On Magufuli na Odinga: CHADEMA wapo sawa!

On Magufuli na Odinga: CHADEMA wapo sawa!

MOds Unganisha hii thread na hii hapa iliyotolewa Desemba,7 .Uzuri mkutano wa ODM/CORD ulirushwa Live na Citizen,Nationtv na Magufuli alitoa mbwembwe nyingi sana, na MC alimtambulisha kama muwakilishi wa CCM na siyo Serikali na ndiyo maana mimi nikiweka mada hiyo.
[h=2]CCM ya Muunga Mkono Raila Odinga Urais Kenya ,Yawakilishwa na Magufuli Mkutano wa Uteuzi[/h]
 
Uvivu wa kufikiri, magufuli hakwenda kuiwakilisha CCM wala serikali, ameenda Kama mtu binafsi Huyu wenje Hana la kuongea tamko limekaa kimajungu majungu, yeye ndiye anatakiwa kuthibitisha iwapo magufuli alisema anaiwakilisha CCM au serikali. CHADEMA wa jipange kushughulika na issues waachane na individuals vinginevyo wanapoteza mwelekeo kwa sasa na kuchezeshwa Kama Joyce wowo sindimba ya CCM
Wewe ni mngonjwa kweli hujui kuwa Maghufuli ni waziri wa serikali ya Tanzania tamko la Maghufuli ni tamko la serikali kama sio CCM athari zake ni kubwa, hebu fikiria endapo Serikali ya Kenya ikachukuliwa na Uhuru Kenyeta je Tanzania tutaficha wapi soni zetu, ua unataka kujenga uadui na jirani zetu???

Mwaka jana Naibu Waziri wa Maendeleo wa Ujerumeni alikuja Tanzania,alichofanya yule waziri mhuni akakutana na wahuni wenzake na kufanya nao kikao hotel moja marangu kilimanjaro baada ya hapo ndio akataka kuonana na Serikali Membe aka mwambia uishie huko huko Chadema! hoja hapa Chadema mwaka huu ndio wametambua protocol za kidiplomasia? Hapa kelele zote ni unafiki tu wa kujikweza,kama hoja ni Magufuli kugombanisha Tanzania na Serikali ya Kenya mbona wao walimleta Naibu Waziri wa Ujerumani Kinyemela,hawakujua kuwa wanaigombanisha Ujerumani na Tanzania? Chadema ulimbukeni na Uchanga wa kisiasa unawasumbua! Afrika hatu hitaji vyama vya Kikabila matatizo ndio kama haya!

Kwahiyo huko hotelini alikuwa akiifanyia CDM kampeni ya uchaguzi upi?? hapa tunaongelea suala la Waziri wa Tanzania kupanda kwenye jukwaa na kumpigia debe mgombea wa nchi nyingine. Hapo lazima ukubali kuwa kuna maswali mengi magumu yanayohitaji majibu sahihi na sio utetezi huu wa kitoto
 
Kuhusu Kenyatta na Ruto siyo kweli kwamba waliiwakilisha serikali yao. Walikuja katika kutafuta kuungwa mkono kwenye alliance yao (na usisahau Ruto hana cheo chochote serikalini. Yeye ni mbunge tu). Kwa nini kidiplomasia isiwe nzuri CCM wanapoenda nje lakini wao wakialika iwe nzuri? Wakati wa Bakili Muluzi CCM walimpeleka Kapteni John Komba na TOT yake kumpigia debe kwa hiyo CCM kusupport mgombea siyo kitu cha ajabu. Hao CDM wenyewe wanasema wana uhusiano na Conservative mbona watu hawajasema hiyo siyo nzuri kidiplomasia? Nachotaka kusema CDM waache kuingia kwenye siasa za maji taka za CCM. CCM kuchafuana na kuitana majina ni tabia yao.

Hapo kwenye red; kama kweli ndilo lilikuwa lengo la safari yao (kuungwa mkono na SERIKALI YA KIGENI) hilo ni kosa kubwa na serikali yetu kama ILIUNGA MKONO itakuwa imefanya kosa kubwa. Si ajabu Odinga na ODM wana haki ya kutafuta upande wa kuwaunga mkono kutoka TZ baada ya kuona wapinzani wao wanaungwa mkono na serikali yetu.

