DOKEZO Chuo Kikuu cha Kampala chini Tanzania kinawadhulumu wafanyakazi wake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Chuo kikuu cha Kampala nchini Tanzania (KIUT) kimekuwa na utaratibu au mazoea ya kukwepa kulipa Wafanyakazi walioacha kazi au kuondoka chuoni hapo mishahara ambayo hayakulipwa kipindi walipokuwa wakifanya kazi chuoni, hata hivyo Wafanyakazi wanaoendelea na kazi wengi bado wanadai mishahara ambayo hawajalipwa kipindi cha nyuma tangu Mwaka 2020 ikiwepo ya wakati wa COVID-19 ambapo chuo kiliamua kuwalipa Wafanyakazi nusu mshahara kwa muda wa miezi mitatu.

Wafanyakazi hawa hata wakifuatilia wanatoa ahadi za uongo bila kutekeleza ahadi zao, wakiwa na lengo la Mfanyakazi kufuatilia kwa muda mrefu na hatimaye kuchoka na kuacha kufuatilia, hivyo wao wanabaki na faida ya pesa za hao wafanyakazi.

Huu umekuwa ni utamaduni wao wa kila mfanyakazi anayeondoka kwao kutowalipa mishahara wanayodai.

Hata wakipelekewa bank statements zinazoonesha madai hayo hawafanyii kazi na kuishia kutoa ahadi kwa muda mrefu ili mfanyakazi huyo apotezee.

Kiuhalisia hii tabia sio sahihi na inawanyima haki wafanyakazi hao kwani walifanya kazi hata bila kulipwa hivyo ni wajibu wa mwajiri huyo kuwalipa.

Mamlaka inayohusika itoe msaada ili wafanyakazi hao wapewe haki yao

Sambamba na hilo chuo kina wakata wafanyakazi makato ya BIMA na NSSF bila kupeleka kwa mamlaka husika hali hii inawapelekea wafanyakazi kushindwa kumudu garama za afya pindi wanapoumwa na ukizingatia wanabahatisha kulipwa mshahara, wafanyakazi wengi NSSF zao zinasoma ZERO ilihali tayari wamehudumu kazini hapo kwa miaka mingi.

Tunaomba mtupazie Sauti ili dhulma hii ijulikane.

PIA SOMA
- Chuo Kikuu Kampala kinawatesa Watanzania

- Kamwe USIJARIBU kusoma Chuo cha Kampala Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom