Ogopa hizi shuhuda

Ogopa hizi shuhuda

Inatisha sana, jamaa yangu hivi karibuni alijaribu kunishawishi ili tutajirike wote. Kuwa ni mambo ya kweli na anahudhuria semina na kiingilio ni 4million. Nilijaribu kudauti kuwa anapigwa akaruka futi 12, nimempotezea. Ila nadhani kisha tapeliwa pakubwa sana. So sad!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka Mshana sema kweli toka nijiunge JF na kuanza kupitia nyuzi zako nimeanza kujifunza vitu tofauti. Ubarikiwe sana

Mi mnamo mwanzoni mwa mwaka huu nilotafuta site hapa Arusha ili kufungua kijiwe cha kuuza juice za matunda, ee bwana wee nikaulizia kwenye mgahawa fulani hivi! Hapo ndipo matatizo yalianzia akanifunga kamba oohh! Hapa upatapiga pesa sana utakuwa unauza litre 20 kwa siku nikaona maisha c ndo haya. Nikalipa kodi 60k kwa mwezi yani sema kweli mpaka mwezi kuja kuisha sikuwahi kuuza zaidi ya litre3.

Somo: hakuna mtu asiyependa hela ukiona mtu anakuhamasisha kufanya kitu fulani ili upate pesa jiulize sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utaskia mtu anakwambia "ukitaka kuwa mfanya biashara mkubwa lazima ujitoe mhanga"lakini kumbuka hata misingi ya idea ya biashara auna,apo mjomba ukijitoa mhanga na viela vyako vya ngama umepotea,na ukipoteza kulusisha ni ngumu,ukipambana sana na ku force utaludi na Covid 19🤣🤣🤣


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa mganga fulani ni kiboko. Kuna madalali mpaka kwenye ulozi.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa kapiga pesa ndefu kwenye kamari. Huyu kaumizwa naye anataka akuumize.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa biashara GLND, FOREVER LIVING QNet nk zinalipa sana. Huyu keshapigwa na ana mzigo mkubwa wa bidhaa na hana wa kumuuzia, Ukikubali unalo lake.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa biashara fulani inalipa na faida yake ni chap chap. Huyu hajui ni mropokaji tu naye kasimuliwa.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa fulani kafanikiwa kupitia njia fulani lakini yeye yuko hapo hapo akiwa hohehahe hana mbele wala nyuma. Hizi ni story za vijiweni,

Hii dunia haina shortcut, hakuna pesa za bure. Kila sent lazima uitolee jasho.

Marafiki wa mitandaoni wanaojifanya wako njema na wanataka mshirikiane kufanya ishu ya pesa. Hawa ni matapeli tu, wezi waganga njaa kama wengine tu.

Mtu anayekushuhudia fursa kwa bashasha na lugha za kuvutia jua ya kwamba tayari aneshakuona wewe ni fursa..

Bahati mbaya sana hata baada ya kusoma hii post bado kuna watu watapigwa na watakuja hapa kulalama.. Na wengine watapigwa hapa hapa na wana JF wenzao

Ishu za madini
Ishu za mali ya Mjerumani
Ishu za pesa za majini
Ishu za Freemason
Ishu za utajiri wa kafara
Ishu ya dola za kusafisha
Ishu za madawa, vipuri, vivyago, magari, vyakula na zabuni mbalimbali kupitia UN kwenda kambi za wakimbizi zote hizi ni wizi na utapeli

MAKINIKA, MAKINIKENI, WAJINGA HAWAISHI ILA KUKUMBUSHANA NI ADA.

Jr

Umesahau wa "Nitumie nauli."
Hawa wanaliza watu kila siku.
 
Hahahaa dah nomaa sana
Unapigiwa simu na rafiki wa kitambo lakini usiyemkumbuka Ila yeye anakujua (kiuhalisia kakudukua tuu) yeye anakupa siri ya dili la kupeleka vitu huko na mlipaji ni UN kisha anakuunganisha na boss wake mzungu anayeongea kiingereza safi kabisa.. Utachanganyiwa habari mpaka utapigwa kama ukiwa na tamaa ya kupata haraka

Jr
Jamaa yangu kilichomwokoa alikuwa na Elfu hamsini tu mfukoni. Alinusurika kupigwa na Madawa ya kilimo. Matapeli Ni hatari sana aisee, usiombe wakufikie ukipona shukuru. Wana strategy Kali sana. Some time wanaweza kukufanya ufanikishe round ya kwanza na unaona hii ni biashara ya kuwa bilionea, wakija kufunga kipindi ukipona wewe unakuwa maskini wa kutupwa yaani ombaomba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa yangu kilichomwokoa alikuwa na Elfu hamsini tu mfukoni. Alinusurika kupigwa na Madawa ya kilimo. Matapeli Ni hatari sana aisee, usiombe wakufikie ukipona shukuru. Wana strategy Kali sana. Some time wanaweza kukufanya ufanikishe round ya kwanza na unaona hii ni biashara ya kuwa bilionea, wakija kufunga kipindi ukipona wewe unakuwa maskini wa kutupwa yaani ombaomba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi tapeli hata awe mkali kiasi gani hanipati. Na nasema kwa uhakika kabisa. Tapeli akifanikiwa kunitapeli basi ujue mimi niliamua kutoa bila kujali kama nitapata hasara na kwenye situation kama hizi huwa sitoi fedha nyingi. Njia moja nzuri sana ya kujiepusha na matapeli ni kutokuwa na tamaa na kufuata sheria. Usikubali kufanya mishe zinazoitwa dili. Fuata sheria na taratibu.
 
Mimi tapeli hata awe mkali kiasi gani hanipati. Na nasema kwa uhakika kabisa. Tapeli akifanikiwa kunitapeli basi ujue mimi niliamua kutoa bila kujali kama nitapata hasara na kwenye situation kama hizi huwa sitoi fedha nyingi. Njia moja nzuri sana ya kujiepusha na matapeli ni kutokuwa na tamaa na kufuata sheria. Usikubali kufanya mishe zinazoitwa dili. Fuata sheria na taratibu.
Mkuu, usizungumze hivyo, hawa jamaa wanajua sana, kwenye hizi biashara au kazi halali. Watu huwa wanafungiwa kipindi. Na huamini Kama kipindi kimefungwa. wanaweza fanya biashara na wewe hata miaka mitatu, kiasi kwamba munakuwa mumedevelop business trust. Watakavyokufungia kipindi hutaamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa yangu hapa kazin watu wa QNet daily lazima waje kumuhamasisha achukue mkopo ajiunge na Qnet, akaja kuniomba ushauri nkamuuliza kama inalipa mbona asiende kuwaita mama take,Dada,kaka mjomba,na shangazi wajiunge ukoo mzima wawe matajiri? Anakufuata fuata ww tu?

If the deal is too easy think twice!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una umri chini ya miaka 40... Anatokea mtu anakuambia mlima fulani kuna mashimo ama mapango yana mali za mjerumani.. Unaweka mashaka lakini anakuaminisha kabisa
Ukimwangalia ni kachala kachoka kabisa lakini anakwambia ukitafuta KIASI fulani cha pesa mkafanya kafara mtapata hiyo mali.. Na kwa ujuha wa kiwango cha juu mno unamuamini na kusahau kabisa kujiuliza haya
Hizo ni mali gani?
Zina thamani gani?
Utauza wapi?
Utamuuzia nani?
Nani kathibitisha uwepo wake? Kwanini yeye hakuchukua?
Ina maana walioweka ni wapumbavu kiasi cha kuacha kuja kuzifuatilia?
Ni nani hapendi utajiri? Ina maana hakuna watu wenye uwezo wa pesa walio tayari kuitafuta hiyo mali kwa njia zozote zile?

CC: Slim5

Jr
😁😁 Hvi bado tu hizi mamboo zipo ,, mi nakumbuka kipind cha nyuma mwak 2010 hv, home hapa jiran Kuna mganga na junk
kadhaa za mtaan hapa ,daily walkuw ni kushindiaa mliman ..wakishawishiana ..Kuna mali za wajerumani ara hzoo..ndan mliman .deep inside .na uwezo wa hata kufukua hawana ..walizingukaaa sana ..daily kukesha .kupigwa na baridi lakn..baad ya miez kadhaa sikuwah kuwaona ...



In short hizi ni akili za usingzin tu ...
 
Back
Top Bottom