OMBI: Serikali idhibiti bei kwenye vifaa vya kujikinga na kupambana dhidi ya Virusi vya Corona

Masokoni raia wanauza na kununua bila kuwa hata na protective gear! Unajua masokoni ni sehemu zenye mkusanyiko wa watu wengi!
Wauzaji wanashindwa gharama ya maak na gloves!
 
Mask ya kutumia kujikinga na covid-19
 

Attachments

  • n95 mask.jpg
    n95 mask.jpg
    6.8 KB · Views: 1
Kumekuwepo na upandaji wa bei za barakoa ambazo ukiangalia ni za aina moja. Bei nilizosikia ni kuanzia 53,000 na wengine wanatangaza bidhaa ile ile kwa TZS90,000 na yawezekana kuna wanaopandisha zaidi.Na nahisi hata hiyo 53,000 ni bei ya juu.

Suala la kujikinga lisiangaliwe kibiashara zaidi, hapa tunaokoa maisha yetu na nchi kwa ujumla, hivyo bei za hizi bidhaa ingekuwa vyema kama mamlaka husika wangeweka bei elekezi ili watu wengi waweze kumudu kuzinunua na kuzuia upandaji wa bei huu tunaouona.

Hii ni vita yetu sote, kipindi hiki hela pia ni ngumu maana biashara nyingi zinafungwa. Hivyo mamlaka zisaidie hizi barakoa zenye ubora zipatikane kwa wingi ila kwa bei ambayo haiumizi watu. Kama mtu anaweza kuuza kitu kile kile kwa 50,000 na mwingine 90,000 ina maana kuna kitu hakipo sawa.
 

Attachments

  • VID-20200419-WA0021.mp4
    7.6 MB
Baada ya Kusafiri miji kadhaa mikubwa Tanzania, nimeona kuna TATIZO Kubwa la barakoa, Sio kwamba hazipatikani kabisa ila (zile zenye viwango zinazopatikana BEI ipo juu sana mf kutoka bei ya rejareja ya shs 500pc hadi bei kati ya shs2000 na shs5000pc. Na hapo utasikia wafafanyakazi wa Afya wanashauri ivaliwe masaa mane (4) halafu mtu abadilishe.

Nafikiri bila Serikali kuingilia kati hapa, kampeni nyingi zitakazohusisha kuvaa Barakoa, zitakuwa na ufanisi hafifu
Napendekeza

Serikali iagiza Barakoa za kutosha (zenye nembo maalumu na bei elekezi ) na kuziweka kwenye MSD au hospitali za Wilaya kwa watu kuzinunua kwa gharama nafuu na kwa utaratibu maalum.

Ikithibitika mfanyakazi anatumia nafasi hiyo kujinufaisha kwa Barakoa za Serikali apewe adhabu kali inayo endana ka kosa la kuhatarisha maisha ya watu kwa kukusudia
 
Bongo kila mtu ni mtaalamu wata zifua ziki kauka wanavaa tena

Sent from my SM-A105G using Tapatalk
 
Back
Top Bottom