Hii peke yake inaanza kuleta msuguano baina ya nchi jirani; imagine Odinga akishinda uchaguzi itakuwaje? EA Community itakuwa imefikia mwisho. Au baada ya serikali na CCM kuona wamebugi step kuwaunga mkono akina Ruto wakaona wa-neutralize kwa kumtuma Magufuli kwa Odinga? May be this is the case.

Hapo kwenye
navy; kila nchi ina sheria na taratibu zake. Si ajabu Malawi na kwingineko wanasiasa au viongozi wa kiserikali kutafuta au kutoa support za kisiasa wanasiasa wa kigeni inaruhusiwa; japo ni nchi chache mno zinaweza kuwa na utaratibu huo.

Kumbuka Komba sio kiongozi wa kiserikali zaidi ya kuwa "mpiga filimbi" wa CCM ambaye walimtumia kum-support rafiki yao Bakili Muluzi. Hata kwa hili dogo (la Komba na TOT) baada ya Muluzi kuondoka madarakani, je, unaona matokeo yake? Kinachoendelea hapo Ziwa Nyasa nadhani wote tunakifahamu; kwa nini tusiamini kina uhusiano na mambo haya ya kuingilia siasa za ng'ambo?

Hata Marekani inapotaka kuingilia siasa za kigeni hutafuta "kuungwa mkono" na jamii ya kimataifa kabla ya kufanya hivyo; sisi tunaingia kichwa kichwa na "umasikini" wetu.

ALL in ALL, sio sahihi sisi kutuma au kualika VIONGOZI WA KISERIKALI kwenda au kutoka ng'ambo kwa ajili ya masuala ya kisiasa na hasa inapokuwa ni siasa za majukwaani. Imagine umwone Kagame au Museveni jukwaani akimnadi mgombea wa CCM. Hii ni hatari!
 
Ambacho mnashindwa kuelewa ni kuwa Magufuli na Odinga ni marafiki sana ambapo sasa wamekuwa kama ndugu, hata kama magufuli ni waziri wa JMT je akienda kumfanyia kampeni Odinga yeye binafsi, kipi kibaya ? acheni fitna zenu cdm na habari tulizo nazo ni kuwa kile chama rafiki cha kwenu kenya ndicho ambacho kimeonyesha wazi kuwa kinashindwa,kwa hiyo aibu yao itakuwa yenu pia. Nendeni mkajipange upya hakuna cha maana kwenye thread yako zaidi ya wivu wa kike

- Tunaishi kwa kuongozwa na Sheria za Jamhuri, Magufuli ni Waziri Masaa 24/7, kwenda kwake kwenye kampeni za siasa za Taiafa lingine kunatakiwa kutolewa maelezo ya kina na Chama chake in this case CCM, angeuliwa akiwa huko unafikiri ni familia yake tu ndio ingehitaji maelezo kutoka Serikali ya Kenya? Au Taifa zima la Tanzania lingehitaji maelezo?

- Mengine muwe mnatumia akili kidogo tu kuliko Uchama kipofu na ishu kama hizi ndio sometimes zinakuwa ni abuse of power!!

Es!
 
FEMES kweli umekomaa kisiasa siku hizi, siamini kama wewe ndo umeileta hii issue hapa- few years back this would have been impossible!. Ndugu zangu wanazi wa CDM tujifunze kitu kwa huyu bwana hapa, sio kila siku mnaleta habari za kusifia chama chenu tu hadi mmeifanya JF ionekane kama ni ya CDM wakati we all know kwamba that is not the case.

- Unajua I thank God kwamba nina msimamo so huwa sisumbuliwi na hizi, wewe unasema Few Years back na wengine wamesema Few Years back nilikuwa Chadema, unaona the contradiction? Ndio maana huwa siawasikilizi sana ninasimama na what I stand for, in this case kama hakuna maelezo ya kutosha kutoka kwetu CCM, automatically inakuwa ni Abuse of power nitamtafuta Kinana mimi mwenyewe on this!

Es!
 
