Nyeti za siri zinapochafukwa

Nyeti za siri zinapochafukwa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
370,426
Reaction score
857,705
Mji mzito sana huu

Sir buyer hakuimbiwa parapanda, sasa limezukwa jipya.

Nyeti lazima ziwe za siri, hata zikichafukwa hazianikwi upenuni, labda zioze na kutoa uvundo mkali, lakini bado unaweza kuziswafi na tindikali kisha ukazihifadhi kwenye jokofu lililogandama kipupwe cha nyuzi baridi centigrade hasi 100.

Mji mzito sana huu. Kuna tafauti ndogo sana kati ya hasidi na hashua, japo kinyume chake kina kima cha kipenyo
Kama pembe la moo halifichiki, basi usijifanye kwio mbuni kufutika medulla ardhini ili kujikinga na hadhira isikutie machoni.

Mji mzito kwelikweli

Nyeti za siri zimeshaanza kudoda, kila mtu anatamba na kikingio chake. Hivi kudoda na kuvuja vinashabihiana ama kibantu kina maingiliano? Kwasababu tundu na tobo vinafanana lakini havishabihiani.

Je, uwazi nao ni tundu au ni tobo? Ama ni kipenyo?

Kipenyo penye uwazi, mwanya? Hupenyeza panapopenyeka na waja hupenyezeana. Wengine hupenyana
Bado tu utajinasibu na nyeti za siri?

Hivi hizi ni fununu ama ni tetesi au ni minong'ono?

Penye fununu hufunuliwa, penye minong'ono hunong'onwa, penye tetesi je? Panatestiwaa.

Nyatunyatu huleta kimuhemuhe kama kilivyo kisebubu japo hiki ni kiroho papo. Sio kiroho paaa, hiyo itakuwa blinking news! Habari za kumweka mweka

Mma yana hulka moja; hayazuiliki. Unaweza kuyakinga lakini si kuyazuia lazima yatatafuta upenyo yapenye. Na hata kama utayakinga yana kima chake. Yakizidi kima yatapasua na kuvunja kingo, na madhara yatakuwa kwa wengine wengi.

Hebu tufanyeni kikowa na kulimaliza hili lisifutikwe mchagoni, ndimi hazitatulia na midomo haitapumbaa....! na ndimi zisipotulia mafikara yataundiwa uhalisia kisha midomo itaropoka ropo!

Wakulaumiwa atakuwa nani?

Lisemwalo lipo kama halipo haliwezi kusemwa asilani.
 
Ngoja zibaki fununu Mungu atafunua mwenyewe, wakale walisema kiburi si maungwana, Angelazwa mtu pema labda tungepata adabu na heshima ya kutoficha uchi ili tuzae! Sote bado twajiuliza kwanini ukimbilie kuomba mboga kwa jirani ili hali ya kuwa wewe umekuwa ukijinasibu una hela na mboga za kutosha na hakuna jirani wa kukutisha?

Ikiwa wewe ndio mwasisi wa kuamini masufuria na moto wa kuni katika upishi wako na ndio yamejaa jikoni kwako, Kwanini sasa usiyatumie hata ulipota mgeni? badala yake ukimbilie kwa jirani kumuomba gesi yake ili uivishe chakula chako hii ni aibu kwako jirani.. kimekushinda nini kupikia sufuria zako zilizo nyumbani kwako ukiamini chakula kinaiva tu vizuri bila shida.

Lazima tukubari kwamba shamba letu lina ngedere na tuanze msako ili tunusuru mahindi yetu. Yanini kujipalia mkaa?
 
Mabeuberu ni hatari kukukurunziza NI rahisi Kama kunywa uji wa mtimdi,Gwaudafi,Swaudwaumu,Huogu Chavez,etc,Uuougojwa Jambo la beberu new world order ulipo wapo wamewekeza vya kutosha wanauwezo they control weather think it man and take it seriously
 
Sikujua kama wewe na @ warumi ni mabinamu [emoji23]
Mji mzito series hii imejaa vitendawili, misemo na methali na tungo tata!

Everyday is Saturday................................😎
warumi Ni binamu yangu
Ila nina hakika kwenye kiswahili sanifu na kiswahili fasihi, somo la tamathali za semi ulifaulu kufeli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom