Mswahili,
Sintachoka kukupa DAWA!...na Inshaallah utakuja kubali maneno yangu.
Unasema makala hiyo umeipata toka gazeti la Mwananchi...nani kaandika hizo habari? achana na gazeti namtaka mtu aliyeandika hizo habari na pia nakuomba nipe sababu ya kukamatwa kwake!
Pili, Kisa chote cha Sheikh Kassim nakifahamu sii kwa kusimuliwa. hakuna mtu anayeweza kufahamu zaidi ya mwanae na labda hufahamu ya kuwa Nyerere aliwahi kumtembelea Sheikh Kassim akiwa mahtuti na sii Mwinyi muislaam mwenzie wala masheikh hawa wanaopiga maneno magazetini. Woote waliingia mitini utadhani wale wafuasi wa Yesu akina Yuda. Walionekana baada ya kufa kwake siku ya mazishi na kwa unafiki wao wakajitokeza kwa wingi. Walikuwa wapi alipokuwa kawekwa lumande akiteswa na kwa nini hakuna kati yao aliyesimama kutaka kufahamu ukweli wakati Nyerere akiwa hai...
Mwaka 1993 Nyerere alikuwa kesha mshindwa Mwinyi na Mwinyi alikuwa akisema wazi kuwa yeye ndiye rais na atachukua mkondo mwingine!...Mliyasema haya na kumsifia kwa kusimama kidede. Nyerere kafa kwa mengi, mchungu aliyokuwa nayo kwa hawa jamaa yalikuwa mazito na hakuwa na mtu nyuma yake tena. Ndio maana leo hii viongozi wote wezi tu hakuna anayekubali kufuata nyayo za Nyerere na wote hawa ni wanafiki tu wanaposimama majukwaani na kumsifu.
Hayo ya Kighoma Malima kauawa kwa sababu ya siasa kama alivyouawa Mwaikambo,Kombe na wengineo. Ukiwa against dira mpya ya CCM, kifo ni lazima. Viongozi wa ngazi ya juu kuondoka CCM ni Usaliti ambao hukumu yake ni kifo... Hawajali wewe dini gani ama gender ipi!
Nyerere kama angetaka kuwaua basi Kambona asingerudi, Mtei asingekuwepo hai na watu kama Fundikira wangekwisha long time.
Na sidhani kama unaweza kusema Mwaikambo aliuawa kwa sababu alikuwa mkristu.
Kama Nyerere angekuwa mdini asingewachukua wasomi wote wa chama cha hizbu na kuwatumia bara. Na ni haohao wasomi wenu waislaam wa hizbu waliompa intro (darasa) Nyerere kuhusu UJAMAA (socialism), mfumo ambao ulipingwa na wakristu wengi wasomi. na mbona sioni mkisema kuhusu kuchaguliwa kwa Mwinyi kama rais?... Kighoma kuna wakati kakosa kazi ama wadhifa?... mbona alikuwa juu miaka yote hali anachukiwa na Nyerere!
Na Tusivyokuwa aibu tunafikia kudai kwa takwimu ati waislaam walikuwa asilimia 80 shule za msingi miaka ya Nyerere!... jamani? sijui takwimu hizi mmezipata wapi ikiwa shule za msingi nyingi zilikuwa za wakristu. Sijawahi kuona wala kusikia shule yenye waislaam 80% unless shule hiyo ni ya kiislaam.
Hata hivyo..Je, sio sisi tuliokuwa tukililia uhuru kwa sababu watoto wetu walikuwa wakipelekwa Kenya na Uganda kupata elimu ya msingi?..Wewe na mimi na wengine kibao mswahili tumesoma wapi?...
Kisha basi, mwaka 1983 tulikuwa na shule za sekondari nchini zisizozidi 190, Je, kabla ya Nyerere zilikuwa ngapi ambazo wewe na mimi tungeweza kusoma... Ukweli almost zero!
Tazama basi waliokaa mtihani mwaka huohuo 1983 ni zaidi ya laki moja (150,000) only chini ya 10,000 walipata nafasi ya kwenda mbele!...yaani chini ya asilimia 10. Je, hamuwezi kuona kuwa tatizo hilo lilikuwa la kitaifa isipokuwa mnaliweka kuwa la waislaam pekee..Zaidi ya wanafunzi laki moja na arobaini walikosa nafasi ya kwenda mbele nyie mnatazama hesabu ya waislaam wangapi,ndio UDINI huo tunaouzungumzia.
Mbona hamsemi kuwa kila shule ya primary na sekondary za kiislaam asilimia 90 walikuwa watoto wa Kihindi?...Wahindi ni chini ya asilimia 5 ya waislaam wote nchini!...Hizi ndizo fact na usawa ikiwa unataka kutazama nje tazama kwanza kwako. wahindi na waarabu wamekutenga toka hujapata uhuru leo unataka kumsukumia mweusi mwenzako kwa sabau tu ni mkristu.
Mswahili, mwalimu alipokuwa akienda Bagamoyo alikuwa akimwona mzee mwenyewe marehemu mzee Juma bin Chewa!....Ramia alikuwa referal tu ikiwa ngoma nzito!..
By the way Umesema Maleysia waislaam walikuwa wakibaguliwa zamani... Na nani?
Je,unajua population ya waislaam Maleysia?.. Unajua kama Maleysia ni nchi iliyokuwa ikitawaliwa na Sultan wa kiislaam toka karne ya 12. Unazungumza kitu gani ndugu yangu!
Wana JF heshima mbele. Tarehe 14. Oktoba. 2008 tutaadhimisha miaka 9 tangu kufariki Mwalimu Nyerere. Nimekuwa nikitafakari sana zama za utawala wa awamu ya kwanza wa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kwa mtazamo wangu najaribu kukumbuka miongoni mwa maamuzi ninayoaminikwa mtazamo wangu ni magumu mojawapo ni "Kuingiza Tanzania katika Vita ya Kumng'oa nduli Idd Amin Dada wa Uganda aliyeivamia Tanzania" Mwalimu alitangaza vita tarehe 27. Oktoba.1978. Najua kwa nchi kama Tanzania ambayo ni masikini iliyokuwa ikijaribu kujiamsha kutoka katika lindi la matatizo lukuki ya ujinga, maradhi na umasikini kiongozi wake kuwa na ujasiri wa kufanya uamuzi huo kwa kweli kwangu mimi binafsi nachukulia ni changamoto ya aina yake....Wana - JF tujadili kwa yale mnayodhani kuwa pia yalikuwa maamuzi magumu yaliyofanya na Nyerere.
Ni ajabu,Mr.Game Theory, kwamba unaweza kuupinga Ujamaa,now of all times,wakati Federal Reserve,Benki kuu ya Marekani ina bail -outkampuni zilisofilisika. Mpaka Marekani watu wameeiita,USSRA,[kwa utani],United States Socialist Republic of America. Siyo
tu America,this bailing out by the Central Banks is going on all over the world. Huu ni wakati wa kuwaomba msamaha Marx,Lenin,Mao,Castro,Nyerere and all such people.
Kuhusu kumtukuza Mwalimu,kumuona kama Mungu Mtu,sijui una maana gani.These are just empty words,kwa sababu familia ya Nyerere ipo pale Msasani inaishi maisha ya kimaskini.
Kuhusu man,myth and legend,kama wanavyosema mashabiki wa John F. Kennedy,kwamba Kennedy was great,and that was what caused the myth and the legend,not the other way round.
Hakuna mtu anamsifu Mwalimu too much,we haven't seen that.
Kennedy alisema,
To my fellow Americans I say,ask not what America can do for you,but ask what you can do for your country. Haya mambo Kennedy alisema katika inaugration speech.
In the next sentence of that same speech,he said,
To the citizens of the world I say.
If we Americans set a high standard for you to emulate,we ask that you request us to t behave according to those same high standards that we set on you.
Na haya ndiyo yalikuwa maisha ya Mwalimu. It is not for nothing that he is being praised.
Yaani hii nostalgy with Ujamaa is dangerous, because we are romanticizing a very dark era in Tanzania! Socialism is DEAD! Saying that unbridled capitalism has its problems is one thing but Socialism does not work PERIOD!!!!!
The financial meltdown in the US and advanced economy may be scary and as immediate short term solution in order to avoid collapse that is why the government is bailing out, but this is nowhre near SOCIALISM!
Ujamaa was bad for Tanzania and we are just seeing the tip of the iceberg, all the side effects of it, including the mind set of our leaders who were proteges of Nyerere.
..Kama Nyerere angekuwa mdini asingewachukua wasomi wote wa chama cha hizbu na kuwatumia bara. Na ni haohao wasomi wenu waislaam wa whizbu aliompa intro (darasa) Nyerere kuhusu UJAMAA (socialism), mfumo ambao ulipingwa na wakristu wengi wasomi. na mbona sioni mkisema kuhusu kuchaguliwa kwa Mwinyi kama rais?... Kighoma kuna wakati kakosa kazi ama wadhifa?... mbona alikuwa juu miaka yote hali anachukiwa na Nyerere!
..Mkandara unawataja hawa wachache walionusurika kifo huoni na kwa kauli yako nyerere kaplay part katika nusura yao,je unajua wangapi waliochinjwa kinyama katika yale mauaji(genocide)kule unguja na Architect wake si alikuwa yeye Nyerere ?
Sahiba,
..
Hao hao wasomi wenu... una maana gani!..Mkuu hata sikuelewi unazungumza kitu gani hapa..kwani ukisoma hapo juu kisha ukasoma hoja inayofuata nashindwa kuelewa unachojaribu kucheza..
..
kweli Nyerere alikuwa Mdini Maana nimesikia kwenye BBC swahili, kwamba aliomba Fedha kwa Gadaffi ili kujenga Msikiti Butiama.nawasilisha Hoja
?????????????????????????????????????????????Mwalim alikuwa ana cheza mchezo kukidhi mambo yake kufanya hilo ni moja ya mbinu zake kuonesha ulimwengu anajali dini zote lakini kumbe alikuwa ni kama panya anakutafuna huku anakupuliza hata ukimuangalia wakati waislamu wanamchukuwa katika kupigania nchi bila ya kujali uislam wao mwalim alitumia ujanja na kufika kuvaa mavazi ya kislam ili aonekani kuwa yupo pamoja nao na hasa ukiangalia kwa wakati ule waislamu walikuwa na nguvu pale bara na mapenzi kwa kila tu hakukuwa na udini lakini mara tu baada ya mwali kutia madaraka katika makucha yake alianza kuwafyeka mmoja baada ya mwingie kwa kutumia mbinu zake tusijifanye tumesahau Mwali kati ya watu aliwatendea maovu ambayo hata kwa mmungu hatasameheka Alikuwa Bititi Mmungu muweke katika daraja kubwa ndani ya pepo yako alimtesa na kudhalilisha mwisho akampeleka zanzibar kwa karume kuendelea na mateso hakuna asie lijuwa hilo lakini tuekuwa tunaweka pamba masikioni Dua ya mwenye kudhulumiwa hairudi ikiwa muisalma au kristina hilo amelitamka mmmungu ukweli utatoka siku moja na hauko mbali kama ulivyotoka ukweli wa muembe chai maovu ya kambarage yatatoka siku moja kama ilivyotoa roho na kurdi kwa muumba basi maovu yake yatatoka huko yalikojificha na kujulikana na kila kiumbe katika kona ya ulimwengu