Yani nakereka kuhusu maslahi ya inchi mnayajadili ki vyama!!!!!! Hapa nakubali watanzania sisi tunastahili turudi kutawaliwa maana sisi wenyewe hatujiwezi ki fikra,,samahani najua ntawaudhi wengi kwa hili.....
Ni nini maana ya vyama pinzani na
Ni nini maana chama tawala????
Hapa tunahitaji kiboko ili tuelewe,, nilishatanguliza samahani hapo juuu
Ni nini dhana ya siasa na wana siasa???
Kupitia ufinyu wetu wa fikra pevu na wembamba wa kutafakari vitu kwa upembuzi yakinifu na hasa kwa kukosa tafakuri sahihi kwa kukosa uchangamfu wa akili hasa kwa kujenge ufalme wa akili tegemezi miongoni mwetu hapo ndipo taifa la Tanzania linapotea.
Naionea huruma nchi yenye dhana na udongo uliojaa uzalendo kwa kukosa wazalendo. Hapa naaminisha nini?? Tuliowengi wetu tupo kutetea kauli na maslahi ya viongozi wa vyama vyetu. Inauma sana kwa Mtanzania halisi kukaa chini na kupigania kauli za kiongozi wa chama chake bila kujiridhisha pasipo na shaka kua anapaswa kuungwa mkono
Wahusika mtanisamehe na nitaiomba radhi tanzania kwa hili
"" Nchi yangu Tanzania imegeuka kua kama ligi ya mpira wa miguu ambapo ligi hiyo imeshirikisha timu mbalimbali na kila timu husifia wachezaji wake hata kama wanafanya vibaya,, na kuponda wachezaji wa vilabu vingine hata kama wanafanya vizuri"""
Kinachoniuma ni kwamba ccm na ukawa ndio wapinzani wa jadi kama yanga na simba lakini washabiki wao wamesahau kabisa kua hii ni inchi na inapaswa kujengwa na vijana bila kujali ni wa chama kipi
Mwanasiasa wa CHADEMA akihamia CCM maovu yake yoote tunayafuta wana CCM na tuanampokea kwa mikono miwili,,,
Na mwanachama wa CCM akihamia CHADEMA hua uovu wake unafutwa na kutakasa na anapokelewa kwa mikono miwili
Kinachoniuma hapa ni vyama kutugawa kisiasa,, majukwaani tunashirikishwa kumchafua mtu,, lakini siku ya kumpokea hua hatushiriki kama ilibo kwenye usajiri wa wachezaji wa timu
Lakini hili ni tofauti na mipira na kitu cha msingi mno.
Turudi kwenye maada baada ya ufafanuzi mdogo
Swala la matangazo kutolushwa laivu lilikua ni janga la kitaifa na lina mgusa kila mtanzania na si wa CCM au wa UKAWA. Cha kushangaaa li mtu eti kisa ni CCM limekazana kushabikia vitu ambavyo havina msingi wana CCM wazalendo wanajua baba wa taifa alituachia nini na si hivi vinavyoingiliwa na watu wachache kwa manufaaa yao.
Kutoliweka live bunge mumelivua nguo kwani ni chombo muhimu ambacho mnaita ni muhimili wa serikali. Kama sababu zenu zingekua na mashiko mi naamini watanzania nao ni waelewa wangewaelewa tuu
Uzoefu wangu katika kazi ,,ofisi nyingi za uma zina tv na hua wafanya kazi huangalia na huwasaidia kwa matukio muhimu,, lakini mumesema watu wafanye kazi mmeruhusu badala ya kuangalia bunge, waangalie bongo fleva na bongo movies,,
Hilo nilishasema kutoyarusha matangazo kwangu kuelewa siwezi na siku nikielewa mkanipime akili na msisubiri nijiteteee.
Hawa ukawa nao nyinyi mna hoja nzito na nzuri ila uwasilishaji wenu nao kiukweli unatia shaka, mi naamini pasipo matusi na maneno makali mnaweza fikisha ujumbe wenu kwa watu na wakawaelewa,, haiingii akilini kwa kika hoja unayoitoa we nikuizungumzia ccm hata pasipo kuwa na haja ya kuizungumzia,,
Nitaomba mniwie radhi
Dhana ya wizi na ufisadi kama hoja kuu ya chadema nanukawa kwa ujumla tayari na sisi imetutafuna. Imekwishaeleweka kabisaa na wanaukawa nao ni wapiga dili na hapo watanzania katika hoja hiyo wameshindwa kuwaelewa hasa kwetu huku ukawa na ubinafsi umeingilia kati,,
Sasa cha kushangaza na chakuaminika zaidi mpaka mtu wa juu kiongozi anaeaminiwa kukiri hili hapa ni kuua upinzani
Tuakatae tukubali sababu zilizowafanya makamanda wetu kukimbia kambi kujitoa inabidi tuzirekebishe
Ushauri wangu
Nawaombeni vijana na watu wenye nia nzuri ya kulijenga taifa hili tujitenge na misimamo ya vyama vyetu na viongozi wake kwani wanatuchezea akili zetu na hili ni baada ya kugundua kua tunaamini katika siasa badala yake tuwapuuze tuijenge inchi yetu
Ombi kwa wanasiasa wajue kabisa watanzania kuwa hivi ni kwa sababu yao na yoote magumu wayapatayo ni kwa ajiri yao,, na damu yao na kilio chao watakilipa.
Wajue kabisaaa tulipo tumechoshwa na hadithi za nchi ni tajiri na wakati tunaishi chini ya nusu dola
Mi nakubali na usemi wa
Siasa mchezo mchafu ambao huchezwa mchezaji akiwa amevaa suti na tai