OMBI: Serikali idhibiti bei kwenye vifaa vya kujikinga na kupambana dhidi ya Virusi vya Corona

CalvinPower

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,571
882
Tatizo kubwa hapa nchini ni kwamba pale inapotokea janga, mlipuko wa ugonjwa basi wafanya biashara hutumia nafasi hiyo kujinufaisha. Kuna vifaa kama hand sanitizer, medical face masks vimekuwa katika uhitaji mkubwa sana kwa ajili ya kujikinga na virusi vya corona.

Serikali kupitia waziri wa afya imesisitiza uvaaji wa mask, kutumia hand sanitizer ila cha kushangaza bei imepanda mara 200.

Kale kachupa kalikuwa kanauzwa sh 3,000/= sasa kanauzwa sh 15,000/= mpaka sh 20,000/=. kama vitu hivi vitapanda bei basi tutaingia katika risk kubwa sana ya kuusambaza ugonjwa huu. Japo pia serikali imesema pia kutumia njia ya kunawa mikono na sabuni kila wakati, ila sio kila sehemu patakuwa na maji na sabuni.

Hii ni global health crisis ndugu zangu, Supermakets sasaivi hawana bei elekezi ya vifaa hivi japo zamani vilikuwa rahisi sana.

Maisha yetu yapo hatarini kwasababu ya corona virus, serikali lazima wawawajibishe watu hawa wanaotumia nafasi hii kujitajirisha. watu hawa ndio wanalifanya janga hili kuwa kubwa.

Narudia tena law enforcement, na government officials mliangalie hili. Kuna supermarket moshi wanafanya huu ujinga.
1. Rafiki Supermarket
2. Kilimanjaro Supermarket
3.
4.
5. Jazeni na nyie.

Ni nini kitafuta iwapo tutashindwa kufuka makazini? SERIKALI SERIKALI SERIKALI MI NAPITA
 
Serikali ingeagiza vifaa hivyo na igawe bure kwa kila kaya ili kusaidia kupunguza maambukizi na bei ingeshushwa na yeyote atakaenda kinyume apewe kesi ya kuhujumu uchumi na mauaji ya kukusudia.
 
Virus killing supplies. Hizo sanitizer zinaua 99.9% of bacteria. Mnaona kirusi ni kitu cha mchezo mchezo kinakufa ovyo. asee msipoamua kutulia na kusoma kuhusu korona virus mtajazana ujinga tu na kupata hasara ya pesa.
Screenshot_20200316-223239_Chrome.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika ni wakati sasa Serikali iingilie kati bei za vifaa hivi, lakini sio kwa kutumia nguvu, itumie mbinu za kiuchumi, naungana na mchangiaji aliyesema kuwa Serikali iagize Vifaa hivi na kugawa bure, ila sikubaliani na wazo la kuuza bure, wauze kwa bei Ndogo na kwa kipindi kirefu,

pia wabuni mbinu za kutengeneza aina nyingine za sanitizer kwa mfano aliyosema Mheshimiwa Waziri Wa Afya Ummy Mwalimu kuwa tutumie Chlorine kuziweka katika Maji na ambazo zinauzwa shilingi 300 Msd kwa kidonge, Elimu ni muhimu sana kutengeneza Sanitizers mbadala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iagize wapi ndugu? Hizo bidhaa ni adimu kwa sasa kote duniani, China pamoja na technology waliyonayo bado imewawia vigumu kukidhi mahitaji provided that hiyo ni disposable, single use.
Pengine labda serikali iongee na manufacturers wa ndani kama wapo, wazitengeneze kwa wingi.

Na kama bado tunaagiza nje mpaka leo tuvitu tudogo kama masks then we are also a failed state, ni imani yangu Wizara ya afya ilijiandaa kwa haya yote. kanyembwe,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo barakoa [mask] wala hazihitajiki, kama virusi wanasambaa kwa kushika na kugusa [contact] hapo barakoa ina kazi gani.?

Ndiyo maana tunasisitiza kunawa mikono, na kutojilamba au kugusa maeneo ya uso kama macho, pua na mdomo.

