Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Mtikisiko wa mfumo wa fedha duniani umezua jambo nchini Uingereza. Kampuni moja nchini humo ambayo baada ya kuona inapata hasara na inapoteza wafanyakazi wake wengi, iliamua kuwa kila siku ya ijumaa wafanyakazi wake wafanye kazi wakiwa uchi wa mnyama Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la Uingereza, Baada ya kuona kazi haziendi vizuri katika kampuni hiyo, mmiliki wa kampuni hiyo Sam Jackson aliwashawishi wafanyakazi wake kuwa kila siku ya ijumaa wafanye kazi wakiwa uchi wa mnyama ili kuongeza morali wa kazi na kuwafanya wafanye kazi kwa uwazi zaidi. Kampuni hiyo inayojulikana kwa jina la Onebestway inashughulika na utengenezaji wa website, logo na matangazo ya kwenye luninga na ina makazi yake katika mji wa Newcastle. Wakati bosi wa kampuni hiyo alipotoa wazo hilo, wafanyakazi wake walipigwa na bumbuwazi lakini baadae walikubalina na bosi wao na kuamua kila ijumaa watakuwa wakifanya kazi wakiwa uchi. Mmiliki wa kampuni hiyo amedai kwamba kwa kutumia njia hii wafanyakazi wake wameweza kufanya kazi bila kuoneana aibu na uelewano kati ya wafanyakazi umeongezeka. Sam Jackson amedai kwamba hivi sasa shirika lake limeweza kujikwamua kwenye mtikisiko wa uchumi nchini Uingereza na wafanyakazi wake wamekuwa wakifanya kazi kwa ufanisi zaidi. Habari za wafanyakazi wa kampuni hiyo kufanya kazi uchi kila siku ya ijumaa imevivutia vyombo vingi vya habari nchini Uingereza na kupelekea kutengenezwa kwa documentary kuhusiana na kampuni hiyo itakayorushwa kwenye televisheni ya Virgin 1 ya nchini humo julai 9 mwaka huu.
nifahamishe.com
nifahamishe.com
Last edited by a moderator: