Nyuma ya pazia Bunge live

Nyuma ya pazia Bunge live

Whaaat? mkuu hivi wewe huwa unawaamini wanasiasa hivi? wanasiasa wote wana sura mbili na wanafikina Magufuli sio exception na inawezekana hili la kuzuia bunge ni direct order ya magufuli, unaweza ukabisha sasa hivi lakini baadae utakuja kujua
Laiti tungewachukulia wanasiasa kuwa wana sura mbili kiujumla wao bila kujali kama ni upinzani au ccm basi wasingetuchezea akili.
 
Sasa kama unakubali kuwa kwa kuwaona wabunge live hakuna kinachobadilisha chochote katika uwajibikaji wao,je kuna umuhimu gani wa kubishana hapa juu ya kuwa bunge liwe live au lisiwe live?

hukumwelewa,wewe unaweza ukasema fulani amefanya jambo la hovyo na la kipuuzi,hiyo ni kwa mujibu wako wewe.Si kila mmoja ataona ni jambo la kipuuzi.Hivyo basi ni bora kila mtu akapata fursa ya kuona na kufanya judgement mwenyewe na sio kuja kuhadithiwa kuwa fulani alifanya upuuzi.
 
Watala wengi hupenda mwananchi ahubiri kole anachokipenda tu, asiyoyapenda ni nongwa kwa mtawala, hii inshu ya kutorusha bunge live ni mkakati unaotaka kuwaaminisha wananchi kuwa serikali ya mjomba magu haina dosari, na hii itawezekana tu
 
"I'm just trying..to think deeply beyonds,....Nadhani ccq watakuwa walikutana fargha na kuona kipitia bunge na jinsi maswali yanavyoulizwa kiufundi bila kuwa naajibu ya kutosheleza inachangia ccq kuporomoka" hivyo tupige ban!/
kumbe ban wangestahili kupiga 2010.
KWA SEREKALI YA MAGUFULI WOTE TUMEIRIDHIA NA TUNAIPENDA.
TUONDOLEE FARAGHA.
 
Waambieni wabunge wenu wasusie bunge.
FaizaFoxy huwa nakuamini sana kwenye hoja zito zinazohusu maslahi ya nchi kwani kwenye ukweli huwa hupindishi kwakuonyesha uzalendo wa nchi yako kwanza vyama baadaye.Lakini ktk hili umeteleza kidogo kwani kama kubana matumizi kwa TBC kunauhusiano gani na kuzuia vyombo vingine kuonyesha?.Ukuwapi uhuru wa habari ambao ni haki ya wananchi?.Kuna taarifa zinasema kuna yameonyesha nia ya kuzami matangazo ya Bunge laivu na yamekataliwa.Je hii ni kwa maslahi ya nani au serekali inaogopa nini?.
 
Laiti tungewachukulia wanasiasa kuwa wana sura mbili kiujumla wao bila kujali kama ni upinzani au ccm basi wasingetuchezea akili.
nimesema wanasiasa, sijataja chama mkuu, hapo inamaanisha wote...hata wa nje ya tz,
 
Nilimsikia Mbuge mmoja akisema Bungeni unaweza kuzini kwa siri lakini huwezi kuugua au kubeba mimba kwa siri, Wacha wajifungie kwa siri labda wanafikiri hawatarudi tena kwa wananchi.
 
Ni vema kama ungeweka pia mijadala mizito yenye maslahi kwa Umma ambapo ilisababisha serikali ichukue hatua madhubuti.Kuleta hizo video peke yake zinazoonyesha mtafaruku ni kujaribu kutuaminisha kuwa bunge halina maana na kazi yake ni vurugu.Kwenye mawazo kinzani lazima msuguano utatokea,hilo likitokea basi ni bahati mbaya lakini cha msingi suluhu ipatikane.Huko uingereza unakosema,kuna chanel maalum ya bunge ambapo yeyote anayetaka kurusha bunge basi anachukua kutoka kwenye feeder.Uhuru upo wa chombo chochote kuonesha au kutoonesha,uko huko hujui chochote mpaka sisi tukuhabarishe mambo ya huko?shame
Unazidi kupotosha kuwa wapinzani wanapigania agenda moja,hujui hata yanayoendelea bungeni sasa wewe umejuaje kuwa wanapigania agenda moja?Au unachanganya wapinzani na sisi wananchi ambao ndio tunalalamikia bunge kupewa uhuru wa kuoneshwa na chombo chochote kinachojisikia kufanya hivyo.
Hilo la msigwa umemnukuu wapi na lini akisema bunge kurushwa ndio litamaliza matatizo?Hapa tunazungumzia uhuru wa kupata habari bila kuhaririwa.
Ona mabunge haya ulimwenguni,sio tanzania tu migongano inatokea

Naona umeamua kukurupuka tu kuijibu hoja yangu bila kusoma nilichoaandika, kilichokufanya uijibu hoja yangu ni hizo video. Mimi nimetaka kujua ni kwanini wabunge wanakomalia issue ya bunge kuonyeshwa live mada ambayo ilishapita muda wa miezi kama mitatu. Na nikasema badala ya wao kupigania mambo ya muhimu kama ya kufichua madhambi ya serikali wanapoteza muda kujadili mambo ya bunge kuonyeshwa live. Hiyo video niliyoiweka ya bunge la uingereza ni ku confirm hoja yangu kuwa shughuli muhimu tu wenzetu wanaonyesha live na ni kwa muda wa dakika 30 kama hiyo video inavyoonekana. Kama mtu anataka kuona yalijiri bungeni hua kuna channel initwa BBC Parliament hiyo inaonyesha matukio ya mabunge tofauti ya UK, kama vile House of Common (MPS), House of Lords ( ma Peers), Scottish Parliament, wales n.k halafu siyo kila mtu anaweza kuona hiyo labda uwe unalipia sky decoder ama uwe na free view. Hapa kwetu TBC ingekua na Channel kama hiyo kuonyesha hata kinachojili Baraza la wawakilishi na siyo kuonyesha Dodoma tu. Ndiyo lengo langu mimi sipo katika siasa kama wewe na wenzako wanapigania kutetea serikali sababu wao ni ccm ama kutetea kina Peter Msigwa sababu wapo UKAWA. Matukio Muhimu kama ya kusomwa kwa Budget, rais kuhutbia Bunge lazima yawe Live lakini ukiniambia wabunge kujadili budget za serikali TBC waache mambo mengine watuonyeshe Bunge tu huo ni upuuzi tu na zaidi wengi mnataka Bunge lionyeshwe live si kwasababu mnataka kusikia nini kinajadiliwa bali mnataka kuona vituko, sasa kwanini serikali iingie hasara ya kutuonyesha vituko?????
 
okay,basi kusiwe na mijadala bungeni,mambo yawe kimya kimya.Yakishapangwa na serikali pamoja na kamati za bunge ndio iwe basi.Wabunge wakatekeleze kimya kimya.Si ndicho unajaribu kusema?
Tulipokua ahtuna TV ya serikali kulikuwaje naomba mnisaidie??????
 
..waache waminye Uhuru wa kupeana habari..kuna siku itakula kwao..pale watakapotaka kuonyesha mazuri yao kwa uhalisia watakwama...maana hakuna mtu makini anaangalia ujinga wa TBC...nlidhani kuja kwa mkuu mpya TBC kuna manufaa.. Kumbe ni majanga bado...seems wanapokea orders toka juu kwa kina nape....nchi hii tuna shida sana...
 
Naona umeamua kukurupuka tu kuijibu hoja yangu bila kusoma nilichoaandika, kilichokufanya uijibu hoja yangu ni hizo video. Mimi nimetaka kujua ni kwanini wabunge wanakomalia issue ya bunge kuonyeshwa live mada ambayo ilishapita muda wa miezi kama mitatu. Na nikasema badala ya wao kupigania mambo ya muhimu kama ya kufichua madhambi ya serikali wanapoteza muda kujadili mambo ya bunge kuonyeshwa live. Hiyo video niliyoiweka ya bunge la uingereza ni ku confirm hoja yangu kuwa shughuli muhimu tu wenzetu wanaonyesha live na ni kwa muda wa dakika 30 kama hiyo video inavyoonekana. Kama mtu anataka kuona yalijiri bungeni hua kuna channel initwa BBC Parliament hiyo inaonyesha matukio ya mabunge tofauti ya UK, kama vile House of Common (MPS), House of Lords ( ma Peers), Scottish Parliament, wales n.k Hapa kwetu TBC ingekua na Channel kama hiyo kuonyesha hata kinachojili Baraza la wawakilishi na siyo kuonyesha Dodoma tu. Ndiyo lengo langu mimi sipo katika siasa kama wewe na wenzako wanapigania kutetea serikali sababu wao ni ccm ama kutetea kina Peter Msigwa sababu wapo UKAWA. Matukio Muhimu kama ya kusomwa kwa Budget, rais kuhutbia Bunge lazima yawe Live lakini ukiniambia wabunge kujadili budget za serikali TBC waache mambo mengine watuonyeshe Bunge tu huo ni upuuzi tu na zaidi wengi mnataka Bunge lionyeshwe live si kwasababu mnataka kusikia nini kinajadiliwa bali mnataka kuona vituko, sasa kwanini serikali iingie hasara ya kutuonyesha vituko?????

Angle yako ya habari imeonekana wazi kwenye ile comment yako,pia wewe hujaelewa.Malalamiko sio TBC kwanini isioneshe live,suala hapa ni kuzuia kurushwa vikao vya bunge kwa vituo vya Television vyote hata ambavyo ni binafsi na viliamua viingie gharama zao kurusha live.Hayo madhambi unayosema yafichuliwe ndio serikali inajaribu kuwaficha wananchi kwa kuwanyima kuona bunge ili hata wabunge wakisema habari zisifike kwa mwananchi au zikifika ziwe zimehaririwa.
Hivi unaweza thibitisha kwamba watu wanataka live ili kuona vituko?Unatumia hisia zako binafsi kusemea nafsi za watu.
 
Mimi namshangaa Magu anachoogopa ni nii? Kama anasema tumuombee sisi watanzania huku anatuwekea ukungu kwenye mambo yanayotuhusu si muelewi vile!



Sio Magufuli Muoga bali ni mawaziri wake na speaker wa Bunge .
Wakiongozwa hasa na waziri wa habari.

Wanaogopa bajeti kivuli ya wapinzani.
Miaka yote ndiyo iliyokuwa inafanana na haya anayofanya Rais.
Mfano Kabwe aliyetumbuliwa na Makonda Juzi alisemwa sana Bungeni na Wapinzani lakini CCM walikejeli sana wakiongozwa na Speaker wao.
Leo hao hao wanamsifia Rais kinafiki zaidi.
 
ccm wanajaribu kujificha kwenye shamba la karanga wakifikiri hawataonekana...duuh eti serikali sikivu
 
Back
Top Bottom