Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Maskini FaizaFoxy,leo nimeijua rangi yake,kwake yeye mtu muhimu ni yule anaetaka kukumbukwa kama"Bwana Maendeleo".....Nyerere Dunia mzima inamueshimu..Faiza nani bwana wakati hata mtaani kwake hana mchango wa mawazo,huu mnakasha kiwango cha chini sana!!!!!!!
Masikini FF
#Ex Tanzania Simper aliquid novi#
 
Watu wanalalamika "Nyerere hakutuachia TV, yeye tu alitaka aangalie Ikulu"; leo kuna TV kila mahali na watoto wenu wanafaulu zaidi? Hivi mlitaka Nyerere awatengenezee nchi nyinyi mje kula na kulala tu? Mlitaka ajenge shule zote, vyuo vyote, hospitali zote, aondoe matatizo yote halafu nyinyi na watoto wenu mje kufanya nini? kudeka kulikopitiliza!
 
Kama baba alijenga nyumba yenye msingi mbovu, mtoto ukiisha kua bomoa na jenga msingi imara wenye nyumba imara viongozi wetu walitakiwa kuweka kwa muda wote ambao Nyerere hayupo madarakani na ktk dunia hii.TUMHESHIMU NYERERE KWA YALE ALIOYAFANYA KWA TAIFA HILI KWA WAKATI hule na tujadili viongozi wetu wanafanya nn kwa wakati huu!
 
Wala sijapinga kuwa nyerere kama binadamu alifanya makossa mengi tuu na alikiri kufanya hivyo, sasa nitakuwa mwendawazimu kusema hakufanya kosa. Tofauti ya nyerere na wasanii wetu wa siku hizi ni hii ni kwamba yeye liishi kile alichokiamini hata kama alikuwa kakosea.......akisema tufunge mkanda yeye wa kwanza na familia yake kufanya hivyo...ipo mifano mingi tu. Yeye binafsi aliwahi kuwashangaa wale aliowaacha madarakani kwa kuendeleza mambo ya hovyo na nikukumbushe alichosema:

Ikulu pale nimekaa miaka ishirini na mitatu...huu sio muda mfupi hata kidogo...sasa kuna mambo mengi tumefanya pale...mengine mazuri, mengine ya hovyo. Sasa cha ajabu badala ya kuendeleza yale mazuri mmeyaacha na mnaendeleza na kufanya mengine ya hovyo kabisa...

Sasa hoja ya udini ni kweli hujaiweka leo katika post yako lkn nifukunyue unayoandika humu jukwaani kuhusu nyerere na kuonesha chuki zako za wazi zenye mwelekeo huo? Ni mara ngapi umekuwa muasisi wa dhana potofu kuwa nyerere alianzisha kiini macho mnachokiita mfumo kristu?

Ninakufahamu msimamo na muelekeo wako ndio maana nikaelekea ulipo na unaposimamia hata kama hukuyaweka kwenye post yako hii. Kwani mimi na wewe tumeanza leo JF?? Nimemwambia hata chama kwenye post # 349 kuwa nimeandika kwa kuzingatia Muktadha na wajihi wa mleta hoja. I know where you are heading to na ukibisha nitakuwekea link zenye hoja ya leo na haya ninayoyasema so nakufahamu vizuri sio lazima uwe umeyataja.

Vinginevyo kama umezaliwa upya na umefanikiwa "Kuokoka" toka kwenye hiyo dhambi mnayomsingizia Mwalimu basi uweke wazi leo kuwa unayakana ambayo umekuwa ukiyasimamia na kuyaandika hapa.

Hapo umekiri kuwa wewe ndio unaeanzisha udini kutaka kubadili mada na bado unaendelea.

Kuwa makini wakati wakati unajadiliana na watu, kama unataka kujibu kuhusu mambo ya dini nenda kwenye posta unazotaka "kufukunyuwa" ukajibu huko. Wacha ushambenga.

Pia umekiri kuwa Nyerere alifanya makosa. Na hayo makosa ndio huo msingi mbovu. Rais wa kwanza baada ya kujitawala anakubali kuwa amefanya makosa na ndio aliyetazamiwa kuwa ataweka msingi usio na makosa ili nyumba isitoke nyufa baada ya muda mchache tu.

Kumbuka kuwa hayo makosa ndio yaliyotufikisha pabaya, lakini huu uongozi wa sasa umeonesha ujasiri wa kusambaratisha misingi mibovu iliyowekwa na Nyerere na vikaragosi wake (Mwinyi na Mkapa) na kujenga misingi mipya (mfano mzuri ni katiba mpya) ambae hakuna aliyethubutu kabla ya sasa. Upo hapo ulipo?
 
Kama upo unauchungulia kwa mbali ni wazi huna jipya hebu tueleze mbadala wa kutafuta maendeleo ya taifa hili badala ya kupoteza muda mwingi kulaumu misingi ambayo watawala wanaweza kuivunja na kuweka mipya; nimekuwekea mifano ya nchi ambazo ziliwachukua chini ya miaka 20 kubadili misingi ya uchumi na kuleta mfumuko wa maendeleo ya nchi zao; Argentina ni mfano wa nchi hizo 1999-2002; nina uhakika nafsi yako inakusuta elimu yako uliyonayo ni moja sera za Nyerere nina uhakika asilimia 100% kama sio sera za Nyerere ungekuwa muuza vitumbua Kipata; hapa hakuna utumbo yote yanayoongelewa na yana mshiko na kama wewe ni mtoa mada ambaye ulikuwa na nia njema ya kumjadili Nyerere mapungufu yake basi ungeyajibu ila hizi zako ni kejeli na dhihaka ndio maana kila siku unakuja na utumbo uleule unachobadili ni kichwa cha habari!
Kwanza tuyajadili makosa ya kuweka msingi mbovu aliyotuwekea Nyerere akatufikisha kuwa masikini wa mwisho duniani. Tukiiyajadili hayo makosa tutapata ufumbuzi wa haraka kwa kujikamuwa. Naona Kikwete anajitahidi sana kusambaratisha msingi mbovu wa Nyerere na kisha amuwa kutuletea katiba mpya na kuachana na katiba ya Nyerere, ni hatua nzuri sana.
 
1. (a)Msingi maana yake ni nn?
(b) Maono maana yake ni nini?
Msingi & Maono are phylosophical words with more than one meaning depending on scholar's perspectives.
(c) wewe mwenye maono umefanya nini?
2.Baada ya kugundua hajaweka misingi umefanya nn ili kuweka hiyo misingi.
3. Unajua watendaji aliofanya nao kaz (kuanzia ngazi ya kijiji mpk serikal kuu) those days walikuwa na uelewa gan wa uongozi,achilia kiwango chao cha elimu?
4. Hao wanaokulipa buku 7 mbona hatuon wanachofanya.
KWELI WEWE NI FOX ( carnivorous animal of the dog family) bse ata ufahamu wako niwa kama fox,anayetapika na kulamba...

1. (a) = Kwa lugha nyepesi "foundation".
(b) = Perception
(c) = Nimefanya ndio maana nikagunduwa kuwa Nyerere alitupeleka pabaya.

2. Nimemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete akubali kuunda katiba mpya na asambaratishe msingi mbovu uliowekwa na Nyerere na karidhia na matokeo unayajuwa.

3. Hayo sio matatizo yangu wala yako ni matatizo ya Nyerere, wasomi walikuwepo na wenye uelewa walikuwepo. Nalo ni moja katika maamuzi mabovu ya Nyerere, kujiwekea wanaoweza kazi na wenye elimu ofisini kwake na kutuwekea mambumbumbu kwenye utendaji mfani hai na kwa uchache ni pamoja na Kawawa, Songambele, Nnauye.

4. Achana na mimi binafsi, jibu hoja.
 
BABA WA TAIFA..alikua na muono tena wa mbali sana na alikua anaipenda nchi yake kuliko mtanzania yeyote aliupenda ujamaa na kujitegemea ila hakuzungukwa na wajamaa bali alizungukwa na mafisadi kama kina mtei na wengine ila watu wachache hasa wenye mawazo finyu kama mleta mada ndio wanafikiri hakua na muono ila nyerere atabaki kuwa kiongozi bora tanzania na ambae hatakuja tokea mpaka baada ya miaka 200....OVER

Hapo ndipo unadhihirisha kuwa alikuwa hana muono kwa kutaka kulazimisha vitu vya kufikirika. Kuipenda nchi sio kuwa na muono. Fikiri.
 
Wakuu wapendwa Mubuheri,
kama wasemavyo " you cann't blame yesterday's by todays values " Hakuna alokamilika, UKAMILIFU ni wa Mwenyezzi Mungu.... Maoni yangu binafsi :- kupewa Uhuru 1961, ulikwa makosa. Tulitakiwa tukomae kisasa hayo yamepelekesha sasa kila mTanzania ni mwana Siasa na nyanja zote nchini ni siasa tu !! makosa Yapo katika utawala wa awamu zote 4 na Mafanikio yapo katika utawala wa awamu zote 4 lakini matokeo hakuna utendaji/Uwajibikaji/kujituma..!!
Hivi sasa watakuja WaChina na waMagharibi kujenga nyeti zenye masilahi yao. Nasiye WaTZ. tutabaki na SIASA na URASIMU na zaidi VIKAO VIKAO VIKAO bila tija !! AFRICA NOT IN HURRY ndiyo zetu.
Samahanini..still tuPamoja
 
................Tukisema CHADEMA ni chama cha kidini mnakataa.
Hayo maneno hapo juu kasema nani, au
kwa kuwa kumbukumbu zako zinakuja na kuondoka.




​

Weka na hayo maneno yalikuwa yanajibu nini. Au unataka kupindisha ukweli?
 
quote_icon.png
By MAN OF CHANGES 1. (a)Msingi maana yake ni nn?
(b) Maono maana yake ni nini?
Msingi & Maono are phylosophical words with more than one meaning depending on scholar's perspectives.
(c) wewe mwenye maono umefanya nini?
2.Baada ya kugundua hajaweka misingi umefanya nn ili kuweka hiyo misingi.
3. Unajua watendaji aliofanya nao kaz (kuanzia ngazi ya kijiji mpk serikal kuu) those days walikuwa na uelewa gan wa uongozi,achilia kiwango chao cha elimu?
4. Hao wanaokulipa buku 7 mbona hatuon wanachofanya.
KWELI WEWE NI FOX ( carnivorous animal of the dog family) bse ata ufahamu wako niwa kama fox,anayetapika na kulamba...



1. (a) = Kwa lugha nyepesi "foundation".
(b) = Perception
(c) = Nimefanya ndio maana nikagunduwa kuwa Nyerere alitupeleka pabaya.

2. Nimemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete akubali kuunda katiba mpya na asambaratishe msingi mbovu uliowekwa na Nyerere na karidhia na matokeo unayajuwa.

3. Hayo sio matatizo yangu wala yako ni matatizo ya Nyerere, wasomi walikuwepo na wenye uelewa walikuwepo. Nalo ni moja katika maamuzi mabovu ya Nyerere, kujiwekea wanaoweza kazi na wenye elimu ofisini kwake na kutuwekea mambumbumbu kwenye utendaji mfani hai na kwa uchache ni pamoja na Kawawa, Songambele, Nnauye.

4. Achana na mimi binafsi, jibu hoja.

Mkuu FF hebu andikeni kiswahili basi, wengine tumesoma shule za Kikwete jamani. kuna mtu kanambia eti maono ni vision sio perception.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

1. Sidhani ni sahihi kumlaumu Nyerere pekee wakati nchi nzima ilikuwa na watu kibao, Nyerere ni mtu mmoja tu, hao wengine walikuwa maboya?
2. Nani alimuweka Nyerere madarakani? Mi ninavyojua ni chama cha TANU. kwa hiyo kama nyerere alikuwa mbovu, na waliomuweka madarakani ndio wakulaumiwa, basi walaumiwe wanachama wa TANU kwa kutuchagulia mtu bomu especially wale tunaoambiwa walimchangia hela, wakamuhifadhi majumbani mwao kariakoo n.k kama sheikh takadir, sykes, mwapachu, chaurembo na wengineo. kwa sababu hawa wangeweza kumchagua mtu mwingine zaidi ya Mwl kuongoza nchi kupitia TANU.
 
Kwanza tuyajadili makosa ya kuweka msingi mbovu aliyotuwekea Nyerere akatufikisha kuwa masikini wa mwisho duniani. Tukiiyajadili hayo makosa tutapata ufumbuzi wa haraka kwa kujikamuwa. Naona Kikwete anajitahidi sana kusambaratisha msingi mbovu wa Nyerere na kisha amuwa kutuletea katiba mpya na kuachana na katiba ya Nyerere, ni hatua nzuri sana.
kabla ya kukufikisha kuwa maskini wa mwisho duniani watanganyika tulikuwa wapi, watanganyika tulikuwa matajiri kiasi gani?
 
Maoni yangu mimi ni Mwalimu kitu cha kwanza alichokuwa anakitaka [pamoja na wazee wetu] ni political independence.
Huwezi kujua adha ya ukoloni kama kutawaliwa kwani 'mkoloni' aliwagawa watu kwa tabaka ambayo ilikuwa
1. mzungu
2. mhindi
3. waarabu
4. viji kabila vidogo vidogo vyenye asili ya nje kama wangazija nk
Kulikuwa na ubaguzi kuanzia kwenye tiba, kura,elimu, biashara, maeneo ya kuishi nk.
Kwa kipindi kile cha msingi ilikuwa ni kipindi cha 'uhuru na umoja' katika kipindi kile cha siasa aliua uchifu na utemi ili kuleta umoja na mshikamano. Baada ya muungano na znz[ ambao walikuwa wamesaidiwa sana na eastern block] ndipo wafadhili walipoona tunaelekea mashariki wakakata misaada na ndipo ujamaa na kujitegemea ukaanza kama sera ya kutukomboa. Lakini kikubwa zaidi ni ule mtizamo wake kuwa tanzania haiwezi kuwa huru iwapo kuna nchi ya kiafrika iliyokuwa chini ya mkoloni. Tulitumia raslimali ndogo tulizokuwa nazo [pamoja na raslimali watu] kusaidia ukombozi na hapo ndipo tulipoanza kudidimia kiuchumi kwani nchi ilikuwa na mahitaji lakini pia ukombozi nao ulikuwa na mahitaji. Hicho ndicho chanzo cha sisi kuporomoka mengine yalikuja baadaye sana tu. mfano mzuri kenya ambayo ilikuwa mbele kidogo kimaendeleo haikujihusisha kabisa na mambo ya ukombozi na ndiyo maana nchi za magharibi iliikumbatia kwa kuipa misaada mingi ili iwe mfano wa tofauti kati ya ujamaa na ubepari.
Leo ukiniuliza suala hilo na kama nikiangalia yaliyotokea kati ya 1964-1985 siwezi kuthubutu kusema mzee nyerere alikosea au alikuwa sababu ya sisi kuwa katika hali hii.
na kuwa
 
Kumjadili Nyerere ni kukosa akili...Alikwisha sema, YALE MAZURI YA SERIKALI YANGU CHUKUENI, YALE MABAYA YAWEKENI KANDO, AKAENDELEA KUSEMA, TATIZO LETU HATA YALE MAZURI TUNAYAWEKA KANDO NAKUCHUKUKUA YA KIPUUZI. Nadhani kama Nyerere akuweka misingi? Basi tungepaswa kuona akina Mwinyi, Mkapa na Jakaya waweke hiyo misingi, sasa mbona nao wanafanya yaleyale? Ulitaka mwalimu Nyerere aweke misingi ipi? Maana alitujengea misingi ya muhimu sana yaani UDUGU, AMANI, UMOJA NA USHIRIKIANO...Misingi hii ingekuwa ni chachu ya kulipeleka Taifa hili mbele sana, tatizo waliofuata walitumia misingi hii kama faida ya kuiba na kunajisi Taifa hili. Wakatumia amani yetu kama sehemu ya kuiba mali zetu.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Kwa hoja hizi kweli wewe ni fox.
 
Hata Nyerere mwenyewe alisema kuna mazuri aliyofanya na kuna mambo mengine hakufanya vizuri, anachoshangaa viongozi wa sasa ni kuacha hata yale mazuri aliyoyaanzisha.
 
Kajifunze kuandika Kiingereza ndio uje nikuelewe una maanisha nini.

Huo ndio msingi uliowekwa na Nyerere. Hujuwi Kiingereza na nna uhakika hata Kiswahili hukijui.

elewa content ya sms,acha kukengehuka mapema
 
Back
Top Bottom