Ogopa hizi shuhuda

Ogopa hizi shuhuda

Vipi kuhusu anayetoa ushuhuda wa Corona, apuuzwe?


Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa mganga fulani ni kiboko. Kuna madalali mpaka kwenye ulozi.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa kapiga pesa ndefu kwenye kamari. Huyu kaumizwa naye anataka akuumize.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa biashara GLND, FOREVER LIVING QNet nk zinalipa sana. Huyu keshapigwa na ana mzigo mkubwa wa bidhaa na hana wa kumuuzia, Ukikubali unalo lake.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa biashara fulani inalipa na faida yake ni chap chap. Huyu hajui ni mropokaji tu naye kasimuliwa.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa fulani kafanikiwa kupitia njia fulani lakini yeye yuko hapo hapo akiwa hohehahe hana mbele wala nyuma. Hizi ni story za vijiweni,

Hii dunia haina shortcut, hakuna pesa za bure. Kila sent lazima uitolee jasho.

Marafiki wa mitandaoni wanaojifanya wako njema na wanataka mshirikiane kufanya ishu ya pesa. Hawa ni matapeli tu, wezi waganga njaa kama wengine tu.

Mtu anayekushuhudia fursa kwa bashasha na lugha za kuvutia jua ya kwamba tayari aneshakuona wewe ni fursa..

Bahati mbaya sana hata baada ya kusoma hii post bado kuna watu watapigwa na watakuja hapa kulalama.. Na wengine watapigwa hapa hapa na wana JF wenzao

Ishu za madini
Ishu za mali ya Mjerumani
Ishu za pesa za majini
Ishu za Freemason
Ishu za utajiri wa kafara
Ishu ya dola za kusafisha
Ishu za madawa, vipuri, vivyago, magari, vyakula na zabuni mbalimbali kupitia UN kwenda kambi za wakimbizi zote hizi ni wizi na utapeli

MAKINIKA, MAKINIKENI, WAJINGA HAWAISHI ILA KUKUMBUSHANA NI ADA.

Jr
 
Shida ya kubet ipo kwenye bahati

Sent using Jamii Forums mobile app
Mleta hoja alitoa orodha ya vipindi au vipigo ikiwemo betting ya mpira. Ndo nilikataa hapo. Unaweza pata au kosa ukiachilia uhakika ni mdogo. Ila mengine ni vipigo pure kuanzia nia yenyewe, mchakato na matokeo. Tunaita kipigo ab initio. Kuna mtu anapigwa akikusimlia unataman kwa elim yake umuongezee kofi!
 
Kuna jamaa yangu hapa kazin watu wa QNet daily lazima waje kumuhamasisha achukue mkopo ajiunge na Qnet, akaja kuniomba ushauri nkamuuliza kama inalipa mbona asiende kuwaita mama take,Dada,kaka mjomba,na shangazi wajiunge ukoo mzima wawe matajiri? Anakufuata fuata ww tu?

If the deal is too easy think twice!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani umepanda mbuyu moyoni na akilini mwake.

Sent using iphone pro max
 
Kuna siku nilikua zangu nyumbani likizo fupi.basi nikiwa sina hili wala lile nilishangaa meseji inaingia kwenye simu yangu frm mamdogo wangu yupo Arusha.Akaniambia amepata matatizo nimsaidie elf 50 kwa mpesa atanirudishia akijisort.nikaamua kumpigia ajabu akawa hapokei.nikapiga kama mara nne nilitaka kumuuliza kama kuna tigopesa maana mimi mpesa yangu nilikua na 2000 tu.wapi?hapokei.

Basi nikamtumia hivyo hivyo atajijua mwenyewe maana simu hapokei.kama nusu saa hivi dadaangu nae ananipigia kuniambia kama mamdogo amekwama lakini nimemsort.nikamwambia basi tumemtumia kwa wakati mmoja.sio kesi.sijakaa sawa mama ananiambia hebu mpigieni mama yenu mdogo mimi nikimpigia hapokei kasema kuna tatizo anaomba hela.apo alarm ikalia.

Nikampigia mume wake.eti mamdogo yuko wapi?akasema sijui maana kanitumia meseji eti amepata shida nirushie elf 50 sasa nikipiga hapatikani.na akipatikana hapokei.tukahisi tumeliwa.muda huo huo na mamdogo akampigia mumewe kumwambia kama kaibiwa simu na anarudi nyumbani.daah heka heka iliopita hapo si mchezo.mbio mpaka kwa

wakala.yangu ilifanikiwa kurudishwa ila zingine zilienda maana alikua anatumia tigo na mimi nilituma tigopesa kwa hiyo ikashindwa kutolewa.ile zile laki moja mpesa za dada na mama zikaliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa mitandao ya simu, Kuna haja ya kufanya urekebishaji, wa hiyo miamala.

Walichelewa Sana kutupa mamlaka ya kurejesha miamala unapokuwa umekosea namba,.

Badae wakatupatia mamlaka na ukomo. Ukirusha hela kwenda mtandao Mwingine Kama umekosea huwezi kurudisha, hili Ni tatizo pia.

Kwakuwa wameamua kuingiza kipengele Cha kurusha miamala kwenda mtandao Mwingine wakubali kutupa mamlaka ya kurudisha pia, kwani pale huibi, unarudisha hela yako.

Sio mpaka tupige simu kwao. Huko Ni kujiongezea kazi wao zisizo za Lazima.

Enyi watu wa mitandao, Vodacom, Tigo, TTCL, Airtel, Zantel, na Halotel sikieni hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una umri chini ya miaka 40... Anatokea mtu anakuambia mlima fulani kuna mashimo ama mapango yana mali za mjerumani.. Unaweka mashaka lakini anakuaminisha kabisa
Ukimwangalia ni kachala kachoka kabisa lakini anakwambia ukitafuta KIASI fulani cha pesa mkafanya kafara mtapata hiyo mali.. Na kwa ujuha wa kiwango cha juu mno unamuamini na kusahau kabisa kujiuliza haya
Hizo ni mali gani?
Zina thamani gani?
Utauza wapi?
Utamuuzia nani?
Nani kathibitisha uwepo wake? Kwanini yeye hakuchukua?
Ina maana walioweka ni wapumbavu kiasi cha kuacha kuja kuzifuatilia?
Ni nani hapendi utajiri? Ina maana hakuna watu wenye uwezo wa pesa walio tayari kuitafuta hiyo mali kwa njia zozote zile?

CC: Slim5

Jr

Haya Maswali Ni mazuri Sana, Kuna mmoja ananisumbua na mambo ya ALLIANCE AIM GLOBAL huwa namchora tu. Kajiingiza kichwakichwa AIM GLOBAL bila kujua Ni kautapeli mi nacheka anavyonishawishi eti kujiunga laki tano 😂😂😂
 
Ndo maana watu waliofanikiwa hawasemagi siri ya mafanikio yao. Kuna kitu nimejifunza.
 
Muogope zaidi anayeaminisha watu kwa kutumia madhabahu kwamba nchi yetu haitaguswa aslani na COVID 19. Na watu, kama mazuzu, wanashangilia kwa nguvu na kuwazomea wale ambao walikuwa wanawahimiza kufuata masharti ili kuepukana na gonjwa hili.
vipi mpaka kufikia sasa una lipi la kusema kuhusu janga hilo na nchi yetu kwa ujumla...
 
Muogope zaidi anayeaminisha watu kwa kutumia madhabahu kwamba nchi yetu haitaguswa aslani na COVID 19. Na watu, kama mazuzu, wanashangilia kwa nguvu na kuwazomea wale ambao walikuwa wanawahimiza kufuata masharti ili kuepukana na gonjwa hili.
vipi mpaka kufikia sasa una lipi la kusema kuhusu janga hilo na nchi yetu kwa ujumla...
 
Haya Maswali Ni mazuri Sana, Kuna mmoja ananisumbua na mambo ya ALLIANCE AIM GLOBAL huwa namchora tu. Kajiingiza kichwakichwa AIM GLOBAL bila kujua Ni kautapeli mi nacheka anavyonishawishi eti kujiunga laki tano
Ameshaliwa uyo
 
Bravo Mshana! Unfeigned speaking not in a clandestine you're a great man! I always subscribe whatever you share herein, I eulogize this , our difference is shown only in politics but all in all this is amazing thread!

With regards!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna maneno kwenye hii comment nlitafuta kamusi..Thank you for increasing my Vocabulary.
 
Doooh! Rafiki yangu fulani alinihakikishia kuwa kilimo cha viazi ulaya kinalipa ile mbaya.Basi bwana, tukaandaa mpango mzima na nikamwaga million kadhaa. Kweli tulilima but mvua zimenyesha hadi kero, viazi full kuugua ugonjwa wa mnyauko.Mwisho wa siku mavuno yamekuwa negative na millions zimepotea hivi hivi.

Next time mtu asiniambie sijui upuuzi gani gani unalipa. Kama unalipa dump pesa zako mwenyewe kwenye huo upuuzi ili zikulipe.
Sio Kama kilimo hakilipi...hizo Ni changamoto za utafutaji..kulima wanalima wengi...ingekuwa hailipi tusingeona kitu sokoni
 
Back
Top Bottom