On Magufuli na Odinga: CHADEMA wapo sawa!

Mnawalipa ninyi kina nani?
Nitashangaa sana kama utakuwa unamaanisha majukumu ya serikali ndio majukumu ya CCM, tofauti na hapo sioni CCM inasaidiwa vp

Mkuu,
Tanzania under CCM ki-vitendo hakuna mipaka ya uongozi ndiyo maana siyo ajabu hata wananchi wasio makini wanashindwa kutofautisha kati ya utendaji wa vyama na serikali.
 
naona watu mmemsahau magufuli
1.aliiba nyumba za serikali
2.aliwatukana wakazi masikini wa kigamboni wapige mbizi
3.aliapa kutojenga daraja kule igunga kama wataichagua chadema
4.aliambiwa aache ubabe wakati akitekeleza sheria halali akafyata mkia kwa kupenda uwaziri
5.safari za jk nje ya nchi zinajenga barabara
mburula tu huyu,..utasikia naye anataka urais
 
Hata wakisingizia kwamba alikwenda kwa nauli yake,je majukumu yake alimuachia nani?..............................loading.......................

sio mara ya kwanza kumuona magufuli kwa nikutano ya Raila nadhani wana urafiki maana hata Raila alishakuja kwa magufuli,
 
sio mara ya kwanza kumuona magufuli kwa nikutano ya Raila nadhani wana urafiki maana hata Raila alishakuja kwa magufuli,

urafiki wake unaweza kuliweka taifa matatani.tu assume odinga anaukosa urais na magifuli akaupata unadhani hali itakuwa shwari kati yetu na kenya?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
sasa kama sio kutaka kukuza jambo,Kwanini chadema wasimuulize magufuli kama alitumwa na kikwete kinyume chake wamuulize kikwete?kwani magufuli ndo msemaji wa tanzainia kimataifa?kama sio;kwa nini wadhani katumwa na serikali?
 
- Nimeona Mkurugenzi wa CHADEMA leo akidai maelezo kuhusiana na safari ya hivi karibuni ya Waziri wa CCM Magufuli huko Kenya na kuhusika na mikutano ya kampeni za Urais huko,

- Now kwenye hilo this time CHADEMA wapo on the right side of the coin, CCM itoe maelezo ya kina as to how and why Magufuli didi that, kwa sababu ieleweke kwamba Waziri wa Jamhuri anakuwa On Duty 24 hours akiwakilisha Jamhuri sasa alikwenda huko kuwakilisha Jamhuri au CCM?

- Ni muhimu Serikali ya CCM ikatoa maelezo sasa kabla haijageuka kuwa a big deal ni ishu ndogo sana ila ikiachwa itageuka kuwa kubwa na kutuumiza CCM, so CCM let's get the facts out now!

Es!

Ambacho mnashindwa kuelewa ni kuwa Magufuli na Odinga ni marafiki sana ambapo sasa wamekuwa kama ndugu, hata kama magufuli ni waziri wa JMT je akienda kumfanyia kampeni Odinga yeye binafsi, kipi kibaya ? acheni fitna zenu cdm na habari tulizo nazo ni kuwa kile chama rafiki cha kwenu kenya ndicho ambacho kimeonyesha wazi kuwa kinashindwa,kwa hiyo aibu yao itakuwa yenu pia. Nendeni mkajipange upya hakuna cha maana kwenye thread yako zaidi ya wivu wa kike
 
- Nimeona Mkurugenzi wa CHADEMA leo akidai maelezo kuhusiana na safari ya hivi karibuni ya Waziri wa CCM Magufuli huko Kenya na kuhusika na mikutano ya kampeni za Urais huko,

- Now kwenye hilo this time CHADEMA wapo on the right side of the coin, CCM itoe maelezo ya kina as to how and why Magufuli didi that, kwa sababu ieleweke kwamba Waziri wa Jamhuri anakuwa On Duty 24 hours akiwakilisha Jamhuri sasa alikwenda huko kuwakilisha Jamhuri au CCM?

- Ni muhimu Serikali ya CCM ikatoa maelezo sasa kabla haijageuka kuwa a big deal ni ishu ndogo sana ila ikiachwa itageuka kuwa kubwa na kutuumiza CCM, so CCM let's get the facts out now!

Es!........

Kwa maoni yangu naona kwamba magufuli yuko sawa kabisa,kwani wana siasa wakikaa mda mrefu hawaja ongea kitu wana hisi kama vile wamepotea kwa hiyo issue kama ya magufuli ikitokea wanakomaa nayo na wakati aina tatizo lolote,ushauri wangu kwa chadema wanachi watawachoka mkianza kukomali Vi-issue visivyo na maana kwani kuna mambo mengi ya kudili nayo na si kuvizia mtu mmoja afanye kitu mkomae.

Kuna issue mfano hospitali watu wanakufa kwa kukosa damu salama hizo hamzioni,ajira pia tatizo,maji,umeme na matatizo mengine mengi!

Tena kwa ushauri wangu kama Magufuli anataka Uraisi amutumie huyo huyo rafiki yake wa kenya ampigie debe.
 
FEMES kweli umekomaa kisiasa siku hizi, siamini kama wewe ndo umeileta hii issue hapa- few years back this would have been impossible!. Ndugu zangu wanazi wa CDM tujifunze kitu kwa huyu bwana hapa, sio kila siku mnaleta habari za kusifia chama chenu tu hadi mmeifanya JF ionekane kama ni ya CDM wakati we all know kwamba that is not the case.
 
Uvivu wa kufikiri, magufuli hakwenda kuiwakilisha CCM wala serikali, ameenda Kama mtu binafsi Huyu wenje Hana la kuongea tamko limekaa kimajungu majungu, yeye ndiye anatakiwa kuthibitisha iwapo magufuli alisema anaiwakilisha CCM au serikali. CHADEMA wa jipange kushughulika na issues waachane na individuals vinginevyo wanapoteza mwelekeo kwa sasa na kuchezeshwa Kama Joyce wowo sindimba ya CCM........

MKUU unajua nini maana ya 'public figure'? Hata kama 'arguement' yako kuwa ameenda kama individual, yeye ni 'public figure', ni WAZIRI na KADA wa CCM.

Kila atakachosema au kufanya ni TASWIRA (image) ya Nchi na CHAMA chake. Hivyo huna cha kumtetea hapo. Serikali na Chama CCM kinatakiwa kutoa TAMKO kupinga au kuunga mkono kilichofanywa na WAZIRI na KADA wa CHAMA.
 
Uvivu wa kufikiri, magufuli hakwenda kuiwakilisha CCM wala serikali, ameenda Kama mtu binafsi Huyu wenje Hana la kuongea tamko limekaa kimajungu majungu, yeye ndiye anatakiwa kuthibitisha iwapo magufuli alisema anaiwakilisha CCM au serikali. CHADEMA wa jipange kushughulika na issues waachane na individuals vinginevyo wanapoteza mwelekeo kwa sasa na kuchezeshwa Kama Joyce wowo sindimba ya CCM........

In diplomacy, kitendo alichokifanya waziri, Dr., Mheshimiwa Magufuli ni makosa.

Yeye ni waziri wa serikali ya Jamhuri hii, anapokwenda Kenya katika kampeni za chama fulani bila idhini ya wakubwa wake ni makosa (serikali na chama chake).

Ikitokea Raila akashindwa uchaguzi na wengine wakachukua nchi, diplomacy itakuwaje hapo dhidi ya serikali yetu?
 
Kumbe inshu hapa ni ule mkataba wa kimataifa wa Rome? Ina maana mpaka Magufuli anazungumza hayo hakulijua hilo?
 
Hivi kama CCM wana jeuri ya kufanya upuuzi kama huu tena hadharani hadi nchi za ng'ambo mtashangaa nini jinsi wanavyojigeuza miungu watu kwenye kampeni zetu za ndani?

Yaani ni ujeuri kila mahali bila kufuata sheria, kanuni, miongozo, taratibu. Hata "haya/aibu" ambayo mwanadmu kwa asili ameumbiwa inaonekana hawa jamaa hawana.

Kwa tukio hili mnashangaa nini CCM wanapomwagika kwenye kampeni hadi za udiwadi na resources kibao za serikali - MAGARI, HELIKOPTA, POSHO na hata kutoa ahadi na misaada kibao ya kiserikali? Ujenzi wa madaraja, kutoa vyakula vya njaa kwa wananchi, n.k.?

Mnashangaa nini CCM wanapokuwa na jeuri ya kupandikiza hila chafu kwa wananchi, n.k. Mnashangaa nini CCM wanapokuwa na jeuri ya kutumia resources za wananchi kwa manufaa na faida yao bila kuhojiwa na yeyote? Matumizi ya vyombo vya dola kwa manufaa yao; matumizi ya vyombo vya habari - TBC, magazeti ya serikali, n.k. Hii ndio jeuri ya CCM, waliolewa madaraka.

Mnakumbuka ya Igunga? Mnakumbuka alichofanya Magufuli kule Igunga wakati ule? Mnakumbuka alivyokacha kwenda Mahakamani kutoa ushahidi? Hiyo ndio CCM na huyo ndiye Magufuli; mabingwa wa jeuri na dharau bila hofu yoyote ya kuwajibika au kuwajibishwa!

Lakini ni bahati mbaya sana kwa kujua au kutokujua; kwa tabia hizi wanaliweka taifa hatarini kwa ujinga wao.

- Hapana CCM hapa tuna kesi ya kujibu, Magufuli amekwenda huko kwa mgongo upi? Waziri wa Jamhuri, Mjumbe wa CCM, au Mtu binafsi, CCM ni lazima ithibitishe kwamba Magufuli amekwenda huko kwa nauli yake mwenyewe, hakulipiwa na Serikali wala CCM, na kwamba akiwa huko hakulipiwa anything na Serikali yetu wala ya Kenya, na CCM ni lazima iathibitishe kwamba ni kawaida kwa safari kama hizi kwa MAwaziri wetu kwa kuonyeshwa kuwa zimewahi kufanywa na mawaziri wengine pia!

- So baada ya majibu ya haya maswali kuna mengi ya nyongeza kutokana na majibu yatakayotolewa!!

Es!

Hivi CCM wakati inachagua mgombea wake wa Urais mwaka 2005 haikuwahi kuwatambulisha wawakilishi kutoka DRC, Angola na China? Kama ilifanya hivyo kuna tatizo gani kwa ODM kumtambulisha Magufuli. Halafu si juzi juzi hapa Ruto na Kenyatta walikaribishwa kwa Rais Kikwete. Hivi nongwa iko wapi hapo naomba kueleweshwa.
 
..........

Ruto na Kenyatta walionana na Rais Kikwete Ikulu katika ziara ya kiserikali kwa niaba ya serikali yao na hawakusimama majukwaani kwenye kampeni tofauti na alichofanya Magufuli. Mkuu hapo huoni tofauti?

Kwa habari ya wawakilishi kutoka DRC, Angola, China, n.k. kusimama kwenye kampeni za CCM sina hakika kama walikuwa viongozi wa kiserikali kutoka kwenye nchi zao zaidi ya kuwa viongozi wa kisiasa. Sidhani kwenye hoja iliyoko mezani angeenda Nape au Kinana ingekuwa issue sana japo pia kidiplomasia sio nzuri.

HATA HIVYO, kama hao wa kutoka DRC, Angola, China wangekuwa viongozi wa kiserikali kama ilivyo kwa Magufuli hii ndiyo hoja ya msingi wanayohoji CHADEMA na mleta mada - UNAHITAJIKA UFAFANUZI - KATUMWA NA NANI? Hili ndilo la msingi.
 
Kuhusu Kenyatta na Ruto siyo kweli kwamba waliiwakilisha serikali yao. Walikuja katika kutafuta kuungwa mkono kwenye alliance yao (na usisahau Ruto hana cheo chochote serikalini. Yeye ni mbunge tu). Kwa nini kidiplomasia isiwe nzuri CCM wanapoenda nje lakini wao wakialika iwe nzuri? Wakati wa Bakili Muluzi CCM walimpeleka Kapteni John Komba na TOT yake kumpigia debe kwa hiyo CCM kusupport mgombea siyo kitu cha ajabu. Hao CDM wenyewe wanasema wana uhusiano na Conservative mbona watu hawajasema hiyo siyo nzuri kidiplomasia? Nachotaka kusema CDM waache kuingia kwenye siasa za maji taka za CCM. CCM kuchafuana na kuitana majina ni tabia yao.
 
Uvivu wa kufikiri, magufuli hakwenda kuiwakilisha CCM wala serikali, ameenda Kama mtu binafsi Huyu wenje Hana la kuongea tamko limekaa kimajungu majungu, yeye ndiye anatakiwa kuthibitisha iwapo magufuli alisema anaiwakilisha CCM au serikali. CHADEMA wa jipange kushughulika na issues waachane na individuals vinginevyo wanapoteza mwelekeo kwa sasa na kuchezeshwa Kama Joyce wowo sindimba ya CCM

Hii sio individual issue ndugu yangu, huyu waziri tunamlipa kwa kodi zetu, atueleze siku alipokuwa kwenye hizo kampeni kama alikuwa likizo. Manake huyu anatakiwa awepo ndani ya kazi 24/7 atumikie kodi zetu tunazomlipa na sio kwenda kujiingiza kwenye siasa za nchi za watu
 
Sijaelewa taarifa ya CHADEMA kwani kama Magufuli angekwenda binafsi bila kutumwa na CCM au Serikali ni sahihi?

Nilifikiri hoja ni kosa kwa Mtanzania yoyote na zaidi Magufuli ambaye ni Waziri wa serikali ya Tanzania kushiriki kupindisha uchaguzi wa kidemokrasia wa nchi jirani au nchi nyingine.

Kama ungekuwa ni mapinduzi au uchaguzi usio wa kidemokrasia nchini Kenya basi Tanzania inaweza kuwa na msimamo wa kuunga kundi moja.
 
TOT ile kwaya ya Kapteni Komba ilikwenda Malawi kuimba na kupiga kampeni kuunga mkono kambi ya Rais Bakiri Muluzi sijui kama ni sahihi katika chaguzi za kidemokrasia za nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom