Tokenism katika Bunge letu

Tokenism katika Bunge letu

Izato

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Posts
5,162
Reaction score
11,128
Kuna wanawake wengi bungeni, lakini wingi wao hauwafanyi kuwa na sauti wala mamlaka juu ya maamuzi yenye tija katika mambo ya msingi yanayolikabili Taifa letu.

Kwa muktadha huo "tokenism" katika muhimili huu muhimu wenye jukumu kubwa la kuishauri na kuisimamia serikali inahusishwa na jinsi ambavyo wanateuliwa kimkakati kwa ajili ya kuonekana tuna Bunge lenye usawa wa kijinsia, na wala si kwa sababu ya kuwapa mamlaka halisi ya kutaka kubadilisha mambo muhimu yahusuyo jinsia, kisera, na utawala bora.

Tanzania inatumia mfumo wa Viti Maalum kwa wanawake hivyo basi 30% ya wabunge wanatoka katika kundi hili
Wabunge hawa hawana jimbo la kuwajibika nalo moja kwa moja, hivyo teuzi zao hupitia katika michakato ya ndani ya vyama vyao. Teuzi zao hutolewa kama "token" tu kwao kupitia ushindani dhaifu ndani ya chama husika. Hii inapunguza hadhi yao ya kisiasa na kuwafanya waonekana ni dhaifu zaidi ya wale wanaipitia mchakato mgumu wenye ushindani mkali majimboni mwao dhidi ya wagombea wengine wa vyama shindani.

Wabunge wengi wa Viti Maalum hawapewi fursa ya kushiriki katika kamati nyeti wala hawapewi nafasi za uongozi wa juu katika kamati hizo. Kwa kuwa wanachukuliwa kama wapambaji wa picha ya bunge, na wala siyo wabunge wenye uzito wa kimaamuzi ndani ya Bunge

Ndiyo! Kuna wabunge wanawake wengi ndani ya Bunge la Jamuhiri ya Muungano wa Tanzania, lakini mjadala wa "tokenism" unajitokeza hasa pale tunaposhuhudia idadi hiyo haileti mabadiliko ya kimamlaka na kisera. Wapo wachache wenye ushawishi mkubwa, lakini waliokuwa wengi wapo kwa ajili ya kujazia namba tu.
 
Bunge lilisha ASIWA SIKU NYINGI ...TENA LILIASIWA HUKU WATANZANIA MKISHANGILIA NA KUSIFU ...mambo yaliyo hasi bunge ni mengi yakiwemo haya
1)viti maalum
2)mambo ya usawa wa kijinsia
3)wanawake kuwa wabunge
4)mfumo mbaya wa upigaji kula bungeni kwenye kupitisha jambo au kupinga jambo.
5)bunge letu kazi yake ni kama mihuri tu siyo kupanga na kutunga sera na sheria wala kuisimamia serikali..hizo ni porojo tu.
 
Tokenism haipo kwa wanawake peke yao, hata wanaume wamekuwa political furniture tu.

Tofauti ni kwamba kwa wanawake inaonekana faster sababu jamii tayari ina bias nao.
Kundi linaloathirika zaidi na tokenism ni wanawake. Kwa sababu mchakato wanaopitia ili kuweza kuwapa nafasi za viti maalum ni kwa ajili tu ya kujaza namba yao bumgeni.

Tanzania inatumia viti maalum vya wanawake bungeni ili kufikia lengo la asilimia 30% ya uwepo wa wanawake bungeni.

Wanaume hawana mfumo kama huu, wao mchakato huo wa upendeleo haupo kabisa, anakuwa mbunge kwa kugombea jimbo tu., yeye ana wajibu wa moja kwa moja, labda iwe kupitia zile nafasi 10 za ubunge wa kuteuliwa na Rais

Tokenism hii kwa wakina mama haitokani na kitu chochote zaidi ya shinikizo la kimataifa kupitia UN, AU, ama IPU ambazo zinataka kuona wanawake wengi zaidi wapo bungeni pasipo kujali wanapitia mchakato gani wa kuwaingiza humo. Mashinikizo haya huifanya serikali kukurupuka na teuzi hizi za "token" kwa kujionyesha tu.

Kwa mantiki hiyo tokenism hutokea pale tu kundi kubwa la wanawake wanapondishwa cheo cha ubunge kwa ajili tu ya kuonyesha usawa, na wala si kwa sifa stahiki za uwakilishi wa kijimbo
 
Back
Top Bottom