Kwanini vitu vilianza kupanda bei baada ya Serikali ya awamu ya sita kuingia madarakani?

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
250
408
UKWELI KUHUSU ONGEZEKO LA BEI ZA BIDHAA NA GHARAMA ZA MAISHA

Watu wengi wamekuwa wakitoa maoni yao huku wengi wakiishia kuilaumu Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan juu ya ongezeko la bei za bidhaa na kupanda kwa gharama za maisha... Wengi wanaotoa maoni na lawama hizi wamekuwa wakizilinganisha Serikali ya awamu ya tano na ya sita. Hoja na maoni yao yamejikita kwenye maswali ya msingi ambayo mimi leo nimeleta majawabu yake;

Swali: 1. Kwanini vitu vilianza kupanda bei baada ya Serikali ya awamu ya sita kuingia madarakani?
Kupanda kwa bei za bidhaa hakuna uhusiano na awamu za utawala wa serikali wa viongozi wa Tanzania. Bali haya ni matokeo ya janga la ugonjwa wa Corona kuikumba dunia. Nchi nyingi zenye viwanda vinavyozalisha bidhaa zilisimamisha uzalishaji kama hatua ya kujikinga na kuenea kwa virusi vya corona miongoni mwa wafanyakazi.

Hali hiyo ilipekekea bidhaa kuadimika na kuongezeka bei duniani kote na sio Tanzania tu! Hii ina maana hata utawla wa awamu ya tano hapa Tanzania ungeelea kuwepo bado dunia yetu ingekumbwa na janga hili la mfumuko wa bei za bidhaa na nchi yetu ikiwemo. Hakuna kiongozi ambaye angweza kudhibiti hili moja kwa moja.

Swali: 2. Ugonjwa wa Corona ulianza tangu mwaka 2019 enzi za hayati JPM, kwanini bidhaa hazikupanda hadi zipande sasa?
Jibu: Viwanda vingi vilisimamisha uzalishaji wa bidhaa mwaka 2020&2021, hivyo bidhaa ambazo ziliendelea kutumika miaka ya 2020 na 2021 ni zile zilizokuwa bado zipo kwenye mzunguko tangu kuzalishwa kwake. Inamaana bidhaa hizo zilikuwa zimezalishwa kabla ya janga la Corona kutokea. Kwa kawaida bidhaa inayozalishwa leo, matumizi yake yanaweza kuwa kesho. Mfano mdogo ni kwamba mkulima anayekula wali leo ujue mchele wake ulivunwa shambani mwaka jana au mwaka juzi. Kwa hiyo gharama za bidhaa za sasa ni matokeo ya kusimama kwa uzalishaji kwa miaka miwili au mitatu huko nyuma.

Swali: 3. Nini sababu ya ongezeko la bei ya nishati ya mafuta?
Jibu: Ongezeko la bei ya mafuta limesababishwa mambo makubwa mawili; la kwanza ni janga la covid 19 na la pili ni vita kati ya Urusi na Ukraine. Urusi ni moja kati ya taifa kubwa linalotegemewa na dunia kuuza mafuta lakini baada ya kuanzisha mashambulizi ya vita dhidi ya Ukraine taifa hilo lenye nguvu duniani limewekewa vikwazo vya kuuza bidhaa zake ikiwemo mafuta hali iliyopelekea mnyololo wa mzunguko wa biashara ya mafuta kuyumba na kusababisha bei kupaa. Kwa hiyo ieleweke kwamba sio Serikali ya Tanzania wala Rais Samia ndio waliopandisha bei ya mafuta bali ni kutoka katika soko la dunia. Nchi zote dunuani mafuta yameongezeka bei msimu huu...

Nini hatima ya hali hii?
Serikali imeendelea kuchukua hatua za makusudi kukabiliana na hali hii. Mojawapo ikiwa ni kuvutia wawekezaji waweze kujenga viwanda ili baadhi ya bidhaa zizalishwe nchini kama vile mbolea, sukari, mafuta ya kula nk.
Aidha Serikali imewekeza zaidi kwenye sekta ya kilimo ili kusaidia wakulima wazalishe kwa wingi na kuuza mazao yao kwa bei nzuri na ya kuridhisha.

Hitimisho
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuelewa kwamba changamoto tunazopitia watanzania ni changamoto za kidunia, kwa hiyo hazikuletwa na Serikali ya awamu ya sita wala Rais Samia kama ambavyo wapotoshaji wanavyadai. Hata hivyo Rais wetu amekuwa akipambana sana kutafuta namna mbalimbali kujaribu kupunguza makali ya hali. Kuna wenzetu wa mataifa jirani wana hali mbaya zaidi kuliko sisi. Jambo la msingi tuendelee kushikamana na kuombeana heri ili tuvuke kwenye hili ombwe la mtikisiko wa dunia.
 
Samahani mkuu....
Kwani haukusikia mama alivyo sema kwamba vitu vitapanda bei..🙄
 
UKWELI KUHUSU ONGEZEKO LA BEI ZA BIDHAA NA GHARAMA ZA MAISHA

Watu wengi wamekuwa wakitoa maoni yao huku wengi wakiishia kuilaumu Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan juu ya ongezeko la bei za bidhaa na kupanda kwa gharama za maisha... Wengi wanaotoa maoni na lawama hizi wamekuwa wakizilinganisha Serikali ya awamu ya tano na ya sita. Hoja na maoni yao yamejikita kwenye maswali ya msingi ambayo mimi leo nimeleta majawabu yake;

Swali: 1. Kwanini vitu vilianza kupanda bei baada ya Serikali ya awamu ya sita kuingia madarakani?

Kupanda kwa bei za bidhaa hakuna uhusiano na awamu za utawala wa serikali wa viongozi wa Tanzania. Bali haya ni matokeo ya janga la ugonjwa wa Corona kuikumba dunia. Nchi nyingi zenye viwanda vinavyozalisha bidhaa zilisimamisha uzalishaji kama hatua ya kujikinga na kuenea kwa virusi vya corona miongoni mwa wafanyakazi. Hali hiyo ilipekekea bidhaa kuadimika na kuongezeka bei duniani kote na sio Tanzania tu! Hii ina maana hata utawla wa awamu ya tano hapa Tanzania ungeelea kuwepo bado dunia yetu ingekumbwa na janga hili la mfumuko wa bei za bidhaa na nchi yetu ikiwemo. Hakuna kiongozi ambaye angweza kudhibiti hili moja kwa moja.

Kwanini ukwapuaji mkubwa na ufisadi wa kutisha ulifanyika sana kwenye awamu ya 5?
 
Kinachofanya hii nchi isiendelee ni ujinga,nyege na maradhi.utuambie hapo wewe uko kundi Gani??madeni ya jpm yalitakiwa yaanze kulipwa/kuiva lini??deni la taifa etc etc etc etc.hujaongea kipindi Cha jpm
 
Una uhakika au unaropoka? Vitu vimeanza kupanda bei toka2020 mwishoni ,hata hivyo hivyo vitu havikupanda Tzn tuu bali vilipanda world wide so sio suala la serikali ya awamu ya Sita..

Najua unajua pia na sababu ila kwa vile wewe sio mdau wa awamu ya 6 inajitahidi kutafuta justification za kitoto..

Humu mitandaoni kuna watu waelewa kiasi so labda ungekuwa unawa address wale mnawaitaga wanyonge ingekusaidia .
 
Vitu vilianza kupanda bei rasmi baada ya Samia kutangaza kuwa kila kitu kitapanda bei.

Aidha kwa kujua ama kutokujua yeye kama raisi alitoa ruhusa kwa wafanyabiashara kupandisha vitu bei hata kama hawakuwa wameathirika na vita vya Ukraine na Russia. Kurudia kwake kila mara kuwa vitu vitapanda bei kama vile ni jambo la kujivunia kumetufikisha hapa tulipo, mengine yamechangia tu.

Kuna haja ya kuwa na semina endelevu kwa Raisi wetu juu ya nini anapaswa kusema na jinsi gani anapaswa kusema.
 
Ukweli hapa tumeliwa
 
Back
Top Bottom