Mwaka jana Naibu Waziri wa Maendeleo wa Ujerumeni alikuja Tanzania,alichofanya yule waziri mhuni akakutana na wahuni wenzake na kufanya nao kikao hotel moja marangu kilimanjaro baada ya hapo ndio akataka kuonana na Serikali Membe aka mwambia uishie huko huko Chadema! hoja hapa Chadema mwaka huu ndio wametambua protocol za kidiplomasia? Hapa kelele zote ni unafiki tu wa kujikweza,kama hoja ni Magufuli kugombanisha Tanzania na Serikali ya Kenya mbona wao walimleta Naibu Waziri wa Ujerumani Kinyemela,hawakujua kuwa wanaigombanisha Ujerumani na Tanzania? Chadema ulimbukeni na Uchanga wa kisiasa unawasumbua! Afrika hatu hitaji vyama vya Kikabila matatizo ndio kama haya!

Kimantiki mwanzoni nilidhani viongozi wa kisiasa na kiserikali kuonana kikazi na wenzao wa nje si tataizo bali tatizo ni kushiriki katika kampeni za kisiasa za nchi nyingine wakati wa uchaguzi tena kwa uwazi.

serikali nyingi na vyama vya kisiasa vingi vina wagombea wanaowaunga mkono nje ya nchi lakini si kwa uwazi bali kisirisiri.
 
Lakini pia tuvuke mipaka zaidi tusiangalie kisiasa tu lakini pia tuangalie kijasusi!!!!!!!!!!!

Kama Taarifa za kijasusi zinaonyesha kuwa Tanzania itakuwa salama chini ya Odinga ni sahihi kwa serikali yetu kuwa na mgombea tunayemuunga mkono katika uchaguzi wa Kenya. Tatizo ni ujasusi huo kutumia mbinu za wazi kwenye kampeni za siasa za Kenya.
 
- Kiboko cha nani? Taifa tunawalipa kutusaidia CCM na this is one of their responsibility, unamsifia mtu kwa kufanya wajibu wake?

Es!

Kwa hiyo msha jiharalisha kuwa ni watawala wa nchi hii siyo??

Tatizo lenu nyie watoto wa vigogo mnafikiri CCM itatawala milele na ndiyo maana wazazi wenu wako busy kuwalithisha vyeo.................. Yana MWISHO haya................... Tafuteni ushauri kwa KABURU South, maana walikuwa na mawazo kama yenu!!!
 
MOds Unganisha hii thread na hii hapa iliyotolewa Desemba,7 .Uzuri mkutano wa ODM/CORD ulirushwa Live na Citizen,Nationtv na Magufuli alitoa mbwembwe nyingi sana, na MC alimtambulisha kama muwakilishi wa CCM na siyo Serikali na ndiyo maana mimi nikiweka mada hiyo.
[h=2]CCM ya Muunga Mkono Raila Odinga Urais Kenya ,Yawakilishwa na Magufuli Mkutano wa Uteuzi[/h]
nashukuru kwa ufafanuzi mkuu.kwa hiyo ccm ipo upande wa raila odinga!
Nape njoo utupe ukweli basi!
 
Sikonge.. uhusiano wetu Tanzania utakuwaje ikitokea hawa wanaoambiwa kwamba hawawezi kusafiri nje ya nchi wakashinda na Magufuli akaendelea kuwa waziri katika Tanzania?
Huoni kwamba itakuwa ni jambo la ajabu na aibu na la kuhatarisha mahusiano yetu mema ya kimataifa ndani ya EA... Mfano wake ni Obama na Netanyahu na sasa Netanyahu aona aibu zake kumsogelea Obama ukizingatia kwamba alim- support Romney...inafaa hawa akina Magufuli na wengineo kama yule wa Zimbabwe wawe neutral full stop !

Endapo ni kweli Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau alimuunga mkono Romney dhidi ya Obama na baadaye Obama aliposhinda wameendelea kushirikiana basi hii inaonyesha kuwa wenzetu wamekomaa nimesikia Netanyau akimpongeza Obama kwa kumuunga mkono katika suala la Wapalestina. Lakini pia tuliwahi kushuhudia katika uchaguzi wa kwanza na wa mbili aliyekuwa waziri wa Mambo za nje wa Marekani Collin Poweri (republican) akimuunga mkono Obama wa chama cha Demokratic
 
Ruto na Kenyatta walionana na Rais Kikwete Ikulu katika ziara ya kiserikali kwa niaba ya serikali yao na hawakusimama majukwaani kwenye kampeni tofauti na alichofanya Magufuli. Mkuu hapo huoni tofauti?

Kwa habari ya wawakilishi kutoka DRC, Angola, China, n.k. kusimama kwenye kampeni za CCM sina hakika kama walikuwa viongozi wa kiserikali kutoka kwenye nchi zao zaidi ya kuwa viongozi wa kisiasa. Sidhani kwenye hoja iliyoko mezani angeenda Nape au Kinana ingekuwa issue sana japo pia kidiplomasia sio nzuri.

HATA HIVYO, kama hao wa kutoka DRC, Angola, China wangekuwa viongozi wa kiserikali kama ilivyo kwa Magufuli hii ndiyo hoja ya msingi wanayohoji CHADEMA na mleta mada - UNAHITAJIKA UFAFANUZI - KATUMWA NA NANI? Hili ndilo la msingi.
Hili swala kama hawataki kujibu kwa utaratibu naona CDM kupitia wabunge wake akiwamo Mhe Wenje walipeleke swala hili bungeni majibu yatapatikana hukohuko!!!!

Hapo kwenye red; kama kweli ndilo lilikuwa lengo la safari yao (kuungwa mkono na SERIKALI YA KIGENI) hilo ni kosa kubwa na serikali yetu kama ILIUNGA MKONO itakuwa imefanya kosa kubwa. Si ajabu Odinga na ODM wana haki ya kutafuta upande wa kuwaunga mkono kutoka TZ baada ya kuona wapinzani wao wanaungwa mkono na serikali yetu.

Hii peke yake inaanza kuleta msuguano baina ya nchi jirani; imagine Odinga akishinda uchaguzi itakuwaje? EA Community itakuwa imefikia mwisho. Au baada ya serikali na CCM kuona wamebugi step kuwaunga mkono akina Ruto wakaona wa-neutralize kwa kumtuma Magufuli kwa Odinga? May be this is the case.

Hapo kwenye
navy; kila nchi ina sheria na taratibu zake. Si ajabu Malawi na kwingineko wanasiasa au viongozi wa kiserikali kutafuta au kutoa support za kisiasa wanasiasa wa kigeni inaruhusiwa; japo ni nchi chache mno zinaweza kuwa na utaratibu huo.

Kumbuka Komba sio kiongozi wa kiserikali zaidi ya kuwa "mpiga filimbi" wa CCM ambaye walimtumia kum-support rafiki yao Bakili Muluzi. Hata kwa hili dogo (la Komba na TOT) baada ya Muluzi kuondoka madarakani, je, unaona matokeo yake?Kinachoendelea hapo Ziwa Nyasa nadhani wote tunakifahamu; kwa nini tusiamini kina uhusiano na mambo haya ya kuingilia siasa za ng'ambo?

Hata Marekani inapotaka kuingilia siasa za kigeni hutafuta "kuungwa mkono" na jamii ya kimataifa kabla ya kufanya hivyo; sisi tunaingia kichwa kichwa na "umasikini" wetu.

ALL in ALL, sio sahihi sisi kutuma au kualika VIONGOZI WA KISERIKALI kwenda au kutoka ng'ambo kwa ajili ya masuala ya kisiasa na hasa inapokuwa ni siasa za majukwaani. Imagine umwone Kagame au Museveni jukwaani akimnadi mgombea wa CCM. Hii ni hatari!

Hii point yako ya mwisho nakubaliana na wewe kabisa. Sasa nini cha kufanya, ni kwamba inatakiwa wabunge watunge sheria kali dhidi ya chama chochote kitakachofanya hivyo. Lakini kuanza kuwashambulia watu selectively sidhani kama ni sahihi. Kwa sababu watu wa pande zote upinzani na chama tawala wamekuwa wakijinasibu sana na washirika wao wa nje.
 
Mkuu,
Tanzania under CCM ki-vitendo hakuna mipaka ya uongozi ndiyo maana siyo ajabu hata wananchi wasio makini wanashindwa kutofautisha kati ya utendaji wa vyama na serikali.

CCM wangeweza kutofautisha hilo ingewasaidia sana, haya mambo ya chama kushindwa kukemea watumishi wa serikali wanaoboronga ndio inawaharibia. Kama chama kingekuwa kinaisimamia serikali kingeweza kujitenga na kashfa nyingi za ufisadi maana umetokea serikalini lakini kutetea makada wake kunakigharimu na hakiwezi kujitenga na uchafu huo.
 
kq1.jpg

kq4.jpg
 
Back
Top Bottom