Ndalichako: Maboresho ya Sheria ya fidia kwa Wafanyakazi yaja

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Serikali imewahakikishia majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, kuwa inafanyia kazi maoni na mapendekezo yao kuhusu maboresho ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amesema hayo leo Februari 10,2024 wakati akifunga kikao kazi cha mafunzo ya uelimishaji kwa majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, kanda ya kusini na watendaji wa tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA) mjini Songea.

“Mapendekezo ya kuboresha kifungu cha 39 (2) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 kilichoweka ukomo wa muda wa kuwasilisha madai bila kutoa wigo wa kupokea madai hayo iwapo kuna sababu za msingi za kucheleshwa, tumeyafanyia kazi na tunatarajia muswada wa marekebisho kuwasilishwa bungeni hivi karibuni.”amesema Ndalichako

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mustapher Siyani aliwahimiza waajiri nchini kujisajili kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), na kutoa taarifa za ajira za wafanyakazi wao ili kulinda haki zao pindi wanapopatwa na majanga wakiwa kazini.

Mkurugenzi wa WCF, Dk John Mduma amesema Mahakama ya Tanzania ni wadau muhimu wa mfuko huo katika utekelezaji wa majukumu yake, kwa kuwa unategemea maamuzi mbalimbali ya Mahakama katika utekelezaji wake wa majukumu ikiwemo maamuzi ya kesi za mirathi.
 
Wafanyakaz wa Tamisemi kam maafisa mifugo, WALIMU , watendaji n.k hulipw fidia.. na huo mfuko...
 
Back
Top Bottom