Msaada pekee wa barakoa, ni ‘labda’ vile itazuia mikono yako ‘michafu’ kugusa mdomo, pua na macho.

Nawa mikono kila wakati, epuka ‘kujigusa’.... na hata ukitaka ‘kunyonya’ nakusihi uipake sanitizers kwanza.
 
Wapenzi tuweni na ubinadamu hata kwa nukta moja. Tumesikia na kusoma mengi kuhusu corona. Sasa kwa nini unapandisha bei za vifaa vya kujikinga? Toka jana bei za maski zinapanda kila dakika, bei za vilainishi vya kuoshea mikono (sanitaiza) , bei za wipes!

Hii sio ubinadamu hata kidogo. Pamoja na kwamba mnadhani mnachangamkia fursa bado huu si utu. acheni bei ziwe zile zile na Mungu atabariki biashara yenu! acheni wizi, hamtabarikiwa kamwe!

Ndo nshasema! wenzangu mnaonaje hii iko powa? tuungane kutokomeza corona sio kuumizana na kuibiana!
 
Bora hata nyie mna pesa za kununulia masks wengine hata ela ya kula ni mtihani sembuse hizo mask na mazaga mengine...we kama una nafasi ya kununua nunua tu mkuu hakuna namna maana yajayo yana furahisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumekuwa na tabia ya wafanyabiashara kutumia mgongo wa majanga yeyote ya kitaifa kuonyesha uwezo na nguvu yao kwa sababu ya matatizo kijamii katika kupandisha bei ya bidhaa zozote wanazouza hasa zile zenye matumizi ya muhimu kwa wananchi kulingana na janga husika.

Ni wakati sasa serikali kusimama na kuwatetea wananchi wake kwa jasho na fimbo kuhakikisha bidhaa hazipandi bei katika msimu huu wa mlipuko wa Corona nchini.

Serikali itangaze rasmi kuwa wale wote watakaopandisha bidhaa zao madukani au ghalani wahesabike kama wahujumu uchumi wanaoliibia na kulihujumu taifa.
Ni ushauri wangu kwa mustakabali wa taifa na Tanzania.
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana janga kama hili unakuta MTU ndiyo anataka atajirike....huu ni unyama,Jana jamaa YANGU kaenda huko posta DSM anataka kununua box LA musk hizi za kujikinga kuuliza bei anaambiwa kwa sasa musk moja inauzwa shilingi 8000/=,wakati mwanzo ziliuzwa 500/= yaani ni shida sana hapa ubinaadamu hakuna kabisa.

Unapandisha bei ya bidhaa wakati hilo janga linaweza likakutafuna hiyo faida kubwa sijui utailia akhera,serikali iweke mkazo kwenye hili LA sivyo itakuwa ni maafa ya kutisha.
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana janga kama hili unakuta MTU ndiyo anataka atajirike....huu ni unyama,Jana jamaa YANGU kaenda huko posta DSM anataka kununua box LA musk hizi za kujikinga kuuliza bei anaambiwa kwa sasa musk moja inauzwa shilingi 8000/=,wakati mwanzo ziliuzwa 500/= yaani ni shida sana hapa ubinaadamu hakuna kabisa.

Unapandisha bei ya bidhaa wakati hilo janga linaweza likakutafuna hiyo faida kubwa sijui utailia akhera,serikali iweke mkazo kwenye hili LA sivyo itakuwa ni maafa ya kutisha.
500 hadi 8000!!

Nilivyokuwa mbishi sitoi hiyo 8000 nipambane na Corona nyama kwa nyama.

Serikali lazima itazame hili la mfumko wa bei mapema kabla hali haijaanza kuwa tete. Vyakula, madawa, na usafiri.
 
Mbao za Mawe,
Yaani ni balaa kubwa sana .....ukiwa mbishi inakula kwako!!!
Inabidi serikali iliangalie hili mapema sana....watanzania wengi ni waoga wakujitetea tunakufa na tai shingoni!!
 
Back
Top Bottom