On STAR TV: Ipi misingi ya Amani? Sehemu ya Pili

Raia ama mwananchi yeyote katika nchi huru yenye kufuata utawala wa sheria anao wajibu wa kutimiza katika kulilinda na kuliendeleza Taifa hili.,haitoshi kwa mtu kunadi kuwa sikumuua kwa kuwa sikushika bunduki kumuua lakini ni lazima kupima na kufikiri zaidi juu ya kauli tunazotoa zinazopelekea watu wetu kufa.

Kimsingi ni kuwa Chadema wanatamani madaraka na wanatumia njia zozote wanazofikiria zitawawezesha kufika ikulu, hata ikiwa njia hizo ni za kuharibu na kutoa uhai wa watu wetu. Amani ya nchi hii ni kitu kikubwa kuliko U-CCM na U-CHADEMA

aisee hongera kwa kuwa kada mwaminifu wa CCM, lazima uwaze hivyo kwa akili za uccm na ushabiki. Pole sana ila chamsingi Lissu kakujibu.
 
Swali kwa Nape:

Kama waziri mkuu ameweza kutoa amri kwamba ma- rc na ma- dc lazima wafanye kazi za CCM maeneo wanayoyaongoza. Je, ni sababu zipi zinakufanya utuaminishe kwamba hatoi maagizo ya polisi kuhujumu shughuli za vyama vya upinzani ikiwepo mikutano ya siasa?

Na hao hao ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama huko mikoani/wilayani!
 
Ahsante Star TV kututambua wana JF na JF yenyewe kwa ujumla.

Amani inavunjwa na hii katiba mbovu tuliyonayo, inampa madaraka makubwa rais wa nchi ambaye kila idara yeye ndo anateua wakuu wake.

Kutoka waziri wa mambo ya ndani, msajili wa vyama, IGP, RPC awote ni wateule wa rais, hata iweje watamtumikia kwa chochote atakachosema juu ya maslahi ya chama chao.

Polisi haiwezi kuwa huru katika mfumo huu wa katiba hii mbovu, tubadirishe huu mfumo wa wateule wa rais kila idara, hapo jeshi litakuwa huru na kuepuka kutekeleza amri za chama tawala
Nakubaliana na Mnyika Tatizo ni Raisi Dhaifu... huyu ndie asababishae yote... Nape hivi haya yote yanatokea sababu ya kuacha kwa makusudi mali za nchizinachezewa na kuchukuliwa wapeni wananchi maisha bora hakuna atakaye fungua mdomo na kulalamika haki itolewe kwa wakati
 
Nadhani kuanzia kwenye Mafunzo ya Kijeshi kun dosari kubwa sana...bado jeshi letu (huwa nasita sana kuliita jeshi letu) maana hasa ni jeshi lao...wanafundwa kwa mbinu za kizamani za kikoloni,,,yaani wao wanaamini katika ukoloni ni mabavu na akili kidogo sana...
 
Nataka kumwambia Nape kua amani aijengwi kwa misingi ya uwoga.serekali iache kututisha huku wakijua ndio wana ijenga amani,amani inajengwa kwa msingi wakua tunaitaji amini na sio vinginevo.
 
Kauli hii ya tunaenda kwenye vita ya tundu lissu ina maana gani..?
Ni kuwa wamejiandaa kwa hili..? Wamejiandaa na kupima madhara yatakayotokana na hilo...!

Watu hawa ni lazima kuwa nao makini sana...!

mmetumbua mimacho, mmetega masikio kuvizia maneno magumu kwenu na kwa wasio na uwezo wa kupambanua kwa haraka ili mfungulie maporomoko ya propaganda, unataka kutuambia kama si vita ni nini kiliwakilisha mazingira ya kuuwawa kwa mwangosi kule iringa, limetumika BOMU kuua, bomu ni silaha ya kivita, ene wei unaonekana akili yako imebakwa, unashauriwa usibadili nguo wala kuoga ili ushahidi wa kubakwa uufikishe polisi.
 
aisee hongera kwa kuwa kada mwaminifu wa CCM, lazima uwaze hivyo kwa akili za uccm na ushabiki. Pole sana ila chamsingi Lissu kakujibu.

Huyu "the horse" amani umeshaambiwa hatuna....tuna utulivu tu... mbona huelewi?????????????
na kama chedma wanataka madaraka tu, mbona nyinyi mpo tangu zama za kale lakini hamtaki kutoka wakati hamjafanya lolote zaidi ya kutuibia? absolutely nothing for ccm,,,,,,
 
Nape amefafanua sawa juu ya mgawanyo baina ya serikali na Chama, utendaji na mgawanyo wa majukumu, hakuna katika utaratibu ambao wengine wanaufikiria kuwepo kuwa unatoa fursa na upenyo kwa chama tawala kuwabana wapinzani kwa kutoa direct order kwa wakuu wa polisi, utaratibu huu unafuatwa...!

kwani unamawazo tofauti na hayo?
 
Kauli hii ya tunaenda kwenye vita ya tundu lissu ina maana gani..?
Ni kuwa wamejiandaa kwa hili..? Wamejiandaa na kupima madhara yatakayotokana na hilo...!

Watu hawa ni lazima kuwa nao makini sana...!
Hiyo kauli ni Onyo kwani mwanzo wa vita huanzia kwa mambo yanayotokana na hali tunayoelekea unamchezea Lissu wewe jamaa kichwa kaona mbali...Civil war ni noma kuna nchi zilianza hivi polisi waliuwawa hadi majumbani mwao vita ya ndani ni noma... inafikia hadi wakuu wa dini ukimsogelea anakutolea silaha na ukizidi anakuua... tuombe amnani vita ni sooo polisi waache ujinga wao then wanaficha siri ya muuaji kwa kiini macho hakuna aliyeshtakiwa pale
 
Nakubaliana na Mnyika Tatizo ni Raisi Dhaifu... huyu ndie asababishae yote... Nape hivi haya yote yanatokea sababu ya kuacha kwa makusudi mali za nchizinachezewa na kuchukuliwa wapeni wananchi maisha bora hakuna atakaye fungua mdomo na kulalamika haki itolewe kwa wakati

kweli raisi ni dhaifu, ccm ni dhaifu, lakini wako sharp kuhamishia mali za wananchi nje ya nchi
 
CHADEMA wanakosoa kiwango cha elimu cha askari na wanaponda uelewa wao juu ya sheria na mitazamo ya kiutawala,katika hili wanajijengea uadui katika kufanya hili na wajue kuwa hata wakiingia madarakani watalindwa na jeshi gani ikiwa wao hawana mnasaba mzuri na jeshi.

acha ukada'
 
Polisi tangu awali walialikwa lkn hawakutokea; bilashaka walistuka, wangeumbuliwa..

Pengine wamejishitakia na kesi ipo mahakamani so wameona wasiingilie mihimili ya Dora mwenzao majaji wa T. Lissu...

Asante sana T.Lissu kwa kusaidia mahakama zetu zije kuwa na watu vichwa na sio vlaza kama wa sasa hivi watu wakapige shule sio ubabaishaji kwenye mambo yanayoweza kuhatarisha Amani... hujunu zilikuwa za ajabu ajabu na zinachukua muda mrefu sana
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom