Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
15,989
35,656
Mwaka 1995 Jakaya Kikwete akijifanya ni masikini na Edward Lowassa akinukia noti, walisindikizana kuchukua fomu za kugombea urais, nyuma yao akiwepo king maker Rostam Aziz na Samuel Sitta.

Lowassa aliamua kukodi ndege binafsi chini ya captain Minje baba yake Lilian, walizunguka Tanzania nzima kusaka wadhamini, walikuwa na miaka 42 kwa 45 mtawalia. Wakajiita Boys II Men.

Aliyekodi ndege ni Lowassa Jk alipewa lift tu, makubaliano ni kuwa yeyote ambaye angepita amteue mwenzake kuwa Waziri mkuu na baada ya miaka kumi huyo waziri mkuu agombee urais, hapa ni kama Putin na medinedev wanavyofanyaga.

Taarifa zikamfikia mwalimu Nyerere kuwa kijana Lowassa anagawa pesa kama njugu na amekodi ndege, na akaambiwa anaambatana na mtoto wa rafiki yake marehemu Mrisho Kikwete, yaani Jakaya.

Mwalimu akamuita Jakaya Msasani ili kumuonya akae mbali na EL. JK bila kutambua akampa lift EL kwenye gari aina ya Ssang yong Musso mpaka msasani.

Taarifa zikamfikia mwalimu kuwa Jk kaja na EL, mwalimu akajifanya anatoka nje kwa hasira na kumfokea kuwa amechelewa appointnent atoweke haraka mahali hapo kufumba na kufumbua Jk kwa shingo upande akaondoka bila kujua sababu.

Mwalimu akidhani JK amegundua kosa lake, kumbe wapi, kwenye vikao vya mchujo Jk uso kwa uso tena na mwalimu, na akaulizwa if you become a president who gonna be your prime minister, JK akayakoroka kwa kusema Edward Lowassa, mwalimu akamwambia asante kwa kushiriki ,jina la JK likakatwa kibabe na akapachikwa Benjamin Mkapa.

Matumizi makubwa ya pesa katika kusaka madaraka yalimponza EL.

.....,....Itaendelea
 
Tuliokuwa ndani ya UV CCM wakati huo tunafahamu mengi sana

kama Mama Anna Makinda angeamua kuandika kitabu au kuandika ya nyuma ya pazia angeliandika vyema sana hili

Mwalimu alimwita Anna Makinda na kuna ujumbe aliotumwa binafsi kwa Jakaya na JK kabaki na siri hiyo nadhan hajawahi kuiweka hadharan aliambiwa nini na Anna Makinda

ni kama vile Mama Getrude Mongela alipopewa ujumbe rasmi na Mwalimu ampelekee Ndugu Ally Hassan Mwinyi 1985 muda mchache kabla ya uchukuaji fomu

Siasa ina mengi sana

Hatujui kwanini Jakaya baada ya kushinda kwny CCM 1995 iliamriwa kura zipigwe tena na baada ya hapo akaomba fursa azungumze japo vijana wenzie tulitamani agome

JK alikuwa Makonda wa Mwl Nyerere kwa mliokuwa hamjui

ndie alikuwa Katibu wa vikao vyote vya vita ya Kagera

ndie alietumwa kumshawishi Salim agombee Urais

ndie alie deal na Kighoma Malima n.k

pengine alipewa maelekezo maalum kuhusu Monduli maana hata Edward Moringe alitajwa sana kuwa Mrithi wa Mwalimu na ikashindikana

Hayati Jaka Mwambi aliekuwa Balozi wetu Russia na Msiri wa JK angeweza kuandika kitabu kizuri kuhusu Siasa za Wanamtandao

Huwezi kuzungumza rafu na makando kando ya Wanamtandao bila ya kuwataja Viongozi wa Wanamtandao

JK angelegea na kuruhusu kuachia Nchi wana Mtandao angelaaniwa na kila kiumbe kinachopata sunlight
 
Huu uongo wa kitoto sana.BM alikuwa ni kipenzi cha mwalimu kwa urais wa JMT baada ya Dr Salim,hiyo sababu dhahania haiwezi kutosha kumuondoa BM moyoni mwa mchonga
Salim alikuwa kipenzi namba moja ila akashindwa kumbeba,JK alimzidi kura BWM ila ikapigwa magazijuto ni vile JK kakomaa kisiasa vinginevyo angesharopoka hii siri
 
Mwalimu Nyerere KAMWE asingeweza kumwamini Lowasa kuwa rais wa nchi hiii
Sijakataa hilo,ninachopinga ni kuwa eti JK alinyimwa unyerere kwa vile alikuwa karibu na EL,mchonga alishaamua kuwa rais atakuwa BM iwe jua au mvua hata kama JK alishinda kwenye duru la kwanza.Lowassa alijua kuwa angegombea 2005 angepata shida kwa sababu ya jinamizi la mchonga ndio maana wanamtandao wakamtanguliza JK
 
