda na kuziheshimu haki za raia na si kutumia vyombo vya dora kuzihujumu haki hizo..........
 
Watu wengi ni hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu na wanadhani wanaweza kufanya lolote wakati wowote bila kuzingatia sheria, utawala wala mamlaka iliyo juu yao, wakadhani kuwa wanayoyafikria wao ni sahihi na bora kuliko mawazo na fikra za wengine wote wasio wao.

CHADEMA leo wao wanageuka kuwa ni viongozi-malaika wanachofanya chochote kwao ni sahihi na kila anayewaambia wanakosea ni mkosaji. Wanapambana na kila yule ambaye anawaza tofauti na wao.

HII NI HATARI.
kwa akili za ushabiki wa kichama ni lazima useme hivyo. R.I.P CCM
 
Kauli hii ya tunaenda kwenye vita ya tundu lissu ina maana gani..?
Ni kuwa wamejiandaa kwa hili..? Wamejiandaa na kupima madhara yatakayotokana na hilo...!

Watu hawa ni lazima kuwa nao makini sana...!
 
Kudadeki hichi kipindi nimekikuta mwishoni yani ndio naamka Mbona sijawaona Polisi kama waalikwa maana wao ndio wadau haswa wa Amani
Polisi tangu awali walialikwa lkn hawakutokea; bilashaka walistuka, wangeumbuliwa..
 
the horse,

mimi nahisi wewe ndio waleeeeee CCM damu, mliotulia mali za babu zetu, baba zetu na sasa mnataka kujilimbikizia hata za watoto wetu wajao!!

acha unafiki, unaelewa precisely kuwa Lisu kamaanisha nini, usitake kutuuliza maswali yasiyo na majibu ili tukujibu.

hili ni jibu kwako "the horse"
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom