Nyeti za siri zinapochafukwa

Nyeti za siri zinapochafukwa

Mji mzito sana huu

Sir buyer hakuimbiwa parapanda, sasa limezukwa jipya.

Nyeti lazima ziwe za siri, hata zikichafukwa hazianikwi upenuni, labda zioze na kutoa uvundo mkali, lakini bado unaweza kuziswafi na tindikali kisha ukazihifadhi kwenye jokofu lililogandama kipupwe cha nyuzi baridi centigrade hasi 100.

Mji mzito sana huu. Kuna tafauti ndogo sana kati ya hasidi na hashua, japo kinyume chake kina kima cha kipenyo
Kama pembe la moo halifichiki, basi usijifanye kwio mbuni kufutika medulla ardhini ili kujikinga na hadhira isikutie machoni.

Mji mzito kwelikweli

Nyeti za siri zimeshaanza kudoda, kila mtu anatamba na kikingio chake. Hivi kudoda na kuvuja vinashabihiana ama kibantu kina maingiliano? Kwasababu tundu na tobo vinafanana lakini havishabihiani.

Je, uwazi nao ni tundu au ni tobo? Ama ni kipenyo?

Kipenyo penye uwazi, mwanya? Hupenyeza panapopenyeka na waja hupenyezeana. Wengine hupenyana
Bado tu utajinasibu na nyeti za siri?

Hivi hizi ni fununu ama ni tetesi au ni minong'ono?

Penye fununu hufunuliwa, penye minong'ono hunong'onwa, penye tetesi je? Panatestiwaa.

Nyatunyatu huleta kimuhemuhe kama kilivyo kisebubu japo hiki ni kiroho papo. Sio kiroho paaa, hiyo itakuwa blinking news! Habari za kumweka mweka

Mma yana hulka moja; hayazuiliki. Unaweza kuyakinga lakini si kuyazuia lazima yatatafuta upenyo yapenye. Na hata kama utayakinga yana kima chake. Yakizidi kima yatapasua na kuvunja kingo, na madhara yatakuwa kwa wengine wengi.

Hebu tufanyeni kikowa na kulimaliza hili lisifutikwe mchagoni, ndimi hazitatulia na midomo haitapumbaa....! na ndimi zisipotulia mafikara yataundiwa uhalisia kisha midomo itaropoka ropo!

Wakulaumiwa atakuwa nani?

Lisemwalo lipo kama halipo haliwezi kusemwa asilani.
Aliyeelewa anifanyie samare kidogo. Mpare kaniacha mbali sana
 
Nipo hapa Chattle Capital City naona kuna harakati si za kawaida zinaendelea hapa naona kuna ndege kubwa imetua kuna watu wameshuka wengi kiasi sijui wanakwenda wapi
Mkuu uongo wa namna hii utakusaidia nini?Kwa nini mnapenda kuingiza nchi kwenye taharuki isiyo na sababu?Si vizuri hivi mfanyavyo wakuu
 
Mkuu uongo wa namna hii utakusaidia nini?Kwa nini mnapenda kuingiza nchi kwenye taharuki isiyo na sababu?Si vizuri hivi mfanyavyo wakuu
My apology Kimpyempye hivi hapa nchini tuna sehemu inaitwa Chuttle Capital City? Ni muhimu sana tuzingatie maandishi tusije kupotosha maana
 
ndio nini sasa! si ungeandika kikwenu tu tujue moja. sijaelewa kabisaaaaa! nimenunaaaa
 
ndio nini sasa! si ungeandika kikwenu tu tujue moja. sijaelewa kabisaaaaa! nimenunaaaa
giphy.gif
 
Naam. Wanaojitekenya wakacheka wenyewe, si ajabu maana ni ya Ulimwengu 'RAHA JIPE MWENYEWE'. Lakini wanaojifinya wakalia 'WANA TATIZO' japo si ajabu. Achana nao maana wataumia sana lakini hamna namna. AJABU inabaki kwa wale wanaojifinya wakacheka. Hapo tunamwachia MUNGU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom