Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Imani ya CCM hiyo, ukiiweka katika perspective niliyoiweka hapo juu, "Kazi ni kipimo cha utu" na "binadamu wote ni sawa" zinaleta a philosophical contradiction.

Kama unatafuta cha kukosoa na ukaiweka hiyo kauli mbiu ya kazi ni kipimo cha utu katika maudhui sawa na binadamu wote ni sawa utapata mkanganyiko. Binadamu wote ni sawa inazungumzia mahitaji ya msingi ya binadamu katika maisha. Tajiri na maskini, jambazi na mchapa kazi muadilifu, fisadi na kibaka wote wanahitaji mahitaji ya msingi ili waweze kuishi kama binadamu.

Huwezi kuamini kwamba kazi ni kipimo cha utu, ukajua ukweli usiopingika kwamba kuna watu wenye nguvu na akili wanafanya biashara vizuri sana, na wengine wana nguvu na akili zile zile ni ombaomba, halafu ukasema "binadamu wote ni sawa".

Mimi nadhani unalazimisha ligi kwa kuweka hizo slogan mbili katika perspective moja!

Kwa sababu mtu ambaye amejidhihirisha kuwa mjinga na mfuja mali akija kukuomba limited resources wakati mmoja na mtu ambaye amejidhihirisha kuwa industrious utampa yupi?

Of course nitampa aliyejidhirisha kuwa na busara zaidi. Lakini wote wakinijua wana njaa na hawana chakula sitawaacha wafe njaa. Nitwapa wote kama na mimi ninacho.
 
Si nasikia Nyerere huyo huyo aliambiwa kuwa "Kaputula la Marx Halitamtosha", akainga'ang'ania kuivaa, ikaonekana kituko... yaani kama kavaa Bugaluu...!
 
Kama unatafuta cha kukosoa na ukaiweka hiyo kauli mbiu ya kazi ni kipimo cha utu katika maudhui sawa na binadamu wote ni sawa utapata mkanganyiko. Binadamu wote ni sawa inazungumzia mahitaji ya msingi ya binadamu katika maisha. Tajiri na maskini, jambazi na mchapa kazi muadilifu, fisadi na kibaka wote wanahitaji mahitaji ya msingi ili waweze kuishi kama binadamu.

Mimi nadhani unalazimisha ligi kwa kuweka hizo slogan mbili katika perspective moja!

Of course nitampa aliyejidhirisha kuwa na busara zaidi. Lakini wote wakinijua wana njaa na hawana chakula sitawaacha wafe njaa. Nitwapa wote kama na mimi ninacho.

Sasa CCM / Nyerere watakuwaje na imani mbili zinazokinzana?

On the one hand kazi ni kipimo cha utu, which would imply mtu asiyefanya/penda na kazi utu wake mdogo na hivyo hata kufikiriwa kwake katika msaada, kama ulivyotoa katika mfano wako juu, kuwe kudogo.

On the other hand watu wote wako sawa, kwa hiyo akija mtu industrious amepata matatizo ana njaa na mwingine ana njaa kwa sababu ya uvivu wote wasaidiwe sawa sawa.

Contradiction zaidi ya Bob Marley ambaye wimbo mmoja anakwambia "No Woman, No Cry" wimbo mwingine anasema "Woman go down on your knee and cry"
 
It seems that Nyerere was introducing Capitalism on the back door under socialism heading since if you look deeper what he advocated, the only similarities is that under socialism there could be capitalization as long as it was control and operated by the government. The government would make money though capitalization internally and externally. It would be a socialist country operating under capitalist ideas and using capitalist ideas to provide for their citizens.

Under capitalism the government would allow the citizens to use capitalism to make money to provide for themselves while at the same time the government would use the same system to provide some socialist comforts or the citizens though taxes, and contributions. There are numerous examples like social security system, welfare, health programs, and employment programs etc; these are all socialist programs the capitalistic country like the UK also uses...

Nyerere was a very clever and smart man... That what I can say...
 
His policies have contributed to a lot of dismal performance of our economy. His rule has not solved ANY of our major calamities: UJINGA, UMASIKINI, NJAA NA MARADHI. So I don't see any big deal.
To be fair on him, he was a far better leader than what HE LEFT US WITH!
 
Wewe mzee inaonyesha hata imani yako uniamini kinafiki tu, huwaamini kabisa waliokufa!
Kwani naamini hata kwenye imani yako kuna mananabii/mitume waliokufa wakazikwa wakaoza hadi mifupa na nywele zao lakini unawaamini na kuzingatia maneno yao!! Inakuwaje unaamini watu waliozikwa na kuoza!?

Unantafuta katiaka imani? hayo yaache, usisahau kuwa ni Mwalimu Nyerere mwenyewe ndiyo alieashiria kusema kuwa atazikwa na azimio la arusha namnukuu "....popote ninapokwenda, natembea na vitabu viwili, yaani Bibilia na Azimio la Arusha..."
Sasa Bw.MziziwaMbuyu, Mwalimu kenda akhera...si ndiyo?!...atakuwa kaenda na nini? si lazima awe na Bibilia na Azimio la Arusha mkononi japo moyoni mwake tu.
Na kuhusu hitaji la mawazo yake na azimio la arusha lenyewe, nambie nani katika Tanzania ya leo anafuata au anataka kufuata azimio la arusha au mawazo ya Mwalimu, si serikali wala chama cha Mapinduzi, hiyo ndo maana ya kusema kuwa mambo hayo kafa na kuzikwa nayo na hakuna mwenye haja nayo sasa, watu wapo biz kujitajirisha na kuneemesha matumbo yao.

Unajua saa zingine hizi dharau zetu na kijifanya kujua mambo ndio kitu kikubwa kinachotuondolea uwezo wetu wa kupambanua mambo, na hilo ndio lililo na linalorudisha nyuma taifa letu lenye neema zilizotunzwa na sera unazozikataa za Mwalimu, sijuhi kama Mwalimu asingefuata hilo Azimio na hiyo Miiko ya uongozi hii nchi sijuhi ingekuaje, kwa kifupi kutokana na kutoelewa kwetu nchi kama Norway, Finland na zingine za scandnavia wanatushangaa sana WaTanzania kwa kutomwelewa Mwalimu, Azimio la Arusha ni case study kubwa sana kwenye vyuo vya Norway na theory nyingi tu za Mwalimu wanazipractise na zinawork out, na baada ya kutuona atumwelewi mwalimu walikuja Tanzania kutusaidia kwenye hii self reliance, hao jamaa walikuja na DANIDA, FINIDA etc na walijikita sana kwenye vyuo vya VETA, lakini wapi wapo watu ambao wanajua kila kitu, miiko ya ungozi zirro,Lakini mimi nadhani ni sisi waTanzania tu tusiokuwa na uelewa sahihi wa kile mwalimu alichokuwa anazungumza, yeye alikuwa kwenye Dunia nyingine kabisa ambayo sisi bado hatujafika, lakini iam sure Wazungu wengi hata hao sisi tunaowaona mabepari wanamkubali na wanapractice baadhi ya theory zake

Hapa hapana cha dharau, rejea majibu ya hapo juu kwa Mkuu MMk.
 
SERA ZA ZAMANI hazina nafasi katika uchumi wa kisasa na kama mnataka turudi kule ambako tlipotoka wakati tunaishi Dunia ya watu walioelimika.Watu wenye kutumia teknolojia Basi tutashindwa.

Mwalimu alikuwa BORA ila siyo kila jambo aliloseam Mwalimu tulienzi!
 
1. 'WATU WOTE NI SAWA'
"...Kama hukubali hilo, yaani kama unadhani watu wengine ni miungu wengine, malaika, wengine nusu-nyani, basi hukubali ujamaa. Ujamaa kwako hauna maana, kwa sababu ujamaa unahusu usawa wa watu: hapo ndipo unapoanza...Sisemi usawa wa urefu wala ufupi; kwa urefu namzidi Kawawa, sana tena. Sisemi maguvu, hata; nasema utu, watu, na ubinadamu wao. Kuna binadamu zaidi ya mwenziwe? Kama huliamini hilo, utakuwa mjamaa? Hilo la kwanza... mkaliulize-ulize, mlielewe maana yake. Na mtu anayepinga ujamaa naye ajiulize kama anapinga hilo nalo. Mtu mpingaji ujamaa aseme, 'Hilo nalo, usawa wa watu, napinga; kwamba binadamu wote hivi si sawa'" - Mwalimu Julius K. Nyerere

2. 'LAZIMA MTU AFANYE KAZI'
"...Binadamu hao unaotuona hapa, na hao waliosambaa dunia nzima wanaishi kwa kazi. Hawana namna nyingine ya kuishi. Wakiacha kufanya kazi watakufa; hawana namna nyingine; kuishi kwao, na kuendelea kuishi, lazima wafanye kazi...Lakini binadamu haishi kama farasi. Binadamu haridhiki kuishi kama farasi au punda; binadamu ana kitu anakiita maendeleo; lazima aendelee...Wakati mwingine ili kusudi maendeleo haya yaje wana shughuli za kupigana misasa akili, wanapanuana mawazo tu, nayo ni kazi...nendeni mkaulizane...kama kazi si kitu cha lazima, kama binadamu anaweza kujikalia tu hafanyi kazi, akaishi, na maendeleo yakaja bila kazi. Na huyo anayepinga ujamaa naye ajiulize kama hilo analipinga? Na hilo la kufanya kazi analipinga au kuna jingine analopinga?" - Julius K. Nyerere

3. 'HAKUNA MTU KUMNYONYA MTU'
"...Kama binadamu ni sawa, tunalikubali hilo...Pili tunasema kitu kazi ni jambo la lazima kwa kila mtu, hakuna aliyesamehewa kazi. Basi siwezi kukufanyia kazi. Kukufanyia kazi maana yake ni kwamba wewe unasamehewa kazi! Siwezi kukufanyia kazi. Wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya. Sio mimi nifanye, wewe hufanyi; lazima ufanye kazi. Kwa hiyo wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya kazi; kila mtu atafanya kazi. Yaani namna ya kulitamka hilo ni kwamba kunyonyana hakuna. Hakuna mtu kumnyonya mtu; sasa tena msingi wa kumnyonya unatoka wapi? Tumesema watu sawa; na mtu ili aishi hana budi afanye kazi, na kazi ndio msingi wa maendeleo. Sasa mwanachama... ajiulize kama anaweza kuwa mjamaa na huku ananyonya! Unamnyonya mkeo; mkeo anakwenda kufanya kazi wewe unakwenda kupiga chibuku; hivi kweli mjamaa wewe? Tunasema kazi jambo la lazima, lakini wewe hufanyi kazi, unamnyonya mkeo. Wewe mjamaa? Nasema na hilo mjiulize...Unaweza kuwa mjamaa na huku unanyonya? Na anayepinga ujamaa ajiulize hilo nalo analipinga, kwamba yeye anaona kunyonya ni sawa tu! Sawa yeye kunyonya mwingine au wengine kumnyonya yeye, huyu anayesema kunyonya ni sawa. Kama kunyonya ni sawa baba, sasa tuanze kunyonya, au mkuki kwa nguruwe?" - Julius K. Nyerere

4. 'VYOMBO MUHIMU VIMILIKIWE PAMOJA'
"...Kama watu ni sawa; binadamu wote ni sawa; kazi ni jambo la lazima kabisa; kunyonya ni haramu; la nne linafuata: Vyombo vyote vya lazima, vinavyohitajika kwa maisha ya binadamu kwa kufanyia kazi lazima vimilikiwe kwa jumla. Ardhi lazima imilikiwe kwa jumla maana tusipoimiliki ardhi kwa jumla tutamwachia Rashidi Kawawa na Sheikh Karume wao wawe ndio wenye ardhi, na ardhi ni kitu cha lazima kwa maisha, hebu tuone kwanza usawa utakuwaje. Itakuwa lazima twende kwa Rashidi na kwa Karume, 'tafadhali bwana nataka ardhi'. Umekwishamwita 'Bwana' huyu; usawa umekwisha. Lakini vilevile kama Sheikh Kawawa ana ardhi, na Sheikh Karume ana ardhi, hawa hawalazimiki kufanya kazi. Kwa nini wafanye kazi? Hawawezi kufanya kazi. Tumesema kazi ni kitu cha lazima kwa kila mtu, lakini hawa hawawezi kufanya kazi, watakaa tu wanatutoza kodi kwa ardhi yao. Ndiyo wanatunyonya hivyo tena. Mimi nafanya kazi; mimi nalima. Halafu Rashidi anasema, 'Ukishalima mahindi ukapata magunia matano, moja langu'. Ndio ananyonya hivyo. Anavunja kanuni ya usawa; anavunja kanuni ya kazi; anavunja kanuni ya kutonyonya. Kwa nini? Kwa sababu tumemruhusu amiliki yeye vitu ambavyo vinastahili viwe vya wote. Mtu ambaye yeye ana ardhi; umemkabidhi viwanda, ukishakuwa umemkabidhi majambo mengine haya, umemwongezea nguvu zake, yeye utu wake umeongezeka-ongezeka na wangu mimi umeupunguza-punguza. Kwa hiyo vitu vilivyo vya lazima kwa kila mtu, kama ardhi ambayo ni ya lazima kwa kila mtu, lazima vimilikiwe na wote. Sasa...mjiulize kama unaweza kuwa mjamaa kweli huku unajidai ardhi yangu? Na wanaopinga wanatakaje? Hao wanaosema ujamaa mbaya. 'Eti vitu vyote viwe vya ujumla'; wengine waongo, 'Eti wanasema hata wakina mama wawe wa jumla'. Tunasema ardhi, hatusemi kina mama, tunasema ardhi viwanda, madini: kwa nini mtu mmoja anakwenda kuvinyakua vikawa vyake hivi!" - Julius K. Nyerere

5. 'KUUNDA NCHI BILA MATABAKA'
"..Kama tunakubali kuwa watu wote ni sawa; na watu wote ni lazima wafanye kazi, mtu asimnyonye mtu; na mali, mali kubwa, sikusema shati langu liwe la Rashidi: misingi ya uchumi kama mabasi yale yanapita iwe kwamba tunasema mabasi yetu, asiweko mheshimiwa mmoja pale anasema 'Basi langu lile!' Basi lako! Yupo dereva mle anaendesha, anasema dereva wake! 'Dereva wangu' - dereva wako, wewe unaweza kuwa na dereva? Dereva anaweza kuwa dereva wa umma, sio dereva wako. Dereva ni sawa sawa na mwalimu; mwalimu wa umma, daktari wa umma, dereva wa umma. Huyu anakuwaje 'wako'? Hata askari siku moja utasema wako. Kama tunakubali watu wote ni sawa; watu wote lazima wafanye kazi, hakuna kunyonyana; mali,vitu vyote vile vya jumla lazima viwe vya umma; maana yake ndio kusema tunataka kuunda nchi ambayo haina tabaka: hakuna mabwana na watwana." - Julius K. Nyerere

- Haya mawazo yote yamepitwa na wakati, huenda yalikuwa valid with time yaliposemwa, not anymore na it does not in anyway diminish Mwalimu's accomplishments ambazo in my opinion were education, and re-locationism only!

- Maapologists wa Mwalimu, mfike mahali mkubali kwamba Mwalimu alikuwa bina-adam mwenye mapungufu makubwa sana kama sisi wengine wote, na ni mapungufu yake kama bin-adam na kiongozi ndiyo yametukwamisha Tanzania 19 years toka atoke, kwa sababu scientifically inachukua atleast 100 years kabla binadam hajaachana na mawazo na tabia mbaya au nzuri alizolazimishwa kuzi-conform against his will bila kuamua kama ni nzuri au mbaya kwake na kwa future yake, that is exactly what Mwalimu did.

Maendeleo ya taifa huanzia majumbani mwa wananchi wa taifa lile, wananchi waliokuwa wakiishi kwa wasi wasi kusubiri kukuche ili wakajipange foleni kila siku kununua unga wa njano tu, sasa kweli utashangaa kwamba kwanini leo tuna taifa la wasi wasi? Nenda majuu uingie nyumba nyingi za wabongo utakuta jitu limejaza unga wa ugali, masukari, michele, minyama kwenye freezer unafikiri ni kwa nini hasa mkuu? Wakati hivi vitu havijawahi kukosekana huko madukani majuu hata siku moja? Ni watu ambao pamoja na kuwa majuu bado wana ile tabia ya wasi wasi, waliyofundishwa na siasa za Mwalimu, who was a good man lakini politically naive ndio maana akaishia kutuachia kina Mwinyi, Mkapa, na Muungwana!

- Sasa simple math ni:- 100 years - 19= 81 more years of misery! Pheeeeew!

Respect.

Kamanda FMEs!
 
FMES,
Maapologists wa Mwalimu bado tupo. Tunaamini Mwalimu alikuwa visionary na mawazo yake hayajapitwa na wakati. History is going to prove us right!
 
FMES,
Maapologists wa Mwalimu bado tupo. Tunaamini Mwalimu alikuwa visionary na mawazo yake hayajapitwa na wakati. History is going to prove us right!

- What is there to prove zaidi ya wananchi waliolala usingizi wanaodhani Rostam anaweza kuwafadhili upinzani kwa siri, bila CCM na serikali as whole kujua? au kuwa involved, i mean enough said jamani na huu uzumbukuku wetu wa siasa!

Respect.

Kamanda FMEs!
 
FMES,
Kwa taarifa yako wananchi hawajalala. Otherwise tunapoteza muda wetu bure hapa JF. Waliolala ni CCM na hao wanamkingia kifua RA.
 
- JF hatujalala lakini kuna mnaotaka kutulaza kila tunapotaka kuamuka, na nyimbo za Mwalimu, wakati tunajionea kwa macho yetu wenyewe aliyotuachia yaani kina Mwinyi, Mkapa na Muungwana, please tuacheni wananchi tuamue njia tunayotaka kwenda baada ya kuwa chini ya minyororo ya utumwa for 24 years, sasa tuko huru leave us alone!

- Mawazo yaliyomshinda tha originator mwenyewe, akaiona NBC ikiuzwa kwa bei poa, hayawezi kutusaidia wananchi wa Tanzania in any way or form, waliofaidika under his system ya nchi bila matabaka tunawaona kila siku, pleasee tuacheni tuhangaike lakini siku moja tutaiona njia kwa kutumia mawazo yetu mapya sio yalitopitwa na wakati, na yaliyomshinda the originator mwenyewe!

Kamanda FMEs!
 
It seems that Nyerere was introducing Capitalism on the back door under socialism heading since if you look deeper what he advocated, the only similarities is that under socialism there could be capitalization as long as it was control and operated by the government. The government would make money though capitalization internally and externally. It would be a socialist country operating under capitalist ideas and using capitalist ideas to provide for their citizens.

Under capitalism the government would allow the citizens to use capitalism to make money to provide for themselves while at the same time the government would use the same system to provide some socialist comforts or the citizens though taxes, and contributions. There are numerous examples like social security system, welfare, health programs, and employment programs etc; these are all socialist programs the capitalistic country like the UK also uses...

Nyerere was a very clever and smart man... That what I can say...

Ndugu hii kitu inaitwa STATE CAPITALISM, kina CLR James na Raya Dunayesvkaya walishaichambua aina hii ya Ubepari wa Dola miaka ya 50.
 
Si nasikia Nyerere huyo huyo aliambiwa kuwa "Kaputula la Marx Halitamtosha", akainga'ang'ania kuivaa, ikaonekana kituko... yaani kama kavaa Bugaluu...!

Jamani kuweni wakweli hata kama hamumkubali Mwalimu. Hata 'mwanzilishi'/mtunzi wa hilo dongo la 'Kaptula la Marx', Prof. Kezilahabi, anajua fika kuwa Nyerere hakuwa Mmarxisti - Wamarxisti wa Kiafrika tunawajua. Mwalimu hakuvaa kabisa kaptula la Marx na ndio maana Ujamaa wake ulikuwa sio wa Kimarxisti bali ulikuwa ni Usoshalisti wa Kiafrika uliojikita katika hizo nguzo 5 alizozianisha katika hotuba yake ya Saba Saba, 1970. Nyerere alivaa Lubega la Kinjeketile na kubeba Kifimbo cha Mkwawa. Rejea maneno yake mwenyewe hapo chini:

"If you are building society in terms of equality - even from a purely Marxist point of view (and I was not a Marxist) - all basic societies (what they call primitive societies) build upon the individual, but an individual in society. And I said, why don't you begin from there? In the modern world you are thinking in terms of a big society, but where the central communities are strong and some people have destroyed them, we are trying to build them - or we still have them. So why don't we build Ujamaa on the basis the attitudes which we already have here?" - Mwalimu JK Nyerere as interviewed by Bill Sutherland & Matt Meyer in Butiama.
 
Unless you are using this to show that Nyerere was disassociating himself with the Marxists (and whats with the past tense in that?) the rest is just unremarkably stating the obvious, unless of course the context is lost due to the shortness of the quote.

But nothing remarkable at all in that quote, just stating the obvious, some would even go as far as seeing this as self defeatist in that if he knew so much about focusing on the individual then why was he such a collectivist?
 
- Haya mawazo yote yamepitwa na wakati, huenda yalikuwa valid with time yaliposemwa, not anymore na it does not in anyway diminish Mwalimu's accomplishments ambazo in my opinion were education, and re-locationism only!

Respect.

Kamanda FMEs!

kitu gani kimepitwa na wakati
1. watu wote ni sawa - watu wote wapate haki sawa mahakamani/ polisi n.k
2.lazima mtu afanye kazi - ili taifa liendelee lazima watu wafanye kazi
3.hakuna mtu kumnyonya mwezake - wote lazima wawajibike kama ufanyi kazi unatakiwa uwe sacked, najua sio hivyo serikali inategemea na nani unamjua
4.vyombo muhimu vimilikiwe kwa pamoja - vyombo muhimu vimilikiwe na serikali, ardhi una lease kwa 33, 66 ,99yrs na hii hipo hata uk leo hii
5. KUUNDA NCHI BILA MATABAKA - watoto wa vigogo tu ndio wanafanya kazi za juu bot, kama vile ccm ni watoto wa vigogo tu hilo ni tabaka tiyari

inategemea na wewe unataka kuzitafsiri vipi ukitaka zionekane zimepitwa na wakati, zitakuwa zimepitwa na wakati.

hii ni misingi ya haki ambayo ipo western world, na ndio maana waTZ wengi wakifika wanafurai kuondokana na minyanyaso ya matabaka iliyopo africa.

ajenda za socialism nyerere amezitoa uk, akiwa edignburg univeristy, alikuwa kwenye labour left think tank
mfano vijiji vya ujamaa ukiwa uk kila eneo(kitongoji) kuna shule, hospitali na local centre, kwa wale wanaoishi vijijini wako mbali na shule hospitali n.k, ndio maana nyerere akawaambia kaeni karibu ili muweze kupata huduma za jamii kwa pamoja,serikali aiwezi ku-afford kuwajengea mkiwa mbalimbali
 
Last edited:

Semilong,
FMES may be right ukiangalia CCM ya sasa inayokwenda na wakati.
1. Watu wote Tanzania ya leo si sawa. Kuna wale wanaojiona more equal than others. Hasa ndani ya CCM.
2.Lazima mtu afanye kazi. Leo katika CCM kuna njia ya mkato. Inaitwa tajirika kwa ufisadi.
3. Hakuna mtu kumnyonya mwenzake--imeshapitwa na wakati. Wakubwa leo wanashirikiana na akina Sinclair kuwanyonya Watanzania wanyonge.
4. Vyombo muhimu vimilikiwe kwa pamoja---CCM ya leo imeshayakataa hayo tangu walipokwenda Zanzibar. Lazima, na wamo njiani kuunda tabaka la wamiliki wa vyombo muhimu. Kwa hiyo sishangai FMES na wana CCM wengine leo kudai kuwa fikra za Mwalimu zimeshapitwa na wakati. Angalia mambo wanayoyafanya ndani ya Tanzania ya leo. And you can go on ad infinitum.
 
Junius na hili The Junius Pamphlet limezikwa, hakuna anayelitaka saa hizi?
Though i support the work of Rosa Luxemburge, but i am different from her....very different....I am sir Francis Bacon....sharing the same pen name with Rosa. Bacon,is he, whose works and ideas still works, whose sacrifice for the freedom of expression is still live, who dared to open his mouth and throgh pen he wrote and tell the king under the Pseudonymous name "junius" that "king can do wrongs....and its never true that king can do no wrongs..." ref: Wilkes v/s Woods,
compared me more to the likes of Demosthenes, Seneca and Cicero, classical authors who had like me ended their lives in disgrace because of telling the truth.
If you find it comfortable refer to the 'junius's works of 'novum magnum' and 'Proficience and Advancement of Learning'.
 
Ujamaa... ujamaa, wachaaaaa....che walifaidika... Na weeeeengi wakaathirika. Leo siyasa ya ujamaa, imefirisika. Nchi nyingi Ujamaa wameuzika.
 
Back
Top Bottom