Nyerere alisingiziwa mengi sana

Nyerere alisingiziwa mengi sana

Kweli alitaifisha shule za kanisa lakini hata za waislam nazo alizitaifisha.
Mm nahisi vijijini anachukiwa zaidi kuliko mjini hasa lililo mchukiza ni uhujumu uchumi.
Ukizingatia waislam wengi ni wajasiria mali kuliko kuajiriwa.
Na usiwaone kina mzee ilunga na ponda tu kila utwala wake unawatu wanauchukia leo tunao kina gwajima na mapadri wengi tu wanaohubiri chuki dhidi ya utawala halali wa ccm na kikwete.
Kuhusu ustawi wa kanisa hili halina shaka kuwa serikali ina msukumo mkubwa ktk ustawi huo leo serikali inatoa mabilion ya shg kwenda ktk kanisa na sijawahi kusikia Cag akikagua matumizi ya pesa hizo.
Kama mm mtu wa mtaani nitajuaje kama zinatumika kwa malengo yalio kusudiwa?
Nikisema pesa hizo zinajenga makanisa zina nunua magari ya mapdri zinasomesha wakiristo tu nk nitakuwa nimekosea?

Serikali kutoa mabilioni kwenda kwenye kanisa hilo halikwepeki. Hivi wewe ukijenga Hospitali zako halafu serikali ikasema inataka pia watu wake watibiwe kwenye hospitali hizo kwa bei nafuu, wewe utatoa bure?, je kama utasema Serikali nayo ichangie gharama utahitaji tena Serikali ijue unatumiaje/CAG?, kutumia si juu yako?. Mfano pale Muheza, kuna hospitali moja kubwa inaitwa Teule, hii ilijengwa na kanisa, lakini kama 85% ya wakazi wa Muheza ni Waislam, wanahudumiwa na hospitali hii, sasa kwanini serikali isitoe ruzuku watu wapate huduma.

Kuhusu Kikwete kuchukiwa na Mapadre sina uhakika sana maana asilimia kubwa ya Uzinduzi wa Project za Kanisa zimezinduliwa na Kikwete, sijui hiyo kama ndio definition ya kuchukiwa. Viongozi wa dini hawamchikii Kikwete bali bali wanamkosoa kwa Idea yake ya kugawa watu kwa dini zao kwa kuahidi Mahakama ya kadhi wakati akijua kuwa nchii hairuhusu dini kuingia kwenye katiba. Ukristo hauna chuki na mtu, ukikuta Mkristo ana chuki ujue ni shetani tu kamuingia maana Yesu anasema amri kuu kupita zote ni UPENDO
 
Asilimia kubwa ya waislam japo si wote, ila wengi wao wanamchukia nyerere, sijajua wanafundishiana wapi hizo chuki kwa nyerere, na sababu kubwa kabisa sijaijua mpaka leo,
 
IQ ya kikwete ni kubwa sana anagalia mafanikio yake kwa miaka 10 tu alio ikaa ikulu. Anzia elimu, afya, miundo mbinu, mawasiliano nk....
Ndio utajua nini maana IQ mtu amekaa robo karne ikulu lakini tulikuwa tunakaa fuleni ya boflo tu. Sembuse mahitaji mengine.
Jiulize robo karne alikuta lami km ngapi na alicha km ngapi? Mm ninayoijua ni dar to tunduma na sijui kama hawakujenga mzee mabotu na kaunda..kwa kuwa walikuwa wanapitishia mizigo yao.

Hahaha pole sana, Nyerere alikuta nchi iko gizani, wenye degree hawafiki hata 5, Nyerere akaanzisha shule, vyuo, Mahaspitali, Akaanzisha viwanda nk.

Kikwete anamaliza kuapishwa anapelekwa Ikulu na Benz yenye AC, anakuta Ikulu kuna Mayai, Mkate na kila aina ya anasa. Kikwete anakuta kuna ndege ya Rais, Kikwete akiangalia BOT anakuta Mkapa kamuachia Mamilioni ya Dola kwa ajili ya kuanzia kazi. Any way, mkuu sahim1, maisha aliyopitia babu yako na wewe ni tofauti sana. Pia watu kupangana foleni, hizi zilikuwa ni siasa za mlengo wa ujamaa, lengo lilikuwa zuri, tumuhukumu mtu kwa malengo yake na siyo kwa failure yake. Ni sawa na mtu kukushawishi mvuke mto muende ng'ambo mkatafute mali, lakini mkiwa njiani Mamba anakukata mguu halafu ukamlaumu yule alietaka ukapate mali ng'ambo ya mto
 
Pitia tu hii nyuzi, mengi yatajitokeza.

Unajuwa sababu kubwa ya kuuweka huu uzi ni double standard iliyopo sasa hivi.

Namba 1.

Nyerere hakupigania Uhuru na alidai Uhuru tena akiwa si peke yake, wazee wa Dar walimpokea na akashirikiana nao kwa hali na mali katika kutimiza hilo, wazee wa Dar walifurahi sana kupata kijana msomi aliyesoma hukohuko kwa wazungu kuwa kaja kuwatafuta na kuwanao bega kwa bega, walimheshimi sana Nyerere. Rejea kitabu cha Mohamed Said, The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-68). Utaona jinsi Nyerere alivyoishi na hao watu wa Dar., na mikakati yao iliyofanyika ya kudai Uhuru.

Cha kushangaza hao wazee aliowatafuta mwenyewe Nyerere Dar., na waliompokea na waliokuwa naye bega kwa bega kudai Uhuru, leo wamesahauliwa kabisa katika historia na ili ionekane ni jitihada za Nyerere pekee basi limtungwa neno "kapigania Uhuru" na si "kadai Uhuru".

Leo neno hili linazuwa mapya, sasa kuna chama cha kisiasa kina sera za "wapiganaji", ukiwauliza mnapigania nini? majibu ni "kuikomboa Tanzania". Kuikomboa kutoka kwa nani?

Cha kushangaza zaidi, wale waliopigania kujiweka huru na utawala wa kikoloni na waliomwaga damu zao, rejea vita ya majimaji, vita ya Mkwawa, vita ya Bushiri. Hao wote hawatajwi kupigania na hata majina yao hayajulikani na walipoteza roho zao kwa kutaka wasitawaliwe. Kulikoni?

Tunataka historia iwe ya ukweli na vizazi vijavyo viuelewe ukweli na si historia ya kupindishwa pindishwa.

Ntakuja na maelezo mafupi kwa mengine. Kila tunavyoendelea.

Hizo point nimeziweka makusudi ili watu waje wafunguke. Kuna wachache waliokwenda sshule wameliona hilo na wanafunguka ki aina yao, lakini "majority" wanaacha hoja wananishambulia binafsi, nilitegemea hilo pia lakini nnawaona ni misukule wasiojuwa walinenalo na zinawashika hasira mpaka povu linawatoka na wanasahau kuwa hata Nyereree mwenye alisema, yeye si malaika na yale aliyokosea tuyaache.

Sasa hapa waje na yale ambayo si makosa ya Nyerere tuyashike na yale tunayoona kuwa ni makosa tuyazungumze ili tuyaache tusiyarudie.

ishi kwani wazee wa DAR tu, nakati alizunguka Tanganyika nzima kuongea na kushauriana na wazee...kama ni wazee inafaa heshima yake iwe wazee na kwa ufasaha zaidi waitwe watanganyika kwani sio hao wa DAR tu ndo walifanikisha uhuru....utakua umebagua na wazee wengine walioshiriki uhuru.....Hakuna namna yakulalamika kuwa wapo walio pigania uhuru na hawakutajwa....Nyerere ndo aliibuka shujaa na ndoanayefaa kupewa kipaumbele.....siku zote nyuma ya mafanikio ya mtu kunawatu wengi sana.....hujui hata mke wake kasaidia kipi katika kupatikana uhuru wa nchi hii......hakuna waliosahaulika unaweza kuiongezea historia tu....
 
Kweli alitaifisha shule za kanisa lakini hata za waislam nazo alizitaifisha.
Mm nahisi vijijini anachukiwa zaidi kuliko mjini hasa lililo mchukiza ni uhujumu uchumi.
Ukizingatia waislam wengi ni wajasiria mali kuliko kuajiriwa.
Na usiwaone kina mzee ilunga na ponda tu kila utwala wake unawatu wanauchukia leo tunao kina gwajima na mapadri wengi tu wanaohubiri chuki dhidi ya utawala halali wa ccm na kikwete.
Kuhusu ustawi wa kanisa hili halina shaka kuwa serikali ina msukumo mkubwa ktk ustawi huo leo serikali inatoa mabilion ya shg kwenda ktk kanisa na sijawahi kusikia Cag akikagua matumizi ya pesa hizo.
Kama mm mtu wa mtaani nitajuaje kama zinatumika kwa malengo yalio kusudiwa?
Nikisema pesa hizo zinajenga makanisa zina nunua magari ya mapdri zinasomesha wakiristo tu nk nitakuwa nimekosea?
Nakusoma kwa ukaribu mno naendelea kupata darsa.
 
Kuhusu ustawi wa kanisa hili halina shaka kuwa serikali ina msukumo mkubwa ktk ustawi huo leo serikali inatoa mabilion ya shg kwenda ktk kanisa na sijawahi kusikia Cag akikagua matumizi ya pesa hizo.

Kanisa limekuwa likitoa huduma hata kabla ya nchi iitwayo Tanganyika kufikiriwa kuwepo, unaposema serikali inanufaisha kanisa ni kudhalilisha kanisa, 26% ya Hospitali zote duniani ziko chini ya Roman Catholic, bado ujaweka Anglican, Lutheran, Othodox nk. Kama ngeli inapanda soma hii,



The Roman Catholic Church is the largest non-government provider of health care services in the world.[SUP][1][/SUP] It has around 18,000 clinics, 16,000 homes for the elderly and those with special needs, and 5,500 hospitals, with 65 per cent of them located in developing countries.[SUP][2][/SUP] In 2010, the Church's Pontifical Council for Pastoral Assistance to Health Care Workers said that the Church manages 26% of the world's health care facilities.[SUP][3][/SUP] The Church's involvement in health care has ancient origins.

"In the United States, 50 percent of social services are provided by the Catholic church," said Keating, who now serves as president and CEO of the American Bankers Association.

For more

Catholic Church and health care - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Nakusoma kwa ukaribu mno naendelea kupata darsa.

Pata na hili

The Roman Catholic Church is the largest non-government provider of health care services in the world.[SUP][1][/SUP] It has around 18,000 clinics, 16,000 homes for the elderly and those with special needs, and 5,500 hospitals, with 65 per cent of them located in developing countries.[SUP][2][/SUP] In 2010, the Church's Pontifical Council for Pastoral Assistance to Health Care Workers said that the Church manages 26% of the world's health care facilities.[SUP][3][/SUP] The Church's involvement in health care has ancient origins.

Catholic Church and health care - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Kanisome tena hakuna pahala nimesema "Nyerere na Mtei walichoma Bank.

Wewe kweli Zero unataka kunilisha maneno ambayo sijaandika?

We Mrs Ritz una matatizo ya akili ....... Ritz, mpeleke mkeo akatolewe majini.
 
Last edited by a moderator:
Hilo hapo juu fanya utafiti kidogo kwanza kabla hujawalisha uongo wasiokuwa na nafasi ya kutafuta ukweli hasa wale wa kwenye vijiwe!. Jambo hili limejadiliwa kwa sana.
Mkuu nilidhani hiyo link kutoka serikalini kumbe hapa hapa JF.
 
Presha sina na nimekuelwa unaposema "kanisa Catholic halilazimishi miujiza", lakini wafuasi wake hawawezi kusingizia mema ili tu kipenzi chao awe "mtakatifu"?

Msome: Ludovick Simon Mwijage kitabu chake kinaitwa Julius K. Nyerere: Servant of God or Untarnished Tyrant?

Kanisa katoliki likiamua kumpa Nyerere utakatifu ni sawa tu, Kikwete Mwenyewe mnaemshabikia leo hii amekiri mara kadhaa kwa kinywa chake kwamba bila kanisa katholiki hasingekuwa hapo alipo yeye, yeye ni tunda la Kanisa, hajawahi kusema kuwa yeye ni tunda la Msikiti
 
Mkuu nilidhani hiyo link kutoka serikalini kumbe hapa hapa JF.

Ya serikali nenda magogoni nadhani watakupa Kopi ya MOU-haina uhusiano na Jeshi kwa hiyo haiwezi kuwa siri.

Nimeweka hiyo akajisomee maoni ya Watu.

Hii ni pamoja na wewe-
Je umeshawahi kubaguliwa na Hospitali ya Kanisa?
Je ni Waislamu wangapi wamepata kutibiwa hospitali za Kanisa?
Je waisilamu wanakatazwa/wamekataliwa nao komba MOU na Serikali yao?
Je CAG amepata kuhitaji kufanyia ukaguzi fedha inayotolewa kwa Hospitali za Makanisa nakagomewa?
Sheria inasemaje kuhusiana fedha za Taasisi za dini?

 
Wewe Mama utalaaniwa!! Unajua mti wenye matunda mengi ndio unapigwa mawe!? Nyerere alipendwa na watu wa haiba yako ndio waliojaribu kumuua kama wewe unavyowawinda wazalendo! Huna jipya kila siku Nyerere Nyerere! hadi nataka nitukane!
 
hapo kuna tofauti kati ya hao unaowataja
kwanza China hawana habari na Mao , wao wanamuna Deo Xiaping ndio mkombozi wao na sio Mao mleta ya ujima na kumwaubudu mtu badala ya Budha.Same kama ilivokuwa hapa
Ghandi hakudhulumu mtu
Lincorn alifuta ukoloni na utumwa hakubagua wala kupendela raia wake , hapa kwetu alilipa kanisa nafasi lijitanue
Mandela alipigana na ubaguzi wa aiana zote , hakua na mawazo ya kuwabagua wazungu au watu wenye asili mbali ya Kiafrika , au pia mandela hakudhulumu au kutaifisha mali za wazungu hivyo yupo tofauti raia wake wote wanamuaona mtu wao

Russia wala hawana haja ya kumuenzi mtu kama Stalin au Lenin
Romania pia hawamuenzi Causuescu
Korea pia hawatamuenzi Kim Ill Sung
Eithiopia nao hawatamuenzi Haille sallasie aliwa ficha kuwa watu wake mamilioni wanakufa njaa
wala Uganda hawata mkumbuka Obote aliewabagua watu wake kwa makabila

ni sheria tu kuwa Nyerere ni baba wa taifa lakini anaenziwa zaidi na wakristo , tujiulize kwa nini ? kwani si waislam ndio wao walompokea kumsaidia kupata uhuru ? iweje tena wabadilike ? jibu aliwabagua baada ya kupata ukubwa
kama alikosoea tumkosoe tu hata kama hayupo ili iwe funzo., na kama zipo sifa zake pia tuzitaje




h

Mandela alipigana na ubaguzi wa aiana zote , hakua na mawazo ya kuwabagua wazungu au

hapo neno alipigana lina maanisha nini?...

Nyerere ndo alikua anakataa UDINI na UKABILA....Nyerere alikua naakili sana hakuta kwenda pupa na Waislam kwani alijua ni wadini na ni damu moja na waarabu, ndomana akaona ainusuru zanzibar kwa Muungano wowote tu ilimradi tuungane na Zanzibar isewe ya kidini.....kwa vyovyote vile tusinge ungana na Zanzibar basi ingerudi tena kua koloni la kiarabu afu shida ikawa kwa Tanganyika aliona mbali.....hakua mdini bali hakupenda udini wa waislam.......
 
Eti Mtei ajibu hoja za mtu ambaye kila alichosema JF as on records kimeishia kuwa kinyume chake ni sahihi, ona aibu wewe ni binadamu sio mnyama ambaye akili yako ni kula na kulala.
 
FaizaFoxy

Tunaendelea
8. Walimsingizia eti alizilinda rasilimàli za taifa (madini),si kweli kwani madini yote aliwagawia Wazungu na akina Mwinyi ndio waliorudisha hizi rasilimali mikononi mwa Watanzani.

9.Wanasema aliasisi sera za uchumi wa kujitegemea kwa kuanzisha viwanda vingi kwa msaada wa washirika wake mataifa ya kijamaa (China,Cuba,USSR), si kweli hakuna kiwanda chochote kilichojengwa enzi za utawala wake kwani viwanda vimejengwa enzi za akina Mwinyi.

10.Wanasema eti utawala wa Nyerere haukuwa na madeni makubwa,si kweli kwani utawala wake uliandamwa na madeni lukuki na tawala zilizofuatia ndizo zilizopunguza madeni ya taifa hasa utawala wa Kikwete.

mama hizi chuki zako za dini zitnakupeleka pabaya,viwanda,mwatex,urafiki,bora nk,vilikuwepo hata kabla ya mwinyi ajawa raisi,sasa kina mwinyi gani hao unaowazungumzia kwamba ndio waliojenga viwanda,mwinyi kaingia ikulu 1985,kavikuta viwanda
 
Mkuu, Kanisa kujitanua si kwa sababu ya Nyerere, kwanza Nyerere karudisha nyuma kanisa kwa kutaifisha Rasilimali zake. Kanisa linatanuka kutokana na desturi yake, Ukristo ni zaidi ya kanisa, ukristo ni pamoja na kusaidia watu kupitia matibabu kama hospital, kupitia elimu kama shule, kupitia vituo vya kulelea yatima nk. Hata leo hii Palestina kuna Shule na Mahospital ya kanisa, hata Pale Mosul Iraq kulikuwa na Hospital na shule, tatizo IS wamebomoa.
Somalia kwenyewe kuna shirika linaitwa Catholic relief services linahudumia Wasomali na uislam wao, isipokuwa ofisi ziko Nairobi. Marekani kwenyewe 15% ya hospitals ziko chini ya kanisa, so kutokana na desturi hiyo kanisa liko strong popote pale ambapo limeruhusiwa kuwekeza, Nyerere mmehamua kumuonea tu, yaani Idea yake ya kutaifisha shule za Kanisa ili Waislam nao wasome mmeisahau kabisa.

Kuhusu kwamba Nyerere anaenziwa na Wakristo tu huo ni uongo. Waislam wasio muenzi nyerere ni baadhi ya hawa wa mjini tu ambao wamelishwa na mafundisho ya chuki kutoka kwa akina PONDA na akina Marehemu Ilunga, wale walio vijijini wanamtambua Nyerere vizuri sana na kumkubali, labda muende mkawape sumu

Hakuwarudisha nyuma ni mbinu tu hivyo vitu na shools zipate bajeti ya serikali , ni sawa na promotion ya kanisa wakati nchi ina njaaa kutokana na foleni na sera mbovu za ujamaa , kanisa lilipewa na kuruhusiwa kuagiza kila kitu , lengo ni kupata utajiri na kuwabatiza waislam wasiojiweza kwa njaa .
Huu utabaki ni ukweli na kanisa ndio maana wanajua mchango wake kwao lazima wampe sijui cheo gani
 
Ya serikali nenda magogoni nadhani watakupa Kopi ya MOU-haina uhusiano na Jeshi kwa hiyo haiwezi kuwa siri.

Nimeweka hiyo akajisomee maoni ya Watu.

Hii ni pamoja na wewe-
Je umeshawahi kubaguliwa na Hospitali ya Kanisa?
Je ni Waislamu wangapi wamepata kutibiwa hospitali za Kanisa?
Je waisilamu wanakatazwa/wamekataliwa nao komba MOU na Serikali yao?
Je CAG amepata kuhitaji kufanyia ukaguzi fedha inayotolewa kwa Hospitali za Makanisa nakagomewa?
Sheria inasemaje kuhusiana fedha za Taasisi za dini?

Mara nyingi tu wanabagua bila pesa unakufa nenda Bugando bila pesa kama ujafia mapokezi bei zao hamna tofauti na private kama TMJ au Aghakan wakati Bugando wanapokea ruzuku serikalini.
 
Back
Top Bottom