Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Nyerere bado hana mbadala ktk nchi hii, hata zifanyike juhudi za kumbeza mchana na usiku.
Tunaweza kuona makosa ya Nyerere kwa sababu hatuko katika nafasi yake.

Kama ni soka Nyerere alikuwa anacheza live wengine sasa tunaona replay tena kwa slow motion kisha tunajifanya tunajua kuona makosa
 
Mkirua Huo udini uko wapi, soma post namba moja uuoneshe, ukishindwa, basi wewe ndio mdini na unahamu ya kuibadilisha mada kuipeleka pasipo.

Ikiwa Nyerere mwenyewe alishasema yeye si "malaika" na kuna makosa ameyafanya, wewe ni kama nani wa kumpinga?
 
Last edited by a moderator:
FaizaFoxy nilikuwa nakupa respect kama mkubwa mwenzangu
aliyepata maendeleo na kustaarabika; nimekuja kujua kuwa
huna kumbukumbu ya huko ulikotoka hata unakoenda kumejaa giza tororo;

Mi kivyangu napenda uislamu kuliko hata ukristo;
kwanini unanilazimisha nijiuulize ulize tena bi dada.

Uislam na Ukristo umeanzaje katika hii mada? mimi sikumbuki kuandika hayo katika hii mada, kulikoni?
 
Mtoa mada aliyeanzisha yuko wapi? Hapa tunataka tukuelemishe hii kulikimbia jukwaa ni kujiabisha; wazushi siku zote mnaishiwa cha kusema lakini ukweli utasimama daima hakuna hata kiongozi mmoja wa kumfananisha na Nyerere; Nyerere alikuwa kiongozi wa kimataifa ndio maana wataznania tunaendelea kuheshimika kwasababu ya misingi bora aliyotuachia hizi lawama zenu tunaomba mje na njia mbadala ya nini kifanyike

Sijawahi kukimbia mjadala. Nipo nimejaa tele.

Mpaka sasa nilikuwa nasubiri nione nani yupo kwenye mada na nani anaeleta utumbo. Si kila post inayopaswa kujibiwa.

Tatizo lako nini?
 
Huo udini uko wapi, soma post namba moja uuoneshe, ukishindwa, basi wewe ndio mdini na unahamu ya kuibadilisha mada kuipeleka pasipo.

Ikiwa Nyerere mwenyewe alishasema yeye si "malaika" na kuna makosa ameyafanya, wewe ni kama nani wa kumpinga?

Wala sijapinga kuwa nyerere kama binadamu alifanya makossa mengi tuu na alikiri kufanya hivyo, sasa nitakuwa mwendawazimu kusema hakufanya kosa. Tofauti ya nyerere na wasanii wetu wa siku hizi ni hii ni kwamba yeye liishi kile alichokiamini hata kama alikuwa kakosea.......akisema tufunge mkanda yeye wa kwanza na familia yake kufanya hivyo...ipo mifano mingi tu. Yeye binafsi aliwahi kuwashangaa wale aliowaacha madarakani kwa kuendeleza mambo ya hovyo na nikukumbushe alichosema:

Ikulu pale nimekaa miaka ishirini na mitatu...huu sio muda mfupi hata kidogo...sasa kuna mambo mengi tumefanya pale...mengine mazuri, mengine ya hovyo. Sasa cha ajabu badala ya kuendeleza yale mazuri mmeyaacha na mnaendeleza na kufanya mengine ya hovyo kabisa...

Sasa hoja ya udini ni kweli hujaiweka leo katika post yako lkn nifukunyue unayoandika humu jukwaani kuhusu nyerere na kuonesha chuki zako za wazi zenye mwelekeo huo? Ni mara ngapi umekuwa muasisi wa dhana potofu kuwa nyerere alianzisha kiini macho mnachokiita mfumo kristu?

Ninakufahamu msimamo na muelekeo wako ndio maana nikaelekea ulipo na unaposimamia hata kama hukuyaweka kwenye post yako hii. Kwani mimi na wewe tumeanza leo JF?? Nimemwambia hata chama kwenye post # 349 kuwa nimeandika kwa kuzingatia Muktadha na wajihi wa mleta hoja. I know where you are heading to na ukibisha nitakuwekea link zenye hoja ya leo na haya ninayoyasema so nakufahamu vizuri sio lazima uwe umeyataja.

Vinginevyo kama umezaliwa upya na umefanikiwa "Kuokoka" toka kwenye hiyo dhambi mnayomsingizia Mwalimu basi uweke wazi leo kuwa unayakana ambayo umekuwa ukiyasimamia na kuyaandika hapa.
 
................Tukisema CHADEMA ni chama cha kidini mnakataa.
Hayo maneno hapo juu kasema nani, au
kwa kuwa kumbukumbu zako zinakuja na kuondoka.

Uislam na Ukristo umeanzaje katika hii mada? mimi sikumbuki kuandika hayo katika hii mada, kulikoni?

​
 
Hivi wewe unajua kama Tz ni nchi inayoongoza kwa watu wajinga duniani.....Huyu mzee alikuwa msanii tu.....

Wait a minute! Wajinga ni watu wa aina gani?

Kama unamaanisha kutojua kusoma na kuandika ndiyo ujinga. Basi tujadili hili.

Tujadili kwa takwimu chifu. Cheki hapa, nakuonyesha mwaka na kiwango cha literacy.

1975:61%
1977:73%
1981:79%
1983:85%
1986:90.4%
1992:84%

www.unesco.org/education/wef/countryreports/tanzania/rapport_2_2_2.html

2007-2011: 73%

http://global-4-lvs-hopper.opera-mini.net/ha11-07-07/20270/0/-1/www.unesco.org/450816097/TZ_EDFactSheet.pdf

www.unicef.org/infobycountry/tanzania_statistics.html

Wengine wanasema:

The current literacy situation in Tanzania is shocking. By the mid-1880s, Tanzania was one of the countries with the highest literacy rates in Africa, reaching 98%. Tanzania has experienced a 20% drop in literacy rate for the past 30 years, a situation that is deeply worrying education stakeholders in the country. In the 1980s Tanzania had a literacy rate of over 90% but recent studies as compiled by a UN agency showed that this had dropped to 72 percent.

envaya.org/yestz/post/58586

Sasa kwa takwimu hizo na tukienda na ile maana ya ujinga niliyoisema hapo juu, ni dhahiri watanzania wamekuwa wajinga katika zama hizi za kaka wa taifa. Hapo Mwalimu unamlaumu vipi?

Kama una maana jingine ya 'ujinga' sema tujadili pia.
 
ingia jukwaa la historia usome wewe, kambona aliwashawishi askari waka achana na mapinduzi akamchukua kawawa na nyerere mafichoni. jumbe alihoji hati ya muungano mna mezeshwa sumu
ni kawaida kama tuko timu moja na ukaanza kufanya mambo kinyume na matarajio ya timu kwa kificho unastahili kifo kwa usaliti. adhabu aliyopata Jumbe ilikuwa nyepesi. kutana na mzee Abbas Sykes akueleze undani wa Kambona. Waziri anawaahidi mabalozi wakutane saa tano halafu anakuja ofisini saa tisa alasiri! propaganda zenu pelekeni kwa watu wasiojua historia na wasioweza kupambanua mambo.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
BABA WA TAIFA..alikua na muono tena wa mbali sana na alikua anaipenda nchi yake kuliko mtanzania yeyote aliupenda ujamaa na kujitegemea ila hakuzungukwa na wajamaa bali alizungukwa na mafisadi kama kina mtei na wengine ila watu wachache hasa wenye mawazo finyu kama mleta mada ndio wanafikiri hakua na muono ila nyerere atabaki kuwa kiongozi bora tanzania na ambae hatakuja tokea mpaka baada ya miaka 200....OVER
 
Siyo kweli! Mwalimu was right,hata kama alifanya makosa ni madogo kulinganisha na huyu chekibobu!
Mkuu, kweli baadhi yetu ni ama wavivu au wajinga maana baba wa taifa aliisha kiri kuwa pana makosa wakati wa awamu yake waliyafanya kibin-adam na kutuasa tuyaache.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

1. Msingi maana yake ni nn?
2.Baada ya kugundua hajaweka misingi umefanya nn ili kuweka hiyo misingi.
3. Unajua watendaji aliofanya nao kaz (kuanzia ngazi ya kijiji mpk serikal kuu) those days walikuwa na uelewa gan wa uongozi,achilia kiwango chao cha elimu?
4. Hao wanaokulipa buku 7 mbona hatuon wanachofanya.
KWELI WEWE NI FOX ( carnivorous animal of the dog family) bse ata ufahamu wako niwa kama fox,anayetapika na kulamba...
 
1. (a)Msingi maana yake ni nn?
(b) Maono maana yake ni nini?
Msingi & Maono are phylosophical words with more than one meaning depending on scholar's perspectives.
(c) wewe mwenye maono umefanya nini?
2.Baada ya kugundua hajaweka misingi umefanya nn ili kuweka hiyo misingi.
3. Unajua watendaji aliofanya nao kaz (kuanzia ngazi ya kijiji mpk serikal kuu) those days walikuwa na uelewa gan wa uongozi,achilia kiwango chao cha elimu?
4. Hao wanaokulipa buku 7 mbona hatuon wanachofanya.
KWELI WEWE NI FOX ( carnivorous animal of the dog family) bse ata ufahamu wako niwa kama fox,anayetapika na kulamba...
 
Kajifunze kuandika Kiingereza ndio uje nikuelewe una maanisha nini.

Huo ndio msingi uliowekwa na Nyerere. Hujuwi Kiingereza na nna uhakika hata Kiswahili hukijui.

Tatizo ngano za mzee mudi said zimewaharibu
 
Hebu fafanua tuijadili vizuri hapo kwenye red, mimi naanza halafu wewe pinga hoja zangu......tujadiliane.

-Madini
Alikuachieni tena kwa ahadi kwamba mtavuna mkiwa teyari

-Elimu
wakati wake JK Nyerere, japo walifaidika wachache lakini wote masikini kwa matajiri walisoma shule za aina moja na waliofaulu waliendelezwa mpaka mwisho, leo hii watu binadamu fedha, walalahoi shule za kata hakuna chochote....

-Dawa za kulevya,
Wakati wa nyerere mlipata kusikia ujinga wa madawa haya kama ilivyo sasa na jinsi watanzania wanavyoteketea?

-Afya,
Pamoja na uchache wa dhahati na vituo vya afya, ukienda kutibiwa unapata dawa za uhakika, bure wahudumu na madakitari walifundwa na walikuwa wazalendo wa kweli.

-Polisi, jeshi na usalama wa raia,
Wakati wa Nyerere vikosi hivi vilitawaliwa na nidhamu ya hali ya juu, uzalendo na ushilikiano kwa raia, walihifadhi siri za serikali kwa umakini mkubwa leo hii kila kitu ni upuuzi tu

-Mbuga za wanyama na maliasili

Mliwahi kusikia meli kusafilisha meno ya tembo?, Ndege kubebe twiga, Loliondo kupigwa mnada na akina Katabalo kuuwawa?

-Udini na mshikamano miongoni mwa raia wa tanzania
Mliwahikusikia watu kugawanyika kama ilivyo sasa kwa mitazamo ya udini, ukabila na ukanda? (Tulisifika duniani kote kwa jina moja - tuliitana Ndugu FaizaFoxy, Ndugu Red Giant nk)

Mnataka misingigani nyinyi??? unaweza kumpeleka punda hadi mtoni lakini jukum la kunywa au asinywe maji linabaki kuwa hiari yake sio mchungaji.

How many people had access to right information?

Kulikuwa na magazeti mangapi? Yalikuwa yanamilikiwa na nani?

Usiposikia kitu haimaanishi kuwa hakipo, wake up...

Yaani mkuu hoja yote hiyo hapo juu,ndo umeijibu kwa sentensi hizo mbili tu?
Mie naomba ujipange uje upya la sivyo utakuwa unakwepa hoja nzito na za maana kama hizi!
JIPANGE UJE KIVINGINE!
 
Sijawahi kukimbia mjadala. Nipo nimejaa tele.

Mpaka sasa nilikuwa nasubiri nione nani yupo kwenye mada na nani anaeleta utumbo. Si kila post inayopaswa kujibiwa.

Tatizo lako nini?

Kama upo unauchungulia kwa mbali ni wazi huna jipya hebu tueleze mbadala wa kutafuta maendeleo ya taifa hili badala ya kupoteza muda mwingi kulaumu misingi ambayo watawala wanaweza kuivunja na kuweka mipya; nimekuwekea mifano ya nchi ambazo ziliwachukua chini ya miaka 20 kubadili misingi ya uchumi na kuleta mfumuko wa maendeleo ya nchi zao; Argentina ni mfano wa nchi hizo 1999-2002; nina uhakika nafsi yako inakusuta elimu yako uliyonayo ni moja sera za Nyerere nina uhakika asilimia 100% kama sio sera za Nyerere ungekuwa muuza vitumbua Kipata; hapa hakuna utumbo yote yanayoongelewa na yana mshiko na kama wewe ni mtoa mada ambaye ulikuwa na nia njema ya kumjadili Nyerere mapungufu yake basi ungeyajibu ila hizi zako ni kejeli na dhihaka ndio maana kila siku unakuja na utumbo uleule unachobadili ni kichwa cha habari!
 
chama,
nikupongeze kwa kumpa fact mleta mada japo anaonekana kuchanja mbuga sehemu kusikojulikana.

kimsingi hana chochote anachokijua bali kakaririshwa kutoka kwenye magenge ya kahawa na kama ilivyo kawaida yao kwani wao ni akili kuambiwa kabeba jinsi yalivyo bila hata kuushughulisha ubongo wake.
ona sasa maji yamezidi unga kakurupukia ku-attack watu pasi na hoja.

watu walishajua dhamira yako na wanajua character zako kuwa unasumbuliwa na muwasho wa fangasi za udini na unatafuta wa kukusugua.
chama tosha alikutafuta kakupata naona umekidhi haja ya hilo juha lisilokuwa na utofauti na layman .

kaacha kutoa ufafanuzi wa hoja alioianzisha katumbukia kwenye mipasho ya taarabu.
 
................Tukisema CHADEMA ni chama cha kidini mnakataa.
Hayo maneno hapo juu kasema nani, au
kwa kuwa kumbukumbu zako zinakuja na kuondoka.

​

Hawatasema neno moja....kwa vile maneno yasiyoeleweka ni sehemu ya kuwashikilia ktk ujinga.Im sure kuna values ktk CDM hazimfurahishi shetani.Ukiona mtu anakuchukia kwa kuiona sura yako tuu wakati hakuna mpango wa kuwa wachumba ujue kua mengi nyuma yake.

Haha kuna jamaa aliwahi nichukia ,na kuniambia natabasamu nini..kwa shari kubwa sana..Kumbe mwanamke aliyekuwa akimpenda na kutumia nguvu kumpata.Aliwahi mwambia kuwa napenda smile langu..Mwanamke mwenyewe sikuwa namjua, ila nilikuja recall miezi kadhaa kw akukutana naye akaniambia alikuwa kaimwambia yule boya kuwa anapenda smile langu jamaa akawa anakuwa mbogo.

CDM wana values ambazo hawa jamaa wanakwazika sana,values ambazo pengine ktk ulimwengu wa roho zinapingana.kaulizilizopindapinda zinatosha wapotosha hadi wao ili wabaki ktk hiyo imani.
 
chama nisaidie hii hesabu kama iko sawa
...............Jumlisha hivi vyama hapa chini;

Jibu lake ni sawa na =ccm

Back
Top Bottom