On STAR TV: Ipi misingi ya Amani? Sehemu ya Pili

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Habari za J2?

Wadau karibuni katika sehemu ya pili na ya mwisho ya mjadala wetu tukija na njia ya nini cha kufanya kudumisha Amani yetu.

Tujitahidi kutorejea Yale tuliyouliza last week ( https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ipi-misingi-ya-kuendeleza-amani-tanzania.html ) nimeyajumuisha yote ktk utangulizi na tumeanzia hapo

Wageni wote wa wiki iliyopita wapo:

  • Mh. Tundu Lisu
  • Nape Nnauye
  • Juju Danda
Na Mwanza tuna mchambuzi mahiri Donald Kasongi

Karibuni
 
Mkuu,

Ni ukweli usiopingika kuwa polisi ndio wanaovunja Amani, kwa shinikizo la wanasiasa... amani ikitaka kubaki jeshi la polisi libadilike liwe la kisasa.
 
Naomba bwana Nape atupe maoni yake kuhusu - vurugu na mauaji ya Zanzibar 2001 ambayo watu waliuwawa kule Pemba, Mabomu aliyokuwa anapigwa Mrema miaka ya 2005 ambayo jeshi la polisi walikuwa wanawanyamazisha nguvu ya Mrema na Pia kauli ya IGP Mahita alipowaambia CUF kuwa kama wao Ngangari pilisi ni Ngunguri na taarifa ya polisi kuwa wameingiza visu nhini... hii ilikuwa kuashiria mapambano na CUF ambayo wakati huo kilikuwa chama cha upinzani chenye nguvu; na sasa tunaona harakati za polisi kwa CHADENA na hatujaona Serikali ikikemea hali hiyo.
 
Habari studio.

Namna pekee ya kudumisha amani ni kuhakikisha haki inatekelezwa kwa usawa, leo amani inaanza kutetereka kwa sababu ya double standard, huyu akifanya hivi ni sawa lakini mwingine akitaka kufanya hichohicho anakatazwa na zinatumika nguvu kubwa kumdhibiti na hata mauaji.

Amani ya nchi hii inahatarishwa na hofu ya chama tawala kudhani kuwa kikitoa uhuru kwa vyama vingine kufanya siasa kwa uhuru vyama hivyo vitaimarika kama ilivyo sasa na mwisho kitaondolewa madarakani.

Hakuna kitakachoinusuru CCM kung'olewa madarakani kama ilivyokuwa kwa UNIP, KANU na wenzao wengi. Watende haki na ikibidi wakabidhi nchi kwa amani.

MIMI - MFEREJI MARINGO - MTWARA
 
Amani ni tunda la haki! Na ikiwa haki inakwenda na wajibu, inakuwaje vyombo vya dola ndivyo vinaongoza kwa kukiuka haki za kiraia? Je kwa kufanya hivyo amani tunayojivunia itaendelea kuwepo?
 
Yahya,

Amani ni tunu, hujengwa nasi wananchi pasipo kujijali, kujali nini utapata, kujali ubinafsi. Bali amani yapaswa kuhusisha nafsi ya mmoja kumtakia amani mwenzake na hata kutengeneza misingi ya kumuweka mwananchi mwenzake katika amani pasipo kujua anaihitaji leo ama kesho ama sasa hivi.

Amani pia inaweza kujengeka pale tu kuwapo na rika la usawa katika hali za kiujumla kiuchumi, baina ya tabaka na tabaka. Pengo kubwa baina ya matabaka ndio chimbuko mojawapo la kutoimarisha amani na kuiona ikiporomoka na kuiwia ugumu jamii kuiimarisha.

Mpevu.
 
Hata Nape akikataa, ukweli ni kwamba CCM wanatawala kwa mabavu kwa kutumia dola!
 
Amani itakuja siku ambapo jeshi la polisi litaweka wazi job description zake na nini haki ya raia mbele ya polisi na vice-versa

Ni suala la elimu ya uraia tu. Na vyombo vya habari vina sehemu kubwa sana juu ya hili
 
Tanzania hatuna amani bali tuna utulivu na ili kurejesha amani inabidi serikali iondoe matabaka ya kuwalinda walio nacho kwa kutoa fursa sawa kwa kila Mtanzania ktk nyanja zote za kimaisha na mikutano ya vyama vya siasa ipewe kipaumbele km vle chama tawala kinavyofanyiwa badala ya polisi kutumia nguvu kuwatawanya waandamanaji .
 
Jeshi la polisi limekuwa na kauli mbiu ya utii wa sheria bila shurti katika dhana nzima ya kutunza amani.

Lakini imethibitika kwamba mara zote polisi wamekuwa chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani nchini.

Je, ni namna gani jeshi la polisi na lenyewe linatii sheria bila shurti katika kudumisha amani? Nani anatakiwa kulisimamia litii sheria?
 
Tanzania hakuna amani bali kuna utulivu wa wananchi kutojuwa haki zao...

Hakuna amani kama mwananchi hapati dawa hospitali, shuleni hakuna elimu bora na yenye tija, wakulima wa pamba wanadhulumiwa pamba yao, wakulima wa korosho wapunjwa bei ya korosho yao kuliko bei inayouzwa katika super markets, wakulima wa mahindi wanazuiwa kuuza mahindi yao nje, wananchi wanauwawa kila siku kwenye migodi na serikali imekaa kimya; watu wanateswa (mfano wa Dr. Ulimboka) na serikali haichukui hatuwa, tunaona watoto wa viongozi wakubwa wanavyotanua na kuwa watawala wadogo!

KATIKA HALI KAMA HII HUWEZI KUWA NA AMANI WAKATI SERIKALI HAITIMIZI WAJIBU WAKE
 
Mkuu,

Ni ukweli usiopingika kuwa polisi ndio wanaovunja Amani, kwa shinikizo la wanasiasa... amani ikitaka kubaki jeshi la polisi libadilike liwe la kisasa.

Tatizo lililopo jeshini ni kile kitendo cha maofisa wa ngazi za juu kuanzia makamishina, file zao kuhifadhiwa magogoni. Kwa kitendo hiki kinawafanya watumike kisiasa kwa kumini kuwa bosi atawajali na kdumisha madaraka yao.

Hata kwa maofisa walioko chini, wanajitahidi kuweka kumbu za utendaji wao, waonekane mbele ya bosi na wateule wake ni kwa jinsi waliisaidia CCM. Hiki ndicho kinachochangia uvunjifu wa aman.
 
Kuna haja ya kuwa na ugawaji ulio sawa wa demokrasia kwa makundi yote katika jamii.

Inapotokea kundi moja linapendelewa zaidi, upande wa pili huona kuwa wameonewa na hapo ndipo hutokea kupotea kwa amani. Inahitajika iwepo tofauti dhahiri ya kiutendaji kati ya Chama kama mtoaji wa malengo na Serikali kama mtekelezaji kwa kuzingatia taratiibu zilizopo.

Kwa ujumla inatakiwa kuwepo na fair ground kwa makundi yote katika jamii
 
Habari ya Yahya M,

Naomba umuulize Nape CCM na Serikali yake imejifunza kutokana na maandamano yasiyo na taarifa wala kibali ya waumini wa kiislamu kwenda wizara ya mambo ndani ambayo yaliisha kwa amani bila damu kumwagika.

Naomba lisijidaliwe katika mtizamo wa kidini bali kama uhusiano kati ya wananchi wasio na silaha na askari wetu.
 
Misingi ya amani Tanzania ni pamoja na kupata elimu ya uraia ili tujitambue, katiba ya nchi ifahamike kwa wananchi.

Haki ya kupata na kutumia maliasili za nchi bila kubaguana kwa dini ukabila na maeneo ndani ya nchi yetu.
Haki ya kutumia huduma za jamii kama elimu afya ulinzi kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vya siasa.

Zaidi ya yote kusiwepo na pengo kubwa kati ya walionacho na wasionacho. Hapo tutadumu na amani yetu.
 
Nape atuambie ni Kwanini RPC wa Iringa asiwajibishwe Kwa kushindwa kuzuia kifo cha Mwangosi wakati alikuwepo wakati akipigwa na hatimaye kulipuliwa Kwa bomu. Wakati alikuwa akimjua na hata baadhi ya waandishi walimuomba amsaidie Mwangosi
 
Hakuna Amani bila Haki. Taasisi zote zitimize wajibu wake.

Vyama vya siasa vitimize wajibu wa kupeleka elimu kwa wananchi na polisi watimize wajibu wa kulinda raia.
 
There is a very thin membrine btn political part ccm and the government in force. tundulisu kazi sana kutofautisha kati ya selikari na chama.
 
Naomba Nape anijibu swala moja tuu, yeye anasema hana uwezo wa kuwaamuru Mawaziri wala mkuu wa mkoa au RPS, Mkuu wa Wilaya kwa sababu mawasiliano kati ya chama na dola hufanywa kati ya chama na serikali hufanywa kupitia waziri mkuu, sasa Nape aseme kwenye simu yake namba alizo nazo za mawaziri na watendaji wengine woote huwa anawasiliana nao kwa ajili ya mambo ya kijamii tuu?

Nasema hivyo kwa sababu ninauhakika kuwa huwa anawasiliana nao akiwapa ORDER kama boss wao. Si kweli kuwa mara zote huwasiliana nao ili wakutane kwenye nyama choma au sherehe za kijamii tuu.... kwani akitaka kumuuliza waziri Nchimbi swala la kiutendaji huanzakumpigia waziri mkuu kwanza?
 

Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom