Nyuma ya pazia Bunge live

Nyuma ya pazia Bunge live

Nimecheka sana, serikali ya viwanda iko shida

Miaka mitano itapita tunatumbua vipele,hivyo viwanda bado sijaona mpango mahususi wa serikali na sera inayoweza kulifanikisha hilo.
 
Bunge kuonyeshwa au kutokuonyeshwa live, kunawapunguzia nini Wabunge jukumu lao la kuishauri na kuisimamia Serikali?

Wakae ndani humo humo waisimamie Serikali kwa hoja zenye mashiko sio fitina fitina na uchochezi tu, baadhi Wabunge wanataka kugeuza Bunge kama ukumbi wa kufanya siasa ili kujipatia umaarufu mwepesi mwepesi huku wakionekana live.

Sasa tuone kama Bunge lisiporushwa live watatueleza walikwenda Bungeni kuonekana live, au walikwenda kuwasilisha hoja za msingi juu ya matatizo ya wananchi na kuisimamia Serikali kuhakikisha inawajibika?
Kwa hiyo unaona ni sawa bunge kutooneshwa au kutangazwa moja kwa moja? Wazee wa ndiyoooo katika ubora wao
 
Huna hoja kabisa kama Lowasa tu.

misukule wa lumumba wazito kuelewa,mkija kuelewa mnabadilika kama bendera fuata upepo.Mtaelewa tu na mtakuja hapa kupamba upya,ndio madhara ya kuwa chambo.
 
Kila kitu kiwekwa wazi. Watu ndio waamue kuangalia au la kwa nn kuwapangia? Kwani huo wa live ulishawahi kulalamikiwa na wananchi? Naona hili la ku edit ndilo linalalamikiwa
 
ujinga kipaji,hujui maslahi yako na kizazi chako ndio yanatetewa.Unaleta mipasho tu hapa,bila hao wapinzani ufisadi mwingi wa nchi hii ungefukiwa.
Ni ujinga kuamini kuwa wapinzani ndio wanaofumua uozo ndani ya serikali. Uozo huondolewa na wabunge wa ccm kwani bila wao kushinikiza serikali yao hakuna kuwajibishana.
Kabla hujakuwa tulikuwa na wabunge machachari kwa kuibua uozo serikalini na mawaziri waliwajibishwa mfano ni Mzindakaya. Bila wabunge wa ccm kuingilia swala hakuna mahali upinzani utafanya kitu bungeni labda tutaona mbwembwe tofautitofauti za kutoka bungeni na kuomba miongozo ya kijinga kuhusu kuvuliwa shanga mbele ya kadamnasi.
Kwa ujumla wananchi wa Tanzania wametaka nchi hii iongozwe na ccm hivyo wapinzani wamo kwenye mafunzo ya uongozi kwa vitendo kwa baadhi na wengine ni wasaka tonge tu.
 
Kwanza Kabisa nichukue muda huu kukupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya, mimi kama mzalendo kwa badhi ya mambo naridhika sana, usitetereke katika msimamo wako ila naomba uelewe kuwa yapo baadhi ya mambo yanatia hofu utendaji wako wa kazi.

Giza ndani ya bunge-Hili ni jambo ambalo linatia hofu sana katika utoaji wa habari katika awamu ya tano, ukiwa unajinasibu kuwa muwazi lakini serikali yako inaonekana kuwa kinyume na yale unayosimama na kuyahubiri, tunashindwa kuelewa serikali inayohubiri uhuru iweje leo igeuke na kuweka mambo gizani?

Mheshimiwa najua uko busy sana, nadhan kuna kitu kinatengenenezwa nyuma ya pazia, kuna mambo ynafichwa na sijui kama ni sahihi katika kuyafanya haya, mtambue fika kuwa hakuna siri chini ya jua, naelewa manafilter some of information zisifike kwa wananchi but this is totally unacceptable,wananchi tulikupa dhamana ya kuleta utawala ulio huru na haki, unaminya haki ya kuwaruuhusu wananchi kuwashuhudia wawakilishi wao? kwa nini unayafanya haya na kwa manufaa ya wananchi? au kwa manufaa ya nani?

Tunaomba kujulishwa kilicho nyuma ya pazia.
 
Ni ujinga kuamini kuwa wapinzani ndio wanaofumua uozo ndani ya serikali. Uozo huondolewa na wabunge wa ccm kwani bila wao kushinikiza serikali yao hakuna kuwajibishana.
Kabla hujakuwa tulikuwa na wabunge machachari kwa kuibua uozo serikalini na mawaziri waliwajibishwa mfano ni Mzindakaya. Bila wabunge wa ccm kuingilia swala hakuna mahali upinzani utafanya kitu bungeni labda tutaona mbwembwe tofautitofauti za kutoka bungeni na kuomba miongozo ya kijinga kuhusu kuvuliwa shanga mbele ya kadamnasi.
Kwa ujumla wananchi wa Tanzania wametaka nchi hii iongozwe na ccm hivyo wapinzani wamo kwenye mafunzo ya uongozi kwa vitendo kwa baadhi na wengine ni wasaka tonge tu.

Huu ndio ujinga wa wengi,elimu ya uraia bado inahitajika.Hivi umesahau kwanini samweli sitta alitoswa uspika akapata Anne Makinda?Hujui kuwa chama kilichukizwa na hatua yake ya kuruhusu mijadala ya ufisadi bungeni ambayo ilikuwa imeshikiliwa na upinzani?Hukumbuki maneno ya Chenge kuwa bora wakose wote?Hivi hukuona mjadala wa Escrow wabunge wengi wa ccm walivyowageuka watz na kutetea mafisadi?Hivi huoni wabunge wengi wa ccm kugeuka wasemaji wa serikali kana kwamba wao ni mawaziri pale serikali inapokuwa imebanwa na bunge?Jamani hadi zile ndiyoooo kwa maswala ya kijinga yasiyo na manufaa kwa wananchi huzionagi?kujitoa ufahamu kipaji,sio kila mtu anawez,hongera kwa hilo
 
Kitu pekee ambacho "mwanasiasa" anaweza kusema na akaaminika na kikabaki hivyo hivyo siku zote bila kubadilika ni KUTAJA JINA LAKE. Mengine yote aaaaaaaaaaaa!!!!
 
Mleta mada una-kila dalili ya kuwa jipuuu...na Tutakutumbua...Ngoja Vijana wamalize kuwarekodi waliosema oc hazitoshi turudi kwa hawa wa haki za binadamu wanaotuibia mchana kweupe kisha tutamalizia na nyie majipu ya kulilia bunge lionyeshwe muda wa kazi...Lazima Tulale na wewe mbeleee.

Ahahahahaha...dont Question dont ask....Hapa Kazi kwanza story baadae.
By the way ...unataka Kujua kilichoko nyuma ya pazia kikusaidie nini?...subiri Muda ukifika utakijua.... Ila mie ningeomba tuu..kwa Vile jumamosi sio siku ya kazi tupo majumbani..basi Bunge lionyeshwe laivu bila chenga... Kama na hapo hawatakubali..Basi Kuna vitu nyuma ya pazia na sio vizuri wananchi wote tujuwe.
 
Kwa kweli hata mimi nashangaa wanaogopa nini kurusha matangazo ya live bila kuhakikiwa, wana mapungufu gani wanayoyaficha
 
Bunge LA 2010 to 2015....lilishusha heshima ya Bunge....maadili mabovu ya wabunge Wa upinzani...linatakiwa Bunge lisiwe live...litawapunguza MISIFA wabunge Wa Upinzani.......
 
Kwa vile Watanzania Wooote muda wao wa kazi ni zile saa za Bunge (National Assembly) napendekeza vituo vyote vya TV vifunguliwe SAA 11 jioni ili watu wafanye kazi.
Naishanga serikali kuonyesha bunge mpaka SAA 4.30 asubuhi live kipindi cha maswali wakati ni wa kazi.
Najua kipindi cha maswali na majibu ni muhimu sana (kwa vile kimejaa upuuzi na uongo) kwa serikali lakini wazime tuu
 
Hii ni laani na itawala wao na vizazi vyao wote,machoni wanaoneakana kama watu lakini kumbe ni mbwa mwitu wakali wararuao!Shame!!
 
Ubora wa Mbunge siyo yale anayoyasema bungeni, au kuonekana kwenye TV akichangia. Ubora wa Mbuge ni kuisimamia Serikali katika maendeleo jimboni kwake. Uvuvuzela wabunge waupeleke kwenye sanaa.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Nadhani kuna watu bado hawajamuelewa magufuli!!!OK ni moja ya marais hapa Nchini anayependa na mwenye maono ya Tanzania mpya anahitaji ufanye kazi kisha vipindi vya bunge utaonyeshwa ukiwa umepumzika yaani baada ya kazi(baadhi)hii itaondoa dhana ya wale wanaorundikana asubuhi kwa watu kuangalia bunge bila kutimiza protocol ya kazi tu
 
Back
Top Bottom