Nyuma ya pazia Bunge live

Nyuma ya pazia Bunge live

tunaelekea kubaya,hawa wanaoshangilia wanaona wanawakomoa upinzani bila kujua mwananchi ndiye anayepiganiwa haki zake
acheni uzushi hali hiyo ya kuto onesha matangazo ipo nchi za kidikteta siyo kwetu jamani heee!!!!!!!
 
KAMA SERIKALI NI YA WANANCHI NA WANANCHI WENGI WANATAKA BUNGE LIONESHWE LIVE, SEREKALI SIKIVU NA INAYOJALI WANANCHI WANYONGE BILA SHAKA HAITAPUUZA KILIO HIKI.
 
Serikali ya Awamu ya tano imekubali kuikandamiza demokrasia nauona uoga wa magu na CCM yake kuogopa Kukosolewa na wapinzani kulizuia bunge kuoneshwa ni kuirudisha nyuma jamii ya kitanzania iliyoanza kupata Urazini kuhusu madudu yanayofanywa na serikali yao kuna mwisho nao u karibu maigizo yakiisha tutaona kipi kinafata.
 
ushahidi upo na picha zinazoonyesha wanalala bungeni zipo. ina maana wewe hujawahi kuwaona mkuu?
Na wale waliyokuwa wanapiga kelele bungeni kama watoto na kutoka nje ya nje ila posho kama kawa nao hakuna ushahidi?
Au ndivyo mlivyowatuma?
 
Yani nchi iingie kwenye mtikisiko kisa bunge kutooneshwa live?ama kweli waafrika tuna matatizo.
Siyo itaingia ila imeshaingia, tumenyimwa misaada tayari hilo ni tatizo, watawala hawaoni kabisa tuonane 2020
 
Serikali ya Awamu ya tano imekubali kuikandamiza demokrasia nauona uoga wa magu na CCM yake kuogopa Kukosolewa na wapinzani kulizuia bunge kuoneshwa ni kuirudisha nyuma jamii ya kitanzania iliyoanza kupata Urazini kuhusu madudu yanayofanywa na serikali yao kuna mwisho nao u karibu maigizo yakiisha tutaona kipi kinafata.
tuonane 2020
 
Mawaziri wa4 wamepigwa chini,mfano wassira.Kule kulala bungeni ndio kumemshusha.Lete pia mfano wa waliofanya mambo ya hovyo na matukio tuweke kumbukumbu sawa
Unawezaje kuthibitisha kuwa hao waliyopigwa chini ni kutokana na matangazo ya bunge live?maana hata mie naweza nikataja wabunge wa upinzani waliyopigwa chini na nikasema wamepigwa chini kutokana na matangazo ya live ya bunge.
 
Wanabodi,

Wote tunajua kuwa serikali imekuwa ikitafuta grounds mbalimbali za kuzuia kwanini bunge lisirushwe live.Hapo awali ilielezwa na waziri wa habari kuwa sababu kuu ni kubana matumizi ya serikali.Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa muda wa bunge uko sambamba na muda wa kufanya kazi hivyo watu wengi wanakuwa makazini.

Sababu hizo zilipingwa na wadau mbalimbali kwa hoja zenye mashiko lakini serikali haikusikia na mjadala wa hotuba ya Rais ukajadiliwa gizani. Wakati vikao vya bunge vinaenda kuanza, Kuna Taasisi iliamua kujitolea kulipa gharama ili bunge lirushwe live lakini sasa serikali imezuia vyombo vyote hata binafsi kurusha live muda wote kipindi cha bunge isipokuwa kipindi cha maswali na majibu. Hapa imeonekana hoja sio kubana matumizi. Pia hoja ya muda wa kazi iliisha juzi baada ya Rais kurushwa live ufunguzi wa daraja Kigamboni kwa kuwa ulikuwa muda wa kazi na watu hawakupaswa kuangalia kwa sababu walikuwa makazini.

Pamoja na kutafuta grounds mbalimbali ni sababu hizi pekee ambazo zinaweza kuingia akilini kwanini serikali haitaki bunge lirushwe live:

1.Wabunge wengi wa CCM kuwa na utamaduni wa kutowajibika bungeni, hii imepelekea wao kuwa watu wa "ndiyoo" hata kwa mambo yasiyo na faida kwa mtanzania, hata likiwa jambo la kipuuzi ilimradi limeletwa na serikali wao ni ndiyoo. Hii imepelekea kuishushia serikali na CCM heshima kwa wananchi.

2.Wabunge wengi wa CCM kutokuwa na hoja za maana za kuisimamia serikali, hii imetokana na wengi wao kubebwa bila kuwa na sifa. Hapa tunaona hata Dr anachangia kama mtoto wa darasa la pili (rejea kauli ya msigwa juu ya watu hawa kwa mkazo zaidi), hii inapelekea wao kupwaya na kuonekana wapinzani ndio husimamia serikali.

3.Uimara wa wabunge wa upinzani katika kujenga hoja, kuisimamia serikali na kutetea wananchi katika maswala yote.mfano halisi ni wakati wa sakata la ESCROW.

4.Wabunge na mawaziri wa CCM kulala bungeni hovyo, hili huwashushia heshima sana.

5.Spika na uongozi kuwaonea wapinzani bungeni.

Mambo hayo ukiyatafakari kwa makini utagundua ndio sababu pekee ambazo ni sensible na reasonable ambazo serikali inataka wananchi wasizione ili kulinda heshima na uhai wa chama. Sehemu kubwa ambayo upinzani umejijengea jina na heshima kwa wananchi ni bungeni, ndio maana serikali inataka kuminya mwanya huo. Sababu za kubana matumizi na muda wa kazi ni geresha tu, kwani zote zimeprove failure. Mwenye kuelewa ataelewa, wale wakushikiwa akili kutafuta uteuzi njooni mpambane huenda kesho ikawa zamu yenu.
 
ila wewe hujui jinsi ya kuendelea akili mgando zako peleka huko
Na wale waliyokuwa wanapiga kelele bungeni kama watoto na kutoka nje ya nje ila posho kama kawa nao hakuna ushahidi?
Au ndivyo mlivyowatuma?
 
Unawezaje kuthibitisha kuwa hao waliyopigwa chini ni kutokana na matangazo ya bunge live?maana hata mie naweza nikataja wabunge wa upinzani waliyopigwa chini na nikasema wamepigwa chini kutokana na matangazo ya live ya bunge.
Ndiyoo!!!!! 100%
 
wananchi ndio waamuzi, kama ukiona hivyo basi ujuwe wananchi wanaowakilishwa na hao wabunge hawajaona kama 'HAYO MAMBO YA OVYO' unayosema WEWE yanamzuia mbunge wao kuwatumikia. hivyo basi, nakubaliana nawe bunge lionyeshwe laivu....tuachane na wale wapuuzi wanaodai kwamba wananchi wasiowaone wawakilishi wao wanavyowawakilisha.
Sasa kama unakubali kuwa kwa kuwaona wabunge live hakuna kinachobadilisha chochote katika uwajibikaji wao,je kuna umuhimu gani wa kubishana hapa juu ya kuwa bunge liwe live au lisiwe live?
 
SIFIKIRI KAMA HILI LA KIZUIA BUNGE NI AJENDA YA RAIS WETU MPENDWA NAKATAA KWA 100%,KWA VYOVYOTE HILI NI AGIZO LA CHAMA KIPENDACHO USIRI NA FARAGHA
Whaaat? mkuu hivi wewe huwa unawaamini wanasiasa hivi? wanasiasa wote wana sura mbili na wanafikina Magufuli sio exception na inawezekana hili la kuzuia bunge ni direct order ya magufuli, unaweza ukabisha sasa hivi lakini baadae utakuja kujua
 
Unawezaje kuthibitisha kuwa hao waliyopigwa chini ni kutokana na matangazo ya bunge live?maana hata mie naweza nikataja wabunge wa upinzani waliyopigwa chini na nikasema wamepigwa chini kutokana na matangazo ya live ya bunge.
wewe huwezi jua kwa vila una mgando wa akili
 
KAMA SERIKALI NI YA WANANCHI NA WANANCHI WENGI WANATAKA BUNGE LIONESHWE LIVE, SEREKALI SIKIVU NA INAYOJALI WANANCHI WANYONGE BILA SHAKA HAITAPUUZA KILIO HIKI.
Imejulikana vp wanaotaka bunge live ndio wengi?
 
Whaaat? mkuu hivi wewe huwa unawaamini wanasiasa hivi? wanasiasa wote wana sura mbili na wanafikina Magufuli sio exception na inawezekana hili la kuzuia bunge ni direct order ya magufuli, unaweza ukabisha sasa hivi lakini baadae utakuja kujua

anaweza akawa amemtuma waziri kufanya haya,siku upepo ukimuelemea anatoka nakusema kwa lafudhi yake,"sasa bunge ni live,hakuna kufichaficha",baada ya hapo akina wenzangu na mimi kuvizia uteuzi tutakuja humu na vichwa mbalimbali kama "Magu kipenzi cha watu asikia kilio cha wananchi",hahaaaaaaaaaa,mnatuchosha sana viwavi
 
Back
Top Bottom