Kila mtu anajuwa kazi ya mapenzi wake na anajuwa ratiba zake kuna mapenzi unakuta yupo busy kiasi kwamba unaweza mtumia ujumbe asubuhi ajibu sa 8 usiku na usione shida.
Hujui wanaume wewe.
Mm na friends wa kiume ambao na pia najuana na ma girlfriends wao.
Kuna friend wangu mmoja nilikuwa napenda akiwa na mdada Fulani, ila huyu rafiki huwezi amini hana time naye.
Gf wake Mara kibao anakuja niambia niongee na rafiki yangu kwa nn anamfanyia hivyo.Mara hamtafuti mara nini....
Nikaja ongea na rafiki yangu hili ndo jibu alilonipa.
" huyo Dada napenda ila simtaki na siwezi mwambia ndo maana simtafuti ili yeye ajiongeze, ni mzuri, ni mpole, hana gharama,ana heshima nahisi nitamuumiza ni mwema kwangu ila sitomuoa namuonesha Singh zote simtaki ila haelewi.namuhitaji nikiwa na hamu nae basi tu, kama vip nisaidie kumwambia"
Mmmh nilichoka.