Inataka kuwa kama Korea kaskazini, live coverage ni ya kiongozi mkuu tuu mengine subirini mtapewa repoti na vyombo vinavyo chuja habariTutajuaje kuwa wabunge wetu wanawajibika?Yaani tuletewe story tu kama za vijiweni
Sasa kama miaka yote iliyokuwa bunge live na bado wabunge walikuwa wanalala na hawafanyi kazi. je,sasa kutokuoneshwa ndio kunatofauti gani?kama kuna wabunge hawafanyi kazi hadi bunge lioneshwi live basi hao wana matatizo.
Bunge kuonyeshwa au kutokuonyeshwa live, kunawapunguzia nini Wabunge jukumu lao la kuishauri na kuisimamia Serikali?Wanabodi,
Wote tunajua kuwa serikali imekuwa ikitafuta grounds mbalimbali za kuzuia kwanini bunge lisirushwe live.Hapo awali ilielezwa na waziri wa habari kuwa sababu kuu ni kubana matumizi ya serikali.Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa muda wa bunge uko sambamba na muda wa kufanya kazi hivyo watu wengi wanakuwa makazini.
Sababu hizo zilipingwa na wadau mbalimbali kwa hoja zenye mashiko lakini serikali haikusikia na mjadala wa hotuba ya Rais ukajadiliwa gizani. Wakati vikao vya bunge vinaenda kuanza, Kuna Taasisi iliamua kujitolea kulipa gharama ili bunge lirushwe live lakini sasa serikali imezuia vyombo vyote hata binafsi kurusha live muda wote kipindi cha bunge isipokuwa kipindi cha maswali na majibu. Hapa imeonekana hoja sio kubana matumizi. Pia hoja ya muda wa kazi iliisha juzi baada ya Rais kurushwa live ufunguzi wa daraja Kigamboni kwa kuwa ulikuwa muda wa kazi na watu hawakupaswa kuangalia kwa sababu walikuwa makazini.
Pamoja na kutafuta grounds mbalimbali ni sababu hizi pekee ambazo zinaweza kuingia akilini kwanini serikali haitaki bunge lirushwe live:
1.Wabunge wengi wa CCM kuwa na utamaduni wa kutowajibika bungeni, hii imepelekea wao kuwa watu wa "ndiyoo" hata kwa mambo yasiyo na faida kwa mtanzania, hata likiwa jambo la kipuuzi ilimradi limeletwa na serikali wao ni ndiyoo. Hii imepelekea kuishushia serikali na CCM heshima kwa wananchi.
2.Wabunge wengi wa CCM kutokuwa na hoja za maana za kuisimamia serikali, hii imetokana na wengi wao kubebwa bila kuwa na sifa. Hapa tunaona hata Dr anachangia kama mtoto wa darasa la pili (rejea kauli ya msigwa juu ya watu hawa kwa mkazo zaidi), hii inapelekea wao kupwaya na kuonekana wapinzani ndio husimamia serikali.
3.Uimara wa wabunge wa upinzani katika kujenga hoja, kuisimamia serikali na kutetea wananchi katika maswala yote.mfano halisi ni wakati wa sakata la ESCROW.
4.Wabunge na mawaziri wa CCM kulala bungeni hovyo, hili huwashushia heshima sana.
5.Spika na uongozi kuwaonea wapinzani bungeni.
Mambo hayo ukiyatafakari kwa makini utagundua ndio sababu pekee ambazo ni sensible na reasonable ambazo serikali inataka wananchi wasizione ili kulinda heshima na uhai wa chama. Sehemu kubwa ambayo upinzani umejijengea jina na heshima kwa wananchi ni bungeni, ndio maana serikali inataka kuminya mwanya huo. Sababu za kubana matumizi na muda wa kazi ni geresha tu, kwani zote zimeprove failure. Mwenye kuelewa ataelewa, wale wakushikiwa akili kutafuta uteuzi njooni mpambane huenda kesho ikawa zamu yenu.
Nimecheka sana, serikali ya viwanda iko shida
Bunge kuonyeshwa au kutokuonyeshwa live, kunawapunguzia nini Wabunge jukumu lao la kuishauri na kuisimamia Serikali?
Wakae ndani humo humo waisimamie Serikali kwa hoja zenye mashiko sio fitina fitina na uchochezi tu, baadhi Wabunge wanataka kugeuza Bunge kama ukumbi wa kufanya siasa ili kujipatia umaarufu mwepesi mwepesi huku wakionekana live.
Sasa tuone kama Bunge lisiporushwa live watatueleza walikwenda Bungeni kuonekana live, au walikwenda kuwasilisha hoja za msingi juu ya matatizo ya wananchi na kuisimamia Serikali kuhakikisha inawajibika?
A burning candle should not hestate its frame. Cjui hawajiamini? Rusha live tuone serikali ya dr. iavyonyanyambuliwa kwa hoja za vyama mbadala maana group dynamic theory inakubaliana na informal groups cha kufanya ni ku-excel na idea zao katika kufikia organisational goal. Siasa kama huwezi kujenga hoja unapoteza mvuto dakika sifur.
Shame on me? No, shame on u brother, kwani hakuna namna nyingine ya sisi kujulishwa kilichokuwa kikiendelea Bungeni iwe na Wabunge wetu au hizo Media, badala ya watu kukaa mwanzo mwisho wanaangalia live, nyinyi hamna kazi za kufanya?shame on u,yaani mipango ya mustakabali wa maisha ya watanzania upangiwe gizani?Hao tumewatuma wakapange matumizi ya fedha zetu halafu waingie mitini kujadili.Kwanin wanaogopa uwazi?Tutajuaje kama wabunge wanawajibika kuisimamia serikali?
Ile clip ya Wenje kwenye Bunge la Serikali iliyopita kuhusu Mkurugenzi Wilson kabwe nadhani utakuwa umeiona leo.Kwa hayo machache tu inatosha wewe kukubali upinzani ni very strong.
Bunge kuonyeshwa au kutokuonyeshwa live, kunawapunguzia nini Wabunge jukumu lao la kuishauri na kuisimamia Serikali?
Wakae ndani humo humo waisimamie Serikali kwa hoja zenye mashiko sio fitina fitina na uchochezi tu, baadhi Wabunge wanataka kugeuza Bunge kama ukumbi wa kufanya siasa ili kujipatia umaarufu mwepesi mwepesi huku wakionekana live.
Sasa tuone kama Bunge lisiporushwa live watatueleza walikwenda Bungeni kuonekana live, au walikwenda kuwasilisha hoja za msingi juu ya matatizo ya wananchi na kuisimamia Serikali kuhakikisha inawajibika?
Shame on me? No, shame on u brother, kwani hakuna namna nyingine ya sisi kujulishwa kilichokuwa kikiendelea Bungeni iwe na Wabunge wetu au hizo Media, badala ya watu kukaa mwanzo mwisho wanaangalia live, nyinyi hamna kazi za kufanya?