Mwaka 1995 Jakaya Kikwete akijifanya ni masikini na Edward Lowassa akinukia noti,walisindikizana kychukua fomu za kugombea urais,nyuma yao akiwepo king maker Rostam Aziz na Samuel Sitta,
Lowassa aliamua kukodi ndege binafsi chini ya captain Minje baba yake Lilian,walizunguka Tanzania nzima kusaka wadhamini,walikuwa na miaka 42 kwa 45 mtawalia,
Wakajiita Boys II Men.
Aliyekodi ndege ni Lowassa Jk alipewa lift tu,makubaliano ni kuwa yeyote ambaye angepita amteue mwenzake kuwa wqziri mkuu ,na baada ya miaka kumi huyo waziri mkuu agombee urais,hapa ni kama Putin na medinedev wanavyofanyaga.

Taarifa zikamfikia mwalimu Nyerere kuwa kijana Lowassa anagawa pesa kama njugu na amekodi ndege,na akaambiwa anaambatana na mtoto wa rafiki yake marehemu Mrisho Kikwete ,yaani Jakaya .
Mwalimu akamuita Jakaya Msasani ili kumuonya akae mbali na EL,
JK bila kutambua akampa lift EL kwenye gari aina ya Ssang yong Musso mpaka msasani.
Taarifa zikamfikia mwalimu kuwa Jk kaja na EL,mwalimu akajifanya anatoka nje kwa hasira na kumfokea kuwa amechelewa appointnent atoweke haraka mahali hapo kufumba na kufumbua.Jk kwa shingo upande akaondoka bila kujua sababu,
Mwalimu akidhani JK amegundua kosa lake,kumbe wapi,kwenye vikao vya mchujo Jk uso kwa uso tena na mwalimu,na akaulizwa if you brcome a president who gonna be your prime minister,JK akayakoroka kwa kusema Edward Lowassa,mwalimu akamwambia asante kwa kushiriki,jina la JK likakatwa kibabe na akapachikwa Benjamin Mkapa.
Matumizi makubwa ya pesa katika kusaka madaraka yalimponza EL.
.....,....Itaendelea
Another sadist fella
 
Naona zimeanza kugeuzwa stories baada ya hayati kutajwa na kila mtu kua hakua na ubaya wala usaliti. Zimefufuliwa makala za kumsafisha aliechafuka kwenye msiba.

Kiukweli hata Mkwere mwenyewe moyo na nafsi vinamsuta kwa aliyoyafanya kwa Lowassa..

Waliyafanya kwa Mkapa,akaja akayafanya kwa Lowassa, nafikiri pia akayafanya kwa Magufuli.
 
Tuliokuwa ndani ya UV CCM wakati huo tunafahamu mengi sana

kama Mama Anna Makinda angeamua kuandika kitabu au kuandika ya nyuma ya pazia angeliandika vyema sana hili

Mwalimu alimwita Anna Makinda na kuna ujumbe aliotumwa binafsi kwa Jakaya na JK kabaki na siri hiyo nadhan hajawahi kuiweka hadharan aliambiwa nini na Anna Makinda

ni kama vile Mama Getrude Mongela alipopewa ujumbe rasmi na Mwalimu ampelekee Ndugu Ally Hassan Mwinyi 1985 muda mchache kabla ya uchukuaji fomu

Siasa ina mengi sana

Hatujui kwanini Jakaya baada ya kushinda kwny CCM 1995 iliamriwa kura zipigwe tena na baada ya hapo akaomba fursa azungumze japo vijana wenzie tulitamani agome

JK alikuwa Makonda wa Mwl Nyerere kwa mliokuwa hamjui

ndie alikuwa Katibu wa vikao vyote vya vita ya Kagera

ndie alietumwa kumshawishi Salim agombee Urais

ndie alie deal na Kighoma Malima n.k

pengine alipewa maelekezo maalum kuhusu Monduli maana hata Edward Moringe alitajwa sana kuwa Mrithi wa Mwalimu na ikashindikana

Hayati Jaka Mwambi aliekuwa Balozi wetu Russia na Msiri wa JK angeweza kuandika kitabu kizuri kuhusu Siasa za Wanamtandao

Huwezi kuzungumza rafu na makando kando ya Wanamtandao bila ya kuwataja Viongozi wa Wanamtandao

JK angelegea na kuruhusu kuachia Nchi wana Mtandao angelaaniwa na kila kiumbe kinachopata sunlight
Duh kwa hiyo mwaka 95 wewe ulikuwa kijana rika la j.k?
 
Back
Top Bottom