Ogopa hizi shuhuda

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa mganga fulani ni kiboko. Kuna madalali mpaka kwenye ulozi.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa kapiga pesa ndefu kwenye kamari. Huyu kaumizwa naye anataka akuumize.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa biashara GLND, FOREVER LIVING QNet nk zinalipa sana. Huyu keshapigwa na ana mzigo mkubwa wa bidhaa na hana wa kumuuzia, Ukikubali unalo lake.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa biashara fulani inalipa na faida yake ni chap chap. Huyu hajui ni mropokaji tu naye kasimuliwa.

Mtu anayekushuhudia kwa hakika kuwa fulani kafanikiwa kupitia njia fulani lakini yeye yuko hapo hapo akiwa hohehahe hana mbele wala nyuma. Hizi ni story za vijiweni,

Hii dunia haina shortcut, hakuna pesa za bure. Kila sent lazima uitolee jasho.

Marafiki wa mitandaoni wanaojifanya wako njema na wanataka mshirikiane kufanya ishu ya pesa. Hawa ni matapeli tu, wezi waganga njaa kama wengine tu.

Mtu anayekushuhudia fursa kwa bashasha na lugha za kuvutia jua ya kwamba tayari aneshakuona wewe ni fursa..

Bahati mbaya sana hata baada ya kusoma hii post bado kuna watu watapigwa na watakuja hapa kulalama.. Na wengine watapigwa hapa hapa na wana JF wenzao

Ishu za madini
Ishu za mali ya Mjerumani
Ishu za pesa za majini
Ishu za Freemason
Ishu za utajiri wa kafara
Ishu ya dola za kusafisha
Ishu za madawa, vipuri, vivyago, magari, vyakula na zabuni mbalimbali kupitia UN kwenda kambi za wakimbizi zote hizi ni wizi na utapeli

MAKINIKA, MAKINIKENI, WAJINGA HAWAISHI ILA KUKUMBUSHANA NI ADA.

Jr
 
Daaah hichi kitu ni kweli kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Una umri chini ya miaka 40... Anatokea mtu anakuambia mlima fulani kuna mashimo ama mapango yana mali za mjerumani.. Unaweka mashaka lakini anakuaminisha kabisa
Ukimwangalia ni kachala kachoka kabisa lakini anakwambia ukitafuta KIASI fulani cha pesa mkafanya kafara mtapata hiyo mali.. Na kwa ujuha wa kiwango cha juu mno unamuamini na kusahau kabisa kujiuliza haya
Hizo ni mali gani?
Zina thamani gani?
Utauza wapi?
Utamuuzia nani?
Nani kathibitisha uwepo wake? Kwanini yeye hakuchukua?
Ina maana walioweka ni wapumbavu kiasi cha kuacha kuja kuzifuatilia?
Ni nani hapendi utajiri? Ina maana hakuna watu wenye uwezo wa pesa walio tayari kuitafuta hiyo mali kwa njia zozote zile?

CC: Slim5

Jr
 
Mercury za mapangoni
Mbona tunadanyika kirahisi sana?
Kabla hujaamua kukubali kulishwa matango pori si ingia hata Google basi ujiridhishe fact kadhaa?
Mercury ninini?
Inapatikanaje?
Ina thamani gani?
Soko lake likoje? Liko wapi?

Pesa za majini
Je unafahamu nini juu ya hili?
Ni wangapi umewaona wamepata utajiri kupitia hizi pesa

Pesa za majini zipo.. Unatengenezewa hapo marundo kwa marundo... Lakini kamwe hazidumu.. Life span yake ni fupi sana na zina kikomo cha eneo... Ukiingia kingi umeliwa na utabaki na majuto yasiyoisha

Jr
 
Back
Top Bottom