nape bado anadhani yeye ni mwenezi wa chama,anaendeleza zile figisufigisuSio Magufuli Muoga bali ni mawaziri wake na speaker wa Bunge .
Wakiongozwa hasa na waziri wa habari.
Wanaogopa bajeti kivuli ya wapinzani.
Miaka yote ndiyo iliyokuwa inafanana na haya anayofanya Rais.
Mfano Kabwe aliyetumbuliwa na Makonda Juzi alisemwa sana Bungeni na Wapinzani lakini CCM walikejeli sana wakiongozwa na Speaker wao.
Leo hao hao wanamsifia Rais kinafiki zaidi.
Huko kuonekana live ndipo kunakowafanya watake kuonekane ili wapate umaarufu,na ndipo yanapoibuka mambo ya hovyo ambayo unataka et mie labda tu ndiyo nayaona kuwa ya hovyo.hukumwelewa,wewe unaweza ukasema fulani amefanya jambo la hovyo na la kipuuzi,hiyo ni kwa mujibu wako wewe.Si kila mmoja ataona ni jambo la kipuuzi.Hivyo basi ni bora kila mtu akapata fursa ya kuona na kufanya judgement mwenyewe na sio kuja kuhadithiwa kuwa fulani alifanya upuuzi.
Wananchi gani unaowazungumzia?maana tumeona mafisadi wakirudi kwa wananchi huku wakishangiliwa,na fisadi mwengine akapewa na nafasi ya kugombea urais.Nilimsikia Mbuge mmoja akisema Bungeni unaweza kuzini kwa siri lakini huwezi kuugua au kubeba mimba kwa siri, Wacha wajifungie kwa siri labda wanafikiri hawatarudi tena kwa wananchi.
Huko kuonekana live ndipo kunakowafanya watake kuonekane ili wapate umaarufu,na ndipo yanapoibuka mambo ya hovyo ambayo unataka et mie labda tu ndiyo nayaona kuwa ya hovyo.
mawazo mazuriYani nakereka kuhusu maslahi ya inchi mnayajadili ki vyama!!!!!! Hapa nakubali watanzania sisi tunastahili turudi kutawaliwa maana sisi wenyewe hatujiwezi ki fikra,,samahani najua ntawaudhi wengi kwa hili.....
Ni nini maana ya vyama pinzani na
Ni nini maana chama tawala????
Hapa tunahitaji kiboko ili tuelewe,, nilishatanguliza samahani hapo juuu
Ni nini dhana ya siasa na wana siasa???
Kupitia ufinyu wetu wa fikra pevu na wembamba wa kutafakari vitu kwa upembuzi yakinifu na hasa kwa kukosa tafakuri sahihi kwa kukosa uchangamfu wa akili hasa kwa kujenge ufalme wa akili tegemezi miongoni mwetu hapo ndipo taifa la Tanzania linapotea.
Naionea huruma nchi yenye dhana na udongo uliojaa uzalendo kwa kukosa wazalendo. Hapa naaminisha nini?? Tuliowengi wetu tupo kutetea kauli na maslahi ya viongozi wa vyama vyetu. Inauma sana kwa Mtanzania halisi kukaa chini na kupigania kauli za kiongozi wa chama chake bila kujiridhisha pasipo na shaka kua anapaswa kuungwa mkono
Wahusika mtanisamehe na nitaiomba radhi tanzania kwa hili
"" Nchi yangu Tanzania imegeuka kua kama ligi ya mpira wa miguu ambapo ligi hiyo imeshirikisha timu mbalimbali na kila timu husifia wachezaji wake hata kama wanafanya vibaya,, na kuponda wachezaji wa vilabu vingine hata kama wanafanya vizuri"""
Kinachoniuma ni kwamba ccm na ukawa ndio wapinzani wa jadi kama yanga na simba lakini washabiki wao wamesahau kabisa kua hii ni inchi na inapaswa kujengwa na vijana bila kujali ni wa chama kipi
Mwanasiasa wa CHADEMA akihamia CCM maovu yake yoote tunayafuta wana CCM na tuanampokea kwa mikono miwili,,,
Na mwanachama wa CCM akihamia CHADEMA hua uovu wake unafutwa na kutakasa na anapokelewa kwa mikono miwili
Kinachoniuma hapa ni vyama kutugawa kisiasa,, majukwaani tunashirikishwa kumchafua mtu,, lakini siku ya kumpokea hua hatushiriki kama ilibo kwenye usajiri wa wachezaji wa timu
Lakini hili ni tofauti na mipira na kitu cha msingi mno.
Turudi kwenye maada baada ya ufafanuzi mdogo
Swala la matangazo kutolushwa laivu lilikua ni janga la kitaifa na lina mgusa kila mtanzania na si wa CCM au wa UKAWA. Cha kushangaaa li mtu eti kisa ni CCM limekazana kushabikia vitu ambavyo havina msingi wana CCM wazalendo wanajua baba wa taifa alituachia nini na si hivi vinavyoingiliwa na watu wachache kwa manufaaa yao.
Kutoliweka live bunge mumelivua nguo kwani ni chombo muhimu ambacho mnaita ni muhimili wa serikali. Kama sababu zenu zingekua na mashiko mi naamini watanzania nao ni waelewa wangewaelewa tuu
Uzoefu wangu katika kazi ,,ofisi nyingi za uma zina tv na hua wafanya kazi huangalia na huwasaidia kwa matukio muhimu,, lakini mumesema watu wafanye kazi mmeruhusu badala ya kuangalia bunge, waangalie bongo fleva na bongo movies,,
Hilo nilishasema kutoyarusha matangazo kwangu kuelewa siwezi na siku nikielewa mkanipime akili na msisubiri nijiteteee.
Hawa ukawa nao nyinyi mna hoja nzito na nzuri ila uwasilishaji wenu nao kiukweli unatia shaka, mi naamini pasipo matusi na maneno makali mnaweza fikisha ujumbe wenu kwa watu na wakawaelewa,, haiingii akilini kwa kika hoja unayoitoa we nikuizungumzia ccm hata pasipo kuwa na haja ya kuizungumzia,,
Nitaomba mniwie radhi
Dhana ya wizi na ufisadi kama hoja kuu ya chadema nanukawa kwa ujumla tayari na sisi imetutafuna. Imekwishaeleweka kabisaa na wanaukawa nao ni wapiga dili na hapo watanzania katika hoja hiyo wameshindwa kuwaelewa hasa kwetu huku ukawa na ubinafsi umeingilia kati,,
Sasa cha kushangaza na chakuaminika zaidi mpaka mtu wa juu kiongozi anaeaminiwa kukiri hili hapa ni kuua upinzani
Tuakatae tukubali sababu zilizowafanya makamanda wetu kukimbia kambi kujitoa inabidi tuzirekebishe
Ushauri wangu
Nawaombeni vijana na watu wenye nia nzuri ya kulijenga taifa hili tujitenge na misimamo ya vyama vyetu na viongozi wake kwani wanatuchezea akili zetu na hili ni baada ya kugundua kua tunaamini katika siasa badala yake tuwapuuze tuijenge inchi yetu
Ombi kwa wanasiasa wajue kabisa watanzania kuwa hivi ni kwa sababu yao na yoote magumu wayapatayo ni kwa ajiri yao,, na damu yao na kilio chao watakilipa.
Wajue kabisaaa tulipo tumechoshwa na hadithi za nchi ni tajiri na wakati tunaishi chini ya nusu dola
Mi nakubali na usemi wa
Siasa mchezo mchafu ambao huchezwa mchezaji akiwa amevaa suti na tai
Temeke kuna nini mkuu?
Chama CHAKAVU[emoji2] [emoji2]Naunga Mkono Hoja Yako Mtoa Post,
Hili Halihitaji Elimu Kubwa ya kiwango cha P.h.d Kulijua,
Imetokana Na Uimara Na Hoja Nzito Za Wa Wabunge Wa Upinzani,huku wabunge wa chama cha magamba na majipu wakikoroma na kumwagika udenda, Jambo Ambalo Limezidi kukishushia Heshima chama chakavu (CCM )mbele ya wananchi. ndio maana wame amua wasionekane live ili kujaribu kujivika nguo kidogo. katika karne hii ya sayansi na teknoloji jambo hilo ni ujuha mkubwa. linapaswa kulaaniwa na kila mwenye pumzi.
Mtukane tu Mkuu! Ile Sheria ya The cybercrime Act of 2015 inaapply kwa viongozi tuBahati yako tcra wananiona lakini ulikuwa halali yangu kukushona matusi yote makubwa duniani.....yakiwemo na yanguoni lkn basi huu mfumo wa zuia matusi na bunge ofline umekupakichwa na sii bure wewe ni moja kati yawaliopitisha upuuzi huu wa kuweka vitu ofline maana uwezo wako wakujenga hoja ndo vile tena,lkn nadhani weweeeeee ni......😵!
Hoja nzuri na yenye mashiko kimantiki. Lakini kihalisia bado vinchi vyetu hivi haviwejafika hatua ya demokrasia kama tunavyodhani. huwezi kuwa na demokrasia na maendeleo ya watu ( na siyo ya vitu), kama tunajadili watu badala ya hoja. katika michango mingi ya hapa jukwaani ni mara chache kuzumgumzia hoja. Hivyo tusahau kwa sasa. Maendeleo ya watu yanataka vichwa vitumike ZAIDI badala ya sehemu nyingine za mwili. Na wale wanaotumia akili mara nyingi huona vitu kitofauti. Kubinya UMWINGINE ambao kwa kiswahili chetu tunauita UPINZANI, ni kubinya fursa za kutoona kifarasi aliyefungwa nira. Ni tabia za watu wanaokariri badala ya kufikiri. Fikra wakati wote upasua miamba iliyozoeleka. Kutetea mfumo tulio nao ni kifo kwa wote WANAOFIKIRI.Wanabodi,
Wote tunajua kuwa serikali imekuwa ikitafuta grounds mbalimbali za kuzuia kwanini bunge lisirushwe live.Hapo awali ilielezwa na waziri wa habari kuwa sababu kuu ni kubana matumizi ya serikali.Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa muda wa bunge uko sambamba na muda wa kufanya kazi hivyo watu wengi wanakuwa makazini.
Sababu hizo zilipingwa na wadau mbalimbali kwa hoja zenye mashiko lakini serikali haikusikia na mjadala wa hotuba ya Rais ukajadiliwa gizani. Wakati vikao vya bunge vinaenda kuanza, Kuna Taasisi iliamua kujitolea kulipa gharama ili bunge lirushwe live lakini sasa serikali imezuia vyombo vyote hata binafsi kurusha live muda wote kipindi cha bunge isipokuwa kipindi cha maswali na majibu. Hapa imeonekana hoja sio kubana matumizi. Pia hoja ya muda wa kazi iliisha juzi baada ya Rais kurushwa live ufunguzi wa daraja Kigamboni kwa kuwa ulikuwa muda wa kazi na watu hawakupaswa kuangalia kwa sababu walikuwa makazini.
Pamoja na kutafuta grounds mbalimbali ni sababu hizi pekee ambazo zinaweza kuingia akilini kwanini serikali haitaki bunge lirushwe live:
1.Wabunge wengi wa CCM kuwa na utamaduni wa kutowajibika bungeni, hii imepelekea wao kuwa watu wa "ndiyoo" hata kwa mambo yasiyo na faida kwa mtanzania, hata likiwa jambo la kipuuzi ilimradi limeletwa na serikali wao ni ndiyoo. Hii imepelekea kuishushia serikali na CCM heshima kwa wananchi.
2.Wabunge wengi wa CCM kutokuwa na hoja za maana za kuisimamia serikali, hii imetokana na wengi wao kubebwa bila kuwa na sifa. Hapa tunaona hata Dr anachangia kama mtoto wa darasa la pili (rejea kauli ya msigwa juu ya watu hawa kwa mkazo zaidi), hii inapelekea wao kupwaya na kuonekana wapinzani ndio husimamia serikali.
3.Uimara wa wabunge wa upinzani katika kujenga hoja, kuisimamia serikali na kutetea wananchi katika maswala yote.mfano halisi ni wakati wa sakata la ESCROW.
4.Wabunge na mawaziri wa CCM kulala bungeni hovyo, hili huwashushia heshima sana.
5.Spika na uongozi kuwaonea wapinzani bungeni.
Mambo hayo ukiyatafakari kwa makini utagundua ndio sababu pekee ambazo ni sensible na reasonable ambazo serikali inataka wananchi wasizione ili kulinda heshima na uhai wa chama. Sehemu kubwa ambayo upinzani umejijengea jina na heshima kwa wananchi ni bungeni, ndio maana serikali inataka kuminya mwanya huo. Sababu za kubana matumizi na muda wa kazi ni geresha tu, kwani zote zimeprove failure. Mwenye kuelewa ataelewa, wale wakushikiwa akili kutafuta uteuzi njooni mpambane huenda kesho ikawa zamu yenu.
Wanabodi,

kwanza hicho kitakachokuja kuonyeshwa baadae bila shaka wanakuwa washaedit kuondoa sehemu mbovu mbovu... wakati watanzania wanataka kitu live bila chenga. Huu si uzalendo
Kwanini wao watuchagulie cha kuangalia wakati wao wanatutumikia sisi wananchi?
wewe always una post pumba hapa tuu" kwani bunge likiwa live wewe inakukera nini haswa?Acha ulimbukeni wamiaka 300 BCWaambieni wabunge wenu wasusie bunge.
Wataalam wa kususa si wale wa " Lowassa mabadiliko mabadiliko Lowassa" [emoji28]wabunge wetu ndio wapi hao?