On Magufuli na Odinga: CHADEMA wapo sawa!

Apr 27, 2006
26,588
10,374
- Nimeona Mkurugenzi wa CHADEMA leo akidai maelezo kuhusiana na safari ya hivi karibuni ya Waziri wa CCM Magufuli huko Kenya na kuhusika na mikutano ya kampeni za Urais huko,

- Now kwenye hilo this time CHADEMA wapo on the right side of the coin, CCM itoe maelezo ya kina as to how and why Magufuli didi that, kwa sababu ieleweke kwamba Waziri wa Jamhuri anakuwa On Duty 24 hours akiwakilisha Jamhuri sasa alikwenda huko kuwakilisha Jamhuri au CCM?

- Ni muhimu Serikali ya CCM ikatoa maelezo sasa kabla haijageuka kuwa a big deal ni ishu ndogo sana ila ikiachwa itageuka kuwa kubwa na kutuumiza CCM, so CCM let's get the facts out now!

Es!
Mwananchi - Dec 13 said:
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kueleza kama msimamo alioutoa katika kampeni za Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga ni wa Serikali au wake.

Chama hicho kimesema kuwa msimamo alioutoa Magufuli wa kuunga mkono Chama cha ODM ni hatari kwa Tanzania hasa katika uhusiano na nchi hiyo na ni kinyume na mkataba wa kimataifa wa Rome.

Pia kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kueleza kama alimtuma Magufuli katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika Desemba 7 mwaka huu, uwanja wa Kasarani na kusema Watanzania wanaunga mkono ODM au la.

Msimamo huo wa Chadema ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa chama hicho, Ezekieah Wenje.

"Hatujui kama Magufuli alikwenda Kenya kama Serikali au alikuwa amekwenda kama rafiki. Hilo linatupa wasiwasi kwa kuwa hotuba yake ilionekana kama ametumwa na Serikali," alisema Wenje na kuongeza;

"Alichukua upande katika siasa za Kenya, alimsifia sana Odinga kwamba Tanzania wanampenda wakati kuna mikataba ya kimataifa inayokataza nchi nyingine kuingilia siasa za nchi nyingine kama ilivyoelezwa kwenye Rome Statute."

Wenje alisema kutokana na hilo ambalo Magufuli amefanya itakuwa mbaya kama mgombea wa chama kingine atashinda nchini Kenya kwa kuwa imeshajionyesha kuwa Tanzania inamuunga mkono Odinga.

"Waziri kuchukua upande kwenye siasa za Kenya ni hatari kwa taifa letu na Watanzania wanaishi nchini Kenya.

Itakuwa ni matatizo kwao na hata machafuko yakitokea Tanzania inaweza kuonekana ni chanzo," alisema Wenje.

Alisema ni muhimu Rais Kikwete akaeleza umma kama alimtuma Magufuli Kenya au la ili ujumbe alioutoa ujulikane ni wa nani kwa sababu kama alichokisema ni msimamo wa Serikali basi alitumwa na Rais Kikwete.

Alisema ni muhimu ikajulikana alitumwa na nani kwani taarifa ambazo Chadema inazo ni kwamba CCM hawakualikwa kwenye mkutano huo."Kama Kenyatta(Uhuru) akishinda humuoni kama italeta shida hapo baadaye? alihoji Wenje.

Alisema ni muhimu Serikali ikajua kwamba Rais wa Kenya atachaguliwa na Wakenya wenyewe na si vinginevyo.

Magufuli alipotafutwa kuzungumzia suala hilo hakupatikana kwa simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe ili atoe ufafanuzi hakujibu chochote.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, baada ya simu yake ya mkononi kutoita na taarifa zilizopatikana baadaye kutoka kwa mwandishi wake msaidizi, Irene Bwire, zilieleza kuwa alikuwa kwenye kikao cha baraza la Mawaziri.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape aling'aka akitaka waulizwe ODM ili waeleze walimwalika Magufuli kwa wadhifa upo.

