Nyuma ya pazia Bunge live

Hapa sioni hoja yoyote ya msingi,uliyoitoa zaidi naona unatoa mapovu tu ma Mihemko yako ya kisiasasiasa!


 
Mwisho wa siku watasema bunge limekubaliana hata kama wengine wanapinga na hawataki tusikie hoja zinzotolewa kupinga jambo lolote
Naangalia habari sasa hivi hapa ITV kuhusu tukio la kusikitisha sana na la kizembe huko Dar es Salaam. kwenye pantoni la kwenda Kigamboni.
Msoma habari kasema kuwa mlango wa kivuko haukufungwa vizuri hivyo wakati kivuko kiko katikati ukafunguka na gari ikaserereka na kutumbukia baharini.
Dada mmoja msemaji wa TEMESA anaseema gari ilikuwa imesimama kwenye eneo la kuingilia kwenye kivuko na ndio ikaserereka na kutumbukia baharini.
Mtu wa timu ya uokozi anasema kuna kina kirefu sana hapo gari ilipodumbukia na wanatumia miwani na tochi za kawaida kuisaka huko chini ya bahari lakini hawawezi kuiona kutokana na matope na mawe.
Maelezo ya hawa watu watatu ni kuwa mtu wa TEMESA hatuwezi kumwamini wakati ndiye muhimu zaidi ya wote maana ndiyo anatoa offical statement.
Kwa maana hiyo ni bora kila kitu kikawekwa 'live' ili kila mtu aelewe kwa akili yake ili hata pale anapolipa hizo kodi ajue wanaozitumbua ni akina nani!
 
kazi gani na viwanda mmeuza na walionunua wamegeuza godown .

Hujaomba kazi kwa Dangote?

Hujaomba kazi kwenye kampuni zaidi ya 20 za gas?

Wageni wamejazana Tanzania kwa fursa zilizokuwepo za kazi za kila aina lakini hamzioni.

Sishangai kwanini huzioni kwani time ya watu kufanya kazi wewe unataka kutazama bunge.

Kalagabaho.
 
mkuu kuwa muelewa. hapa hatuongelei UWAJIBIKAJI WA WABUNGE bali tunaongelea WANANCHI KUNYIMWA TAARIFA KUTOKA KWA WAWAKILISHI WAWAKILISHI (WABUNGE) WAO. umeelewa sasa? kama hujaelewa uliza.
 
Rais kufungua bunge live,waziri mkuu kuhutubia bunge live,mawaziri kuhutubia bunge live,mawaziri kujibu maswali live ila "wabunge kujadili hotuba ya Rais,waziri mkuu na bajeti za wizara gizani"
Hii maana yake nini?uhuni tu
Africa kawaida kabisa!aibu,wenzetu wanapiga hatua mbele sisi tunapiga hatua kurudi nyuma!
 
Tunakoelekea ili kumpa "kick" Rais wao Magufuli itaamuriwa au utapitishwa utaratibu wa kuhakikisha hakuna platform yoyote ambayo wote wanaomkosoa "mfalme" au wanopingana na maamuzi ya serikali wataitumia!!

Mfano inawezekana ukaja wakati hata JF itapigwa marufuku kuruhusu aidha kuchapa maoni mbadala pinzani ya bajeti kuu au ya wizara flani kama ambavyo mara nyingi imekuwa ikifanyika miaka ya nyuma.

Inawezekana kabisa pia huko mbeleni ikaja ikatolewa amri au maagizo ya electronic na publishing media yoyote kupigwa marufuku kumpa airtime au page mbunge au mtu yeyote aliye kinyume na mtazamo wa viongozi wa serikali kutoa maoni yake!!

Mpaka sasa kuna kila dalili kuwa magazeti au vituo vya TV au Redio ambavyo vina uelekeo wa kumkosoa Magufuli au serikali yake vitapigwa kufuli!!

Naona kabisa kwa upande wa magazeti ya mfano wa MwanaHalisi, Mtanzania, Tanzania Daima, Dira ya Mtanzania, MwanaHabari na mengine ya namna hiyo yakiwekwa kifungoni au kufutwa kabisa kumfuata Mawio!!

Huyu jamaa (Magufuli) si mvumilivu, ni mtu wa visasi, si mkweli na ana kila dalili za chembechembe ambazo kama hatadhibitiwa zitageuka kuwa cheche za udikteta!!

Na tayari anajitengenezea au anatengenezewa mazingira ya kutodhibitiwa na mazingira yenyewe ndiyo haya sasa; dhibiti bunge, fungia magazeti au futa kabisa, tunga sheria kandamizi nk...

Kwa sababu ukiicheki hii ishu ya bunge live broadcasting inavyoepukwa na serikali, mtu mwenye akili timamu hawezi kuelewa ni nini kipo nyuma ya pazia zaidi ya haya 100%!!

Twendeni tu tutaona huko mbeleni....
 
Mimi namshangaa Magu anachoogopa ni nii? Kama anasema tumuombee sisi watanzania huku anatuwekea ukungu kwenye mambo yanayotuhusu si muelewi vile!
Fanyeni kazi, maana wenzenu muda huo wanakuwa kazini.
 
Mr misifa hataki serikali yake ikosolewe wakati yeye ni mungu huwa hakosei
 
Kwa kumtaja msigwa kwenye uzi wako umeharibu kila kitu cjuu kama kuna chiz yyte akaendelea kumsikiliza huyu pungutwo
 
Utajuaje kama amekuwasilisha vyema. Huu si ndio mwanzo wa kuongopeana
 
Inaonyesha mawazo yako yameishia kuwakomoa wapinzani badala ya kuboresha ufanisi.
 
Kweli kaka
 
Mi namshauri Rais aruhusu au aamrishe bunge lionyeshwe live. Kwa sababu sera zake ni kidhibiti wizi na ufisadi, bunge kutoonyeshwa live ni sawa na mtu kusema kuwa unahitaji nuru kisha taa ya kukuwezesha hiyo nuru unaifunika isiangaze!
Katika kipindi hiki tungependa bunge liwe live ili ufisadi wote na uzembe wote uonekane kwa wote ili tujue kama wezi wote wanatumbuliwa? Dunia hii ya sasa si kipindi cha kunyimana haki ya kupata habari. Serikali iliangalie vyema, isiogope wala kuona aibu madhaifu ya waliopita yakiwekwa hadharani, yaonekane yote mabaya na mazuri.
 
Nawasihi wabunge wa upinzani wasikubaliane na uhuni. . wasishiliki vikao mpaka lioneshwe live.. Mzee wa msoga big up kwa hili tutakukumbuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…