"Sikiliza siwezi kuzungumzia suala la ... kama Wenje, kwani itakuwa tunafanya majibizano, we waeleze alipopigiwa Nape alisema waulizwe ODM walimwalika nani," alisema Nnauye na kuongeza;

Desemba 7 mwaka huu, Magufuli aliungana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsavangirai kumpigia debe Odinga, huku akieleza kuwa mwasiasa huyo mkongwe nchini Kenya ndiye anayestahili kuwa Rais wa nchi hiyo.

Alisema hakuna sababu zozote za zitakazowafanya Wakenya wasimchague Odinga kwa kuwa ni mcha mungu, hivyo wanatakiwa kujua hilo.

"Nataka kuwaambia Wakenya kwamba Odinga ni mcha Mungu, mnatakiwa kujua hilo. Kama mimi ningekuwa Mkenya ningempigia Odinga kura ili aongoze nchi. Lakini siruhusiwi hata kupiga kura basi nawambia msiache kumchagua huyu atawaongozeni vizuri,"alisema Magufuli.

Magufuli alisema katika wagombea wote waliojitokeza kuwania kiti cha urais nchini Kenya, hakuna anayemfikia Odinga na hiyo inaonyesha kuwa wakimchagua atawasaidia bila ubaguzi.

  • Mkurugenzi wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa EZEKIEL WENJE

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia CHADEMA kimeitaka Serikali kutolea ufafanuzi suala la WazirI wa ujenzi Dr. John Magufuli kuhudhuria Sherehe za kutambulishwa kwa mgombea urais chama cha ODM Kenya Raila Odinga endapo suala hilo lina uhusiano wowote wa Kiserikali.

Mkurugenzi wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Ezekiel Wenje amesema kitendo cha waziri huyo kuhudhuria sherehe za kutambulishwa wa Raila kinatoa picha mbaya ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Kenya iliyopo Madarakani kutokana na ushirikiano wa muda mrefu kati ya serikali hizo.

kwenye sentensi nyingine Wenje amesema Magufuli kupanda jukwaani kuanza kumnadi kiongozi wa ODM ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za kimataifa ambapo amedai kwa mujibu wa kanuni za Umoja wa mataifa ni kosa kubwa Taifa moja kuingilia siasa za Taifa jingine hata kama hayo mataifa yanaushirikiano wowote.
 
Mie nafikiri Magufuli kafanya jambo la maana kwani kashaanza kupanua mipaka ya CCM.

Ukiacha ya kufungua Matawi nje ya nchi, sasa wanaanza kuingia hadi kwenye vyama vya Siasa nje ya Tanzania maana vya Tanzania wameshamaliza kwa kupanda watu wao na hilo wote tunalielewa.

HONGERA SANA NGOSHA Magufuli.
 
Sio hili la Magufuri tu bali hata la makada wa CCM(Nape, Kinana) kuwaita watumishi wa umma kwenye mikutano ya CCM ili wajieleze wamelipata wapi? Wanatumia sheria gani? Wanatumia mamlaka ipi?
 
- Kiboko cha nani? Taifa tunawalipa kutusaidia CCM na this is one of their responsibility, unamsifia mtu kwa kufanya wajibu wake?

Es!

Mnawalipa ninyi kina nani?
Nitashangaa sana kama utakuwa unamaanisha majukumu ya serikali ndio majukumu ya CCM, tofauti na hapo sioni CCM inasaidiwa vp
 
Hapa ndipo utakajua kuwa CHADEMA ndio inayoongoza hii nchi japokuwa CCM ndio wanaotawala.
Maana hoja za Chadema siku zote zina ujumbe mzito sio kama za CCM za kizezeta.
 
Uvivu wa kufikiri, magufuli hakwenda kuiwakilisha CCM wala serikali, ameenda Kama mtu binafsi Huyu wenje Hana la kuongea tamko limekaa kimajungu majungu, yeye ndiye anatakiwa kuthibitisha iwapo magufuli alisema anaiwakilisha CCM au serikali. CHADEMA wa jipange kushughulika na issues waachane na individuals vinginevyo wanapoteza mwelekeo kwa sasa na kuchezeshwa Kama Joyce wowo sindimba ya CCM
 
hivi Nape alipowapiga mkwara watumishi wa serikali alikuwa anajiwakilisha nafsi yake? Hii ni tabia ya wanaCCM usitetee ujinga.
 
- Kiboko cha nani? Taifa tunawalipa kutusaidia CCM na this is one of their responsibility, unamsifia mtu kwa kufanya wajibu wake?

Es!

Le mutuz Kumbe na wewe unatambua wajibu wa viongozi? Kumbe CHADEMA huwa wanakuwa sahihi kutokubaliana na sofa za kijinga
 
Utashangaa CCM itakavyokuja na majibu rahisi kwenye maswali muhimu kama hili.
Kwa mfano, CCM itajibu hivi
''Magufuli hakutumwa na Serikali na wala CCM bali alikwenda yeye binafsi''
 
I cant beleive it....is it you?
Heeeee, kumbe watu wana two sides.
Still laoding...
 
Uvivu wa kufikiri, magufuli hakwenda kuiwakilisha CCM wala serikali, ameenda Kama mtu binafsi Huyu wenje Hana la kuongea tamko limekaa kimajungu majungu, yeye ndiye anatakiwa kuthibitisha iwapo magufuli alisema anaiwakilisha CCM au serikali.chadema wa jipange kushughulika na issues waachane na individuals vinginevyo wanapoteza mwelekeo kwa sasa na kuchezeshwa Kama Joyce wowo sindimba ya ccm
Mkuu PhD,
Mbona umejivua nguo? Wakati wa function ile, Magufuri alitambulishwa kama mwakilishi wa CCM.
 
Last edited by a moderator:
Uvivu wa kufikiri, magufuli hakwenda kuiwakilisha CCM wala serikali, ameenda Kama mtu binafsi Huyu wenje Hana la kuongea tamko limekaa kimajungu majungu, yeye ndiye anatakiwa kuthibitisha iwapo magufuli alisema anaiwakilisha CCM au serikali.chadema wa jipange kushughulika na issues waachane na individuals vinginevyo wanapoteza mwelekeo kwa sasa na kuchezeshwa Kama Joyce wowo sindimba ya ccm

Unata kusema Magufuli siku hiyo alikuwa likizo au me sijakuelewa?
 
  • Thanks
Reactions: PhD
Uvivu wa kufikiri, magufuli hakwenda kuiwakilisha CCM wala serikali, ameenda Kama mtu binafsi Huyu wenje Hana la kuongea tamko limekaa kimajungu majungu, yeye ndiye anatakiwa kuthibitisha iwapo magufuli alisema anaiwakilisha CCM au serikali.chadema wa jipange kushughulika na issues waachane na individuals vinginevyo wanapoteza mwelekeo kwa sasa na kuchezeshwa Kama Joyce wowo sindimba ya ccm

- Hapana CCM hapa tuna kesi ya kujibu, Magufuli amekwenda huko kwa mgongo upi? Waziri wa Jamhuri, Mjumbe wa CCM, au Mtu binafsi, CCM ni lazima ithibitishe kwamba Magufuli amekwenda huko kwa nauli yake mwenyewe, hakulipiwa na Serikali wala CCM, na kwamba akiwa huko hakulipiwa anything na Serikali yetu wala ya Kenya, na CCM ni lazima iathibitishe kwamba ni kawaida kwa safari kama hizi kwa MAwaziri wetu kwa kuonyeshwa kuwa zimewahi kufanywa na mawaziri wengine pia!

- So baada ya majibu ya haya maswali kuna mengi ya nyongeza kutokana na majibu yatakayotolewa!!

Hata wakisingizia kwamba alikwenda kwa nauli yake,je majukumu yake alimuachia nani?..............................loading.......................
 
Back
Top Bottom